Home → ushauri
→ Nawaandikieni nyie waume, maana Mungu amewapa hekima na busara ya kuwa kichwa na kutawala yale yaliyo chini yenu.
Unafahamu kwamba vitu unavyovifanya wakati mwanamke wako anapokua mjamzito vina-influence afya ya mama na mtoto aliye tumboni?
Brothers nisikilizeni hua nashangaa sana mnavyokua mnawasumbua wake zenu wakiwa wajawazito na kushindwa kuendana na mabadiliko wanayopitia.
Ni miezi tisa tu ile wala sio ndio milele watakua vile. Mimba hainunuliwi sokoni, wala sio software kwamba utaipakua kwenye internet. Ile ni mbegu iliyopandwa na wewe. Na lazima awepo mtu wa kuibeba ikue vema na kuweza kuzaa kile kilicho bora. Na wanawake wamepewa uwezo huo wa kuibeba hiyo mbegu
Mimba ni maandalizi ya kumkaribisha member mpya katika familia. Ujauzito ni adventure safari ..iliyojaa furaha, faraja, na kila aina ya disappointment. Wanawake wanatofautiana katika mabadiliko ya mwili na tabia wawapo wajawazito.
■ Kuna kipindi atakuwa ni mlalamikaji sana
■ Kuna kipindi atakuwa akikuomba vitu ambavyo ni vya ajabu mfano chai iliyowekwa nazi au supu ya miguu ya mbuzi.
■ Kuna kipindi atakuwa mvivu kukupikia chakula.
■ Kuna kipindi atatamani umkande miguu na kumbembeleza kama mtoto mdogo.
Tafadhali sana brother msikilize wala usimpotezee...kubeba mtoto sio kazi ndogo eti. Ninauhakika ungehamishiwa ubebe wewe hata kwa siku moja ungeona jinsi ilivyo tabu.
Tafadhali sana, vumilia hiyo hali..hata hivyo mbona ni wakati mzuri sana...hakuna kipindi kizuri kama mwanamke akiwa mjamzito..kadiri utakavyomtunza ndivyo atakavyozidi kuonekana bomba na wa kuvutia
ZINGATIA HAYA.
1. Siku zote observe miguu ya mkeo wakati akiwa mjamzito, mara nyingi miguu huvimba. Tafadhali chukua maji na kitambaa mkande miguu mara kwa mara, ni kitu ambacho wanawake hukipenda sana pindi wawapo wajawazito.
2. Muuluze mara kwa mara anajisikiaje na mtoto tumboni yukoje. Yeye ndie amembeba anafahamu movement za mtoto tumboni.
3. Mueleze ni kwa jinsi gani alivyo mzuri kipindi akiwa na ujauzito..mfano "Honeylove ukiwa na mimba unaonekana mzuri kweli ntakua nakupa mimba kila siku" au "Hivi ni mwanangu ndio anakufanya uonekane mzuri hivi"..kwa vitu vidogo kama hivi mkeo atajisikia faraja sana na atajivunia kukubebea mtoto wako tumboni mwake.
4. Usikasirike pale anapokuamsha usiku wa manane na kumsaidia anavojisikia vibaya. Unatakiwa nawe ujali maumivu yake. Hatakiwi kuugulia maumivu peke yake...ni mtoto wako pia mnatakiwa muumie pamoja.
5. Hakuna sheria inayozuia tendo la ndoa wakati wa ujauzito. Kiufupi ndio kipind ambacho sex ni good kama ukiifanya kwa utaratibu mzuri.
6. Usijisikie fedheha kutoka out na mkeo mjamzito..mpeleke maeneo mazuri ambayo ulikuwa unampeleka kipindi unamfukuzia..she will love you to death...
Muda mwingine nashangaa mambo wanayoyawaza wanaume pindi wake zao wakiwa wajawazito. Kubeba mtoto kwa kpindi cha miezi tisa sio kazi ndogo.
Wanaume wote tuwe karibu na wake zetu pindi wakiwa wajawazito...ni kipindi ambacho wanatuhitaji sanaa.
Heko kubwa kwa wanaume wote ambao wanasimama kidete kuhakikisha mwana member mpya wa familia aliyepo tumboni anahudumiwa vizuri kupitia aliyembeba. Mungu awabariki sana.
“A baby will make love stronger, days shorter, nights longer, bankroll smaller, home happier, clothes shabbier, the past forgotten and the future worth living for.”
Share
Nawaandikieni nyie waume, maana Mungu amewapa hekima na busara ya kuwa kichwa na kutawala yale yaliyo chini yenu. Unafahamu kwamba vitu unavyovifanya wakati mwanamke wako anapokua mjamzito vina-influence afya ya mama na mtoto aliye tumboni? Brothers nisikilizeni hua nashangaa sana mnavyokua mnawasumbua wake zenu wakiwa wajawazito na kushindwa kuendana na mabadiliko wanayopitia. Ni miezi tisa tu ile wala sio ndio milele watakua vile. Mimba hainunuliwi sokoni, wala sio software kwamba utaipakua kwenye internet. Ile ni mbegu iliyopandwa na wewe. Na lazima awepo mtu wa kuibeba ikue vema na kuweza kuzaa kile kilicho bora. Na wanawake wamepewa uwezo huo wa kuibeba hiyo mbegu Mimba ni maandalizi ya kumkaribisha member mpya katika familia. Ujauzito ni adventure safari ..iliyojaa furaha, faraja, na kila aina ya disappointment. Wanawake wanatofautiana katika mabadiliko ya mwili na tabia wawapo wajawazito. ■ Kuna kipindi atakuwa ni mlalamikaji sana ■ Kuna kipindi atakuwa akikuomba vitu ambavyo ni vya ajabu mfano chai iliyowekwa nazi au supu ya miguu ya mbuzi. ■ Kuna kipindi atakuwa mvivu kukupikia chakula. ■ Kuna kipindi atatamani umkande miguu na kumbembeleza kama mtoto mdogo. Tafadhali sana brother msikilize wala usimpotezee...kubeba mtoto sio kazi ndogo eti. Ninauhakika ungehamishiwa ubebe wewe hata kwa siku moja ungeona jinsi ilivyo tabu. Tafadhali sana, vumilia hiyo hali..hata hivyo mbona ni wakati mzuri sana...hakuna kipindi kizuri kama mwanamke akiwa mjamzito..kadiri utakavyomtunza ndivyo atakavyozidi kuonekana bomba na wa kuvutia ZINGATIA HAYA. 1. Siku zote observe miguu ya mkeo wakati akiwa mjamzito, mara nyingi miguu huvimba. Tafadhali chukua maji na kitambaa mkande miguu mara kwa mara, ni kitu ambacho wanawake hukipenda sana pindi wawapo wajawazito. 2. Muuluze mara kwa mara anajisikiaje na mtoto tumboni yukoje. Yeye ndie amembeba anafahamu movement za mtoto tumboni. 3. Mueleze ni kwa jinsi gani alivyo mzuri kipindi akiwa na ujauzito..mfano "Honeylove ukiwa na mimba unaonekana mzuri kweli ntakua nakupa mimba kila siku" au "Hivi ni mwanangu ndio anakufanya uonekane mzuri hivi"..kwa vitu vidogo kama hivi mkeo atajisikia faraja sana na atajivunia kukubebea mtoto wako tumboni mwake. 4. Usikasirike pale anapokuamsha usiku wa manane na kumsaidia anavojisikia vibaya. Unatakiwa nawe ujali maumivu yake. Hatakiwi kuugulia maumivu peke yake...ni mtoto wako pia mnatakiwa muumie pamoja. 5. Hakuna sheria inayozuia tendo la ndoa wakati wa ujauzito. Kiufupi ndio kipind ambacho sex ni good kama ukiifanya kwa utaratibu mzuri. 6. Usijisikie fedheha kutoka out na mkeo mjamzito..mpeleke maeneo mazuri ambayo ulikuwa unampeleka kipindi unamfukuzia..she will love you to death... Muda mwingine nashangaa mambo wanayoyawaza wanaume pindi wake zao wakiwa wajawazito. Kubeba mtoto kwa kpindi cha miezi tisa sio kazi ndogo. Wanaume wote tuwe karibu na wake zetu pindi wakiwa wajawazito...ni kipindi ambacho wanatuhitaji sanaa. Heko kubwa kwa wanaume wote ambao wanasimama kidete kuhakikisha mwana member mpya wa familia aliyepo tumboni anahudumiwa vizuri kupitia aliyembeba. Mungu awabariki sana. “A baby will make love stronger, days shorter, nights longer, bankroll smaller, home happier, clothes shabbier, the past forgotten and the future worth living for.” Share
Artikel Terkait
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
Mbinu za kufufua penzi lenu 1. Badilisha mavazi yako . Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako. Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo. Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile. 2. Hamia nyumba mpya Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako. Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja. 3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala. Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako. Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo. 4. Omba msamaha nawe umsamehe. Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa. Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu. Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa. 5. Endeni mjivinjari kwa tarehe Endeni likizo au tokeni nje pamoja. Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja. 6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana. Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana. Jiulize mbona watu huangalia picha hizi? Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?. Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe. Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua? Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu. Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi. Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake. 7. Jisalimishe upya Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu. Je unampenda kama awali? Je unanipenda kweli? Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu. Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao. 8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba. Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee . Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika. 9. Epuka kuumiza mwenzako Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako. Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda. 10. Mbusu mpenzi wako zaidi. Mabusu huleta watu pamoja. Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi. 11. Omba Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu. Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu. 12. Tenga wakati wa Faragha Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako. Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda . Ni muhimu sana. 13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani. Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe. Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako. 14. Weka teknolijia mbali Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo . Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ? Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe . Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ? Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia . 15. Chezeni pamoja Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba. Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani ! Chezeni miili yenu ikigusana! 16 Kaeni msemezane Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ? Unamwambia nini kitandani ? Unazungumzia kuhusu madeni yako? Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye . 17. Andikianeni barua za kimapenzi. Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako. 18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja. Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!! Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu. Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu 19.Nunua marashi mapya Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe. 20.Jiachilie Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba Mchezee shere Mtanie mpenzi wako ... Read More
Je Wajua Kwanini Wanawake Hula Vyakula vya Ajabu Ajabu Wakiwa Wajawazito?  Tabia hii inayojulikana kwa Kiingereza kama “Pica” inatokana na mtu kutamani kula vitu vyenye virutubisho kidogo sana au visivyo na virutubisho vya aina yoyote kwa mwili. Tamaa hizi huwa zinawapata watoto au mama mjamzito kutafuna vitu ambavyo kimsingi si chakula – kama udongo au chaki. Jina hili la pica ni aina ya ndege ambaye anajulikana kwakuwa anakula kitu chochote, hana anachochagua. Ni kweli kwamba wajawazito wengi hupata hamu ya kula vitu ambavyo si vyakula walivyozoea kula mara kwa mara wakiwa si wajawazito; wengi wao ni rahisi kuwaelewa kwa sababu hukimbilia mchele, barafu na vinginevyo ambavyo si vitu vibaya kula. Kwa watoto, hii ni tabia iliyozoelekakwakuwa inawatokea watoto wengi ambao ni kati ya asilimia 25 na 30% ya watoto wote; lakini kwa wanawake wajawazito, inatakiwa iwe kwa kiwango cha chini zaidi. Nini kinasababisha tabia hii kwa wajawazito? Sababu ya baadhi ya wanawake kuwa na tabia hii wakati wa ujauzito haijulikani hasa. Kwa sasa hakuna sababu maalumu, lakini kwa mujibu wa Jarida la Chama cha Watu Wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari nchini Marekani, tabia hii yawezekana ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Baadhi wanadai kwamba hali hii inaashiria kwamba mwili unajaribu kupata vitamini na madini mengine yanayokosekana kwenye chakula cha kawaida ambacho mtu anakula. Muda wingine tabia hii yawezaikatokana na kuumwa viungo au akili kwa muda mrefu. Baadhi ya vitu vya ajabu ambavyo wajawazito hupenda kula Vitu vinavyopendwa zaidi na wajawazito wengi ni udongo, uchafu. Vitu vingine ni njiti za kiberiti zilizochomwa, mawe, mkaa, barafu, dawa ya meno, sabuni na mchanga. Mjamzito anapokula vitu hivi hujisikii raha kana kwamba amekula chakula chenye faida kubwa kwake na kwa mtoto aliye tumboni. Kuna hatari yoyote kwa mtoto aliye tumboni? Kula vitu ambavyo si vyakula kimsingi ni jambo linaloweza kusababisha madhara kwa mjamzito mwenyewe na mtoto aliye tumboni. Kula vitu hivi kunaweza kuharibu mfumo wa kawaida wa kunyonya virutubisho kutoka kwenye vyakula na kusababisha mwili wako upungukiwe na madini muhimu unayoyahitaji kwa afya yako na ya ukuaji wa mtoto vilevile. Tabia hii ni hatarishi sana kwakuwa vitu ambavyo si vyakula vinaweza kuwa na viambata ambavyo ni sumu au vyenye vijidudu vinavyoathiri mwili. Kudhibiti tabia hii Usihamaki unapojikuta unatamani vitu vya ajabu ajabu wakati wa ujauzito: inatokea sana na si jambo la kushangaza kwako pia. Jambo la muhimu ni kumjulisha muuguzi wako au wahudumu wa kliniki unayohudhuria kujua maendeleo yako ya mtoto tumboni ili akuelimishe na ahakikishe kwamba una uelewa kuhusu hatari zinazoambatana na tabia hiyo. Baadhi ya mbinu za kutumia kushinda tamaa hizo Mtaarifu mhudumu wako wa afya kwenye kliniki unayohudhuria na muangalie kumbukumbu za ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na hali yako ya kiafyaFatilia kiwango chako cha madini ya chuma mwilini pamoja na kiwango cha vitamini na madini mengine unayotakiwa kulaOmba ushauri kuhusu kitu gani uwe unakula ili kubadili ili kuepuka vitu vya ajabu (waweza kumung’unya/ kutafuna vitu kama pipi au ‘big g’ isiyo na sukariMwambie hata rafiki yako mmoja kuhusu hamu hizi na umtake awe anakukataza unapokula vitu vya ajabu ... Read More
UNAJUA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO????  Kama inavyoeleweka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la "Tantric Sex." Kama inavyoelewaka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la “Tantric Sex.” As if hii duinia, especially hii century haiko overloaded na information kuhusu mambo ya mapenzi, jinsi ya kufanya mapenzi and whats hot in the bedroom, whats in and whats not. So, lately nimeona a lot of tzmoms readers wamekuwa wakitembelea sana na kusoma page ya “mapenzi baada ya ujauzito” na “kufanyamapenzi wakati wa ujauzito.” And I thought well, writing about Tantric Sex will be nyongeza kwa kila mmoja, aliye mama na mbaye bado damu inachemka katika mambo ya mapenzi. Anyhu, kama “SEX/MAPENZI” yangekuwa yanaweza kuyu-nite the world/countries/makabila/people I think hii fani ingeshinda. Well, so kama umeshawahi kujifungua ama kama wewe ni mama, you definitely understand ni jinsi gani ni vigumu kuwa upbeat kuhusu mapenzi ama kumfurahisha mumeo/mpenzio everyday. Well, once in a while maybe but not everyday. Ila kama we ni mdada/binti ambaye hujazaa bado well, damu yako bado inachemka so energy bado ipo nyingi ya kukurupushana na mpenzio. Having said that, si maanishi mtu ukishazaa ndo fani ya kuenjoy mapenzi imekwisha but nguvu zinapungua for sure however, kuna vitu vingi tuu ambavyo vinaweza kusaidia kuleta nguvu ya kutaka kukurupushana chumbani lol. Kukosa nguvu/energy to wanna work it all the time its not because mwanamke ni mvivu but hutokana na kuwa na mambo mengi sana ya kutend nyumbani i.e. kuhakikisha watoto wako taken care of, labda kazini pia unahitajika, etc una kuta hupati muda wa kujifurahisha mwenyewe ama na mpenzi wako. Therefore, mara nyingi before you know mupenzi anaanza kulalamika or hata mwanamke mwenyewe unaweza kufeel like you are not doing enough so mambo ndo hivyo yanaanza kwenda south chumbani. Hivyo basi, lets dig in tuone Tantric Sex inatoa msaada wa aina gani ili kurevamp mapenzi. Kwanza kabisa, FYI tantric sex can be weird at the beginning ila nitajitahidi kutoingia so indepth ili kusave miyoyo ya watu wengine. Kwamaana hii ni soft porn “according to me.” Lol. so usishtuke ama kushangaa sana. Well, anythign “sex” can be unconfortable anyways. Okay, so, kwanza kabisa, with Tantric Sex, mtu na mpenziwe wanatakiwa kuwa; SPIRITUALLY CONNECTED (usishtuke sio kidini lol).. Hii inamaainisha kwamba wewe na patner wako kwa pamoja mnajua mnataka nini emotionally and physically. Kwa kufanya hivi inasaidia kuwafanya kwa pamoja kuwa “FREE” na kuondoa wasiwasi wa labda mwenzangu atanijudge kwamba labda mimi ni malaya ama fuska etc. In other words hii process inaitwa “Dropping the Veil, between “Self” and “Other/patner.” THE ENVIRONMENT/mazingira. Wakati mnapractice tantric sex of course, just like when you are in the bedroom unaweza ukavaa lingerie/kuo za ndani zinazovutia or “kuwa kama mlivyotoka tumboni mwa mama zenu” (you know what i mean). Tatu, wapenzi wanaanza kupapasana lol, but in a way kwamba you are feeling the energy of the other person. Na hii energy unaweza kuifeel kwasababu mko free hamna anayemjudge mwingine/there are no worries. You are just in your own created world. Nne, wakati wa kufeel energy ya mwingine lazima wapenzi wawe wana pumua heavely yaani just feeling every move made but the other person mpaka mnapofikia mahali were you are breathing so hard and you are feeling each other. then you start kissing the lips, and then deeper for minutes even hours. Then mengineyo yanaweza kuendelea. So, all this time kumbuka its not about going straight into sex with your partner rather its about getting high by touching and feeling connected with each other. hivyo basi, once in a while take that time and revamp your intimacy, dress good, feel sexy and heey have fun!!. By 🅱 ... Read More
Kwanii Wanaume Waaminifu Kwenye Uhusiano Huachwa.....  Kuachwa na mpenzi kwa sababu umekuwa ni muaminifu sana yaonekane ni jambo lisiloingia akilini lakini linatokea. Moja ya mambo ya ajabu unayoweza kuwa ushawahi kuyasikia ni kwamba mara nyingine uamuzi wako wa kuwa mwanaume mwema sana na unayejitahidi kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uwe mzuri muda wote unaweza kukugharimu na kujikuta unaachwa kabisa. Haitakiwi kuwa hivyo lakini mara nyingine inatokea, na inatokea kwa sababu wazo la mwenza wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi laweza likawa tofauti na ulionao wewe. Wengine wana mawazo hasi kuhusu jinsi uhusiano/ndoa inavyotakiwa kuwa. Hii ndio sababu hutakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye na vipaumbele sawa na vya kwako au asiye na mtazamo mmoja wa kimaisha kama ulionao wewe. Usipozingatia hilo, utajikuta unaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hatakujali vya kutosha kwakuwa labda humfokei au kumpiga anapokukosea – au utajikuta ameshakupanda kichwani na kuanza kukudai mambo ambayo huwezi kuyatimiza lakini ukajikuta unajitutumua kumtimizia kwa sababu unataka kumfurahisha mpenzi wako na analijua jambo hilo. Kwa sababu baadhi ya wanaume wanapenda kulinda siri na kuwaachia uhuru wapenzi wao, wanajikuta wakiwapa ruhusa wanawake zao kwenda popote wanapojisikia bila kuwafatilia wanachofanya. Nini kinafata baada ya hapo? Mwanamke anatoka, anatafuta mchepuko na kukusaliti. Mwisho inakufanya wewe mwanaume uonekane mjinga mbele ya wengine. Tatizo ni kwamba tabia hii inaibuka kutokana na mazoea ya watu kuingia kwenye uhusiano wakiwa wameficha tabia zao halisi na kuja kufungua makucha yao baada ya kuona ameshaishi na wewe kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi tena kumuacha. Hii inasababisha wanaume walioathirika kutokana na tabia kama hizi kutoka kwa waliokuwa wapenzi wao wasiweze kuwaamini wanawake wengine tena kwa kuona kwamba wote ni sawa na wale waliowaumiza na kusababisha wasiweze kuwaonesha wenza wao wapya mapenzi kwa kiwango cha juu wakihofia kuumizwa tena. Kuwa mpole, mkarimu na mwenye upendo wa hali ya juu kwa mpenzi wako ndio jambo linalotarajiwa kwenye uhusiano. Mtu hatakiwi kufanywa ajisikie vibaya kwa kumuonesha mapenzi ya kweli mwenza wake. Kama wewe unakuwa muaminifu na mwema kwa mpenzi wako lakini umekuwa unadharauliwa au ukaachwa kutokana na tabia hiyo, kaa ukiwa na amani kabisa kwamba lawama za kuvunjika kwa uhusiano huo hazikuhusu wewe – lawama ni za mpenzi wako aliyeshindwa kujua wewe umekuwa mwema kiasi gani kwake. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: