SIRI ZA GIZANI 1 Naitwa Awa, mtoto wa kwanza katika familia ya mzee Shaheem, mama yangu mzazi alifariki dunia nikiwa mdogo sana hivyo nilikuwa katika malezi ya mzazi mmoja yaani baba yangu tu. Ila nilikuwa namshangaa sana baba kipindi nipo mdogo! maana baba alikuwa anapenda sana kuswali, yani alikuwa hapitwi na swala maana kila baada ya mda anaenda msikitini, sasa kilicho kuwa kina niumiza zaidi ni zile swala za jioni ambazo baba alipenda tuswali pamoja kabla ya kulala, sasa hapo ndipo nilikuwa sipendi kabisaaaa, yaani nili tamani kujifungia chumbani na kulala mapemaaa ili asiniite. Uvumilivu ulinishinda ikabidi niwe muwazi tu, ili kumuuliza baba kwanini ana swali kila siku, anafaidika nini sasa? maana mimi nilikuwa naona kama upotezaji wa mda. Nikamuuliza kwamba, "baba hivi kwanini unapenda kuswali faida gani unaipata baba yangu" baba akasema, "weee, unaongea nini hicho, kwahiyo wewe hupendi kuswali au" baba akasema, "mwanangu kuswali ni muhimu, unapo mkumbuka mungu na yeye pia anakukumbuka na anakuepusha na mengi sana, maana dunia ya sasa ni ya laana, ushetani, uzinzi, na matukio mengi ya ajabu na sio hivyo tu, ndugu zangu wengi nimewapoteza kishirikina tu kwa sababu ya uzembe wao wa kumkumbuka mungu, maana mfano kama baba yako mkubwa alie fariki mwaka jana, yeye huyo angekuwa ana swali kwa imani yeye na familia yake nzima wasinge fariki kizembekizembe vile" nikamuuliza baba kwamba, "kizembekizembe kivipi baba" baba akasema ni hadithi ndefu sana hatuwezi kuimaliza sahivi maana tayari ni usiku ila kesho mapema nikumbushe nikusimulie. Kweli kesho yake mapema nikam'bana sana baba anisimulie nijue kwanini baba mkubwa alifariki kizembe. Baba akasema "dahh Awa binti yangu, usahau tu, haya sawa ebu keti kwenye kiti nikusimulie" nilipo kaa ndipo baba akaanza kunisimulia kwamba. "baba mkubwa wako alikuwa anaitwa Abdaal, yeye alikuwa na mke wake pamoja na watoto wawili, sasa kaka Abdaal pamoja na mke wake walikuwa wasomi sana na wote walikuwa wanajiweza kifedha, hivyo familia yao ilikuwa ya upendo sana na furaha pia, walikuwa na nyumba nzuriii, magari matatu na biashara mbalimbali, siku moja, Afra yaani mke wa kaka Abdaal, alikuwa ametembelewa na wageni nyumbani kwake.. itaendelea

at 10:52 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top