Home → ushauri
→ Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati
ANAVYOKUTAZAMA
Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50.
Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.
MIPANGO
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.
ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha.
ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.
ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.
UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.
ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.
ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.
ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.
ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.
KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!!
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!!
Artikel Terkait
Kwa wanawake tu! Jinsi ya kujisafisha uke  Naomba kufahamishwa na wanawake jinsi ya kujisafisha kwenye papuchi(mwanaume atakaye shauri naomba awe doctor au mwenyewe experience ya kutosha kuhusu maumbile ya mwanamke) Mimi huwa nikienda kuoga natumia sabuni ya jamaa kusafisha juu kabisa ya papuchi yaani kwenye mapaja na pale juu kwenye nyw**le...then natumia maji mengi kujisuuza na kuingiza kidole ndani kidogo ya K kutoa uchafu either wa period kama niko P na sometimes nakuta kuna ule uchafu mweupe wanaita(utoko) but huo uchafu huwa ni mweupe kama barafu na pia haunuki kabisaa..... Sasa swali ni kwamba kuna watu wanadai hatupaswi kutoa huo uchafu eti ni bacteria wa kukinga K isipate madhra so hupaswi kuingiza kidole kabisa.... tuoshe juujuu tu...... Second wengine wanasema tusinawe na sabuni kabisaa(japo kama nilivyosema mimi sabuni napitisha kwa juu kabisa tena nikiwa nimesimama ili isiweze kuingia kwenye K coz siamin kama kujisafisha bila sabuni harufu ya mkojo, harufu ya P na jasho itaisha kwa kunawa na maji tu.....na situmii sabuni zenye chemical). Naomba wanake wenzangu mnipe experience zenu juu ya hili ... Read More
UNAJUA KUMWONYESHA MPENZI WAKO KAMA UNAMPENDA????  Kwa upendo wao wote, kwa nguvu zao zote, na uzuri , mahusiano ni kama mmea ambao unahitaji kumwagilia maji na kuwekewa mbolea na kupata jua la kutosha ili uweze kunawiri vizuri Sababu kubwa ambayo watu hukosa kujua kama wanapendwa ni kutohisi upendo. Kwa nini? Kwa sababu hata kama wanasema I love you mwisho wa kuongea kwenye simu au kabla ya kwenda kazini, hayo maneno hayana miujiza bila ya kuwa na mengine yalio rahisi . Kuna vitu vidogo vidogo sana vinavyoonyesha upendo na kumfanya mtu ajisikie kupendwa. 1.Usisahau kumkumbatia kabla ya kusema kwa heri. Uelewa wa kimwili ni wa muhimu kuliko maneno 2.Mwambie jinsi alivyo muhimu kwako. Hii huenda zaidi ya neno i love you. 3.Express understanding panapohitajika kusema. Nimeelewa unachokisema. Kama hujaelewa elezea, kwa kusema hivi , Niambie jinsi unavyojisikia ili nikuelewe. 4.Sema mara nyingi jinsi unavyomkubali anapokuwa amefanya jambo kwako. Husband and wife in park 5.Mwambie jinsi gani unafurahia vipengele vya upekee wake. Kwa mfano , napenda uchangamfu wako, mpongeze. 6.Toka nae siku nzima bila ya kusema kitu chochote zaidi ya kumsifia. 7.Mnunulie chakula anachokipenda bila yeye kusema. 8.Msaidie kupika 9.Kama mna watoto wapeleke kutembea, ili kufurahia michezo ya watoto ili kumwacha awe peke yake kwa utulivu. 10.Tuma ujumbe wa kimapenzi kwa mwenza wako bila sababu . 11.Mtumie email wakati yuko kazini ili kujua anajisikiaje. 12.Mpigie wakati akiwa break kusema tu hujambo 13.Karibia gari, meza, au kochi na umshike mikono yake japo kwa muda kidogo. 14.Mvutie kiti anapotaka kukaa au mfungulie mlango anapotaka kutoka au kuingia. 15.Kumbuka kumpa tabasamu, sio fake, lile ambalo umetunza kwa ajili yake . 16.Badala ya kumweleza jinsi ulivyokuwa na siku mbaya kazini, mwambie kuwa siku hio ulihitaji kuwa na yeye kwa sababu…au nimekuwa na siku mbaya nahitaji unikumbatie. 17.Fanya utani na ucheke nae 18.Nendeni kulala kwa wakati mmoja, ongeeni pamoja au kama kusoma msome pamoja au kama kutulia kwa muda fanyeni pamoja. 19.Kama una watoto mpongeze mwenza wako mbele yao. Watoto watafurahi pia. 20.Mkumbatie mbele za watu, ingawa ataona aibu lakini atafurahia. 21.Tafuta njia nzuri za kuambiana badala ya I love you 22.Muwe na tabia ya kutoka japo mara moja kwa wiki kama mkiweza 23.Mpe zawadi 24.Mpeleke movie 25.mpe massage bila sababu au kwa ajili ya kazi nyingi 26.Mwambie kuwa yeye ni rafiki yako 27.Usiogope kumshirikisha hisia zako, Ni vizuri kufahamu kama una furaha au huna furaha wakati huo na kwa nini 28.Sikiliza anapokuambia jinsi anavyojisikia 29.Kumbuka kila mara unapoweza nunua kitu kidogo kwa ajili yake. 30.Andika ujumbe mdogo wa kimapenzi na kuacha sehemu ambapo atafika 31.Mshike mikono yake mbele za watu 32.Mpate fundisho pamoja, halijalishi ni aina gani 33.Omba msamaha unapokosea 34.Wakati mwingine yeye awe sahihi 35.Mcheze game pamoja 36.Mpe nafasi anapohitaji hivyo.lakini afahamu kuwa upo kama atakuhitaji 37.Mchemshie maji ya kuoga anapokuwa na stress 38.Mwoshee gari yake 39.Jaribu kufanya kitu cha wema kila siku kwa ajili yake 40.Jaribuni kufanya kitu kipya pamoja. Changamoto moja ni bora 41.Mwache alale miguu pako 42.Mtengenezee breakfast, kama inawezekana mpelekee kitandani 43.Mkumbushe kuwa yeye yuko hot au sexy 44.Mkatembee kwenye hewa nzuri pamoja 45.Mnaweza kuvaa nguo za kufanana mnapotoka kupunga upepo 46.Mjitolee pamoja 47.Mtengeneze nywele zake 48.Muweke lengo kama wanandoa, kwa ajili ya fitness, finance, na personal growth 49.Kusafiri pamoja 50.Mpe compani anapoenda mpirani, kwenye game na uwe mmoja wao 51.Chukua muda wa kuwajua rafiki wa mwenza wako 52.Mwache atoke peke yake wakati mwingine 53.Mwekee nyimbo anazozipenda na mcheze pamoja 54.Usiwe serious sana, uwe mcheshi wakati mwingine 55.Mwimbie nyimbo anazopenda 56.Mwambie unampenda zaidi ya jana 57.Kama una siku mbaya , sikiliza kila unachotaka kusema 58.Mwambie kuwa anavutia kuliko wakati mliokutana mara ya kwanza 59.Mwambie unamfikiria kila mara 60.Mwambie kuwa unamsaidia kwa kuwa umemwelewa 61.Mwambie unapenda mwili na akili yake 62.Mwambie unachokifurahia siku hio. Na jinsi gani kinakukumbusha kuhusu yeye. 63.Siku yako imeendaje leo Kila ukiamka mwambie habari za asubuhi kila siku 65.Kila siku ukitaka kulala mwambie usiku mwema 66.Hakikisha anafahamu kuwa yeye ni namba moja kwako 67.Mwonyeshe kuwa unamuheshimu kwa kusikiliza mawazo yake kwenye maamuzi muhimu 68.Onyesha kukubali alichokifikiria na kukiamua hata kama unaona kabisa hukubaliani nacho. 69.Mwambie akuchagulie nguo za kuvaa kazini 70.Nendeni gym pamoja 71.Mnunulie kadi bila sababu , hata kama hakuna sikuku 72.Tamani kumkiss kila mara 73.Mwambie kuwa umepata bahati ya kuwa na yeye na kuwa umebadilika tangu ukiwa nae 74.Kuwa mkweli . mfahamishe makosa uliyoyafanya 75.Kuwa mpole kwake kwa sababu mwanamke ni laini 76.Mwonyeshe kuwa unamwamini ili nae awe wazi kwako 77.Pigeni picha pamoja 78.Fanyeni mambo ya kijinga pamoja 79.Alika familia yake kwenye chakula cha jioni 80.Mwombe mwenza wako mshirikishane ndoto zenu 81.Cheka anapotania,hata kama utani huo hauchekeshi 82.Uwe rahisi ili aweze kukupenda. Utagundua kuwa kumbe ni mkarimu na ana wema. ... Read More
Wanawake: Mumeo akikukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana  Usiku kama mumeo kakukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana, hata malaika baraka hawawezi shuka kwenu. Huyo ulionae amezaliwa kwao kaja na tabia zake na wewe umezaliwa kwenu una tabia zako. Sasa ukitaka kila kitu kiwe wewe unavyotaka atakuwa mwanao tena huyo sio mumeo samehaneni kwa kila mnalofanyiana. Usiweke vinyongo tena ukajua unamkomoa mana unavyonuna ndo mchepuko unavopata chance ya kuwasiliana na si kila mwanaume anamchepuko wengine washkaji tu sasa ukijitia umenuna kisa umemuona kachat, sijui umekuta meseji sijui nini utakonda uzikwe na presha na unavyotiwa kaburini tu huku wenzio wanamtext pole kazi ya Mungu mpenzi. Gangamala mtoto wa kike sio kidogo kununa kama unga wa ngano ulokosa amira. Tabasamu njia nzuri na sahihi ya kumuua mtu akikosea ukatabasamu ataanza kutafuta mchawi kumbe mchawi mwenyewe, ataanza kutoka kujua kwanini hujakasirika atatulia tu akiamini anakuvizia kumbe anajivizia. ... Read More
Mbinu za kufufua penzi lenu 1. Badilisha mavazi yako . Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako. Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo. Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile. 2. Hamia nyumba mpya Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako. Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja. 3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala. Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako. Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo. 4. Omba msamaha nawe umsamehe. Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa. Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu. Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa. 5. Endeni mjivinjari kwa tarehe Endeni likizo au tokeni nje pamoja. Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja. 6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana. Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana. Jiulize mbona watu huangalia picha hizi? Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?. Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe. Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua? Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu. Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi. Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake. 7. Jisalimishe upya Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu. Je unampenda kama awali? Je unanipenda kweli? Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu. Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao. 8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba. Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee . Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika. 9. Epuka kuumiza mwenzako Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako. Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda. 10. Mbusu mpenzi wako zaidi. Mabusu huleta watu pamoja. Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi. 11. Omba Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu. Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu. 12. Tenga wakati wa Faragha Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako. Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda . Ni muhimu sana. 13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani. Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe. Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako. 14. Weka teknolijia mbali Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo . Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ? Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe . Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ? Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia . 15. Chezeni pamoja Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba. Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani ! Chezeni miili yenu ikigusana! 16 Kaeni msemezane Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ? Unamwambia nini kitandani ? Unazungumzia kuhusu madeni yako? Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye . 17. Andikianeni barua za kimapenzi. Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako. 18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja. Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!! Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu. Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu 19.Nunua marashi mapya Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe. 20.Jiachilie Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba Mchezee shere Mtanie mpenzi wako ... Read More
*SIMULIZI DARASA* *STORY FUPI* *USIMDHARAU USIYEMJUA* Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda. Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila alipopata nafasiya kuomba. Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa…hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake. Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo… Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake.. Akamsifia sana, akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake. Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho… Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana. Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!! Lahaula… watu wote wakastaajabu.. mkate??? Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!! Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.!! Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi high table na kusema “baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii. Lakini kama ungetambua thamani ya zawadi hii, usingefanya haya..” Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday. Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema “Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa.. ..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza..” Kisha akachukua mkate wake, huyoo akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late.. MORAL OF THE STORY..! Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana.. Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida… kuna vingi vya thamani ndani yako. Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!! 🌹TUELIMISHANE MEMA🌹 Subra ndio inayotakiwa katika maisha. *akida* ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: