Home → simulizi
→ Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya saba (7) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp.... 0769673145 Ilipoishia....... Baada ya masaa mawili mbele mzee Joel alirejea nyumbani akiwa pamoja na mgeni wake. Geti lilifunguliwa na mlinzi na gari likaingia mpaka ndani na kupaki sehemu yake. "karibu Sana kuwa huru." akaongea mzee Joel huku akimfungulia Dick mlango wa gari. ******Endelea ***** Mzee Joel aliongozana na mgeni wake mpaka sebuleni ambapo watoto wake wote walikuwepo hapo pamoja na mke wake. "Afadhali nimewakuta wote mkiwa hapa mpokeeni mgeni bas." akaongea mzee Joel. Lakini hakuna mtu alieyehangaika kumpokea mgeni yule isipokuwa Irene peke yake, ambaye ndiyo alimpokea na kumuonesha sehemu ya kuketi. "Penina mgeni wako huyu." akaongea mzee Joel huku akimuangalia Penina. Penina hakujibu kitu alibaki kimya kama hakusikia alichoambiwa na baba yake. "Nolan na Irene huyu ni shemegi yenu kwa maana nyingine huyu ndio mume mtarajiwa wa Penina naomba mlitambue hilo kuanzia Sasa." akaongea mzee Joel kwa kusisitiza. "Nimeelewa baba nadhani kila mtu ameelewa pia." akaongea Irene kuonesha yupo pamoja na baba yake. "Irene acha upumbavu mdogo wangu kama wewe umeelewa mi sijaelewa kitu, baba samahani sana huyo mtu wako hawezi kuwa shemegi yangu kamwe." akaongea Nolan kwa jazba. "Nolan wewe na mimi nani baba kwenye hii nyumba?" akahoji mzee Joel. "wewe ndio mkubwa." akajibu Nolan. "Sasa kama mimi ndio mkubwa lazima ufuate kile ninachokisema." akaongea mzee Joel huku akimuangalia Nolan kwa hasira. "siwezi kufuata upuuzi wako unaoutaka wewe never." akaongea Nolan Kisha akanyanyuka na kuondoka pale sebuleni. "Baba asante kwa chaguo lako lakini mimi sio chaguo langu." akaongea Penina kwa upole kumuambia baba yake Kisha na yeye akanyanyuka na kuondoka pale sebuleni na kumfuata Nolan. Mzee Joel alibaki ametumbua macho asijue afanye nini kwa wakati ule. "Usijali Dick huu ni ushambaa wa huku kwetu Africa Ila usijali nitaweka mambo Sawa, hebu njoo tuonge kidogo." akaongea mzee Joel kumwambia Dick, Kisha wakanyanyuka wote na kuongozana mpaka nje ya nyumba Ile kubwa ya kifahari. "Unajua Dick huyu kijana wangu anayeitwa Nolan ndio anamfundisha Dada yake ujinga ili asiolewe na wewe, ila nakuahidi lazima utamuoa Penina." akaongea mzee Joel kumwambia Dick. "hakuna tatizo mimi nakusikiliza wewe na kama nikimuoa huyo mtoto wako nitakupatia pesa nyingi Sana." akaongea Dick kumwambia mzee Joel. "usijali yule ni wako na lazima utamuoa." akaongea mzee Joel kumpa moyo mzee Joel. "bas Sawa mimi naondoka mambo yakiwa Sawa utanipa taarifa." Dick akamwambia mzee Joel na Kisha akaingia kwenye gari na kuondoka, na kumuacha mzee Joel akiwa anakuna kichwa baada ya kusikia atapewa pesa nyingi kama Dick akifanikiwa kumuoa Penina. "alafu huyu Nolan naona anampa kichwa Sana Penina Sasa ngoja nimfundishe adhabu pumbavu yeye." akajisemea mzee Joel kimoyo moyo Kisha akatoa simu yake na kumpigia Zaza. "yes mzee Joel." akaongea zaza baada ya kupokea simu. "Zaza kuna huyu kijana wangu anaitwa Nolan unamfahamu?" akaongea mzee Joel na kuuliza. "ndio tunamfahamu vizuri Sana." akajibu Zaza. "Vizuri Sana Sasa nataka nimfundishe adhabu huyu kijana maana naona anataka kunipanda kichwani." akaongea mzee Joel kumwambia Zaza. "kivip mzee wangu?" akahoji zaza. "sikiliza Zaza nataka mumkamate huyo kijana wangu mumpelekee sehemu mumtandike mpaka ashike adhabu tumeelewana?" akaongea mzee Joel na kuhoji. "nimekupata vizuri mzee wangu na tuko tayari kwa kazi." akajibu Zaza. "OK bas kuna sehemu nitamtuma alafu nitawaambia ni wapi ili mkamatie hapo." akaongea mzee Joel kumwambia Zaza. "OK hamna shinda mzee Joel." akajibu Zaza na simu ikakatwa. "nimefurahi Sana kaka kwa jinsi ulivyonitetea nakupenda Sana kaka yangu." alikuwa Penina akimuambia Nolan. "usijali mdogo wangu lazima nisimame Katika haki siko tayari kuona haki ikipindishwa kwasababu ya pesa." akaongea Nolan kumuambia Penina. Lakini wakiwa bado wanaendelea kuongea Nolan alisikia sauti ya baba yake ikimuita. "hebu ngoja nikamsikilize nasikia ananiita huko." Nolan akamwambia Penina na kuondoka kwenda kumsikiliza baba yake. "Chukua gari hiyo nenda kaniwekee mafuta sehemu tunayowkaga kila siku." mzee Joel akamwambia Nolan huku akimkabidhi pesa kias kadhaa. Nolan alishangaa kwa kuwa ilikuwa sio kawaida yeye kutumwa Muda kama ule, lakini hata hivyo hakuwa na namna aliaaliamua kwenda kuepusha malumbano na baba yake. Baada ya dakika mbili Nolan kuondoka mzee Joel alitoa simu yake Mara moja na kumpigia Zaza, Kisha akamwelekeza sehemu ambayo wataweza kumkamata Nolan na kwenda kumfundisha adhabu. Baada ya Zaza kupata habari Ile Mara moja aliingia kwenye gari pamoja na vijana wake wanne na kuelekea sehemu ambayo walielekezwa na mzee Joel kumkamata Nolan. * Huku msituni hatimaye Frank alimaliza siku mbili za mapumziko, Kisha akagaana na mzee yule aliyemsaidia na kuanza safari ya kuelekea tabora mjini kwa ajili ya kurudi dar es salam. Frank alitakiwa kutumia siku tatu ili aweze kufika tabora mjini, lakini kwa jinsi Frank alivyokuwa na hasira ya kurejea dar es salam ili aweze kuonana tena na mpenzi wake, alijikuta akitumia siku moja na nusu kufika tabora mjini. Baada ya kufika mjini Frank alianza kuhangaika kutafuta usafiri wa kurejea dar es salam bila kufanikiwa kutokana na kukosa pesa. Frank aliamua kujiunga na vijana wengine waliokuwa pale tabora mjini na kuanza kazi ya kuosha magari ili aweze kupata pesa ambayo itamsaidia kurejea dar es salam.* Nolan akiwa amebakiza mita chache kufika Katika sheli iliyokuwa mbele kidogo na sehemu alipokuwa. ghafla alishtukia gari nyeusi ikifunga break mbele yake na kumzuia njia asiweze kupita. Nolan akiwa bado anashangaa kinachoendelea, ghafla akaona wanaume watatu wakitoka kwenye lile gari huku kila mmoja akiwa na fimbo mkononi na kuanza kuanza kusogea Kuja kwenye gari la Nolan. Mara moja Nolan akatambua hawa watu si wema hata kidogo. Lakini Sasa watu wale ambao walikuwa ni wakina Zaza hawakujua wanamfuata nani. Wazimu wa wazimu Nolan naye alifungua mlango na kutoka kwenye gari Lake na kuanza kuwafuata wakina Zaza bila kuwa na uoga wowote.* ......... Itaendelea
Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya saba (7) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp.... 0769673145 Ilipoishia....... Baada ya masaa mawili mbele mzee Joel alirejea nyumbani akiwa pamoja na mgeni wake. Geti lilifunguliwa na mlinzi na gari likaingia mpaka ndani na kupaki sehemu yake. "karibu Sana kuwa huru." akaongea mzee Joel huku akimfungulia Dick mlango wa gari. ******Endelea ***** Mzee Joel aliongozana na mgeni wake mpaka sebuleni ambapo watoto wake wote walikuwepo hapo pamoja na mke wake. "Afadhali nimewakuta wote mkiwa hapa mpokeeni mgeni bas." akaongea mzee Joel. Lakini hakuna mtu alieyehangaika kumpokea mgeni yule isipokuwa Irene peke yake, ambaye ndiyo alimpokea na kumuonesha sehemu ya kuketi. "Penina mgeni wako huyu." akaongea mzee Joel huku akimuangalia Penina. Penina hakujibu kitu alibaki kimya kama hakusikia alichoambiwa na baba yake. "Nolan na Irene huyu ni shemegi yenu kwa maana nyingine huyu ndio mume mtarajiwa wa Penina naomba mlitambue hilo kuanzia Sasa." akaongea mzee Joel kwa kusisitiza. "Nimeelewa baba nadhani kila mtu ameelewa pia." akaongea Irene kuonesha yupo pamoja na baba yake. "Irene acha upumbavu mdogo wangu kama wewe umeelewa mi sijaelewa kitu, baba samahani sana huyo mtu wako hawezi kuwa shemegi yangu kamwe." akaongea Nolan kwa jazba. "Nolan wewe na mimi nani baba kwenye hii nyumba?" akahoji mzee Joel. "wewe ndio mkubwa." akajibu Nolan. "Sasa kama mimi ndio mkubwa lazima ufuate kile ninachokisema." akaongea mzee Joel huku akimuangalia Nolan kwa hasira. "siwezi kufuata upuuzi wako unaoutaka wewe never." akaongea Nolan Kisha akanyanyuka na kuondoka pale sebuleni. "Baba asante kwa chaguo lako lakini mimi sio chaguo langu." akaongea Penina kwa upole kumuambia baba yake Kisha na yeye akanyanyuka na kuondoka pale sebuleni na kumfuata Nolan. Mzee Joel alibaki ametumbua macho asijue afanye nini kwa wakati ule. "Usijali Dick huu ni ushambaa wa huku kwetu Africa Ila usijali nitaweka mambo Sawa, hebu njoo tuonge kidogo." akaongea mzee Joel kumwambia Dick, Kisha wakanyanyuka wote na kuongozana mpaka nje ya nyumba Ile kubwa ya kifahari. "Unajua Dick huyu kijana wangu anayeitwa Nolan ndio anamfundisha Dada yake ujinga ili asiolewe na wewe, ila nakuahidi lazima utamuoa Penina." akaongea mzee Joel kumwambia Dick. "hakuna tatizo mimi nakusikiliza wewe na kama nikimuoa huyo mtoto wako nitakupatia pesa nyingi Sana." akaongea Dick kumwambia mzee Joel. "usijali yule ni wako na lazima utamuoa." akaongea mzee Joel kumpa moyo mzee Joel. "bas Sawa mimi naondoka mambo yakiwa Sawa utanipa taarifa." Dick akamwambia mzee Joel na Kisha akaingia kwenye gari na kuondoka, na kumuacha mzee Joel akiwa anakuna kichwa baada ya kusikia atapewa pesa nyingi kama Dick akifanikiwa kumuoa Penina. "alafu huyu Nolan naona anampa kichwa Sana Penina Sasa ngoja nimfundishe adhabu pumbavu yeye." akajisemea mzee Joel kimoyo moyo Kisha akatoa simu yake na kumpigia Zaza. "yes mzee Joel." akaongea zaza baada ya kupokea simu. "Zaza kuna huyu kijana wangu anaitwa Nolan unamfahamu?" akaongea mzee Joel na kuuliza. "ndio tunamfahamu vizuri Sana." akajibu Zaza. "Vizuri Sana Sasa nataka nimfundishe adhabu huyu kijana maana naona anataka kunipanda kichwani." akaongea mzee Joel kumwambia Zaza. "kivip mzee wangu?" akahoji zaza. "sikiliza Zaza nataka mumkamate huyo kijana wangu mumpelekee sehemu mumtandike mpaka ashike adhabu tumeelewana?" akaongea mzee Joel na kuhoji. "nimekupata vizuri mzee wangu na tuko tayari kwa kazi." akajibu Zaza. "OK bas kuna sehemu nitamtuma alafu nitawaambia ni wapi ili mkamatie hapo." akaongea mzee Joel kumwambia Zaza. "OK hamna shinda mzee Joel." akajibu Zaza na simu ikakatwa. "nimefurahi Sana kaka kwa jinsi ulivyonitetea nakupenda Sana kaka yangu." alikuwa Penina akimuambia Nolan. "usijali mdogo wangu lazima nisimame Katika haki siko tayari kuona haki ikipindishwa kwasababu ya pesa." akaongea Nolan kumuambia Penina. Lakini wakiwa bado wanaendelea kuongea Nolan alisikia sauti ya baba yake ikimuita. "hebu ngoja nikamsikilize nasikia ananiita huko." Nolan akamwambia Penina na kuondoka kwenda kumsikiliza baba yake. "Chukua gari hiyo nenda kaniwekee mafuta sehemu tunayowkaga kila siku." mzee Joel akamwambia Nolan huku akimkabidhi pesa kias kadhaa. Nolan alishangaa kwa kuwa ilikuwa sio kawaida yeye kutumwa Muda kama ule, lakini hata hivyo hakuwa na namna aliaaliamua kwenda kuepusha malumbano na baba yake. Baada ya dakika mbili Nolan kuondoka mzee Joel alitoa simu yake Mara moja na kumpigia Zaza, Kisha akamwelekeza sehemu ambayo wataweza kumkamata Nolan na kwenda kumfundisha adhabu. Baada ya Zaza kupata habari Ile Mara moja aliingia kwenye gari pamoja na vijana wake wanne na kuelekea sehemu ambayo walielekezwa na mzee Joel kumkamata Nolan. * Huku msituni hatimaye Frank alimaliza siku mbili za mapumziko, Kisha akagaana na mzee yule aliyemsaidia na kuanza safari ya kuelekea tabora mjini kwa ajili ya kurudi dar es salam. Frank alitakiwa kutumia siku tatu ili aweze kufika tabora mjini, lakini kwa jinsi Frank alivyokuwa na hasira ya kurejea dar es salam ili aweze kuonana tena na mpenzi wake, alijikuta akitumia siku moja na nusu kufika tabora mjini. Baada ya kufika mjini Frank alianza kuhangaika kutafuta usafiri wa kurejea dar es salam bila kufanikiwa kutokana na kukosa pesa. Frank aliamua kujiunga na vijana wengine waliokuwa pale tabora mjini na kuanza kazi ya kuosha magari ili aweze kupata pesa ambayo itamsaidia kurejea dar es salam.* Nolan akiwa amebakiza mita chache kufika Katika sheli iliyokuwa mbele kidogo na sehemu alipokuwa. ghafla alishtukia gari nyeusi ikifunga break mbele yake na kumzuia njia asiweze kupita. Nolan akiwa bado anashangaa kinachoendelea, ghafla akaona wanaume watatu wakitoka kwenye lile gari huku kila mmoja akiwa na fimbo mkononi na kuanza kuanza kusogea Kuja kwenye gari la Nolan. Mara moja Nolan akatambua hawa watu si wema hata kidogo. Lakini Sasa watu wale ambao walikuwa ni wakina Zaza hawakujua wanamfuata nani. Wazimu wa wazimu Nolan naye alifungua mlango na kutoka kwenye gari Lake na kuanza kuwafuata wakina Zaza bila kuwa na uoga wowote.* ......... Itaendelea
Artikel Terkait
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA TATU (03) ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI : kas0ro Niram peke yake ambae alisema, "wala sina mpango huo, ntampeleka wapii mimi, ila nimemsifiatu! sababu katika wavulana niliowai kuwaona, kwa hapa mtanzania, yule kaka ni handsome sanaa" alisema Niram huku anawaangalia marafiki zake, ambao wakakubaliana nae, kwakiikisa vicwavyao juu chini, na wakati huo kengele ya darasani ikagongwa, wakasimama tayari kwa kuanza safari ya kuingia darasani, ENDELEA....... Waliingia darasani, na vipindi vikaedelea kama kawaida. Niram alitafakari sana maneno ya rafiki zake,,akujua hata kwanini awazia lile jambo, maana hata sababu ya kuliwazia akuiona. "mmh mimi sasa ntakuwa nataka kurukwa na hakili haki ya Mungu" alijisemea kimoyo moyo Niram. Ila akaamua aachane na fikra zile, ambazo mwenyewe alizoziona za kipuuzi, na kuendelea na ratiba zake nyengine. ****** "hallo mmewangu nimekumisi mno utakuja lini?".ilikuwa sauti ya mama niram, aliye kuwa amepozi kwenye moja ya kochi zuri huku ameweka miguu juu ya meza. "ooh mkewangu kipenzi ratiba zinabana kazi zimekuwa nyingi mno hata mi nimekumisi kipenzi ila sina la kufanya mama".ilisikika sauti upande wa pili, ikiongea kwa masikitiko na mapenzi makubwa kwa mkewe. "ooh darling uwezi kuomba ruhusa ukaja hata kwa siku chache tu?".aliongea kwa kudeka mama niram huku akimpachika na swali mumewe huyo,aliyekuwa mbali na nchi ya Tanzania. "ooh sitawahi, unajua natakiwa kwenda india kuna Mahafali ya Razaki".ilisisitiza sauti ya baba niram. "ooh Mungu wangu nilisahau nasikitika sitoenda kwenye mahafali ya mwanangu".aliongea mama niram kwa unyonge ilionyesha hakuwa na furaha kuikosa hiyo sherehe ya mtoto wake wakiume. "usijali mke wangu, najua uwezi kuja sababu niramu hatokuwa na wakubaki nae wacha niende kukuwakilisha mimi sawa mamaa".aliongea kwakubembeleza baba niram huku akimfariji mkewe ili asijione mkosefu. "oky honey kazi njema nitafute baadae utapomaliza kazi".alisisitiza mama niram, "oky honey byeee ilove you"."love u too mume wangu byee". Waliagana mtu na mumewe, mama niramu akanyanyuka kuelekea jikoni,kuangalia kama msichana wake kama ameshamaliza kupika chakula cha mchana. ********* "eeeh ujue vincent ukumalizia story".alisikika suma akimuambia vicent, wakati huo walikuwa katika uwanja wa mpira, wakiangalia watu wanaofanya mazoezi, akiwemo Richard, yeye alikuwa akifanya mazoezi ya mpira wa kikapu, vicent na suma walikuwa wakimuangalia rafiki yao huyo, ambae alijua kuutumia uwanja vizuri aliku Hodari kweli kweli katika mchezo huo, "hahhhhah suma wewe mshkaji wangu mmbeya sana duuuh! yani kumbe ulisubiri tutoke tu!, yani wewe sikuwezi" aliongea vicent, vikafata vicheko vikaliii, suma alikuwa hana mbavuuu, ungewaona ungesema walikuwa wameona jambo la kuchekesha hapo walipo, "sasa mi nimesubiri we unihadithie naona kimya nikaona bora niseme yanini nife kiholo".aliongea suma huku anakalisha tako vizuri akimgeukua mlengwa. Basi vicent alimuadithia mwanzo mwisho, jinsi alivyokutana nae mpaka ilipofikia kusahau kumuomba namba. "hahahhhah hizo ndoto ndugu yangu yani ndo maana ukamzingua vanessa?".aliongea suma kwa mbwembwe, huku akumuona rafiki yake huyo kama anaota ndoto za mchana kweupe. "sikia suma vanessa mimi simpendi bora tu akate tamaa mapema kuliko nikaja kumuumiza zaidi huko mbele na kuhusu huyo dem ata asiponipenda baridi tu! ilimradi mi nimuekeze hisia zangu tu".aliongea vicent kwa msisitizo akimaanisha anachokisemaa. "aaah naona mnakula tu ubuyu". Aliingia Richard, katikati ya mazungumzo, mwili ukiwa umelowa jasho, aka kaa pembeni yao ilionyesha ashamaliza kufanya mazoezi ******* "mama simu inaita".aliita msichana wa kazi wakina Vincent, akimpelekea simu bosi wake ambae alikuwa amekaa nje kwenye bustani. "asante karunde kaendelee na kazi". Alisema mama yake vicent huku anaweka mkonga sikioni. "hallow magreth niambia rafiki yangu".aliongea mama vicent, aikusikika upande wapili,mara mama vicent akaongea na kuaga"aaah! Sawa basi usijali ntakuambia tarehe ikufika nikutakie siku njema".simu ikakatwa.******** "hahahhhh!! Yani na wewe huo ubuyu tule tumekuwa shilawadu?".aliongea vicent huku anacheka, mabega yote yakifanya kazi ya kunesanesa."yani we acha tu katuchukuliaje huyu sijui huyu bwege".alijibu suma huku akimpiga kofi la bega la kiutani utani. "aaah!bac kausheni vipi ile story ya asubuh nimalizie basi mwana".aliongea Richard huku anajiweka sawa kusikiliza. Vilifwata vicheko hatari. "kumbe na wewe shilawadu" aliongea suma baada ya kumaliza kucheka. Basi story zikaanza upyaa, visent akampa fully data. Richard Akuwa na la kuchangia zaidi ya kumtia moyo na kumwambia akaze buti. mara wakasikia ...... Itaendelea......CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA NNE (04) ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU: "aaah! basi kausheni vipi ile story ya asubuh nimalizie basi mwana".aliongea Richard huku anajiweka sawa kusikiliza. Vilifwata vicheko hatari. "kumbe na wewe shilawadu" aliongea suma baada ya kumaliza kucheka. Basi story zikaanza upyaa, visent akampa fully data. Richard Akuwa na la kuchangia zaidi ya kumtia moyo na kumwambia akaze buti. mara wakasikia... endelea....... mara wakasikia, kama kuna vishindo vinakuja mahali walipo wao .ilibidi wakatishe story yao.nakuangalia mbele palipotokea,sauti ya viatu."mmmmh!!", alishusha pumnzi vicent baada ya kumuona mtu huyo aliyekuwa anakuja usawa waliokuwepo wao. Hakuwa mwengine bali ni vanessa, vanessa alizidi kuiongea taratibu kuja mahali pale, walipokuwepo wakina vicent.hatimae alifika."mambo zenu". Aliwasabahi huku akisubiri atajibiwa kwa hali gani salamu yake."nzuri vp vanessa"alijibu suma, mara kabla ajamaliza kuitikia suma, alidakia richard pia."tuambie shemela wa ukweli".kauli hii ili mchukiza, sana vicent alijikuta anamkata jicho moja kali rafiki yake huyo.ila vanessa alipotezea japo vicent,hakujibu salamu yake. "mi niko poa sana samahanini shemeji zangu nilikuwa naomba mnipishe kidogo nna mazungumzo na vicent".aliongea vanesa, huku akiwaangalia shemeji zake hao kwa zamu."ooh!!usijali mama suma eeh tuwapishe wapendanao".aliongea tena richard safari hii huku anatabasamu tabasamu la kichokozi,maana alijua ni jinsi gani anamkera rafiki yake." twenzetu mwanangu uwanja wenu jamani".aliongea suma huku ananyakua kibegi, chake kilicho kuwa pembeni yake, amesimama na kuanza kuondoka,wakati huo richard alikuwa ameshatanguli mbele." oyaa wanangu msifike mbali mnisubiri maana sitachukua mda mwingi hapa".aliongea vicent huku akiwa bize anatazama walipo kuwa wana tokomea wenzie. " poa".walijibu wote kwa pamojaa na kuendelea kutokomea mbele. "nakusikiliza unaweza kuongea" aliongea vicent bila kupepesa macho, akiwa mkavu kabisa." vincent kwani una nini mbona sikuelewi baba"aliongea vannesa huku anakaa pembeni ya vincent. Ila akupata jibu toka upande wapili."vincent si naongea na wewe au kuna kitu nimekukosea niambie ili nijue nikuombe radhi baba,nakupenda sitaki tukosane".aliongea vanesa kwa huzuni huku machozi yakiwa yanalengalenga kwenye macho yake. "sikia vanessa naomba usipoteza muda wako kwa ajili yangu focus katika masomo ujui kuwa tuna karibia mitihani ya kuhitimu kidato cha Sita ".alisema visent bila alama ya uoga,usoni kwake."najua baba lakini hiyo siyo sababu ya kufanya uwe serious ni kuelewana tu" alilalama vanessa huku akijisigeza karibu na vicent."oky basi ndo hivyo vanessa tuzingatie masomo now mapenzi yasimame kwanza".alimaliza vicent huku akijifuta vumbi, kwenye makalio tayari kwakuondoka. "vicent ntawezaje kukuchunia siwezi ntajitahidi nisome kwa bidii ila tusisitishe uhusiano wetu nakupenda sana". "vanessa tuelewane basi au nimefanya kosa kukusikiliza hapa?". Aliuliza vicent,pasipo kusubiri jibu akaanza,kuondoka.ila vanessa alimdaka mkono,na kumvuta asiondoke.daaaaah!! Lilikuwa kosa kubwa maana alisukumwa,akadondoka kama mzigo wa kuni pwaaaaaaah!!.aisee!! Vanessa aliumia akaanza kulia, maana alijiona kama mtu asiekuwa na thamani tena, aliumia kupita kiasi. Kitendo kile, kilimfanya vicent aingiwe na huruma, akaghairisha alipokuwa anakwenda, maana alijiona ana hatia sana. "nyanyuka mpenzi sikuzamilia kufanya hivyo nisamehe mama ". Alisema vicent huku akiinama, kumnyanyua vanessa na kwa bahati nzuri, hakuna alieliona tukio lile. "pole mama nisamehe sana". Alisisitiza vicent akionyeshwa kuchukizwa, na tukio alilolifanya." usijali vicent najua aikuwa kusudio lako kuna vitu haviko sawa kwako". Alijibu vanessa huku anajifuta vumbi, akisaidiwa na vicent. Baada ya hapo vicent alimchukua na kumkalisha chini. " vanessa siyo kama sikupendi laah hasha!! Nakupenda ila nielewe unatakiwa tusome kwanza tukimaliza mitihani tutaendelea, nafanya haya kwaajili yetu mama".aliongea vicent,siyo kama alimaanisha ila aliona si busara, kumuhukumu mtu kisa kampenda ni dhambi kubwa sana. " sawa ila niahidi tutakuwa tuna ongea hata mara moja moja, kwani bila kusikia sauti yako au kukuona sitaweza kusoma". Aliongea kwa kudeka, huku akijiegemeza kwa vicent. " sawa mama itakuwa hivyo ila naona muda unatutupa mkono, sitaki kuwachosha wenzangu wananisubiri". Alisema vicent huku akisimama tayari kwa kuondoka. "oky bby tutawasiliana ukifika".alisema Vanessa huku akiachia, busu matata shavuni mwa vicent. Basi waliagana na vicent akawafata washkaji zake, safari ikaanza..****** Nyumbani kwa kina niramu, palipoa alifika moja kwa moja mpk nyumbani kwao, akamsalimia dada wa kazi " da anna mamy yuko wapi?" aliuliza huku ana jibwaga juu ya kochi, begi akilitupia juu ya meza kubwa ya kioo, " ametoka kaniaga anaenda supermarket kununua bidhaa zimepungua".alijibu anna msichana wao wa kazi.niramu akajizoazoa kivivu, akaliokota begi lake, akaelekea chumbani kwake. Anna aliondoka kuendelea na shughuli zake.******* Vanessa alifika kwao, alikuwa amechoka, alifika akamkuta baba yake, ametulia kwenye kochi,akisoma gazeti. Nyumba yao ilikuwa, kubwa kiasi yenye uzuri wa kawaida.baba yake alikuwa daktari hospitali ya muhimbili, mama yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi.walizaliwa watano yeye ni watatu kati ya wanaume wawili, na wasichana watatu, wakwanza ni kaka yao.alipita akamsalimia baba yake, na kupitiliza chumbani. Hakika alijikuta anawaza sana matukio, yaliyomtokea shule. " mmh!! Au vicent amepata msichana mwengine?". Alijiuliza."kama ni kweli sitakubalii kwanza sina imani hiyo, labda atakuwa na jambo lingine, ila shule ile nzima, hakuna anaenikamata kwa uzuri".alijiwazia mwenyewe,akijiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Ila gafla aka...... Itaendelea SEHEMU YA TANO (05) ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: wakwanza ni kaka yao.alipita akamsalimia baba yake, na kupitiliza chumbani. Hakika alijikuta anawaza sana matukio, yaliyomtokea shule. " mmh!! Au vicent amepata msichana mwengine?". Alijiuliza."kama ni kweli sitakubalii kwanza sina imani hiyo, labda atakuwa na jambo lingine, ila shule ile nzima, hakuna anaenikamata kwa uzuri".alijiwazia mwenyewe,akijiuliza na kujipa majibu mwenyewe. Ila gafla aka...... ENDELEA. Ila gafla akakumbuka kitu. "mmh si alisema kuwa, tunawasiliana kama kawaida ngoja tuone kama itakuwa hivyo kweli". Alijisemea peke yake, vanessa huku akijiuliza, na kujipa majibu mwenyewe.kiufupi mapenzi yalisha mchanganya, hakujua afanye nini, kumueka vicent kwenye mstari. Aliwaza sana, mpka akapitiwa na usingizi,akasahau hadi kwenda kula chakula.. ****** Niram akiwa bado yupo chumbani, alikuwa ana mfikiria sana vicent, mpka akawa anajiuliza,ni kwa nini amfikirie kama vile. " mmh mbona sasa nawaza upuuzi, kipi ambacho kinanifanya nikumbuke lile tukio la asubuhi".ila gafla kuma kitu akakumbuka, kikamfanya aangue kicheko siyo cha nchi hii. "hahhhhhhahhh!! hhhah!! uwiiii mama weeeeh hhh!!". Alicheka niram kama kichaa. " hivi sasa kilichokuwa kimemgandisha mpka asiondoe gari ni nini?".alijiuliza kisha akaendelea. "maana mtu aliduwaa kama kaona ela alafu yupo pekee yake anavizia jinsi ya kuikwapua hahhhah!!".alijisemesha mwenyewe kisha akacheka tena kwanguvu. Mala mlango ukafunguliwa, Akaingia mama yake ,inaelekea ndo kwanza alikuwa anafika,maana kipochi kilikuwa kwapani. " Eeeeh!! Mwenzetu vipi unaumwa ukichaa, mbona unacheka peke yakoo?".aliuliza mama yake,huku akiwa amesimama mlangoni, kwenye chumba cha binti yake.Niram alishtuka, maana hakutegemea uwepo wa mama yake eneo lile. Ila aliuficha mshtuko wake. "Eeeeeh!! Mama bwana kuna mwalimu wetu alianguka, wakati anaingia darasani, basi nikikumbuka nachekaaa".alivunga niram huku akijifanya kuwa makini na anachokingea. "wewe mtoto shetani si bure mwalimu kaanguka ndo unacheka hivyoo haaahhhhah hatarii, haya vua hizo nguo ukale, maana nakujua wewe hapo ulipo ujala ". Aliongea mama niramu, huku anapiga hatua kwenda nje. "sawa mama naja". Alijibu niram, mara ukasikika mlango paaaaah!, alikuwa mama niramu anafunga mlango . "uhhhhhhhhuh!!"alishusha punzi ndefu niramu, maana akutegemea kama angeweza kudanganya, haraka hivyo. Alibadili nguo nakutoka kwenda kuchukua chakula.. ******* Vicent alikuwa chumbani kwake, akichezea laptop yake.huku ana kula lakini mawazo mengi, yalikuwa kwa niramu. Alijiuliza kwanini ametumbukia juu ya mapenzi ya msichana, wakihindi hakika chakula hakikulika ,alikuwa na mawazo ya hatari yaliyo mfanya, chakula aone kichungu. " ntajitahidi kumtafuta naimani ntampata tu".alijiwazia kimoyomoyo, asijue aanzie wapi, amalizie wapi.ila gafla akiwa kwenye dimbwi la mawazo, alisikia simu yake inaitaaa. Ngrrrrrrrri ngrirrrrrrr!! "nani tena huyoo?". Alijiuliza huku akijiinua kuifata ,kwenye kochi maana yeye alikuwa kitandani. " daaaah!! Anataka nini tena huyuuu aaah!!".alilalamika vicent huku anaipokea simu. "hellow vanessa". Aliongea " yes bby nimekumic nikaona nikupigie". Ilisikika simu upande wa pili alikuwa vaness. " Oooh!! Kumbe niambie". "vicent nilikuwa na kukumbusha lile ombi langu nililokuomba". " lipi hilo?".alihoji vicent huku akimsikiliza kwa makini. "ni lini utanipa penzi lako?, nashindwa kujizuia vicent". Alilalama vanessa huku akisubiria, jibu upande wa pili. "Vanessa hivi kumbe jini wako apendi amani eeh!!?".aliuliza vicent, na kabla ajajibiwa akaongeza neno. " hivi leo nilitoka kukuambia nini hivi upo serious kweli wewe?, naomba usinitibue kama unawaza ngono badala ya kusoma ni wewe mimi naomba unikaushie kabisa".aliongea kwa jazba vicent, huku mikunjo kwenye paji la uso,likionyesha ni jinsi gani amechukia. "ooh nisamehe bby, mi nilikueleza tu hisia zangu wala sitaki tugombane".alijitetea vannesa maana alijua ashaharibu. " oky nikutakie jioni njema kesho mungu akipenda" aliongea vicent, na bila kusubiri jibu simu ikakatwa. Kiukweli vanessa, alijilaumu kwanini aliongea vile, aliilaani ile siku kwani aliiona siku mbaya kuliko zote. Baada ya kukata simu, vicent alikirudia kitanda na kujibwaga bado kidogo angemwaga chakula, kwenye kitanda. " Oooohsh!! Yote sababu ya huyu mwanamkee aaah!!". Alilalama vicent, huku lawama zote akimtupia vanessa. Eti wadau ukipenda sana unaonekana msumbufuu eeeh?.. Tuendeleee.. Basi vicent akachukua kile chakula na kukiweka chini akaendelea na ratiba zake . ******** Ilikuwa muda wa saa mbili kamili usiku(02.00) vanessa alikuwa yupo selbeni na mdogo wake wa mwisho wa kike, aliitwa juliana.kifupi unaweza mwita juli, walikuwa wanaangalia tv.wengine wakiwa na mishemishe zao, huku wazazi wao wakiwa wameshaingia chumbani,maana hata muda wa kuangalia taharifa ya habari aukuwepo, kutwa watoto wanaangalia movie zao. Ndio maana mzee wao anaamua ajununulie gazeti.. Muda wote wapo sebleni ila vanessa alikuwa kimya, kama anawaza jambo. Ila juli aliiona hali tofauti aliyokuwa nayo dada yake .. "vipi dada unaumwa mbona ueleweki leo?". Swali la juli lilimshtua vanessa ,kwenye dimbwi la mawazo akawa hana jibu sahihi la kumpa akabaki, kumbabaisha tu " hamna juli mdogo wangu nawaza mitihani sijui itakuwa migumu?".alivunga vanessa na kujifanya kuuliza ili kupoteza mada. " mmmh!! Dada usiwaze mbona nakuaminia itakuwa ya kawaida muhimu usome ". Alimjibu juli, vanessa akatingisha kichwa kukubali. Ila hakukaa sana akamuaga nduguye akaingia ndani kwake. ********* Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho......itaendelea ... Read More
*LOVE BITE EP 03* ILIPOISHIA………. Mawazo yalirudi tena kwenye ile picha na kuamua kuificha bila kuichoma moto kama alivyotaka mwanzo kufanya. Badala yake alienda sehemu ambayo kulikuwa na hati ya nyumba yake na kuiweka ile picha katikati. Ni kweli Prisza alikuwa anampenda na hawakuwahi kuachana. Ni muingiliano tu wa maisha ndi uliowatenganisha. Moyo wake aliona kama si haki kuichoma ile picha kwakua bado alikua na nafasi ndani ya moyo wake japokuwa kuonana na msichana huyo ni ngumu sana. Hata alipomaliza chuo alijitahidi kumtafuta bila mafanikio. Mpaka muda huu anajitegemea ni kipindi kirefu cha miaka sita tuko walipokutana na Prisca kwa mara ya mwisho. Mawazo ya msichana huyo wa kwanza katika maisha yake yalimchanganya kichwa na hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokea na kuanzisha ukurasa mwengine wa maisha yake kwenye mapenzi na shani Baada ya usafi huo wa kabati lake, aliamua kujilaza kitandani na usingizi ukamchukua. SONGA NAYO………… Siku ya pili yake Jothan alienda kazini kama kawaida. Alifanya kazi zake na baada ya kurudi kazini alimkuta Shani amejaa tele nyumbani kwake. “karibu mume wangu “ alikaribisha Shani na kumfuata Jothan na kumpokea mizigo yake. “ahsante.” Aliongea Jothan na kumkabidhi mizigo yake Shani. “una oga kwanza au unakula ndio uende kuoga?” aliuliza Shani baada ya kurudi pale alipokuwa Jothan. “vyovyote tu mke wangu. Maana nahisi joto na hata njaa pia ninayo.” Aliongea Jothan na kumfanya Shani atabasamu. “kaoge kwanza, maana ukiwa vizuri hata chakula kitashuka barabara.” Alishauri Shani na mawazo yake yakapitishwa moja kwa moja na Jothan. Alipotoka kuoga Jothan, alirudi mezani na kukuta Shani ameshaandaa mapocho pocho ya kila aina yaliyochafua meza. “unajua mke wangu, hata niwe na njaa vipi, kama wewe upo nyumbani basi hudiriki kuitunza hiyo njaa kwa sababu unajua sana kupika mke wangu. Muda mwengine naomba nipate na njaa ya ajabu ili nikifakamie kisawasawa chakula chako.” Aliongea Jothan na Shani akabaki anatabasamu na kumuangalia Jothan kwa mapozi. Mapenzi moto moto kutoka kwa Shani yalizidi kupamba moto. Muda wote Shani alijitahidi kumuweka Jothan kwenye kundi la wanaoyafurahia mapenzi. Jothan alijisikia raha kutokana na Shani kila wakati kutokana na mauzo anayoyapata kuwa na msichana High classic. Walitamani kila saa wawe karibu na kulishana ndio style iliyowavutia watu wengi waliowashuhudia wawili hao walionyesha kupendana sana. Siku moja Jothan akiwa anatoka kazini, ghafla aliona gari likiwa limepaki pembeni na kuna msichana akihangaika kulishughulikia lile gari. Jothan alipaki gari lake pembeni na kushuka kwa ajili ya kutoa msaada. Alipomfika eneo la tukio, yule dada aligeuka kumuangalia Jothan na wote wakajikuta wanapigwa na butwaa. “JOTHAN!!” aliita yule dada kwa sauti kubwa iliyoambata na mshangao mkuu. “PRISCA!!” hata jothan naye alilitaja jina la yule msichana na kumfanya Prisca kujiachia na kupitisha mikono yake mgongoni mwa Jothan kupitia kweye makwapa yake kama ishara ya kumkumbatia. Jothan naye akampokeaa vizuri kwa kuzungusha mikono yake kwenye kiuno namba 6 cha Prisca. Baada ya kusalimiana, wakaona haitoshi. Waliacha gari zao pale pale na kutafuta sehemu tulivu na kukaa kwa ajili ya kupigiana story mbili tatu kutokana na kukumbukana kupita kiasi. “ ahsante mungu kwa kunikutanisha na kipenzi changu jamani,.. jothan milima haikutani ila binaadamu tunakutana. Leo hii kauli hiyo ndio naikubali kwa asilimia zote.” Aliongea yule dada huku akionyesha furaha ya wazi juu ya Jothan ambaye wakati huo alikua na tabasamu la usoni lakini kichwani alikua kwenye msongo wa mawazo. Anampenda Prisca lakini kwa sasa Shani amechukua nafasi kubwa kwenye moyo wake kutokana na kumpa kila anachokihitaji tena kwa wakati. Alikiri kuwa kwa sasa Prisca alizidi uzuri na kumfunika hata Shani. Maana Shani alikuwa ameridhika na kuzidi kuwa mnene kiasi japokuwa sio kigezo cha kupunguza uzuri wake. Ila Prisca alikuwa mwembaba lakini aliyekuwa na figa iliyojichonga kama glasi ya wine. Kwenye kiuno alikuwa mnene na kufaya hipsi zake kuonekana sana. Pia kijungu cha wastani kilichotupiwa huko nyuma ndio kilizidi kumpa maksi zaidi na kumfanya azidi kuonekana special na wanaume wote wanaojua viwango vya wanawake wazuri na wenye mvuto katika muonekano wa macho ya marijali. Kiuno kilichoingia ndani na muinuko wa kibinda ndio kilitengeneza namba 6. kiuno hicho mungu kawapendelea wasichana wachache sana. Hata wachina wameshindwa kutengeneza dawa ya kutengeneza kiuno hicho. Sura ya mviringo iliyokuwa na macho yenye kilevi bila ya kunywa kileo chochote ndio kilikuwa kivutio kingine. Ukiachana na weupe halisi ambao ulikuwa kiasi na kufanana na maji ya kunde, pia vijisima vidogo mashavuni vilivyojitokeza kila akifanya tendo lolote liliousumbua mdomo wake vilimfanya mtu yeyote kutamani kumuangalia usoni. Uso uliombwa na haya mbele ya mwanaume ndio ulikuwa kivutio hasa kwa mvulana mwenye kutafuta mtu wa kuweka ndani na kuoa kabisa. Mambo yote hayo ndiyo aliyokutana nayo Jothan baada ya kukutana na Prisca kwa mara nyingine baada ya muda mrefu. Hata yeye mwenye alikutana na majaribu hayo aliyoyafananisha na majaribu ayapatayo mwanamke mjane baada ya kusikia sauti ya mwanaume tajiri aliyekuja kumfariji na kwa kumuahidi kumuoa na kuwa tayari kuwalea watoto wake. Alijikaza kiume na kujaribu kuyaficha madhaifu yake yaliyomkumba na kujifanya yupo kawaida. “Hata mimi nimefurahi kukuona, za miaka?” aliongea Jothan na kumuangalia Prisca ambaye alikua na furaha wakati wote huo toka wameonana. “vipi, leo maaskari hawaji??” aliuliza Prisca na kucheka. “leo hakuna mwanafunzi hapa..au wewe mwanafunzi?..maana siku ile nilikataa kuwa mimi ni mwanafunzi halafu wewe ukajitambulisha kuwa mwanafunzi.” Aliongea Jothan na kufanya kicheko kitawale kwa sekunde kadhaa kati yao. “tumetoka mbali sana Jothan, leo naona kabisa kuwa mungu katufanya tusahau kipindi chote ambacho hatukua pamoja.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kuwa bado alikuwa na mawazo ya mapenzi juu ya Jothan. “hata mimi naona kama vile hatukuonana siku mbili kwa jinsi siku ya leo ilivyofukia mashimo ya miaka mingi niliyoishi bila kuiona sura yako.” Aliongea Jothan na kumuangalia Prisca aliyekuwa na kila kitu cha kutalii umuangalipo usoni. “nikuulize swali Jothan?” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kushangaa kidogo baada ya kuombwa ruhusa ya kuulizwa kitu. Alifikiria kwa nukta kadhaa kisha akaruhusu kusikia kitu alichotaka kuuliza Prisca. “umeshaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine zaidi yangu?” Aliuliza Prisca swali hilo huku akiwa kawaida na kuonyesha wazi kuwa lile swali linahitaji majibu sahihi na yenye utashi juu yake. Jothan hakuamini kama swali lile lingekuja mapema kabla hajaliandalia maandalizi yoyote ya kujibu. Ubongo wake ulikimbia kwa kasi kutafuta jibu la kumpa kati ya ukweli au kumuongopea kwakua wakati huo swala la kumuepuka au kumpotezea msichana huyo aliyeonja penzi lake toka hajakuwa sister du kama hivi sasa. Elimu ya msichana huyo na maisha mazuri anayoishi pia vilikuja kwenye ubongo wake na kufanya machaguo kuwa mengi. Yaani kama ni mtihani, basi lile swali lilikuwa katika mfumo wa matiple choice tena lililokuwa na mfumo wa A,B,C,D,E na F.. “sina.” Alijibu Jothan huku moyo wake ukimuuma kumkana Shani. “wooh… ni wazi hii couple Mwenyezimungu amekuwa akiismamia kwa kipindi kirefu. Unajua kuwa hata mimi nilikuwa naamini kuwa kuna siku tutakuja kuonana tena. Ndio maana sikuona uzito wowote kuwakataa wanaume wengi huku nikiwa sijui ni lini tutakutana. Roho ingeniuma sana ungeniambia kuwa kuna mwengine umeshampa moyo wako.” Aliongea Prisca bila kujua kuwa huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe. Maneno hayo yalimfanya Jothan ajione kuwa hakuwa na makosa kumuongopea kwa sababu angemwambia ukweli chochote kingeweza kutokea na kusababisha maongezi ya amani kati yake na Prisca kutoweka. “unataka kuniambia kuwa mpaka hivi sasa hauna mtu mwengine aliyerithi mikoba yangu?” aliuliza Jothan kimitego. “hakuna… yaani toka uliponiacha sijaguswa na mtu mwengine. Yaani hata kama ungekuwa umenifunga luku basi zingesoma unit zile zile ulizoziacha.” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kutabasamu. Waliongea mengi na kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzake pale. Waliachana baada ya kumrekebishia Prisca gari lake na kila mmoja kupata mawasiiliano yote ya mwenzake. Waliachana na ahadi ya kukutana naye tena walikubaliana kuwa watapeana taarifa kwenye simu. Siku hiyo iliwekwa kwenye Diary ya Jothan ambaye alikuwa anatemba nayo kwenye mkoba wake wa kazini. Usingizi ulikuja ukiambata na ndoto iliyojirudia kuanzia mwanzo hadi pale walipoachana. Aliamka asubuhi na kukuta Shani ameshamuandalia maji ya moto kwa kuwa asubuhi hiyo ilikuwa na kiubaridi kidogo. Alipoamka tu aliletewa nguo za bafuni pamoja na mswaki ambao ulisha wekwa dawa kabisa. Alipokuwa bafuni mawazo yaligeuka upande wa pili na kumfanya amuwaze pia Shani kwa jinsi alivyokuwa akitimiza wajibu wote kama mke bora anavyotakiwa kufanya. Kila aliloliwaza kutendewa na msichana basi Shani alikuwa wa kwanza kufanya hata kabla hajaambiwa fanya. Hayo na mengine mengi ndio yalimfunga Jothan na kuyatuliza macho yake kwa wasichana wengine na kumfanya kuwa mtiifu kwa kurudi nyumbani mapema. Na kama anataka kupata moja moto maja baridi basi hutoka na mpenzi wake huyo ambaye alimfanya kuinjoy kwa kuwa sehemu nyigi walizoingia hakukua na mtu mwenye demu mkali kama wake. Alimaliza kuoga huku kichwani hakujua jibu nini kati ya A au B. kuna wakati alitamani kuyaweka kuwa yote ni majibu. Kuna wakati alitamani arushe shilingi ila alishindwa kumjua nani amuweke mwenge na nani amuweke bichwa. Prisca ndio msichana waliyebikiriana kwakua yeye hakuwahi kufanya mapenzi kabla kutokana na ulinzi thabiti wa wazazi wake alipokuwa anasoma. Na Prisca ndiyo yeye aliyekata utepe. Shani ndio mpenzi wake wa ukubwani ambaye anamuonjesha matamu ya ndoa hata kabla hajafikia maamuzi ya kuoa. Hata sasa anaanza kuonekana na kitambi kidogo kwa sababu ya raha azipatazo kwa mpenzi wake huyo. Japokuwa walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, lakini hawakuwahi kukaa pamoja hata wiki moja kwa sababu kila mmoja alikuwa anaishi na wazazi wake. Ila Shani na yeye wamekuwa wakilala pamoja mara tatu kwa wiki. “itakavyokuwa ndio hivyo hivyo.” Aliongea Jothan baada ya kuona anaisumbua akili yake bila majibu sahihi. Siku waliyo ahidiana kukutana kati ya Jothan na Prisca iliwadia huku kila mmoja akiwa amewasili bila kukosa huku wakiwa wamejitupia vitu vya thamani kila mmoja. Make up na mpangilio wa nguo alizovaa Prisca zilimfanya kuonekana katika muonekano mwengine wa kuvutia zaidi. Jothan hakuamini kuwa ndiye yeye alikuwa analala kwenye kifua cha yule msichana zamani. Pia hakuamini kuwa huyo msichana ndiye aliyekuwa akilipigania penzi lake miaka yote japokuwa walikuwa hawajaonana miaka mingi. Walikutana huku kila mmoja akiwa ameshuka kwenye gari lake na kwenda kwenye hotel moja yenye hadhi hapa Dar. Walipata chakula cha mchana na baadae wakaenda kwenye swimming pool kuogelea. Hamadi !, Macho yalimtoka Jothan baada ya Prisca kuvua nguo zake na kubaki na nguo ya ndani huku juu kukiwa na sidiria ndogo iliyobana maziwa yake na kuyafanya yapande juu na kuonekana sehemu kubwa ya maziwa iliyoteganishwa na msitari mmoja kati kati kuwa wazi. Jothan hakuona ubaya kuvua nguo na yeye na kubaki na boxer na kujumuika naye kwenye swimming pool huku wakiwa peke yao eneo hilo lililokuwa na mabwawa mengi ya kuogelea. Waliogelea na kujikuta michezo yote wanacheza. Kuanzia bembea, mpira wa pete na mwisho wakamaliza na mchezo usio hitaji kocha wala mashabiki japo kuwa unapendwa na watu wengi hapa duniani. Ukiwa mtoto unaambiwa kuwa mchezo huo ni mmbaya lakini ukikuwa bila kufundishwa unajikuta unacheza huku ukijilaumu kwa nini hukuanza kucheza toka mwanzo. Hawakujua walitumia muda gani kwakua taa za ile hotel ziliwaka muda wote na kufanya mtu asitambue wakati kama hajaangalia saa. Mndinyo wa kitanda murua cha hotel hiyo ndio sababu iliyowafanya kudumu muda mrefu huku kila mmoja akiwa ame miss raha za mwenzake. Mechi hiyo ya marudiano ilikuwa kali na kila mmoja alikiri kuwa walihitaji kuwa karibu na kucheza kila mara. Baada ya muda, Jothan aligutuka kuwa hiyo siku ndio siku Shani alikuwa analala kwake. Aliamka fasta na kutupa macho yake kwenye saa ya ukutani “MUNGU WANGU…. SAA SABA USIKU?” Alishtuka kimoyo moyo na kutaja alichokiona kwenye saa. Aliamka ili aenda kuoga kwa ajila ya kwenda nyumbani kwake. “vipi darling, unaenda wapi tena… mwenzio nahitaji kimoja tu cha mwisho.” Alidakwa mkono kimahaba na Prisca aliyekuwa ameyarembua macho yake na kuonyesha ishara zote za kuhitaji kipindi cha pili baada ya mapumziko. “najisikia uchovu ndio maana nilikua nataka kwenda kuoga.” Aliongea Jothan huku akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya Shani kugundua usaliti alioufanya siku ile. “twende wote babie, tukirudi mpango mzima au…” aliongea Prisca na kumfanya Jothan azidi kuchoka. “poa.. twende.” Alikubali kishingo upande na wote wakaenda kuoga na uchokozi alioufaya Prisca huko bafuni ikiwafanya mchezo huo kuanzia huko huko bafuni na kumalizikia kitandani wakiwa hoi na usingizi wa muda wote waliokuwa wakicheza cheza ulikuja na kuwafanya wapate usingizi mnono. Saa nne asubuhi ndio waliachia kitanda na kwenda kuoga. Walipofungua mlango walikutana na wahudumu waliokuwa wakigonga kwa ajili ya kufanya usafi. Walieda kupata supu kutokana na kupotelewa na nguvu nyingi masaa kadhaa yaliyopita. Baada ya hapo. Walijiandaa na kila mmoja akapanda kwenye gari lake huku Prisca akionyesha wazi kuwa aliufurahia uzinduzi wa uhusiano yao uliofanyika kwenye kitanda cha hotel ya SERENA. Jaothan akiwa kwenye gari lake, aliiona simu yake aliyoiacha makusudi kwa ajili usumbufu pindi awapo na Prisca. Alikuta missed call zaidi ya kumi na tano na sms sita zote zikiwa za Shani na zikionyesha kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake. Alihuzunika sana kwa kosa alilolifanya japokuwa hakupanga kulala nje. Maisha ya kuendesha mioyo miwili hakuwahi kuishi na tayari kwa siku hiyo aliona adha yake na kutamani kuchuja na kuwa na mmoja tu. Ni nani ambaye angestahili kubaki na ni nani atoke ndio swali lililokosa majibu kwakua wote alikuwa anawakubali kwa wakati wao. Alivyolala na Prisca alikuwa kama alikuwa anamfungua kwa mara ya kwanza hali iliyomfanya aamini kuwa hakutumika muda mrefu. Aliona sio sawa kumuacha msichana huyo mwenye ndoto naye nyigi za maisha yao toka walipokuwa wanasoma. Na Shani hakustahili kutendewa unyama wowote kwakua hata yeye hajawahi kumfanyia unyama wowote zaidi ya kumfariji anapokuwa ana huzuni na daima aliisimamia furaha yake hata ikibidi kuenda kinyume na matakwa ya dini kwa kukubali kuishi nae bila ndoa. Akiangalia kila mmoja alionyesha kumpenda kwa wakati wake na hawakuwa tayari kumuachia. Ila yeye swali la NIMPENDE NANI lilimsumbua kuliko hata DIAMOND. Aliamua kuwasha gari lake na kuelekea nyumbani. “oooh.. ahsante mungu. Umekumbwa na nini kipenzi changu?.” Aliongea Shani baada ya kuupokea mkoba wa Jothan. Hali hiyo ilimshangaza Jothan kwakua hakutegemea mapokezi kama yale. “samahani mke wangu, sikukupa taarifa kuwa ofisini kuliandaliwa warsha na nikaenda kwa kudhani itaisha siku hiyo. Hata hivyo simu yangu niliisahau kwenye gari na kunifanya nisizione missed call zako mapema.” Aljiuma uma Jothan mbele ya Shani ambaye wakati huo ndio kwanza alikuwa anamvua viatu baada ya kukaa kwenye moja ya masofa yaliyokuwa pale sebuleni. “sawa mpenzi wangu. Nimefarijika tu wewe kurudi salama.. maana nilikuwa na wasi wasi juu ya uzima wako tu.” Aliongea Shani na kumuonyesha Jothan jinsi anavyomjali. “samahani sana mpenzi wangu, nitajaribu kukupigia simu kwa kila siku nitakayochelewa kurudi nyumbani.” Aliongea Jothan na kukiri kuwa amefanya makosa makubwa ambayo hata yeye mwenyewe hakuyategemea. Siku hiyo ilipita kwa Jothan kulala muda mrefu kutokana na uchovu wa jana yake. Asubuhi aliamka na kukuta ameandaliwa nguo za kuvaa kwa ajili ya kwenda kazini zikiwa zimepigwa pasi kabisa. Aliwekewa maji ya uvugu vugu kwa ajili ya kuoga kisha kifungua kinywa matata kilikuwa tayari mezani kinamsubiria yeye tu. “ashante mke wangu.” Alishukuru Jothan baada ya kumaliza kunywa chai. “usijali mume wangu, nakutakia safari njema. Take care honey.” Aliongea Shani na kumfungulia mlango wa gari Jothan. Jothan alifika kazini mapema na kufanya kazi zake kama kawaida. Saa nane alitoka kazini na kurudi nyumbani. Alikuta ameandaliwa chakula cha mchana mezani lakini Shani hakuwepo kwakua ilikuwa ni siku ya kwenda kwao. Alijihisi mpweke na alitamani Shani angekuwepo kwake moja kwa moja. Alikata shauri baada ya kula chakula na kuamua kumtafuta mpenzi wake kwenye simu. “hallow” alipokea Shani kwa mapozi. “I miss u babie, unaweza kuja tutoke baadae kidogo tukale mbuzi maeneo ya Facebook pub?” aliongea Jothan. “noo babie, leo nimeenda kwa mama. Sio vizuri kuonyesha tabia mbaya mbele yake ya kurudi usiku. We vumilia babie. Kesho tutakuwa wote.” Aliongea Shani kwa pozi zilizomfanya Jothan kushindwa kukata simu hata kama maneno ya msingi ya kuongea nae yameisha. “basi sawa. Sijui lini utanipeleka kwa mama.” Aliongea Jothan huku anatabasamu. “si wewe mwenyewe tu hujaamua. Ukiamua hata leo nakuleta huku.” Aliongea Shani huku akionyesha wazi kuwa alikua anacheka. “nitakuja tu mine, si unajua mambo mazuri hayahitaji haraka.” Aliongea Jothan na kukata simu. Siku ya pili yake walitoka pamoja na kwenda kula bata maeneo hayo na kurudi mida ya saa tano usiku. Alipokuwa kazini, alisikia simu yake ikiita kwa mlio tofauti. Kabla hata hajasoma jina la mpgaji wa hiyo simu. Tayari alishamtambua kwakua aliihifadhi namba ya mtu huyo kwa mlio tofauti kwa makusudi. “haloo.” Aliipokea ile simu. “haloo babie, I miss u.” sauti nyororo ya kike ilisikika upande wa pili. “I miss u too Prisca, niambie.”aliongea Jothan huku akiangalia wafanya kazi wenzake waliokuwa bize wakifanya shughuli zao. “hata kunitafuta wangu,.. yaani kama uliniroga mwenzako siku ile. Yaani sijielewi mpaka hivi leo.” Aliongea Prisca kwa sauti ya mahaba. Jothan aliangalia na kuona soo kuendelea kuongea maneno yale mbele ya wafanyakazi wenzake. “sema nini babie, nitakupigia nikiwa free. Now nipo kazini halafu nina kazi nyingi.” Aliongea Jothan kwa sauti ya chini. “sawa wangu, baadae.” Aliitkia Prisca na kukata simu. Jothan alifanya kazi zake na kurudi nyumbani kwake. Baada ya kupata chakula cha mchana, alijitupa kitandani na kuchukua simu yake na kumpigia Prisca. “haya lete maneno.” Aliongea Jothan baada ya Prisca kupokea simu. “nina hamu ya kuonana na wewe babie… sihitaji kuwa mbali na wewe hata kwa dakika moja kwa jinsi nillivyozimika mbaya.” Aliongea Prisca kwa sauti iliyomshinda mwana dada wa kipindi cha ala za roho kinachoruka usiku kwenye kituo cha clouds fm. Sauti ilipenya vizuri kwenye masikio ya Jothan na kuhisi labda Prisca alichanganya sauti ya Loveness love (Diva) na wema sepetu. “tupange week end, sababu katikati ya wiki ni majanga.” Aliongea Jothan. “poa, ijumaa si ulisema unatoka mapema. Unaonaje kama tukikutana siku hiyo.” Aliongea Prisca na wazo lake likapitishwa moja kwa moja na Jothan. Siku ya ijumaa ilipofika. Jathan alimpa taarifa Prisca na wakakutana maeneo ya Peacock hotel iliyopo maeneo ya mnazi mmoja. Jothan alifika na kumkuta Prisca alishafika muda mrefu kidogo na tayari alishaagiza kinywaji na alikua anakunywa taratibu. Alipofika, alipokelewa kwa kukumbatiwa na Prisca na kupewa mabusu matatu matakatifu kwenye mashavu yake na moja likiwa sawia mdomoni mwake. Baada ya salamu hiyo adhimu. Walimuita muhudumu aliyekuja haraka na kumpa oda yao. “tuchukue chumba sasa hivi au baadae?” aliuliza Prisca baada ya kumaliza kula. “hapana, leo sijisikii vizuri kabisa na sipo tayari kushiriki tendo lolote Prisca.” Aliongea Jothan na kumfanya Prisca apigwa na butwaa. Maana alijiandaa kabisa kupata mechi nyingine siku hiyo. “kwanini babie….unaumwa???” aliuliza Prisca kwa mshangao. “siumwi, ila mayo wangu unanisuta kila siku nikiongea na wewe kwenye simu au nikikutana na wewe. Najihisi sifanyi fair kwa nikitendacho.” Aliongea Jothan huku sura yake ikionyesha wazi kuwa hakuwa na furaha ingawaje aliingia kwa muonekano wa mtu aliyefurahia uwepo wao pale. “jamani, tatizo ni nini wangu, mbona una nifumba fumbo ambalo sijui nitalifumbua vipi?…naomba uniambie ukweli kuliko kuniweka mwenzako kwenye uzio wa alama ya kuuliza.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kubadilika kutoka katika hali ya furaha aliyokuwa nayo mwanzo na kuungana na Jothan. “Prisca, hivi bado unanipenda?” aliuliza swali Jothan lililomfanya Prisca apigwe na bumbuwazi kwakua hakulitegemea lile swali. “nakupenda sana tena zaidi ya niwezavyo kuelezea kwa ulimi wangu. Ndio maana nikaweza kukaa kipindi kirefu bila ya kuwa na mtu mwengine japokuwa ni wengi walikuwa wanakuja kunitongoza na bado sikuona umuhimu wa kuanzisha mapenzi mapya kabla mapenzi yako wewe na mimi kufa.” Aliongea Prisca na kumuangalia Jothan aliyekuwa makini kumsikiliza. “hata mimi nakupenda Prisca, ila mimi ni msaliti na sio mwema kwako hata kidogo. Cha kwanza nimekuwa muongo kwa kukuongopea toka siku ya kwanza tulipokutana kwa mara ya pili ukubwani. Cha pili sistahili kuwa wako kwakua tayari nimeshakuharibia mipango na malengo yako kwa kipindi krefu Prisca.” Aliongea Jothan huku akionyesha wazi kuwa alikuwa katia wakati mgumu kufunguka yale yaliyomjaa moyoni. “sikueliwi Jothan.. naomba nidadavulie uyasemayo.” Aliongea Prisca huku akionyesha kuchaganyikiwa. “kwanza naomba unisameha Prisca kwa haya nitakayokuambia. … nilifanya makosa makubwa siku ile kwa kutokuambia ukweli kuwa tayari nina msichana na ninaishi naye. Nampenda sana ingawaje sikuweza kutoka kwenye mitego yako siku ile kwakua wewe ndio wa kwanza kukaa moyoni mwangu na chembe chembe za upendo juu yako ndizo zilizonisukuma mpaka kukuongopea na kukuambia kuwa sina mtu. Siwezi kuweka mafahari wawili kwenya zizi moja. Na kumuacha Shani ni kitu kisichowezekana kwakua ananionyesha mapenzi zaidi ya niliyowahi kufikiria mapenzi kuwa hivyo. Maamuzi yangu ni kwamba. Kuanzia leo sahau kuwa na mimi ni mpenzi wako…. Niwie radhi kwa hili.” Aliongea Jothan huku machozi yakimlenga lenga. Hakika ni uamuzi mgumu aliouchukua kwakua aliamini ilikuwa ni mtihani mkubwa katika mapokezi ya mlengwa. Alipoinua macho yake kumtazama Prisca, tayari mashavu ya prisca yalishalowana kwa machozi huku macho yakiwa mekundu. Kilio cha kwiki kilianza kusikika na kumfanya Jothan kuingiwa na imani baada ya kumtaza mpenzi wake huyo anaye amua kumuacha bila kosa lolote. ITAENDELEA ... Read More
Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na moja (11) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp....... 0769673145 Ilipoishia......... Upande wa Nolan yeye alipanga lazima amfundishe adhabu baba yake kwa namna yoyote ile. "Wewe ni baba yangu ndio sikatai, umenitunza vizuri, umenipa elimu ya kutosha Sawa, lakini kwa unyama huu unaotaka kuufanya hakika sitakuacha lazima nitaenda sambamba na wewe." alijisemea Nolan akiwa chumbani kwake akipanga mipango yake. Lakini pia Nolan aliapa kama asipofanikisha ndoa ya Frank na Penina bas atajiua. *********Endelea ******** Nolan alivunja kibubu chake cha kuhifadhia pesa na kugundua pesa iliyopo huko ni ndogo Sana na haitatosha kutimiza mipango aliyoipanga. Nolan aliamua kuwa mwizi wa ghafla kwa ajili tu ya kutimiza anachokitaka. Lakini hata hivyo hakuenda kuiba sehemu nyingine yoyote, aliamua kumuibia baba yake ikiwa ni njia moja wapo ya kumkomesha baba yake. Nolan alikuwa anajua baba yake ana tabia ya kuhifadhi pesa chumbani kwake. Na baada ya Nolan kugundua kuwa baba yake hayupo haraka akaamua kwenda chumbani kwake na kumuibia pesa kiasi cha shilingi million hamsini. Baada ya zoezi hilo, Nolan alichukua kiasi cha fedha kati ya zile alizomuibia baba yake na Kisha zingine akazificha sehemu ambayo mtu mwingine hawezi kuziona. Kisha Nolan akatoka nje na kuchukua gari Lake na kuondoka nyumbani Muda ule ule. * Mzee Joel alitia nanga Katika kikosi kimoja kilichojulikana kwa Jina la the killer (wauaji) Baada ya kufika mzee Joel alielezea shida Zake zilizompwleka pale na Sasa akitaka Frank pamoja na Nolan wauwawe Mara moja. Mzee Joel alitoa picha ya Nolan pamoja na ya Frank na kumkambidhi mkuu wa kikosi kile cha the killer. "mzee tunahitaji pesa kiasi cha shilingi million thelathini ili kuitimiza kazi yako." akaongea mkuu wa kikosi kile kumwambia mzee Joel. "hakuna tatizo kuhusu pesa nyie fanyeni kazi niliyowapa." akaongea mzee Joel. "Sawa kuanzia Sasa kazi imeanza na tutakuletea majibu Muda si mrefu." mkuu yule wa kikosi cha the killer akamwambia mzee Joel. Mzee Joel aliweza kuondoka huku akiwa na uhakika wa Kaz yake kufanyika kwa ufasaha Sasa. Mkuu wa kikosi kile cha the killer aliwateua vijana wanne kwenda kuanza kazi ya kummaliza Nolan na Kisha wengine wanne akawatuma kwa Frank. * Katika hoteli ile ya kifahari Penina na Frank wakiwa wameketi kitandani wakitizama tv, ghafla bila kutarajia walishtukia kumuona Nolan akigonga mlango. "Eeh kaka mbona umekuja bila taarifa?" akauliza Penina kwa mshangao baada ya kufungua mlango. "lazima nije ghafla na taarifa zangu ziwe za ghafla kwasababu nataka nifanye kitu cha kuwafurahisha, na hivi nimekuja kuwaambia mjiandae tuondoke tayari nimeshawakatia tiketi za kwenda South Africa (Afrika kusini)" akaongea Nolan kumwambia Frank na Penina. Zilikuwa taarifa za ghafla kwa kina Penina na Frank, lakini hata hivyo hawakuwa na namna ilibidi waanze kujiandaa kwa ajili ya safari yao waliyoandaliwa na Nolan. * Vijana wanne waliopewa kazi ya kumuangamiza Frank walichunguza wakachunguza na hatimaye wakafinikiwa kupajua nyumbani kwa kina Frank. Na bila kupoteza muda wakavamia nyumbani kwa kina Frank na kuwaweka chini ya ulinzi Wazazi wake Frank pamoja na mdogo wake Frank. Vijana wale wakawaamuru Wazazi wake Frank waseme sehemu alipo Frank la sivyo watawaangamiza. Wazazi wake Frank kwa kuogopa kuuwawa wakajikuta wakitaja sehemu aliyopo Frank. Vijana wale bila kuchelewa waliachana na Wazazi wake Frank wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea sehemu aliyopo Frank ambapo ni Katika hoteli moja ya kifahari. * Frank pamoja na Penina walimaliza kujiandaa na moja kwa moja wakatoka ndani ya chumba kile na kuelekea mpaka nje ya hoteli ile na kuingia kwenye gari la Nolan. Lakini wakati huo huo vijana wale wanne wa the killer walikuwa tayari wameshawasili kwenye gari lile na waliweza kumuona Frank pamoja na Nolan ambao ndio walikuwa wakiwatafuta wawamalize. Mmoja kati ya vijana wale wanne wa the killer alitoa simu yake na kuwapigia wale vijana wengine wanne waliokuwa wakimtafuta Nolan, na kuwaeleza sehemu aliyoonekana Nolan pamoja na Frank. Vijana wale waliokuwa wakimtafuta Nolan nao walianza safari ya kutoka sehemu nyingine waliyokuwa wakimtafuta Nolan na kushika njia ya kuelekea Katika hotel waliyoelekezwa na wenzao. Wakati huo huo Nolan aliliondoa gari pale hotelini na kuanza safari ya kuelekea Katika uwanja wa ndege. Vijana wale wanne wa the killer nao wakawasha gari Lao na kuanza kuwafuatilia ili waweze kujua wanaelekea wapi na kama ikiwezekana wakaulie huko huko. Safari ikiwa inaendelea, ghafla Nolan aliona gari moja nyekundu ikiwa nyuma na kuitilia mashaka kuwa inawafuatilia. Nolan aliamua kufanya kitu ili apate uhakika kama gari lile linawafuatilia au haliwafuatilii. Nolan alipunguza mwendo wa gari Lao ili lile gari jekundu lililokuwa nyuma yao liwapite. Lakini cha kushangaza gari lile halikuwapita nalo pia lilipunguza mwendo na kwenda taratibu pia. Nolan akaamua kuongeza mwendo wa gari Lao ili kuliacha gari lile, lakini pia gari lile liliongeza mwendo na kuwa Sawa Sawa kabisa na gari la kina Nolan. Nolan hapo Sasa ndio akapata jibu kuwa asilimia Mia moja hilo gari jekundu linawafuatilia vibaya mno. "hawa hawanijui ngoja niwaoneshe mimi ni nani." akajisemea Nolan kimoyo moyo na hapo hapo akaongeza mwendo wa gari Lao ili kuliacha gari lile lililokuwa likiwafuatilia. Wakati huo huo kile kikosi cha pili cha the killer kiliwasili pale hotelini na kuwapigia wenzao simu ambao ni wale wanaowafuatilia wakina Nolan, na kuwatarifu kuwa tayari wameshafika. Kikosi kile cha kwanza kikawapa maelekezo ya sehemu walipo wakiwa bado wanawafuatilia wakina Nolan. Kikosi kile cha pili bila kupoteza Muda nacho kikatoka pale hotelini na kuanza kuwafuatilia wakina Nolan pia. Wakati hayo yote yanaendelea Frank na Penina walikuwa wakicheka na kufurahi kwenye gari bila kufahamu chochote kinachoendelea, na hata Nolan hakutaka kuwaambia chochote kwa kutokutaka kuwavuruga Katika safari yao. Nolan bado alizidi kujaribu kulipoteza gari lile lakini bado hakufanikiwa. Nolan alifika kwenye mataa ya kuongozea magari na baada ya Nolan kuvuka tu kwenye mataa yale, zikawaka taa nyekundu kuashiria magari yaliyokuwa yakitoka upande ule wa kina Nolan yasimame kwa dakika kadhaa. Lakini Nolan wao walikuwa tayari wameshavuka lakini vijana wale wa the killer walikuwa bado hawajavuka hivyo ikawabidi wasimame. Nolan aliweza kugundua kuwa gari lililokuwa likiwafuatilia limesimamishwa kwenye mataa. Lakini Nolan akataka kuwafahamu ni wakina walikuwa wanawafuatilia. Nolan alipaki gari pembeni Kisha akawashusha Frank na Penina na kuwapakiza kwenye tax iliyokuwa pembeni yao, na kuwakabidhi kila kitu kilichostahili kwenye safari yao na kuwataka watangulie na kuanza safari yao. Penina na Frank walishangazwa Sana na maamuzi ya Nolan lakini hata hivyo Nolan hakutaka wamuulize swali lolote, alimwamuru dereva wa tax ile awashe gari na kuondoka. Kisha Nolan naye akaingia kwenye gari yake na kugeuza kuwafuata vijana wale wa the killer na wakati huo walikuwa tayari wameshaungana wote kwa maana ya kikosi kile cha kwanza kilichokuwa kikimtafuta Nolan na kile cha pili kilichokuwa kikimtafuta Frank. ............ Itaendelea ... Read More
Story - - - - - NI WEWE TU PENINA Sehemu ya pili (2) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp___0769673145 Ilipoishia........ Katika bar moja iliyopo maeneo ya sinza kikao kimoja kilikuwa kikiendelea, na huku kilichokuwa kikipangwa Katika kikao kile ni namna ya kulivunja na kuliharibu penzi la Penina na Frank. Mzee Joel ambaye ni baba yake Penina, pamoja na Angel ambaye ni mdogo wake Penina pamoja na vijana wengine watatu wa kiume na mmoja wa kike, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa kikao kile. *********ENDELEA ******** "sitaki mwanangu aolewe na yule mlala hoi kwa namna yoyote Ile naomba muyakatishe mpenzi yao, nitawapa pesa yoyote mnayotaka." alisikika mzee Joel akiwaambia vijana wake. "hamna shinda mzee wetu kuanzia Sasa tupo Katika mipango ya kuliharibu penzi hilo usijali mzee wetu." kijana mmoja aliyeitwa zaza ndio alisikika akiwaambia mzee Joel maneno hayo. "nitafurahi Sana kama hili likifanikiwa siwezi kukubali mwanangu aolewe na yule mnuka jasho." mzee Joel bado alizidi kuongea kwa jazba. "baba hata mimi nakuunga mkono Dada hawezi kuolewa na yule mnuka shombo." aliongea Angel naye kumuunga mkono baba yake. "hamna shida mzee Joel tutafanya mnayotaka." akaongea Zaza. "bas Sawa ngoja niwape pesa ya maji ili muweze kuianza kazi Mara moja." akaongea mzee Joel na kutoa pesa kias cha shilingi laki mbili na kumkabidhi Zaza agawane na wenzake. "Asante Sana mzee wetu na kuanzia Sasa sisi tunaianza Kaz." akaongea Zaza huku akipokea pesa zile, na Kisha wakaagana na mzee Joel na kuondoka.* Katika ukumbi mmoja wa starehe mziki wa taratibu ulikuwa ukipigwa kwa utaratibu wa hali juu kabisa, huku watu wawili wanaopendana kupita maelezo wakiwa ndani ya ukumbi huo huku wakiburudika na mziki mwororo uliokuwa ukipigwa Katika ukumbi ule, watu hao ni Penina pamoja na Frank. "Frank nakupenda Sana mpenzi wangu sijui nifanye nini ili ujue ni kwa kiasi gani, nafahamu jinsi baba yangu anavyokuchukia Ila yeye hawezi kuwa chanzo cha mimi kutokukupenda wewe, hakika nakupenda Sana." aliongea Penina maneno hayo akimuambia Frank na kujilaza kifuani mwake. "nafahamu Penina ni kwa kiasi gani unanipenda na pia unatambua ni kwa kias gani mimi nakupenda, napenda nikuahidi tu kuwa NI WEWE TU PENINA hakuna mwingine zaidi yako." Frank naye alimwambia Penina maneno hayo ambayo yalimfanya Penina azidi kutoa tabasamu tamu usoni mwake na kuzidi kumvuruga Frank, ambaye alijiona ni mwanaume mwenye bahati Sana kuwa na msichana mrembo kama Penina. Kama Kuna zile sifa wanaume huzitafuta kwa wanawake bas Penina alikuwa nazo na zingine za ziada. "yaani mpenzi wangu kila nikikuangalia nakuwa na maswali mengi ya kijinga ya kukuuliza kwa jinsi tu ulivyo mzuri." aliongea Frank akimwambia Penina. "hahahaaaa maswali gani hayo mpenzi wangu hebu niulize moja." akaongea Penina na kumtaka Frank amuulize moja. "swali moja ambalo huwa najiuliza kila ninapokuona huwa najiuliza hivi wewe ulizaliwa na mwanadamu au Mungu ndio alikutengeneza mwenyewe alafu akakuleta duniani?" akauliza Frank huku akiwa anamtazama Penina. "hahahaaaa Frank mpenzi wangu mi nimezaliwa na mwanadamu kama wewe." akajibu Penina huku akicheka kwa maneno ya Frank. "najua wewe umezaliwa na mwanadamu kama mimi Ila wewe ni mrembo Sana Sana sanaaa." akaongea Frank huku akizidi kumsifia Penina. Penina naye alifurahi Sana na kuzidi kuwa na furaha zaidi kwa sifa alizokuwa akipewa na Frank. "Asante Sana mpenzi wangu kwa sifa zote ulizonipa ila Kuna kitu nataka nikuambie." akaongea Penina na kumtizama Frank. "kitu gani tena mpenzi wangu?" akahoji Frank huku akiwa ametumbua macho. "mbona umeshtuka hivyo Sasa?" Penina akamuuliza Frank baada ya kumuona ametumbua macho. "lazima nishtuke si unajua tena namna navyokupenda isije ikawa ni kitu kibaya." Frank akamjibu Penina. "usijali mpenzi sio kitu kibaya na nina Imani utafurahia." Penina akamwambia Frank kumtoa hofu. "ok niambie bas ni kitu gani?" akahoji Frank huku akionekana kuwa na haraka ya kutaka kujua. "nataka siku chache zijazo tufunge ndoa alafu tufanye harusi kubwa ili tuwakomeshe maadui zetu ambao hawataki kutuona tukiwa pamoja.." Penina ndio alimwambia Frank ambaye alikuwa kimya kumsikiliza. "kweli mpenzi wangu hata mimi nimeshaliwaza hilo tatizo lipo kwangu, bila Shaka unatambua hali iliyopo Katika familia yetu, hatuna uwezo kipesa hivyo nahitaji muda zaidi kulitimiza hilo Penina." Frank akamwambia Penina huku akiwa amepoteza tabasamu usoni mwake. "Frank mpenzi wangu ondoa Shaka kuhusu hilo mimi nina uwezo wa kulisimamia hilo mwanzo mpaka mwisho, na kuthibitisha hilo hapa nimekuja na funguo nne, moja ni ya duka kubwa la kuuza bidhaa za jumla na moja, mwingine ni wa gari kubwa la kubebea mizigo, mwingine ni wa nyumba mpya niliyowanunulia wazazi wako kama zawadi ya kunizalia mwanaume anayenipenda kwa dhati na mwingine ni wa gari ndogo nililokununulia wewe mpenzi wangu. " alimaliza Penina kumwambia Frank maneno hayo na kumuacha akiwa mdomo wazi. " waooow ni ngumu Sana kuamini ila acha niamini tu, Asante Sana mpenzi wangu." alisema Frank huku akimkumbatia Penina na kumshushia mabusu mfululizo. "usijali mpenzi wangu ila nataka utambue nayafanya yote haya kwasababu nakupenda Sana, lakini pia ni moja wapo ya maandalizi ya harusi yetu." Penina akamwambia Frank huku akiwa amejilaza kifuani mwake. "nashukuru Sana Penina mpenzi wangu kusikia hivyo na mimi nikuahidi kuwa na wewe mpaka mwisho wa uhai wangu hakika ni wewe tu Penina." Frank akamwambia Penina huku akiwa amemkumbatia kwa nguvu. Wakati huo tayari Muda ulikuwa umeenda Sana na tayari ilikuwa ni saa moja usiku, hivyo Frank na Penina waliondoka kurudi nyumbani huku Penina akimuahidi Frank kumkambidhi vitu vyote alivyomwambia siku inayofuata. Penina alimfikisha Frank nyumbani kwake, Frank akashuka kwenye gari na kumuuga mpenzi wake Penina. Kisha Penina akageuza gari na kuondoka. Baada ya Penina kuondoka tu, Frank kabla hajapiga hata hatua moja kuondoka pale, ghafla alishtukia amezungukwa na vijana watatu wa kiume waliokuwa wamevalia miwani nyeusi kila mmoja. Na hata Frank alipowaangalia hakuweza kuwafahamu. ....... Itaendelea. ... Read More
Story......... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Sita (6) By GIVAN IVAN PHONE & whatsapp ____0769673145 Ilipoishia........ "Eeh Mungu Kwanini unaniacha niteseke hivi? Kama huu ndio mwisho wa maisha yangu bas naomba unichukue haraka usiniache nife Katika mateso makali kiasi hiki." akajisemea Frank kwa sauti ya chini akimuomba Mungu wake. Lakini hata hivyo baada ya masaa mawili mbele, aliweza kupita mzee mmoja aliyekuwa akichunga ngombe, karibu na sehemu Ile aliyotupwa Frank na pia akaweza kumuona Frank akiwa amelala pale chini akiwa hajiwezi kwa lolote. ***********Endelea ******* Mzee yule aliweza kumsogelea Frank na kumfungua kitambaa cheusi alichofungwa usoni. "kijana umepatwa na nini." akauliza mzee yule baada yule baada ya kumfungua Frank usoni. "kwa kwa kwani ha ha hapa ni wapi?" akauliza Frank kwa taabu badala ya kujibu swali aliloulizwa. "hapa ni tabora kwani umepatwa na nini?" akajibu mzee yule na kumuuliza tena Frank. Frank hakuamini kusikia eti yupo tabora, akamwambia mzee yule, "nimetekwa na Kuja kutupwa huku tafadhali naomba nisaidie nina njaa Sana." aliongea Frank kwa taabu kumuambia mzee yule. "ooh pole Sana kijana wangu, wewe kwenu wapi?" akauliza mzee yule huku akimfungua Frank kamba za miguuni pamoja na mikononi. "Tafadhali mzee wangu naomba nisaidie nipate hata maji ya kunywa nakufa mzee wangu." akaongea Frank kwa uchungu Sana. Mzee yule alimwonea huruma Frank kwa jinsi alivyokuwa anaongea na hali mbaya aliyokuwa nayo. Mzee yule alimbeba Frank na kumpeleka mpaka kijumba chake kilichotengenzwa kwa nyasi huku pembeni yake kukiwa na zizi kubwa la ngombe. Mzee yule baada ya kufika alimlaza Frank chini kwenye ngozi ya ngombe, Kisha akamletea maziwa na kuanza kumnywesha Frank. Frank aliweza kupata nguvu kidogo baada ya kunywa maziwa karibia Lita mbili. Baada ya hapo mzee yule alimletea Frank nyama iliyochomwa na kumkambidhi Frank. Frank alianza kula nyama Ile ambayo hakujua ni ya mnyama gani. Baada ya masaa kadhaa Frank aliweza kurudia kwenye hali yake ya kawaida, lakini sasa mawazo yakaanza kumtawala kwa kumkumbuka mpenzi wake Penina. Frank alianza kukumbuka jinsi alivyoongea na Penina kwenye simu na kukubaliana kukutana baada ya dakika kadhaa, lakini pia akakumbuka namna alivyotoka nje kumsubiri Penina lakini baada ya hapo hakukumbuka tena kilichotokea mpaka pale alipokuja kushtuka na kujikuta yupo kwenye gari na baadae kujikuta yupo pale msituni na kusaidiwa na mzee yule. Lakini Frank alikumbuka pia alikuwa na simu lakini alipoitafuta mfukoni hakuiona. Frank alihuzunika sana kwa hichi kilichomtokea, hakujua ni wakina nani wamemfanyia kitendo kile. Frank bado alikumbuka mengi Sana aliyokuwa ameongea na Penina, lakini Sasa alikuwa akiwaza kama ataweza kukutana tena na Penina. "kijana, kijana, kijana" Frank alishtushwa na sauti ya mzee yule ikimuita na hapo na hapo ndio akatoka kwenye mawazo Yale na kumuitikia mzee yule. "naam mzee wangu." akaitikia Frank na kumtizama mzee yule. "inaonekana una mawazo Sana nimekuita zaidi ya Mara tano bila mafanikio una matatizo gani kijana wangu." Akauliza mzee yule huku akionekana kumhurumia Sana Frank. "Mzee wangu nina matatizo makubwa Sana." akaongea Frank huku akitokwa na machozi. "mzee wangu yaani kuna watu wanataka kuniangamiza kwasababu tu ya mwanamke." akazidi kuongea Frank kwa uchungu. "hebu nyamaza bas unielezee vizuri na uniambie unaitwa Nani, jikaze wewe ni mwanaume." akaongea mzee yule huku akimpiga piga Frank mgongoni. "kwanza kabisa mimi naitwa Frank na sababu kubwa ya mimi kuwa hapa Sasa hivi ni kwasababu ya mapenzi." akaongea Frank na kumsimulia mzee yule simulizi fupi ya mapenzi yake na Penina huku pia akimuelezea jinsi ambavyo mzee Joel baba yake Penina hataki yeye Frank amuoe mtoto wake Penina. "pole Sana kijana wangu Frank, lakini nataka nikuambie tu kama kweli huyo mwanamke anakupenda kutoka moyoni, lazima atakusubiri mpaka pale utakaporejea." akaongea mzee yule kumpa moyo Frank. "mimi kweli yule mwanamke ananipenda Sana, lakini atajuaje niko hai mpaka Sasa?" akaongea Frank na kuhoji. "kijana acha kuwa na mawazo potofu kinachotakiwa kwa Sasa na ufanye kazi upate pesa ya kurudi dar es salam shilingi elfu sabini." akaongea mzee yule kumuambia Frank. "lakini hapa inaonekana ni msituni kabisa Nitapata wapi kazi Sasa.?" akahoji Frank kwa mshangao. "ndio hapa ni msituni hujakosea tena huku ni msituni ndani ndani kabisa na kutoka hapa kuelekea tabora mjini ambapo ndio kuna magari ya kuelekea dar es salam kwa miguu huwa tunatumia siku Tatu." akaongea mzee na kumuacha Frank akiwa ametumbua macho. "kwani hamna magari?" akahoji Frank. "huku msituni magari yatoke wapi kijana unataka kuchanganyikiwa.?" mzee yule akamuuliza Frank kwa mshangao. "mpaka hapa mzee wangu nishachanganyikiwa." akaongea Frank huku akiwa ameshika kichwa. "sikiliza kijana nikuambie, wewe ni mwanaume na siku zote mwanaume huwa hakati tamaa, pumzika hapa kwangu kwa siku mbili nikuandae uweze kuanza safari ya kuelekea tabora mjini kwa ajili ya kurudi kwenu wewe sio wa kuishi huku msituni. " akaongea mzee yule kumuambia Frank ambaye alikuwa kama haamini kilichomtokea. * *******Dar es salam ****** " yes Dickson habari yako? " " Habari yangu nzuri Sana hamjambo huko? " " hatujambo kabisa Dickson uko wapi? " " kwa Sasa niko Kenya kuna biashara nafanya halafu kesho nitakuja Tanzania. " " ooh Safi Sana Dick na pia karibu Sana nyumbani uje umuone mpenzi wako." "Ok Asante Sana nitakuja kumuona mpenzi wangu usijali." "Sawa bas nakutakia Kaz njema na safari njema." "Asante mzee Joel." Hayo yalikuwa mazungumzo ya mzee Joel pamoja na kijana mmoja kutoka nchi Norway aliyeitwa Dickson (Dick) ambaye ndio mzee Joel anatarajia aje amuoe mtoto wake Penina. "Kesho kuna mgeni maalumu atakuja hapa nyumbani nataka mumpokee kwa heshima na adhabu ya kutosha mmesikia?" akaongea mzee Joel akiwaambia watoto wake watatu, Nolan, Irene, Penina pamoja na mke wake ambao wote walikuwa sebuleni. "mgeni kutoka wapi na ni wa jinsia gani?" akahoji Nolan baada ya kuhisi kitu. "nimesema kuna mgeni anakuja na nataka mumpokee kwa heshima ya hali ya juu hayo maswali mengine sihitaji kuulizwa." akaongea mzee Joel kwa msisitizo. "ok Sawa." akajibu Nolan na kunyamaza.* Katika familia ya kina Frank furaha ilitoweka kabisa Katika nyumba yao kutokana na kutoweka kwa Frank na ikiwa imetimia wiki moja bila kujulikana alipo Frank.* Siku aliyokuwa anaisubiri mzee Joel ya kukutana na kijana mzungu anayeitwa Dick hatimaye iliwadia. "Penina mwanangu naomba nisikilize na unielewe mimi kama baba yako, Frank nimepata taarifa zake kuna sehemu ameonekana huko arusha akiwa na mwanamke mwingine Sasa ya nini kungangania mwanaume ambaye hajatulia?" akaongea mzee Joel na kumuuliza Penina ambaye alibaki kimya tu. "Mwanangu ngoja nikuletee mwanaume mzuri ambaye anaendana na wewe, mzuri kama wewe na mwenye elimu kama wewe achana na yule muokota makopo Frank." akaongea mzee Joel kumwambia Penina, lakini Penina bado alikuwa kimya tu akimtizama baba yake bila kumjibu kitu. Lakini mzee Joel hakujali ukimya wa Penina, yeye aliingia kwenye gari na kwenda kumpokea Dick Kuja kumuona Penina. Baada ya mzee Joel kuondoka. Machozi yalianza kutiririka usoni mwake baada ya kumkumbuka mpenzi wake Frank. Baada ya masaa mawili mbele mzee Joel alirejea nyumbani akiwa pamoja na mgeni wake. Geti lilifunguliwa na mlinzi na gari likaingia mpaka ndani na kupaki sehemu yake. "karibu Sana kuwa huru." akaongea mzee Joel huku akimfungulia Dick mlango wa gari. ........ Itaendelea ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: