Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya nane (8) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp....... 0769673145 Ilipoishia........ Lakini Sasa watu wale ambao walikuwa ni wakina Zaza hawakujua wanamfuata nani. Wazimu wa wazimu Nolan naye alifungua mlango na kutoka kwenye gari Lake na kuanza kuwafuata wakina Zaza bila kuwa na uoga wowote.* *************Endelea ********* Zaza pamoja na wenzake walishtuka kuona Nolan anashuka kwenye gari na kuona anawafuata bila wasi wasi wowote. Na baada ya sekunde chache Nolan alikuwa mbele yao. "mnataka nini mbona tunapotezeana Muda?" Nolan akawauliza wakina Zaza huku akiwa amesimama mbele yao. "hahahaaaa Nolan kwa siku ya leo huna bahati leo umeingia pabaya." akaongea zaza huku akimsogelea Nolan. "leo hakika tutakufunza adhabu." akaongea zaza na kumshushia Nolan fimbo ya mgongo, lakini kabla fimbo Ile haijamfikia Nolan aliidaka na kuivunja. Kitendo kile kilimshtua Zaza na kumfanya akasirike kwa fimbo yake kuvunjwa. Zaza alimrushia Nolan ngumi ya uso lakini nayo pia ilikingwa vizuri na Nolan. "acha kupoteza Muda wako kupigana na mimi hata mkiwa ishirini bado hamtaniweza." akaongea Nolan kumwambia Zaza. Lakini zaza hakusikia, akachomoa kisu na kutaka kumchoma Nolan cha tumbo, lakini Nolan alimkamata mkono ule wenye kisu Kisha akamtandika ngumi tatu tumboni za haraka haraka na Kisha akauosokota ule mkono wenye kisu na kuuvunja. Zaza alijikuta akipiga kelele kwa maumivu aliyoyapata. Wale vijana wengine kuona mkubwa amevunjwa mkono nao wakachomoa visu vyao na kuanza kumfuata Nolan kwa kasi. Nolan akawaangalia na kuwapigia hesabu za haraka haraka. "wewe nitakupiga teke la tumbo, wewe wa pili nitakupiga ngumi mbili za kichwa alafu wewe wa tatu na wa mwisho nitatukutoboa kwenye paja la mguu na kisu chako mwenyewe." hizo ni hesabu za haraka haraka ambazo Nolan aliwapigia vijana wale. Na wakati huo huo vijana wale walimkaribia Nolan, na kama Nolan alivyowapigia hesabu aliwafanya vile vile na kila mmoja akadondokea upande wake. "nyie ni kina nani na mnataka nini?" Nolan akamuuliza kijana mmoja kati ya wale wanne aliowapiga. "sijui hata sisi ni wakina nani" akajibu kijana yule. "nitakuvunja shingo jibu swali nililokuuliza." Nolan akamuamrisha kijana yule. "si nimesema sijui sisi ni wakina nani." akajibu kijana yule jibu hilo ambalo lilimpelekea apokee ngumi nzito ya uso kutoka kwa Nolan. Lakini kumbe wakati Nolan anamuhoji kijana yule, kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye ni dereva wa kina Zaza yeye alibaki kwenye gari na Nolan hakumuona. Mwanamke yule alishuka kwenye gari taratibu akachomoa kisu chake na kuanza kumsogelea Nolan taratibu bila yeye kujua. Mwanamke yule alipofika sehemu ile aliyokuwa Nolan akimuhoji kijana yule alikinyanyua kisu chake juu kwa mikono miwili na kukusanya nguvu Zake zote na kuanza kuhesabu moja mpaka tatu kwa ajili ya kumshushia Nolan kisu kile cha kichwa. Nolan akiwa bado pale chini akimhoji kijana yule ghafla alishangaa kumuona kijana yule akianza kucheka, kumbe kijana yule alimuona yule Mwanamke ambaye ni mwenzao akijiandaa kummaliza Nolan. Lakini kucheka kwa yule kijana kulimfanya Nolan ahisi kitu. Lakini kidogo hivi Nolan aliona kivuli cha mtu pembeni yake, akageuka haraka kuangalia ni nini kipo nyuma, lakini Ile kugeuka Nolan alikutana na kisu kikija kwa kasi kichwani kwake. Nolan alipojaribu kukikwepa kisu alikuwa tayari ameshachelewa, lakini kwa bahati nzuri kisu kile hakikumpata Nolan kichwani, kwani Ile kugeuka nyuma kulimfanya alindishe kichwa kidogo hivyo kisu kile kikampata Nolan bega karibu na shingo. Nolan alisikia uchungu ambao hajawahi kusikia Katika maisha yake. Lakini mwanamke yule alidhamiria kummaliza Nolan, kwani alikichomoa kisu kile kwenye bega la Nolan na kukirudishia tena pale pale na kumfanya Nolan azidi kupiga kelele kwa maumivu aliyoyapata. Mwanamke yule alikichomoa tena kisu kile na kutaka kummaliza Sasa Nolan kwa kumkata shingo. Mwanamke yule alipotaka kumkata Nolan shingo, Nolan alijijaza licha maumivu aliyokuwa nayo alikikamata kisu. Lakini kwa kukimata kisu kile alijikuta akipokea teke Zito kutoka kwa yule yule Mwanamke na kutupwa mbali. Lakini kwa kupigwa teke lile ilikuwa kama vile Nolan ameamshwa kutoka usingizini. Nolan alinyanyuka na kusimama na kumtizama mwanamke yule huku akiapa lazima amuue. "umenipiga Sana hata wewe Sasa umeisha." akaongea Nolan na kuanza kutoka mbio kumfuata yule Mwanamke. Yule Mwanamke naye akatoka mbio na kuanza kumfuata Nolan huku akiwa na kisu chake mkononi. Walipokaribiana yule Mwanamke akaruka juu huku akiwa amekielekeza kisu kichwani kwa Nolan, Nolan kuona vile naye akaruka juu zaidi ya yule Mwanamke na kupita juu kidogo ya kichwa cha Mwanamke yule na kutua nyuma ya Mwanamke yule. Bila kupoteza hata sekunde moja Nolan aligeuka na kuruka juu na kurusha teke Zito ambalo lilimpata sawia kabisa Mwanamke yule la kichwa na kumuweka chini. Nolan hakusubiri yule Mwanamke anyanyuke, akaruka tena juu na kukunja miguu na kutua kwa magoti mgongoni mwa yule Mwanamke yule na kumvunja mgongoni huku wenzake wakishuhudia lakini wasiweze kufanya lolote kwa kuwa nao walikuwa hoi kwa kichapo walichokipata kutoka kwa Nolan. "wewe lazima nikuue umenijeruhi Sana ngombe wewe." Nolan ndio alimwambia Mwanamke yule Kisha akammaliza kwa kumtandika ngumi nzito ya shingo ambayo ilimpandisha ndege ya kuzimu. Baada ya Nolan kummaliza Mwanamke yule naye alijikuta akidondoka chini na kuzimia kutokana damu nyingi iliyomwangika kutoka kwenye mwili wake. Taarifa zilienea kila mahali kwa mauaji yale yaliyotokea sehemu ile huku wengine wakiwa hoi bin taabani. Polisi pamoja na kikosi cha kutoa huduma ya kwanza kilifika pale na bila kupoteza muda, Nolan pamoja na wakina Zaza wakabebwa na kupelekwa hospital.* Mzee Joel akiwa ametulia nyumbani kwake akipata moja baridi moja ya moto, aliweza kupata taarifa Ile ambayo ilimshangaza Sana. "inakuaje wakina Zaza wako hoi na pia Nolan yupo hoi, kuna nini kilitokea?" akajiuliza mzee Joel bila kupata jibu. Huzuni ilianza upya tena kwa Penina baada ya kupata taarifa ya Nolan mtu pekee ambaye alikuwa akimtegemea kwa chochote, kuwa na yeye yuko hoi bin taabani hospitalini. Bila kupoteza Muda Penina aliingia kwenye gari Lake na kuanza safari ya kuelekea Katika hospital aliyolazwa Nolan, Penina alihisi kuchanganyikiwa hasa akifikiria mambo anayotendewa na baba yake, na pia kupotea kwa mpenzi wake Frank. Hali hiyo ilimfanya Penina akose umakini barabarani na akiwa amebakiza mita chache kufika Katika hospital aliyopo Nolan, Penina alijikuta akikosa balance na kupoteza mwelekeo na kutoka nje ya barabara na kwenda kugonga mti uliokuwa pembeni ya barabara Ile. Pale pale Penina alipoteza fahamu baada ya kugonga mti ule, na alipokuja kushtuka alijikuta yupo hospitalini. Taarifa ilimfikia mzee Joel kwamba Penina amepata ajali Muda mchache uliopita. "shit ni bora afe mtu yoyote lakini sio Penina, utajiri wangu upo kwa Penina." akaongea mzee Joel huku akitoka ndani haraka haraka na kuingia kwenye gari na kuanza kuwahi hospitalini kwenda kumuangalia binti yake Penina.* Baada ya kubangaiza huku na kule kwa siku kadhaa hatimaye Frank alifanikiwa kupata pesa ambayo aliihitaji, na bila kupoteza sekunde, dakika wala masaa, moja kwa moja Frank aliianza safari ya kurudi dar es salam huku mawazo yake yote yakiwa kwa Penina tu Mwanamke aliyempenda kwa moyo wake wote. .......... Itaendelea

at 6:46 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top