Home → ushauri
→ NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI?
Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili).
Jinsi yakutumia samahani kiusahihi
Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali.
Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya.
Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa.
Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena.
Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha.
Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi
Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa)
Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa
Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe)
Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo
Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea.
Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja.
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja.
Artikel Terkait
KWA WANAWAKE TU! NJIA 14 ZA KUJIWEKA ILI WANAUME WATAMANI KUKUTONGOZA  Je umekuwa ukijiuliza kwa nini haukuwi approached na wanawaume kama unavyotaka? Mtandao wa Sayari ya Mapenzi umeamua kukuandalia mbinu na maujanja ya kutumia ili uonekane mwanamke ambaye anaweza kufukuziwa na mwanaume kwa urahisi. Owk.... Kando na itikadi ambazo umekuwa ukifikiria, kuapproachiwa ama kufukuziwa na mwanaume si gemu ya bahati nasimu ambayo mtu anaingojea ijitokezee. Na pia kando na itikadi nyingi za wanawake wanazozifikia, si lazima ufanye kitendo kikubwa ama cha inadi ili mwanaume aweze kukutongoza. Ukweli ni kuwa, kama unaielewa akili ya mwanaume na jinsi inavyofanya kazi kabla ya kuapproach mwanamke, unaweza kumfanya mwanaume yeyote kutaka kuongea na wewe dakika tano atakapokuja katika himaya yako. So mbinu zenyewe ndizo zipi? Zama nami... Njia za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukutongoza Kwanza jiweke nadhifu Hii ni muhimu katika yote kama wataka mwanaume akutambue. Mwanaume kitu cha kwanza anachokiangalia huwa ni mwonekano wa mwanamke. Mwanaume anapoingia katika chumba, inamchukua sekunde ndogo zana kuamua iwapo anataka kuapproach mwanamke mfani au la. Kama umevalia vizuri na unapendeza, itarahisisha kazi yako sana. Pili usionekane kama una shughli Usijishughlishe sana na simu yako, ama kitabu chako, ama kitu kingine. Unaweza kuwa umeboeka na unajaribu kujiweka buzy, lakini fursa iweza kuwa hivi, kufanya hivyo kunaweza kumfanya mwanaume anayetaka kukuapproach kuona ya kuwa uko buzy sana kiasi cha kuwa atashindwa kukufuata kwanu unaweza usiwe interested na maongezi yake. Tatu ni kuwa mko ligi moja? Hii inakinzana na hatua ya kwanza, lakini inaweza kuwa na tatizo iwapo unaoneka kama uko ligi tofauti na mwanaume. Kama utaoneka amakujiweka mtu wa hadhi ya juu wanawake watapenda kukuangalia lakini hawatakuaproach. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hawapendi kudhalilishwa wakati wanapoamua kukuapproach....kiufupi ni kuwa ukiwa unavutia kupindukia wanaume watakuogopa. Lakini tena, kuna wale wanaume ambao wanajiamini kupindukia ambao wanajua thamani ya kukuapproach, nao ni wanaume alfa, wanaume diriki, na pia wale wanaume mapleya. Kama wataka kuteka atenshen ya mwanaume mzuri wa kawaida lakini anayeogopa kukuapproach, jaribu kutumia mbinu ya kuwa jamili na watu wanaokuzunguka. Huwa inasaidia. Ujanja wa kumfanya mwanaume aweze kukuakuaproach 1. Jinsi utakavyovalia Usivalie kana kwamba huna kitu cha kuficha. Utapata atenshen ya kila mtu lakini wanaume ambao wataamua kukuapproach ni wale ambao wanataka kulala nawe kwa usiku mmoja pekee. Enyewe kuvalia kwa kutamanisha kunasaidia kuteka atenshen ya mwanaume, lakini usivuke mipaka ya kawaida. Kumbuka kuwa si lazima uonyeshe viungo vyako vyote vya mwili ili uweze kuteka macho ya mwanaume. Kama unavutia inatosha kumfanya mwanaume akugundue. 2. Unavyomuangalia Mchungulie mara moja na nyingine, halafu mwangalie mara kwa mara. Hakikisha ya kuwa haujisahau ukamwangalia sana kupindukia ama atakuona kama wewe ni rahisi wa kuapproach na anaweza kukupuuza. 3. Mitindo ya kumwangalia Kuna mitindo miwili mikuu ya kumwangalia mwanaume ili kumuonyesha ya kuwa umevutiwa naye. Unaweza kutumia mbinu zote mbili kulingana na vile unataka. i) Kumwangalia polepole - wakati ambapo unaangalia pande zote, angalia upande wake na uyaangalie macho yake kwa sekunde kadhaa huku ukiweka tabasamu. Halafu pole pole zungusha kichwa chako uangalie kwingine. Mbinu hii ni ya kijasiri ya kumwonyesha mwanaume umevutiwa kwake. ii) Kumwangalia kwa uharaka - hii ni mbinu ya kumwangalia kwa uharaka. Anza kumuangalia, ukiona kama anataka kukuangalia, ghafla angalia kando halafu utoe tabasamu ukiangalia chini. Mbinu hii inampa confidence na kukuona wewe ukipendeza. 4.Mfanyie kazi iwe rahisi Inakuwa vigumu kwa mwanaume kumuapproach mwanamke sehemu ambapo yuko kundini na marafiki zake. Kama mawazo yako ni kufuatwa na mwanaume, hakikisha ya kuwa wakati mwingine unajipa time ukiwa pekeako ama zaidi uwe na rafiki yako wa kike mmoja. 5. Sehemu zifaazo Si kila sehemu ni nzuri kufanya maongezi na mtu. Kama unataka mwanaume akuapproach, chagua sehemu ambayo si kila mtu ataanza kujeuza kichwa chake kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yenu. Sehemu za mkawahawa, supermarket, ama bookshop ni sehemu nzuri zaidi za kukutana na mwanaume kupiga stori. 6. Mpatie nafasi aongee na wewe Hata kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe, unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume huyu kuzungumza na wewe. 7. Tabasamu Onekana jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka macho ya mwanaume yamwone. 8. Usiboe Kuwa mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua. Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo na mwanga. 9. Usiwe mjeuri Kama wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa. 10. Usitangamane na wanaume Hii ni muhimu kwa mwanamke yeyote aelewe. Usiwahi kamwe kutangamana na marafiki zako wa kiume kama unataka kukuwa approached na mwanaume. Haitafanya kazi kamwe. 11. Mwoneshe kuwa uko intrested Mwonyeshe kuwa uko interested kwake kwa kutaka kumjulia hali zaidi. Hata kama uko na marafiki zako mnaongea halafu amekaa karibu na wewe, mwangalie iwapo anakuangalia hata kama unawajibu rafiki zako. 12. Onyesha uanawake wako Mwangalie mara kwa mara, halafu ukishika macho yake, peta nywele zako nyuma ya sikio lako. Inaweza kuonekana kama jambo dogo kwako, lakini kwa mwanaume ni kama kugonga ndipo. 13. Mtege Pita mbele yake halafu mwangalie machoni mwake wakati unapompita. Mtese kihisia, ataipenda kuona atenshen yake. 14. Usilazimishe Utakuwa unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia mara moja na nyingine ama kuwatabamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa. Ok hizi ni mbinu ambazo unafaa kuzitumia kama unataka mwanaume yeyote yule akunotice ama akufukuzie. ... Read More
Majina Ya Watoto Wa Kiume (26)  Katika tamaduni nyingi, majina ya watoto wa kiume hutokana na majira au matukio ya wakati wanapozaliwa. Kwa mfano, wakati mmoja, mwanamke Mwethiopia alijifungua mtoto wa kiume. Shangwe yake ikageuka kuwa majonzi alipoona mtoto wake akiwa amelala bila kusonga. Nyanya yake alipomchukua mtoto huyo ili amwoshe, kwa ghafla mtoto akaanza kusonga, kupumua na hata kulia. Hali hii ikawa chanzo cha jina la mtoto na hiyo wazazi wake wakaunganisha jina muujiza na neno linguine la Kiamhara na kumwita mvulana huyo Muujiza Umefanyika. Nchini Burundi, majina memgin yalitokana na wakati wa vita vilivyokuwemo mwanzo wa miaka ya tisini. Mtoto aliyezaliwa huku mzazi akijifichakutokana na machambulizi angepatiwa jina kama Manirakiza amabalo maana yake ni’Mungu Ndiye Anayeokoa’. Majina mengine ya wakati ule ni kama Twagirimana na Mwana wa Imana ambayo pia humaanisha mwana wa Mungu au mtu aliyeponea vita kwa muujiza wa Mungu. Desturi hii ya majina ya watoto wa kiume imeenea kote ulimwenguni ambapo kuna majina mengi yaliyo na maana ya nyakati kam wakati wa vita, njaa, shjrehe, makumbusho au tukio amabalo watu hupenda kukumbuka kwa kuwapa watoto majina. Kuna majina kadhaa amabyo ni mashuhuri sana ulimwenguni ;Noah, Liam, Mason, Jacob, William, Ethan, Michael, Alexander, James, Daniel na mengine. MAANA MAJINA TUKIZINGATIA HERUFI YA JINA LA KWANZA (KIUME) HERUFI A Watoto wenye jina linaloanza kwa herufi hii hupenda mambo makubwa,hujiamini sana na huwa na uwezo wa kutimiza malengo yao. Ni watoto wenye tahadhari,wachangamfu na hupenda matukio. Kwa kawaida hupenda kuheshimiwa,hupenda mamlaka,na ana kiburi,watoto wapenda hasira.Kidesturi herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI B Mwenye jina linaloanziana na herufi hii ni watoto wakarimu,waaminifu na hupenda kazi sana. Ni wajasiri, shujaa na wakatili katika vita au popote pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.Herufi hii huwakilisha nyota yangombe. HERUFI C Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni motto wa kubadilikana,ni washindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda.Ni watu wabunifu na wanapenda mawasiliano,herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI D Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni anayependa usawa,biashara ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi.Ni wajeuri na wenye msimamo. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI E Mwenye jina linaloanza na herufi ni mtu mwenye roho nzuri,mwenye mapenzi na huruma,mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Ubaya wake ni mtu asiyetegemewa na ni kigeugeu.Herufi hii huwakilishwa na nyota ya samba. HERUFI F Mwenye jina linaloanza na herufi hii n mtu mwenye mapenzi,huruma,roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu,ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI G Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni mtu mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho,ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni mtu mwenye hisia kali,msomi,mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri kutoka kwa watu.Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI H Mwemye jina linaloanzia na herufi hii ni mtoto mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,hupata faida kubwa katika anayopenda kutokana na bidii, ni mwenye mawazo mengi,mchoyo na mbinafsi.Herufi hii huwakilisha nge. HERUFI I Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda sharia,ana huruma na utu mzuri.Wakati mwingi ni mtoto mwenye kujiamini sana na mwenye hasira za haraka. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI J Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye matamanio,mkweli,mkarimu na mwerevu.Huwa asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa,wakati mwingine anakuwa ni mtoto mvivu na anayekosa mwelekeo. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI K Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto mjeuri,mwenye msimamo thabiti,mpenda umashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu, ana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana,ni mtoto asiyeridhika. Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI L Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto wa vitendo,mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha,hupatwa na misiba mara kwa mara.Herufi hii huwakilisha nyota ya samaki. HERUFI M Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kujiamini sana,mchapakazi na hupata mafanikio,ni mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI N Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mbunifu, mwenye hisia kali,hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ngombe. HERUFI O Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye subira,mvumilivu,na mwenye bidii ya kusoma.Ni mtoto mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.Herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI P Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye uwezo wa kuamuru na ana hekima kubwa.Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI Q Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtotto mwenye kupenda mambo ya asili,ni watu wasioelezeka,wako na uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya samba. HERUFI R Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mtulivu,mwenye huruma lakini mwenye hasira za haraka.Muda mwingi yeye ni mpenda amani. Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI S Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mvuto kali wa kuleta utajiri,ni mtoto mwenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI T Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda ushauri wa kiroho,anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu, ni watoto wenye hisia kali na wepesi sana kushawishika.Herufi hii huwakilisha nyota ya nge. HERUFI U Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye bahati kwa ujumla,anapenda uhuru katika mapenzi,ni mbinafsi,mwenye tama na anayekosa maamuzi. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI V Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mchapakazi,mwenye bidii asiye choka lakini ni watu wasiotabirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI W Mwemye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mawazo sana,mchangamfu sana,mwenye uwezo wa kutambua watu wabaya na wema, ni wenye tama na hufanya mambo hatari sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI X Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto asiyependa kuwekewa vizuizi hasa katika anasa na ni rahisi kwake kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Y Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mpenda uhuru na hapendi kupingwa katika jambo lolote,ni watoto wanaokosa uamuzi na husababisha kupoteza bahati katika maisha. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Z Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda matumaini na amani,ni wenye msimamo mkali japo ni wenye kukubali ushauri . Herufi hii huwakiisha nyota ya ngombe. ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: