Home → ushauri
→ Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika
Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha.
Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya.
Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana.
Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika.
MPUNGUZE MHEMKO
Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano.
Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi.
MSOME SAIKOLOJIA YAKE
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira.
Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira.
MRUHUSU AKUJIBU
Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake.
EPUKA MARUMBANO
Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena.
“Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano.
MUOMBE MSAMAHA
Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.”
Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako.
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako.
Artikel Terkait
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
MUNGU ATANILIPIA: Nakumbuka nililazimishwa kuolewa ila nilikubali ili kutii amri ya wazazi. Nikabahatika kupata mtoto wa kike niliyempenda sana, kwani sikuwa na raha ya kuishi na mume wangu aliyekuwa mzee sana kwa bahati mbaya mume wangu alikufa kwa ugonjwa wa kisukari. Nikabaki mimi na binti yangu kwakweli sikutaka kuolewa tena niliamua kukaa na kulea mwanangu huyu. Kweli nilimlea na kumsomesha binti yangu, alipofika chuo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Binti yangu akanitaarifu kuwa amepata mchumba na akaja nae nyumbani kumtambulisha kwa ushamba wangu nikashangaa kweli ile gari ya mchumba wa mwanangu na nikaona raha kwa binti yangu kumpata mwanaume mwenye pesa kama yule, ilikuwa ni kipindi cha likizo na yule bwana alikuwa akija mara kwa mara kutusalimia huku akibeba zawadi tofauti tofauti, sikuwa na shaka naye hata akiniambia anataka kutoka na mwanangu nilimpa ruhusu wanaenda halafu anamrudisha nyumbani. Siku moja ambayo siwezi kuisahau kamwe katika maisha yangu, mwanangu akaniaga kuwa anataka kutoka na mchumba ake ila atarudi kesho yake nikamkatalia na kumwambia asifanye hivyo kwani ataonekana hana thamani tena. Badae kidogo alifika mpenzi wake huyo na kuniomba, mwanzoni nilimkatalia ila baada ya kunisihi sana nikakubali kuwa waende basi mwanangu na yule mpenzi wake wakaondoka pale nyumbani nikitegemea mwanangu kurudi kesho yake. Kesho ikafika hadi jioni mwanangu hakurudi, hofu ikaanza kunitawala moyoni mwangu hadi kunakucha mwanangu hakuwa nyumbani pa kuanzia sijui kwani yule kijana ni mgeni kwetu. Siku hiyo nikiwa kwa mbali namwona mwanangu akijikongoja kwa kujivuta, nilimkimbilia mpaka pale alipo nikambeba hadi nyumbani, naye akaniambia maneno haya "mama nakupenda sana ila naomba nikwambie ujumbe huu uwafikishie mabinti wote. Mama, yule kijana nilikutana naye wakati naenda chuo akanipa lifti na kuchukua namba yangu. Mawasiliano yetu yalianzia hapo ila sijui anapoishi wala ndugu zake, aliniomba nije nae nyumbani kumtambulisha kipindi hiki cha likizo na ndio nikafanya hivyo, nilizoea kuzunguka nae hotel, bar, cinema na majumba yote ya starehe. Ila alichonitenda hivi karibuni ni cha kustaajabisha, nilipoondoka naye hapa alinifunga kitambaa machoni na kusema anaenda kunifanyia suprise nilishangaa tukielekea mahali pasipojulikana huko nilienda kupata mateso makubwa mengine hata hayasimuliki ila kuna hili la kunifunga mimi kamba kwenye miti, mikono na miguu ikiwa imetanuliwa halafu wakanifanyisha mapenzi na mbwa watatu, ikiwa hiyo haitoshi lililetwa joka kubwa ambalo liliingizwa sehemu zangu za siri, sijui lilienda kufanya vitu gani ila nilipata maumivu ambayo hayaelezeki nililia hadi kuzimia, nilipozinduka nikajikuta nipo nje ya nyumba yetu nimetupwa ila kabla ya yote waliniambia kuwa sitakiwi kusema chochote kile kwa mtu yoyote kwani nitakufa." Alipomaliza kusema hayo nilikuwa natetemekd mwili mzima kwani nilimuona mwanangu akinyooka na kufa mikononi mwangu. Hata nikieleza maumivu yangu hakuna atakayenielewa, ila niliumia kupita maelezo. Yote namwachia Mungu. Tangu kifo cha mwanangu nimekuwa kama mtu nisiyejielewa, natoa wosia kwa mabinti wengine tafadhari sana angalieni kwa makini wachumba mlionao isije ikawa kama yaliyomkuta binti yangu, wazazi wote kuweni makini. Naumia kumpoteza binti yangu mpenzi tena aliyekufa kwa maumivu makubwa. Ila najua Mungu atatenda jambo. Hadi leo sielewi kwanini mwanangu alitendwa hivi. Kama ujumbe huu umekugusa, dondosha LIKE yako hapo au SHARE ukiweza ili na wengine wapate kitu. ... Read More
MAMBO 10 AMBAYO NI SUMU KATIKA MAPENZI  KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi. Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi. 1. WIVU WA KUPINDUKIA Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi. Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu. 2. KUTOMWACHIA NAFASI MPENZI Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi. Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha. 3. KUMWAMULIA MPENZI MAMBO YAKE Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia. Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako. 4. KUMUULIZA MPENZI MASWALI Iwapo utajikuta ukimuuliza mpenzi wako maswali mengi yanayoonesha wasiwasi wako kuhusiana na mwenendo wake, fahamu kuwa kuna tatizo na tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi utakuwa mwanzo wa mwisho wa uhusiano wenu. Mwanamke angependa umuulize maswali ya kawaida kuhusiana na jinsi siku yake ilivyokuwa na kama marafiki zake hawajambo au la, lakini kila jambo lina mpaka wake. Mwanamke hatarajii kuwa kila mnapokutana atakuwa kama ameingia kwenye chumba cha mtihani au usaili wa kazi. 5. KUTOAMINI ANACHOKWELEZA MPENZI Wakati mwingine watu hushindwa kuwaamini wenzao, lakini kwa sababu ambazo ni za msingi, lakini kuna wakati ambapo mtu hushindwa kumwamini mwenzake bila sababu yoyote ya msingi, au kwa sababu zisizo sahihi, kisingizio kikiwa ni mapenzi. Kuna tatizo la kisaikolojia la kujishuku au kuwashuku wenzako. Hili ni jambo ambalo linaweza kukuharibia mustakabali wako katika mapenzi, maana husababisha kujengeka kwa mazingira ya kutokuaminiana. Ili uweze kwenda sanjari na mpenzi wako, amini kila anachokweleza hadi pale utakapokuwa na sababu za msingi za kutokumwamini. Na hata unapokuwa umelithibitisha jambo, endelea kuwa katika uhalisia wako. 6. KUACHA HOBI, MARAFIKI Mahusiano ya kimapenzi mara nyingi huhusisha kila mmoja kuacha baadhi ya mambo yake kwa ajili ya mwenzake. Hata hivyo, lengo ni kuweka tu uwiano wa mahitaji, si kuacha kila kitu ulichokuwa nacho kwa ajili ya mwenzako, ama kwa shinikizo, au kwa kulewa penzi. Iwapo utabaini kuwa marafiki zako sasa wamekuwa ni marafiki zako wa zamani na hobi zako zimebaki tu katika kumbukumbu japo kwa hakika bado unahisi mapenzi katika hobi hizo, basi tambua kuwa huyo mrembo wako amekunywesha sumu ya penzi na sasa huwezi hata kuitumia vema mantiki yako. Mbaya zaidi, iwapo utabaini kuwa marafiki zako wapya ni marafiki wa siku zote wa mpenzi wako na hobi zako ni zile za mpenzi wako, basi tambua kuwa huna tena nafsi yako, bali umejisalimisha mzima mzima kwa mpenzi wako. Lakini msemo mmoja wa hekima unatwambia usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Yamkini unaelewa. 7. KUKUBALI KUPELEKESHWA Pengine unakumbuka kuwa kuna nyakati ambapo ulikuwa na uwezo wa kujikita katika jambo moja na kulifanya kwa umakini, huku ukiwa pia mwerevu, mjanja na unayejisimamia, lakini leo unayeyuka kirahisi tu kama barafu iliyowekwa juani! Hii ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako. Mbaya zaidi ni pale utakapoiacha kazi yako inayokulipa vizuri na kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako. Ukifika hali hii ujue wewe mwenyewe kuwa hapo hakuna mwanamume. 8. UTAYARI WA KUFA KWA AJILI YAKE Umewahi kujisikia kuwa na utayari wa kufa kwa ajili ya mpenzi wako? Kama jibu ni “ndiyo”, basi fahamu kwa hakika kuwa hayo uliyo nayo si mapenzi bali ni upumbavu. Pengine huku ndiko kunywesha sumu ya mapenzi. Kwa hakika, hakuna mwanamke ambaye anastahili kumfanya mwanamume yeyote kufa kwa ajili yake. Yamkini wanaume wanaolengwa katika makala haya si wavulana wanaosoma sekondari, waliobalehe majuzi, ambao wakipenda au kupendwa hujiona kama wako katika sayari yao. Mwanamume aliyepevuka hujiamini na hayaweki maisha yake yote mikononi mwa mwanamke, hata kama mwanamke huyo angekuwa ndiye mrembo wa dunia. Iwapo, ama kwa ujinga au kwa kufahamu umewahi kumwambia mpenzi wako: “Ukiniacha nitajiua,” na ukawa unaamini hivyo kabisa, basi yamkini unahitaji kutafuta msaada wa ushauri nasaha, maana kwa hakika umepotoka. 9. MUDA WOTE UNAWASILIANA NAYE Vijana wa siku hizi ni watumiaji wazuri sana wa simu, lakini iwapo utabaini kuwa asilimia kubwa ya muda wako unautumia ama kwa kuongea au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi na mpenzi wako, basi fahamu kuwa kuna tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka. Kumbuka kuwa mapenzi hayachukui nafasi ya kila kitu. Yamkini huyo mpenzi wako amekukuta unaishi na kuna mambo ya muhimu ya kufanya. Hebu achana na simu kwanza ufanye mambo ya muhimu kuhusiana na maisha yako. Kama mpenzi wako hakwelewi katika hili basi hakufai. 10. NDUGU ZAKE WANAKUFUATILIA Iwapo utabaini kuwa marafiki, ndugu na jamaa za mpenzi wako wanamtonya mpenzi wako kuhusiana na kile wanachokiita mwenendo wako mbaya, usipuuze hali hii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu hawa wanayo sababu ya kuwa na wasiwasi na mwenendo wako, kwa hiyo jichunguze na kuangalia jinsi unavyoenenda. Hata hivyo, jambo hili si ishara njema ya mustakabali mwema wa uhusiano wenu. Iwapo mpenzi wako ataweka watu wake wakufuatilie, maana yake halisi ni kwamba hakuamini. Katika hali kama hii, haitarajiwi kuwa mustakabali wa uhusiano wenu utakuwa mzuri, kwani kutakuwa na uingilizi mwingi wa ndugu, jamaa na marafiki zake. Unaweza kukubali kuendelea kuishi katika hali hii kwa kisingizio cha mapenzi, lakini ukweli ni kwamba hayatakuwa mapenzi bali karaha. KUWA MAKINI Kama unavyoona, hizi ni baadhi tu ya dalili kuwa mapenzi yako kwa mwanamke sasa yanaelekea katika ulevi, mithili ya ule wa dawa za kulevya. Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kweli mapenzi ni kitu kizuri, lakini pia mapenzi yanahitaji kuwa jambo linaloashiria mustakabali mwema kwa wahusika wawili. Yakiwapo mambo haya kumi hauwezi kuwapo mustakabali mwema katika mapenzi. ... Read More
Tatizo la Ugumba kwa wanawake  Ugumba ni hali ya mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake. Nini husababisha ugumba kwa wanawake? Mayai kutokomaa ipasavyo: Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri. Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema: (1) Matatizo ya kihomoni Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha matatizo katika homoni: Ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ubongo ambayo ina jukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitari ambayo yenyewe tena hutuma uchochezi wa kihomoni kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H na L.H ili kuanzisha ukomaaji wa mayai. Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Tatizo hili linachukuwa asilimia 20 katika kesi za mayai kushindwa kukomaa kiasi kinachohitajika. Ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitari Kazi kubwa ya tezi ya pituitari ni kuzarisha na kutoa homoni mbili maalumu kwa ajili ya mfumo wa uzarishaji kufanya kazi zake vizuri ambazo zinajulikana kitaalamu kama ‘Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na ‘Luteinizing hormone (L.H)’. Mayai yatashindwa kukomaa vizuri ikiwa ama L.H au F.S.H zinatengenezwa chache sana au nyingi sana kuliko inavyohitajika. Hili linaweza kutokea kama sababu ya ajari, uvimbe au kama usawa usio sawa wa kikemikali katika pituitari. (2) Kovu katika Ovari Uharibifu au ajari katika ovari unaweza kupelekea kuzalishwa kwa mayai ambayo hayajakomaa. Kwa mfano, upasuaji mkubwa, uvamizi au upasuaji wa mara nyingi wa uvimbe katika ovari unaweza kusababisha kapsuli ya ovari kupata majeraha au makovu na hivyo kwa namna moja ama nyingine kuweza kuzuia utungwaji wa mayai ambayo hayajakomaa vema. Pia maambukizi katika njia ya uzazi yanaweza kupelekea tatizo hili. (3) Dalili za mwanzo za kukaribia kufunga kuzaa (Menopause) Hii huchangia kwa asilimia chache na kwa sasa halielezeki kisawasawa. Kwamba wanawake wengi wanapokaribia umri wa kuacha kuzaa kuanzia miaka 40 kwenda juu baadhi yao hutokewa na tatizo la kutunga mayai ambayo hayajakomaa vema. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao mapema kabla ya umri uliozoeleka yaani miaka 40 kwenda juu. Kwa sababu hiyo inadhaniwa kwamba uwezo wao wa asili katika kuzalisha mayai unakuwa umepunguwa na wengi wao huwa ni wale walikuwa wakijihusisha zaidi na michezo ya kukimbia au wale wenye historia ya muda mrefu ya kuwa na uzito pungufu na wafanyaji sana wa mazoezi. Tatizo hili pia linaweza kuwa ni la kurithi. (4) Matatizo kwenye kijishimo yai (follicle) katika ovari: Ingawa kwa sasa bado hili nalo halielezeki, hiki kijishimo yai kwa kitaalamu kinajulikana kama ‘’follicle’’ ndicho hupasuka na yai kutoka. Kuna baadhi ya kina mama wanapata dalili za kijishimo yai kutokupasuka “unruptured follicle syndrome” na matokeo yake kila mwezi mama anazalisha yai kama kawaida lakini hiki kijishimo yai kinashindwa kupasuka. Hivyo yai linabaki ndani ya ovari na utungaji wa mimba unashindwa kufanyika. Kinachosababisha ufanyaji kazi dhaifu wa mirija ya uzazi (Fallopian Tubes): Magonjwa katika mirija ya uzazi yanahusika na ugumba kwa karibu ya asilimia 25 ya wanawake wote wagumba. Hali yenyewe inatofautiana toka kwa mmoja hadi kwa mwingine kutoka kugandana au kunatana kidogo hadi kuzibika kabisa kwa mirija. Matibabu ya mirija iliyozibika huhusisha upasuaji au usafishaji wa mwili kwa kula vyakula na vinywaji maalum kwa muda wa majuma kadhaa. Sababu kubwa zinazopelekea kuzibika au kunatana kwa mirija ya uzazi ni pamoja na zifuatazo: (A) Maaambukizi Maambukizi katika njia ya uzazi ambayo yamesababishwa ama na bakteria au virusi na ambayo kwa kawaida ni magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya tendo la ndoa, maambukizi haya kwa kawaida husababisha muwasho au kuungua na kupelekea makovu na uharibifu. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na mengineyo yanaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa wanawake wengi hasa ikiwa hayatatibiwa mapema. (B) Magonjwa yasiyo ya kawaida Magonjwa yasiyo ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kidole tumbo (appendicitis) na uvimbe katika utumbo mpana (colitis), magonjwa ambayo husababisha muwasho au kuungua chini ya uvungu wa utumbo mkubwa na kuiathiri mirija ya falopiani na kama matokeo yake makovu na kuzibika kwa mirija ya uzazi hutokea. (C) Upasuaji uliopita Upasuaji una chukua nafasi kubwa katika kusababisha ugumba kutokana na matokeo yake ya kusababisha magonjwa ya mirija ya uzazi na uharibifu utokanao na huo upasuaji. Upasuaji katika utumbo mkubwa unaweza kupelekea kunatana au kugandana kwa mirija ya uzazi kutakakopelekea mayai kushindwa kusafiri kirahisi katika mirija hiyo ya uzazi. (D) Mimba kutungwa nje ya mji wa uzazi: Hii ni wakati mimba inapotungwa katikati ya mirija ya uzazi yenyewe. Katika hali kama hii hata kama kutatokea bahati kiasi gani bado kunaweza kusababisha uharibifu katika mirija na hali hii ni moja ya hali mbaya sana kiafya na kimaisha. (E) Hali ya kurithi Kwa nadra au kwa asilimia fulani ndogo baadhi ya wanawake huzaliwa na hali ya kuwa na mirija isiyo ya kawaida kwa uzazi na kwa kawaida hali hii huambatana na mji wa uzazi usio wa kawaida pia. . (5) Sababu za kitabia: Inajulikana wazi kwamba baadhi ya tabia na namna tunavyoishi kunaweza kupelekea wanandoa wakashindwa kupata mtoto. Kwa bahati nzuri nyingi kama si zote ya hizo tabia zinaweza kurekebishika au kuachwa kabisa na kupelekea siyo tu kuwa na uwezo wa kuzaa bali pia kuwa na afya nzuri kwa ujumla. Sababu hizo za kitabia ni pamoja na zifuatazo: Lishe na mazoezi Ili mfumo wa uzazi uwe na uwezo mzuri unahitaji vitu viwili mhimu, lishe kamili na mazoezi. Wanawake wenye uzito uliozidi sana au wenye uzito pungufu sana wanaweza wakapatwa na tatizo la kutopata ujauzito kirahisi. Uvutaji sigara Uvutaji wa sigara una mchango mkubwa na ugumba. Uvutaji sigara husababisha uzarishwaji wa mbegu chache kwa mwanaume (lower sperm count) kwamba mwanaume anatoa mbegu chache sana ama pungufu wakati huo huo uvutaji sigara huchangia katika tatizo la kutoka kwa mimba, kuzaa kabla ya miezi 9 (njiti), na kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kwa wanawake. Unywaji pombe Unywaji pombe kupita kiasi una mchango mkubwa sana katika ugumba na hii hata ikitokea mama akapata ujauzito kama bado anaendelea kunywa pombe inaweza kupelekea matatizo hata kwa mtoto mtarajiwa. Unywaji pombe pia huchangia uzarishwaji wa mbegu chache kwa wanaume. Madawa ya kulevya Utumiaji a madawa ya kulevya kama bangi na mengine ya kujidunga kwa sindano kunaweza kuwa sababu ya kuzalisha mbegu chache kwa wanaume. Utumiaji wa dawa za kulevya kama ‘Cocaine’ kwa mama mjamzito kunaweza kusababisha mtindio wa ubongo na matatizo katika figo kwa mtoto mtarajiwa. Matumizi ya madawa ya kulevya inafaa yaepukwe wakati wa kutafuta ujauzito na wakati wa ujauzito. Utowaji mimba Utowaji mimba wa mara kwa mara pia unahusika sana na tatizo la ugumba kwa karibu ya asilimia 20. Utowaji mimba unaweza kusababisha makovu katika mji wa uzazi na hata kuharibika kabisa kwa mji wa uzazi ikiwa utowaji huo haukufanyika kitaalamu au unafanyika mara kwa mara. (6) Sababu za ugumba za kimazingira: Uwezo wa kushika ujauzito unaweza pia kuathiriwa kutokana na kuwa karibu na baadhi ya kemikali au sumu katika maeneo ya kazi au makazi. Vitu viwezavyo kusababisha mabadiliko, dosari za kuzaliwa, utokaji mimba, au utasa huitwa ‘Sumu kwa mfumo wa uzazi’. Kamikali zifuatazo zinahusishwa na ugumba au utasa: Risasi (Lead) Kuwa karibu na kemikali au sumu zinazounda risasi kunaweza kuwa sababu ya ugumba. Risasi hupelekea kuzalishwa kwa mbegu zisizo za kawaida kwa wanaume zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘teratospermias’ na inafikirika pia kuhusika na utokaji mimba kusiko kwa asili (artificial abortion). Baadhi ya matibabu na madawa ya hospitalini Kuwekwa kwenye matibabu yanayohusisha mionzi (x-rays), mionzi ya kawaida au hata ile ya kutibia kansa (chemotherapy), kunaweza kusababisha matatizo katika uzarishwaji wa mbegu kwa mwanaume na wakati huo huo kuchangia kwa sababu kadhaa zinazopelekea kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Pia matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito kwa muda mrefu yamekuwa yakihusishwa na ugumba kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado kuna mjadala mkubwa katika hili. Ethylene Oxide Hii ni kemikali inayotumika kusafishia vifaa vya upasuaji, pia hutumika katika kutengeneza baadhi ya sumu za kuua wadudu. Ethylene oxide inaweza kupelekea matatizo katika uzazi hasa katika miezi ya mwanzo mwanzo ya ujauzito na inahusishwa sana na tatizo la utokaji mimba katika miezi ya mwanzo ya ujauzito (early miscarriage). Dibromochloropropane (DBCP) Hii pia ni kemikali au dawa inayotumika katika kuua wadudu, ikiwa unafanya nayo kazi kila mara inaweza kusababisha kutungwa kwa mayai yasiyokomaa vizuri, kuelekea mapema kwa ukomo wa kutokuzaa kabla hata ya miaka 40 au 45 (early menopause) na kadharika. (7) Sababu zingine zinazoweza kusababisha ugumba kwa mwanamke: Karibu asilimia 10 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya mji wa uzazi usio wa kawaida (abnormal uterus). Hali zingine ni pamoja na uvimbe katika kizazi, kugandana au kunatana kwa mji wa uzazi na mirija ya uzazi. Karibu asilimia 3 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya matatizo ya ute usio wa kawaida katika mlango wa kizazi (femaleís cervical mucus). Ute ute huu unahitaji kuwa na hali fulani maalumu kwa mbegu za kiume kuweza kuogelea kirahisi katikati yake. Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni usawa usio sawa wa homoni za kike ambapo homoni ya uzazi ya kike iitwayo ‘estrogen’ yaweza kuwa ni chache sana au homoni nyingine iitwayo ‘progesterone’ yaweza kuwa ni nyingi sana tofauti na inavyohitajika. Vitu vya kuepuka kwa mtu mwenye tatizo la ugumba: ChipsiVinywaji baridiKaffeinaNyama nyekunduVilevi ... Read More
Kanuni Kumi '10' Muhimu za Kuwa Mke Mwema Katika Ndoa....Ikizishindwa Imekula Kwako  UHALISI WA MAISHA: Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU: Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI: Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia. UTII KWA KWA JAMII: Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa. UAMINIFU KATIKA JAMII: Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote. UNYENYEKEVU WA KWELI: Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima. UWAJIBIKAJI WA DHATI: Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake. USHIRIKIANO WA DHATI: Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora. UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO: Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako. KUFANYA TATHIMINI: Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: