Home → ushauri
→ Kwanii Wanaume Waaminifu Kwenye Uhusiano Huachwa.....

Kuachwa na mpenzi kwa sababu umekuwa ni muaminifu sana yaonekane ni jambo lisiloingia akilini lakini linatokea.
Moja ya mambo ya ajabu unayoweza kuwa ushawahi kuyasikia ni kwamba mara nyingine uamuzi wako wa kuwa mwanaume mwema sana na unayejitahidi kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uwe mzuri muda wote unaweza kukugharimu na kujikuta unaachwa kabisa.
Haitakiwi kuwa hivyo lakini mara nyingine inatokea, na inatokea kwa sababu wazo la mwenza wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi laweza likawa tofauti na ulionao wewe. Wengine wana mawazo hasi kuhusu jinsi uhusiano/ndoa inavyotakiwa kuwa.
Hii ndio sababu hutakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye na vipaumbele sawa na vya kwako au asiye na mtazamo mmoja wa kimaisha kama ulionao wewe.
Usipozingatia hilo, utajikuta unaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hatakujali vya kutosha kwakuwa labda humfokei au kumpiga anapokukosea – au utajikuta ameshakupanda kichwani na kuanza kukudai mambo ambayo huwezi kuyatimiza lakini ukajikuta unajitutumua kumtimizia kwa sababu unataka kumfurahisha mpenzi wako na analijua jambo hilo.
Kwa sababu baadhi ya wanaume wanapenda kulinda siri na kuwaachia uhuru wapenzi wao, wanajikuta wakiwapa ruhusa wanawake zao kwenda popote wanapojisikia bila kuwafatilia wanachofanya.
Nini kinafata baada ya hapo? Mwanamke anatoka, anatafuta mchepuko na kukusaliti. Mwisho inakufanya wewe mwanaume uonekane mjinga mbele ya wengine.
Tatizo ni kwamba tabia hii inaibuka kutokana na mazoea ya watu kuingia kwenye uhusiano wakiwa wameficha tabia zao halisi na kuja kufungua makucha yao baada ya kuona ameshaishi na wewe kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi tena kumuacha.
Hii inasababisha wanaume walioathirika kutokana na tabia kama hizi kutoka kwa waliokuwa wapenzi wao wasiweze kuwaamini wanawake wengine tena kwa kuona kwamba wote ni sawa na wale waliowaumiza na kusababisha wasiweze kuwaonesha wenza wao wapya mapenzi kwa kiwango cha juu wakihofia kuumizwa tena.
Kuwa mpole, mkarimu na mwenye upendo wa hali ya juu kwa mpenzi wako ndio jambo linalotarajiwa kwenye uhusiano. Mtu hatakiwi kufanywa ajisikie vibaya kwa kumuonesha mapenzi ya kweli mwenza wake.
Kama wewe unakuwa muaminifu na mwema kwa mpenzi wako lakini umekuwa unadharauliwa au ukaachwa kutokana na tabia hiyo, kaa ukiwa na amani kabisa kwamba lawama za kuvunjika kwa uhusiano huo hazikuhusu wewe – lawama ni za mpenzi wako aliyeshindwa kujua wewe umekuwa mwema kiasi gani kwake.
Kwanii Wanaume Waaminifu Kwenye Uhusiano Huachwa.....  Kuachwa na mpenzi kwa sababu umekuwa ni muaminifu sana yaonekane ni jambo lisiloingia akilini lakini linatokea. Moja ya mambo ya ajabu unayoweza kuwa ushawahi kuyasikia ni kwamba mara nyingine uamuzi wako wa kuwa mwanaume mwema sana na unayejitahidi kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uwe mzuri muda wote unaweza kukugharimu na kujikuta unaachwa kabisa. Haitakiwi kuwa hivyo lakini mara nyingine inatokea, na inatokea kwa sababu wazo la mwenza wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi laweza likawa tofauti na ulionao wewe. Wengine wana mawazo hasi kuhusu jinsi uhusiano/ndoa inavyotakiwa kuwa. Hii ndio sababu hutakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye na vipaumbele sawa na vya kwako au asiye na mtazamo mmoja wa kimaisha kama ulionao wewe. Usipozingatia hilo, utajikuta unaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hatakujali vya kutosha kwakuwa labda humfokei au kumpiga anapokukosea – au utajikuta ameshakupanda kichwani na kuanza kukudai mambo ambayo huwezi kuyatimiza lakini ukajikuta unajitutumua kumtimizia kwa sababu unataka kumfurahisha mpenzi wako na analijua jambo hilo. Kwa sababu baadhi ya wanaume wanapenda kulinda siri na kuwaachia uhuru wapenzi wao, wanajikuta wakiwapa ruhusa wanawake zao kwenda popote wanapojisikia bila kuwafatilia wanachofanya. Nini kinafata baada ya hapo? Mwanamke anatoka, anatafuta mchepuko na kukusaliti. Mwisho inakufanya wewe mwanaume uonekane mjinga mbele ya wengine. Tatizo ni kwamba tabia hii inaibuka kutokana na mazoea ya watu kuingia kwenye uhusiano wakiwa wameficha tabia zao halisi na kuja kufungua makucha yao baada ya kuona ameshaishi na wewe kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi tena kumuacha. Hii inasababisha wanaume walioathirika kutokana na tabia kama hizi kutoka kwa waliokuwa wapenzi wao wasiweze kuwaamini wanawake wengine tena kwa kuona kwamba wote ni sawa na wale waliowaumiza na kusababisha wasiweze kuwaonesha wenza wao wapya mapenzi kwa kiwango cha juu wakihofia kuumizwa tena. Kuwa mpole, mkarimu na mwenye upendo wa hali ya juu kwa mpenzi wako ndio jambo linalotarajiwa kwenye uhusiano. Mtu hatakiwi kufanywa ajisikie vibaya kwa kumuonesha mapenzi ya kweli mwenza wake. Kama wewe unakuwa muaminifu na mwema kwa mpenzi wako lakini umekuwa unadharauliwa au ukaachwa kutokana na tabia hiyo, kaa ukiwa na amani kabisa kwamba lawama za kuvunjika kwa uhusiano huo hazikuhusu wewe – lawama ni za mpenzi wako aliyeshindwa kujua wewe umekuwa mwema kiasi gani kwake.
Artikel Terkait
SABABU YA KWELI WANAWAKE KUENDELEA KUTEMBEA NA WANAUME WALIO OA  Jane ni mwanamke mwenye mafanikio, anamiliki kampuni ya kutengeneza mifuko ya plastic, ana studio. Ana akili , anavutia na ni mwenye ujasiri. Pia anatembea na mume wa mtu. Amekuwa akiwauliza rafiki , familia yake ambao wanafahamu kuwa kitu gani kinamfanya mwanamke mwenye mafanikio, akili na ujasiri kutembea na mume wa mtu kwa miaka zaidi ya mitatu? Hamu ndio Inayoanza Mwanaume ambaye ameoa anapomkaribia mwanamke , anakuwa na hatari— hatari ambayo inaonyesha kumuhitaji zaidi. Kuwa na muda naye. Huenda kwa meseji au kupata chakula pamoja kwa siri, au kulala nae kwa siri. Huonyesha kuwa na majukumu kama mwanaume single. Lakini mwanaume single huandaa date. Huwa na sababu nyingi za kufanya hivyo, na ukiri wao huwa ni wa makini na huonyesha kuwa hawako interested. Hujikuta wameingia kwenye majukumu ambayo hakuwa amejiandaa. Kwa ushindani, kazi ya mwanaume aliyeoa Inamlinda kutokana na nia yake kwa mwanamke single ili kuonyesha hamu yake. Kama hataweza kuonyesha hisia zake kwa kumtazama macho yake, sauti yake, kumsugua mwanamke mgongo wake, kumfanyia massage kwenye mabega, mwanamke atajuaje kama anamtaka? Na ataendeleaje kubaki nae kama hamtimizii haja zake? Kwa kufanya hayo anaweza kumuwekea ulinzi, mahusiano yao kukomaa na kuwa mazuri na kuwa ya kawaida. Lakini akili Itakuja. Marafiki aliowaambia watamkumbusha.Ni mume wa mtu. Familia watamuuliza , bado yuko na mke wake? Wakati anapoanza kujiuliza ndani yake , mume alienae, Ataanza kuwa na njia mbili. Kwa wanawake wengi, hio imepitwa na wakati. Kwa wengine mchezo utaendelea—kwa kufahamu maamuzi haya…tuangalie sasa 1.Wakati mwanaume anapotoka nje, uwezekano mkubwa hana furaha ndani ya nyumba yake. 2Talaka zinaongezeka . ndoa zinafikia mwisho, na wanaume wanaoa tena. 3.Uzinzi unaongezeka kwa wanaume. Huenda kuishi muda mrefu peke yao sio mpango mzuri. Kwa mtu kama Jane kuishi maisha kama hayo, huenda ni katika kumpata mtu sahihi na kumuondoa kwa mke wake hata kama kutakuwepo hatari katika hisia zake. Mwanamke kama Jane ni wepesi wa kujifunza zaidi kuhusu tabia za wanaume ambao wanacheat kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano ya kudumu. Wengi wa wanaume wanasema , sababu kubwa ya kucheat ni kukosa sex Ni kiasi kidogo sana cha wanaume ambao hupotea katika mapenzi ya nje Baadhi ya wanaume wanaocheat walitoa taarifa kuwa wanafanya hivyo kwa wenza wengi karibu miaka yote Kwa kulinganisha wanawake na wanaume. Wanawake wao huingia kwenye mahusiano kwa mwanaume aliyeoa kwa sababu ya kuwapenda. Lakini sio nzuri kama mtu ameoa ni bora kujiheshimu na kumuheshimu mke wake , Na kama kuna tatizo ni vizuri kurekebisha kuliko kwenda kutafuta majibu ya tatizo lako nje.Kwa nini nasema hivi , ni kwa sababu ipo siku mwanamke huyo atahitaji kuwekwa wazi , utafanyaje na wewe ulikuwa ni mwizi. kwa upande wa mwanamke Utavunjika moyo, inapofika wakati kama huo.Maumivu ya kuachwa na mwanaume aliyeoa ni makubwa kuliko ya kuachwa na mwenza ambaye ni wako kabisa. Black woman hugging her knees 1.Utajisikia kama mkosaji mara mbili. Kwamba hukuweza kumpata mtu ambaye tayari kwanza alikuwa ameoa na amekuacha baada ya kuridhika kwake. 2.Wasaliti wanaokatiza mahusiano huwa wanaonyesha kabisa kuwa hawana hisiana za kutosha kwako. Wanakuchukulia kama wewe ni msichana mkubwa, na unaelewa kitu gani unachokifanya. 4.Mfumo unaompa support unaweza ukawa upo gizani. HUenda ni aibu au hamu ya kumlinda msaliti au vyote. Hakuna mtu ambaye anafahamu. Kama wapo basi ni wa katibu sana. Kwa hio watu kama Jane wataepuka vipi hatari inayotokana na aina hii ya mahusiano? Ukweli ni kwamba, ufahamu una nguvu.Kama msomaji unahusika na mume wa mtu, rudia tena kusoma makala hii kwa makini kabla hujaendelea zaidi. Maisha ni mafupi.Muda wa kumsaidia mume wa mtu ambaye amekosa kitu fulani kwa mwenza wake umekwisha. Mwache akatengeneze kwa mwenza wake. Wanaume Single wako wengi wanakusubiri na hawana hatari kama hizo. Hata kama atakuonyesha kuwa wako cool mwanzoni usidanganyike. ... Read More
JINSI YA KUISHI NA MPENZI MPENDA PESA   HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana. Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha! Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana. Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.” Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha. Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha. Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia. Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili. Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah. Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende tukaone. MWELEZE UKWELI Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi. JENGENI KUSAIDIANA Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake. Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi. ACHA UFUJALI Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo! Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu. BAKI NA HILI Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie. Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo. ... Read More
MWANAUME ANAPOSEMA HATAKI KUKUOA: MWAMINI  Naandika hii makala kwa sababu nimekutana na maswali mengi ambayo yanaumiza wanawake wengi. Swali linakuwa hivi. Nimekuwa na huyu mwanaume kwa muda mrefu na tumekuwa tukishirikiana mambo mengi. Sijawahi kuwa na hisia kama nilizo nazo kwa mwanaume huyu kwa mtu yeyote. Na nilijua tutakuwa pamoja maisha yetu yote. Tatizo ni kwamba anasema hataki kunioa? Nitafanyaje ili aweze kujua kuwa nampenda na tunaendana vizuri pamoja na tunatakiwa tuoane? Wanaume wengi huwa wanaogopa kuweka ahadi kama hawana uhakika na upendo walio nao kwa mwanamke. Semeni ukweli wanaume. Je ameongelea kuhusu maisha ya baadae? Kuna mpango gani? Ni rahisi kubadilisha mwanaume? Unawezaje kumlazimisha akuoe? Kitu gani cha kufanya kama amesema hawezi kukuoa? Kama amesema hatakuoa, Mwamini . Elewa. Najua tayari jibu umepata kwenye maandiko yangu ya juu, lakini napenda kurudia, huwezi kumlazimisha mwanaume akuoe kama amesema hataki kukuoa. Hataweza. Sasa basi sisemi kama haiwezekani kweli. Kuna wanaume ambao husema hawatakuoa na hubadili mawazo yao na kuamua kuoa mwanamke ambaye alikuwa hapendi kumuoa. Lipo hilo. Mwanaume anayesema hatakuoa na wakati anaishi na wewe, mara nyingi anakupotezea muda na atakwenda kuoa mtu mwingine anayempenda kuliko wewe. Tuangalie kwa nini iko hivyo. Ina maana gani anapokuwa anaongea kuhusu kuchukia ndoa Aina ya mwanaume ambaye atakuambia hatakuoa ni yule ambaye anachukizwa na taasisi ya ndoa au sheria yake. Mwanaume huyo hafikirii kama wazo la kuoa ni zuri kwa kila mtu- anaona hata wanandoa ambao wako pamoja hawaonyeshi kama wana upendo wa kutosha, hawana upendo wa kweli ( anaweza kuwa haamini hata kama kuna upendo) Anafikiria hata kama ataona, mbona ndoa nyingi hazifiki mwisho, au mbona ugomvi ndani ya ndoa hauishi. Vyovyote vile , kwa sababu zozote zile, lakini mwanaume huyu anaonyesha kuchukia taasisi ya ndoa, na hataki kuingia huko, ndio maana hataki kuoa. Kama utasikia akisema hivyo mwamini. Haonyeshi kama atatafuta mwingine ambaye ataweza kubadili mawazo yake kuhusu kuoa.hata kama mnakaa pamoja na mnapendana sana , lakini hatafunga ndoa. Ina Maana Gani Anaposema Muda Wa kuoa Bado. Huyu ni aina nyingine tena.Anasema muda bado, anakuwa na sababu nyingi.Kama hali yake ya maisha haijakaa sawa, hajajenga nyumba, hana gari, na sababu kibao. Mwanaume huyu hana tatizo katika kuoa , Ila wakati bado , hataweza kuoa wakati unaotaka wewe, hata kwa sababu zipi hataweza. Unachotakiwa kufanya ni kumwamini anachokisema. Sababu zake hazina msingi. Kitu cha msingi ni Ukweli anaokuambia.Inaumiza lakini ndio ukweli.Inavunja moyo lakini ndio ukweli, Amini hilo na itaokoa muda wa kwako kusubiri.Na wakati huo huo utakuwa unafanya maamuzi ya kusubiri, kukubali jinsi ilivyo. Lakini kumbuka kuwa ndoa ni kitu cha muhimu sana. Wanaume wanaosema hawataoa huongea ukweli.Kama anakuambia hatakuoa Amini tu. Wanaume wanajua ni mwanamke wa aina gani atakayeishi nae maisha yake yote, uwe makini asije akawa anakutumia huku ana mipango yake .Yapo mambo wanaume huyapenda kwa mwanamke, vile vile yapo mambo ambayo wanawake wanapenda kwa mwanaume. Kama unaona unamlazimisha jambo fulani hataki , kuwa makini. ... Read More
UNAJUA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO????  Kama inavyoeleweka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la "Tantric Sex." Kama inavyoelewaka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la “Tantric Sex.” As if hii duinia, especially hii century haiko overloaded na information kuhusu mambo ya mapenzi, jinsi ya kufanya mapenzi and whats hot in the bedroom, whats in and whats not. So, lately nimeona a lot of tzmoms readers wamekuwa wakitembelea sana na kusoma page ya “mapenzi baada ya ujauzito” na “kufanyamapenzi wakati wa ujauzito.” And I thought well, writing about Tantric Sex will be nyongeza kwa kila mmoja, aliye mama na mbaye bado damu inachemka katika mambo ya mapenzi. Anyhu, kama “SEX/MAPENZI” yangekuwa yanaweza kuyu-nite the world/countries/makabila/people I think hii fani ingeshinda. Well, so kama umeshawahi kujifungua ama kama wewe ni mama, you definitely understand ni jinsi gani ni vigumu kuwa upbeat kuhusu mapenzi ama kumfurahisha mumeo/mpenzio everyday. Well, once in a while maybe but not everyday. Ila kama we ni mdada/binti ambaye hujazaa bado well, damu yako bado inachemka so energy bado ipo nyingi ya kukurupushana na mpenzio. Having said that, si maanishi mtu ukishazaa ndo fani ya kuenjoy mapenzi imekwisha but nguvu zinapungua for sure however, kuna vitu vingi tuu ambavyo vinaweza kusaidia kuleta nguvu ya kutaka kukurupushana chumbani lol. Kukosa nguvu/energy to wanna work it all the time its not because mwanamke ni mvivu but hutokana na kuwa na mambo mengi sana ya kutend nyumbani i.e. kuhakikisha watoto wako taken care of, labda kazini pia unahitajika, etc una kuta hupati muda wa kujifurahisha mwenyewe ama na mpenzi wako. Therefore, mara nyingi before you know mupenzi anaanza kulalamika or hata mwanamke mwenyewe unaweza kufeel like you are not doing enough so mambo ndo hivyo yanaanza kwenda south chumbani. Hivyo basi, lets dig in tuone Tantric Sex inatoa msaada wa aina gani ili kurevamp mapenzi. Kwanza kabisa, FYI tantric sex can be weird at the beginning ila nitajitahidi kutoingia so indepth ili kusave miyoyo ya watu wengine. Kwamaana hii ni soft porn “according to me.” Lol. so usishtuke ama kushangaa sana. Well, anythign “sex” can be unconfortable anyways. Okay, so, kwanza kabisa, with Tantric Sex, mtu na mpenziwe wanatakiwa kuwa; SPIRITUALLY CONNECTED (usishtuke sio kidini lol).. Hii inamaainisha kwamba wewe na patner wako kwa pamoja mnajua mnataka nini emotionally and physically. Kwa kufanya hivi inasaidia kuwafanya kwa pamoja kuwa “FREE” na kuondoa wasiwasi wa labda mwenzangu atanijudge kwamba labda mimi ni malaya ama fuska etc. In other words hii process inaitwa “Dropping the Veil, between “Self” and “Other/patner.” THE ENVIRONMENT/mazingira. Wakati mnapractice tantric sex of course, just like when you are in the bedroom unaweza ukavaa lingerie/kuo za ndani zinazovutia or “kuwa kama mlivyotoka tumboni mwa mama zenu” (you know what i mean). Tatu, wapenzi wanaanza kupapasana lol, but in a way kwamba you are feeling the energy of the other person. Na hii energy unaweza kuifeel kwasababu mko free hamna anayemjudge mwingine/there are no worries. You are just in your own created world. Nne, wakati wa kufeel energy ya mwingine lazima wapenzi wawe wana pumua heavely yaani just feeling every move made but the other person mpaka mnapofikia mahali were you are breathing so hard and you are feeling each other. then you start kissing the lips, and then deeper for minutes even hours. Then mengineyo yanaweza kuendelea. So, all this time kumbuka its not about going straight into sex with your partner rather its about getting high by touching and feeling connected with each other. hivyo basi, once in a while take that time and revamp your intimacy, dress good, feel sexy and heey have fun!!. By 🅱 ... Read More
AINA 10 ZA WANAUME AMBAO WANAWAKE HUJUTIA WAKIWA NAO  1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband). HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea. 2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake. 3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband). Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke. 4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband). Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida. 5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband). Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao. 6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband). Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena. 7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband). Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa. 8. Mume Mtalii (Visiting Husband). Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto. 9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke. 10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband). Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: