Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na nne (14) By GIVAN IVAN Ilipoishia....... Nolan naye hakujali alitoa kadi tano za harusi ya Penina na Frank na kumwekea baba yake kwenye Meza iliyokuwa mbele yake. "karibu Sana Katika harusi ya Penina na mpenzi wake wa Muda mrefu Frank, wewe pamoja na rafiki Zako mnakaribishwa. " Nolan ndio alimwambia baba yake mzee Joel baada ya kumuwekea kadi zile kwenye Meza iliyokuwa mbele yake, Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake. ************Endelea"******** Mzee Joel alibaki akiziangalia zile kadi kwa hasira akazichukua na kuzichana. "huyu mtoto huyu lazima auwawe tu hawezi kuniharibia mipango yangu kiasi hiki." akaongea mzee Joel kwa hasira huku akibugia pombe yake kwa fujo. ******South Africa ******** Hakika Penina na Frank walifurahia Sana kuwa pamoja angalau kwa siku chache ambazo wamekaa pale hotelini South Africa Katika jiji la Johannesburg. Hakika walifurahi Sana, kila kitu walichohitaji walikipata bila usumbufu wowote. "yaani mpenzi wangu natamani Mungu angetutengenezea Dunia yetu tukakae sisi wawili tu ili tuzidi kuwa pamoja milele na milele." maneno hayo yalitoka mdomoni mwa Penina akimwambia Frank walipokuwa wameketi pamoja wakipata chakula cha usiku. "lakini mimi naamini hata Mungu asipotutengenezea Dunia yetu wawili bado atazidi kutusimamia na kutupa nguvu na tutadumu milele." akaongea Frank kumwambia mpenzi wake Penina. "ni kweli mpenzi wangu nafurahi Sana kusikia hivyo." akaongea Penina huku akimtizama Frank.* Siku iliyofuata asubuhi na mapema Nolan alijiandaa na kuondoka nyumbani kuendelea na mipango yake ya kukamilisha taratibu zote za harusi ya Frank na Penina. Kadi za harusi ya Frank na Penina zilisambaa kila sehemu na karibu kila mahali watu walikuwa wakiizungumzia harusi hiyo na wengine wakiisubiri kwa hamu. Nolan aliweza kuwasiliana na Frank na Penina na kuwataka wajiandae baada ya wiki mbili watarejea nyumbani kwa ajili ya harusi yao. Zilikuwa taarifa njema na zenye kufurahisha kwa Frank pamoja na Penina. Hakika walifurahi Sana na kuzidi kumuomba Mungu siku hiyo ifike bila kuwa na tatizo lolote. * Nyumbani kwa mzee Joel aliwasili buffalo mkuu wa kikosi cha the killer na kupokewa kwa furaha Sana na mzee Joel. "karibu Sana kiongozi nimefurahi Sana kukuona." akaongea mzee Joel huku akimuonesha buffalo sehemu ya kuketi. "usijali mzee Joel nimeshawasili kutatua matatizo yako yote nasubiri maelezo kutoka kwako." akaongea buffalo kwa kujiamini. "bila Shaka naamini utanisaidia sana, ngoja nimpigie simu huyu mpumbavu ili akija tu ummalize maana ameniharibia mipango yangu Sana." akaongea mzee Joel huku akitoa simu yake na kumpigia Nolan. Nolan akiwa anaendelea na shughuli Zake ghafla alisikia simu yake ikiita na bila kupoteza Muda Nolan aliitoa na kuangalia nani mpigaji wa simu ile. Nolan alishangaa baada ya kukuta mpigaji wa simu ile ni baba yake. "hahahaaaa mzee wangu leo umenikumbuka mpaka umeamua kunipigia simu." akaongea Nolan kwa kucheka baada ya kupokea simu ile. "ndio mwanangu nimefikira nikaona nilichokuwa nakifanya sio kizuri hivyo nimeona ni bora niungane na wewe kuifanikisha ndoa ya Penina na Frank, itakuwa vizuri kama ukija nyumbani Sasa hivi ili tuweze kujadili vizuri zaidi." akaongea mzee Joel kumwambia Nolan. Lakini ukweli ni kwamba mzee Joel alikuwa anamdanganya Nolan ili arudi nyumbani na buffalo aweze kumuangamiza. Nolan bila kujua lolote akakubali na kumuambia baba yake kuwa "atarejea baada ya dakika kadhaa." Mzee Joel alifurahi Sana na kuona Sasa mwisho wa mtoto wake Nolan umefika. licha ya kwamba ni mtoto wake lakini mzee Joel hakutaka kujua hilo. Mzee Joel pamoja na buffalo wakiwa wanamsubiri Nolan afike, ghafla Dick pamoja na vijana wake wanne waliwasili nyumbani kwa mzee Joel huku wakionekana dhahiri kuwa na hasira kali kwenye nyuso zao. Mzee Joel alipowaona wala hakushtuka kwasababu alijiamini yupo na mtu mzito buffalo. "mzee Joel hatuna tena Muda wa kupoteza tunamtaka Penina la sivyo rudisha pesa zote ulizozipokea kutoka kwangu." akaongea Dick bila hata kutoa salamu kwa mzee Dick wala buffalo. "kijana mambo mazuri hayaitaji haraka nishakuambia kuwa mpole la sivyo Penina hutampata na pesa Zako pia hutapata." akaongea mzee Joel kwa Jeuri kwasababu aliamini yupo na mtaalamu wake buffalo. Dickson alipandwa na hasira na kuwaamrisha vijana wake wamkamate mzee Joel ili waondoke nae kwenda kumfundisha adhabu. Lakini ile wanataka kumkata buffalo aliwazuia na kuwataka waachane nae na watoweke pale haraka iwezekenavyo. "Wewe ni nani kwani mpaka uongee hivyo hebu sogea pembeni." akaongea Dick na kumsukuma buffalo, lakini buffalo wala hata hakutikisika. Dick akaamua kumsukuma buffalo kwa mikono miwili, lakini Dick alijikuta akipokea kibao kizito cha uso kutoka kwa buffalo na kujikuta akirudi nyuma hatua kadhaa huku damu zikiwa zimemjaa mdomoni. Vijana wake Dick kuona boss wao amepigwa wakaamua kulianzisha kule ndani kwa kumvamia buffalo. Lakini buffalo alikuwa mtu hatari Sana vijana wale walijikuta wakiwa na mlima mkubwa wa kupanda baada ya kupokea kichapo kizito kutoka kwa buffalo. Vijana wa Dick wakaamua Kumshambulia buffalo kwa pamoja yaani wote wanne wakajipanga sehemu moja Kisha wakaanza Kumshambulia buffalo. Huyu akirusha teke hapo hapo mwingine anarusha ngumi na hapo hapo tena mwingine naye anarusha teke. Lakini bado hawakufua dafu mbele ya buffalo walijikuta wakitandikwa kama watoto na kujikuta wakiwa hoi bin taabani. Kama kuna mtu alifurahi bas ni mzee Joel. Mzee Joel alifurahi Sana na kuamini hapa Sasa amepata mtu wa maana. Wakati huo huo Dick alikuwa amekaa chini huku akiwa ameshika shavu Lake alilotandikwa na buffalo. Sekunde chache baadae ulisikika mlio wa gari likiingia ndani ya nyumba ile na sekunde chache mbele akashuka Nolan kwenye gari Ile huku akiwa na furaha akiwa hajui chochote kinachoendelea Mule ndani. Nolan alisogea mpaka sebuleni lakini alipigwa na butwaa baada ya kukuta watu wanne wakiwa chini wakiugulia maumivu na mbele yake akamuona Dick akiwa ameshikilia shavu Lake huku mdomoni akitokwa na damu. Nolan akiwa haelewi ni nini kinaendelea mule ndani, mbele yake akatokea mzee Joel akiwa na jitu la kutisha buffalo. "hahahaaaa hahahaaaa leo ndio leo shenzi wewe." akacheka Sana mzee Joel na kumuambia Nolan maneno hayo, Kisha akamuamrisha buffalo afanye kazi yake ya kummaliza Nolan. Nolan akiwa bado haelewi kinachoendelea alishtukia ngumi inakuja kwa kasi usoni mwake na Kisha akaikwepa bila wasi wasi wowote. Kabla Nolan hajajiweka Sawa ikaja tena ngumi nyingine kutoka kwa yule yule buffalo, lakini hata hii Nolan aliiona na kuikwepa. Lakini sekunde hiyo hiyo likaja teke ambalo lilimlenga Nolan uso, Nolan aliliona lakini akakosea kulikwepa na kupatwa la uso na kudondokea kwenye Meza ya vioo na kuipasua pasua. Kabla Nolan hajanyanyuka buffalo akaruka juu na kukunja ngumi tayari kwa kumshushia Nolan pale chini. Nolan akaiona na kujiviringisha na kulikwepa ngumi ile ya buffalo ambayo ilitua kwa kasi na kugonga chini na kupasua sakafu. Nolan alishtuka vibaya mno na kuona hapa shughuli ni nzito tena nzito Sana. Lakini mzee Joel ndio alikuwa na furaha Sana kwa kushuhudia kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na buffalo. Nolan alinyanyuka na kujitikisa na kujiweka Sawa kwa ajili ya kuendelea na mpambano. .................. Itaendelea

at 6:48 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top