Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na tano (15) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp..... 0769673145 Ilipoishia...... Nolan alishtuka vibaya mno na kuona hapa shughuli ni nzito tena nzito Sana. Lakini mzee Joel ndio alikuwa na furaha Sana kwa kushuhudia kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na buffalo. Nolan alinyanyuka na kujitikisa na kujiweka Sawa kwa ajili ya kuendelea na mpambano. ***********Endelea *********** Baada ya Nolan kusimama tu buffalo hakumpa hata nafasi ya kumeza mate alimfuata kwa kasi na kumrushia mateke manne mfululizo na yote yakampata Nolan na kumuweka chini kwa Mara ya pili. Shughuli ilikuwa nzito Sana kwa Nolan kwani hajawahi kukutana na mtu mwenye spidi ya kupigana kama buffalo. Kwa Mara nyingine Nolan alinyanyuka tena huku akiwa tayari ameshawekwa alama usoni. Buffalo kama kawaida yake hakutaka kumpa nafasi ya kupumua, akamfuata kwa kasi na kurusha ngumi nyingine nzito lakini hii Nolan akaiona na kuikwepa ikaenda kugonga dirisha na kuvunja lile lote. Nolan naye this time round akasema hata mimi sicheki na wewe, Nolan aliruka na kumtandika buffalo teke la mgongo na kumtupa nje kwa kupitia pale dirishani. Nolan hakutaka kupoteza Muda akaruka na kumfuata buffalo huko huko nje. Dick pamoja na vijana wake wakiwa pamoja na mzee Joel nao wakatoka nje kushuhudia vita ile kali. Nolan baada ya kufika nje akakuta tayari buffalo ameshanyanyuka. Nolan akarusha ngumi nzito lakini buffalo akaikwepa na kurusha teke ambalo Nolan pia alilikwepa. Ngumi nzito ikarushwa na Nolan kwa Mara nyingine na kumkuta buffalo ya kichwa, lakini pia Nolan naye akapatwa teke Zito la tumbo kutoka kwa buffalo. Vita ile ilikuwa kali Sana kati ya buffalo na Nolan. Lakini mwisho wa siku ilikuwa ni lazima mshindi apatikane. Nolan alijikuta akiishiwa nguvu baada ya kupigana muda mrefu na buffalo na kujikuta akishindiliwa ngumi nzito mfululizo kwenye tumbo zisizopungua kumi Kisha akatandikwa moja nzito ya uso na kutupwa mbali na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa. Lakini wakina Dick pamoja na vijana wake waliona huyu jamaa kwa Jina la buffalo hafanyi poa, wakaamua kumsaidia Nolan. Kwa pamoja walianza tena kumshambulia buffalo. Lakini kwa bahati mbaya hawakuwa na uwezo wa kumpiga buffalo wakajikuta wakitandikwa tena kama watoto na buffalo. Mzee Joel alifurahi Sana na kuona Sasa hakuna panya yoyote wa kunisumbua. Lakini kidogo hivi akanyanyuka Nolan akiwa ametokwa na wazimu. "suti ya harusi nimeshaandaa pamoja na taratibu zingine zote inawezekanaje wewe kimtu mmoja uje na kuharibu mipango yangu inawezekanaje??" akajisemea Nolan akiwa tayari amekwisha nyanyuka. Buffalo alimwaangalia Nolan na kucheka kwa dharau, lakini Nolan awamu hii hataki kucheka na mtu anachotaka Sasa ni kuua mtu bila huruma. Nolan akatoka mbio na kuanza kumfuata buffalo kwa kasi nyingine ambayo haielezeki Kisha akaruka na kukunja miguu na kumgonga buffalo kwa magoti na kumtupa chini. Nolan hakutaka kumpiga buffalo akiwa chini akamsubiri anyanyuka. Buffalo aliponyanyuka Nolan akaruka tiktak na kumpata buffalo mateke ya uso na kumuweka buffalo chini kwa Mara nyingine. Nolan akamsubiri tena buffalo anyanyuke kwa Mara nyingine, na buffalo aliponyanyuka Nolan akateleza kwa magoti mpaka kwenye miguu ya buffalo na kuanza kumshindilia buffalo ngumi nzito nzito za tumbo zisizopungua ishirini, Kisha akanyanyuka haraka na kabla buffalo hajaenda chini Nolan akaamua kummaliza kabisa. Nolan aliruka na kutua shingoni mwa buffalo na kumshindilia ngumi zingine za kichwa na kumpasua kichwa hadharani huku mzee Joel pamoja na wakina Dick wakiwa wanashuhudia. Habari ya buffalo ikaishia pale pale. Mzee Joel aliamua kutoroka baada ya kuona mtu aliyekuwa akimtegemea ameshauwawa hivyo akajua kwa vyo vyote vile yeye pia atakuwa Katika wakati mgumu hivyo akaona njia rahisi ni kutoroka tu. Lakini kwenda kutoroka mzee Joel alidakwa na wakina Dick na kuanza kupewa kichapo cha maana. Mzee Joel alitandikwa akatandikwa mpaka Sasa Nolan akamwonea tena huruma baba yake, akawaamuru wakina Dick wamuache. "tumemuacha muheshimiwa Ila tunachotaka atupe pesa zetu au atupe Penina tuondoke nae." akaongea Dick kumwambia Nolan. "mnachoweza kupata ni pesa zenu lakini sio Penina, kwasababu siku chache zijazo Penina anafunga Harusi na kijana mmoja wanaependana kwa dhati." akaongea Nolan maneno hayo ambayo yalikuwa machungu masikioni mwa Dick. "ok nipeni pesa zangu niondoke maana tumepoteza Muda wetu bila faida yoyote." akaongea Dick kinyonge. Lakini hata hivyo mzee akadai hana pesa yoyote, pesa zote amekwishazitumia na zingine akadai walimuibia na hajui nani alimwibia. Nolan alicheka Sana kimoyo moyo kwasababu alijua yeye ndio alikuwa akimwibia baba yake pesa zile. Nolan akaamua kumtetea baba yake, akawaambia wakina Dick hakuna pesa yoyote watapata kwasababu walifanya ujinga kutoa pesa hizo wakati wakijua hawana uhakika wa kumpata Penina. Nolan aliwataka wakina Dick watoweke sehemu ile haraka iwezekanavyo kabla hajawaangamiza na wao. Dick pamoja na vijana wake walijikuta wakiondoka kinyonge huku wakiamini kabisa walifanya makosa makubwa Sana na hivyo wakaamua kuondoka na kurudi nchini mwao bila kinyongo chochote. Huku mzee Joel alipiga magoti na kutubu makosa yake kwa mtoto wake Nolan na kumuomba amsamehe. Yenyewe hata hivyo damu ni nzito kuliko maji, Nolan aliamua kumsamehe baba yake lakini kwa jinsi baba yake alivyompa mateso Nolan akaamua lazima amtandike ngumi moja ya maana kama njia ya kumsamehe. Nolan alimsogelea baba yake na kumuwekelea ngumi moja nzito ya uso na kumuweka baba yake chini, Kisha akaenda akamnyanyua na kumkumbatia na kumsamehe. Baada ya siku kadhaa ya Nolan kuweka mambo Sawa hatimaye Penina na Frank walirejea Tanzania na Kisha harusi yao ikafanyika bila tatizo Lolote huku ikihudhuriwa na watu wengi kupita maelezo. Mzee Joel pia alikuwepo kwenye harusi ile pamoja na mkewe huku wakifurahia harusi ya mtoto wao licha ya kwamba moyo ulikuwa ukimsuta mzee Joel. Kadhalika pia baba yake Frank pamoja na mama yake Frank pia walikuwepo kwenye harusi ile huku wakiwa wameketi kwenye Meza ya heshima kabisa. Nolan pia alikuwepo kwenye harusi ile na yeye ndio alikuwa msimamizi wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea Katika harusi ile. Harusi ilikuwa nzuri na yenye kuvutia na kila mtu alifurahishwa nayo. Hatimaye harusi ilimalizika salama na maisha yakaanza rasmi Sasa kati ya Frank na Penina wakawa Sasa ni baba na mama. Lakini pia Frank na Penina waligeuka kuwa matajiri wakubwa kutokana na zawadi mbali mbali walizokabidhiwa Katika harusi yao. Hivyo pia waliweza kuwafanya Wazazi wao waishi maisha mazuri na kusahau ya nyuma yaliyopita. Lakini heshima kubwa ilienda kwa Nolan kwasababu bila yeye wasingefika hapo walipo. Na hata walipofanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume wakaamua kumuita Nolan kumpa heshima kaka yake Penina na shemeji yake Frank. Frank na Penina walifanikiwa kupata mtoto wa pili naye pia alikuwa ni wa kiume wakaamua eti kumuita VAN B na maisha yakaendelea. **************MWISHO ************** mkumbuke nilisema hii story ni zawadi ya xmas na mwaka mpya haikuwa Katika mipango yangu. Hivyo nawashukuru wote mliokuwa pamoja Nami kwa kulike kucoment pamoja na kushare. Mwisho niwaambie tu kuna story nyingine iko jikoni Mungu akijaalia itaanza kuruka mwezi wa pili. Who killed my father "nani alimuua baba yangu" ndio Jina la story mpya inayokuja. Ukiniita VAN BOY utakuwa hujakosea hata kidogo. Nawapenda Sana.

at 6:48 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top