Home → ushauri
→ Mbinu za kufufua penzi lenu
1. Badilisha mavazi yako .
Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako.
Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo.
Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile.
2. Hamia nyumba mpya
Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako.
Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja.
3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala.
Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako.
Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo.
4. Omba msamaha nawe umsamehe.
Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa.
Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako
Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu.
Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa.
5. Endeni mjivinjari kwa tarehe
Endeni likizo au tokeni nje pamoja.
Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja.
6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana.
Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana.
Jiulize mbona watu huangalia picha hizi?
Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?.
Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe.
Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua?
Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu.
Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi.
Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake.
7. Jisalimishe upya
Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu.
Je unampenda kama awali?
Je unanipenda kweli?
Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu.
Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao.
8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba.
Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee .
Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika.
9. Epuka kuumiza mwenzako
Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako.
Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda.
10. Mbusu mpenzi wako zaidi.
Mabusu huleta watu pamoja.
Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi.
11. Omba
Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu.
Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu.
12. Tenga wakati wa Faragha
Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako.
Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini
Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane
Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda .
Ni muhimu sana.
13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani.
Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe.
Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako.
14. Weka teknolijia mbali
Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo .
Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ?
Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe .
Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ?
Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia .
15. Chezeni pamoja
Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba.
Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani !
Chezeni miili yenu ikigusana!
16 Kaeni msemezane
Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ?
Unamwambia nini kitandani ?
Unazungumzia kuhusu madeni yako?
Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye .
17. Andikianeni barua za kimapenzi.
Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako.
18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu
Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja.
Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!!
Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu.
Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu
19.Nunua marashi mapya
Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe.
20.Jiachilie
Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio
Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi
Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba
Mchezee shere
Mtanie mpenzi wako
Mbinu za kufufua penzi lenu 1. Badilisha mavazi yako . Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako. Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo. Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile. 2. Hamia nyumba mpya Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako. Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja. 3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala. Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako. Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo. 4. Omba msamaha nawe umsamehe. Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa. Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu. Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa. 5. Endeni mjivinjari kwa tarehe Endeni likizo au tokeni nje pamoja. Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja. 6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana. Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana. Jiulize mbona watu huangalia picha hizi? Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?. Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe. Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua? Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu. Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi. Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake. 7. Jisalimishe upya Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu. Je unampenda kama awali? Je unanipenda kweli? Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu. Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao. 8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba. Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee . Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika. 9. Epuka kuumiza mwenzako Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako. Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda. 10. Mbusu mpenzi wako zaidi. Mabusu huleta watu pamoja. Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi. 11. Omba Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu. Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu. 12. Tenga wakati wa Faragha Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako. Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda . Ni muhimu sana. 13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani. Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe. Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako. 14. Weka teknolijia mbali Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo . Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ? Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe . Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ? Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia . 15. Chezeni pamoja Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba. Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani ! Chezeni miili yenu ikigusana! 16 Kaeni msemezane Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ? Unamwambia nini kitandani ? Unazungumzia kuhusu madeni yako? Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye . 17. Andikianeni barua za kimapenzi. Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako. 18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja. Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!! Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu. Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu 19.Nunua marashi mapya Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe. 20.Jiachilie Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba Mchezee shere Mtanie mpenzi wako
Artikel Terkait
NJIA RAHISI 13 ZA KUWA NA FURAHA KILA SIKU  Mabadiliko yalio mepesi kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka Umejikuta uko kwenye siku tofauti, story hizo hizo, imekuwa ni kawaida yako? Basi muda huu , sio kesho , sio wiki ijayo, ni wakati wa kubadilisha historia yako. ni za haraka, rahisi na hazina gharama unapofanya hivyo na matokeo yatakupa furaha unayoitaka. 1.Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku. Kulala usingizi wa kutosha unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala, usitumie chakula kingi wakati wa jioni. 2.Amka mapema , dakika 30 kabla . Kama wewe ni mfanya kazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako. 3.Meditate. Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na hutachanganyikiwa na kazi zako. 4.Jipe nafasi wengi wetu huwa tunajaza vitu nyumbani, ofisini hata vile ambavyo havina kazi, hatuvitumii. inaharibu mfumo mzima wa akili yako, hisia zako, na mwili wako. Ondoa vitu ambavyo huvitumii, tupa nje au gawia watu ambao wanahitaji kuwa navyo, hali yako ya furaha itaboreka. Na hutalemewa na kazi nyingi. 5.Jifunze kitu kipya Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hio ndio changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa sharp. 6.Tembea mara kwa mara Kutembea kwa dakika 30 kwa siku moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira, hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi . 7.Usijihusishe na mambo ya mitandao. Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya. 8.Kuwa mwema. Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri. 9.Kaa na watu wenye furaha. Angalia watu unaoshinda nao, unaofanya nao kazi, ni watu wa aina gani. kwa sababu kuna msemo unasema kuwa ukikaa na ua rose utanukia hata kama ulikuwa hunukii. Fanya hivyo na utaweza kufungua mlango mpya kwa ajili yako maishani. utaiona furaha ikitiririka kama mto. 10.Don’t gossip. Kuseng’enya, umbeya, itakusababishia maradhi ya misongo na kukosa furaha. mtu mmbeya hawezi kusaidia kitu. wakati mwingine jitenge na watu kama hawa, au unapoona kuna kutoelewana na wafanya kazi wenzako, jaribu kutulia kwanza , badilisha negative to positive. Sema kitu kizuri kuhusu mtu. ni vizuri. kwa sababu utajiwekea alama nzuri kwako. 11.Tumia muda wako na watu unaowapenda Unapoongea na familia au marafiki kwenye simu , inatia moyo. mawasiliano hayo yanakupa afya na furaha.Fikiri ilivyo vizuri kama utaenda kula na rafiki yako mahali fulani, au kuamua kupika nyumbani , au kucheza na watoto wako kitu kama game, mpira, inafurahisha. 12.Journal Kuandika vitu vya kufanya kwa siku, au kuandika vitu unavyotaka kuvipata, Lengo hili dogo litaongeza IQ yako na kuleta utulivu wa kuboresha ujasiri wako, ukiwa na tabia hii kila siku , furaha haitakosekana kwako na utapata faida ya akili na hisia zako zitakuwa bora. 13.Jizoeze kujijali. Unapojijali ,Utaona faida zake, pamoja na kuondoa stress na wasiwasi, utakuwa mtu wa kuwaza mazuri na utaboresha immunity.pata muda kila siku kufanya kitu kwa ajili ya furaha, kama vile mazoezi, kupika chakula kizuri, kusoma . utaanza kushangaa jinsi ilivyo rahisi kuwa na furaha unapojijali na utaboresha akili yako na mwili wako, na roho yako. Kama unavyojua , kuna njia nyingi zinazotushambulia kwa siku, Ondoka mahali ambapo panaharibu ratiba yako. sasa, kama kitu kingine chochote,mafanikio ni kufanyia kazi. kwa hio pick one, and let the fun begin! ... Read More
Kwanii Wanaume Waaminifu Kwenye Uhusiano Huachwa.....  Kuachwa na mpenzi kwa sababu umekuwa ni muaminifu sana yaonekane ni jambo lisiloingia akilini lakini linatokea. Moja ya mambo ya ajabu unayoweza kuwa ushawahi kuyasikia ni kwamba mara nyingine uamuzi wako wa kuwa mwanaume mwema sana na unayejitahidi kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uwe mzuri muda wote unaweza kukugharimu na kujikuta unaachwa kabisa. Haitakiwi kuwa hivyo lakini mara nyingine inatokea, na inatokea kwa sababu wazo la mwenza wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi laweza likawa tofauti na ulionao wewe. Wengine wana mawazo hasi kuhusu jinsi uhusiano/ndoa inavyotakiwa kuwa. Hii ndio sababu hutakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye na vipaumbele sawa na vya kwako au asiye na mtazamo mmoja wa kimaisha kama ulionao wewe. Usipozingatia hilo, utajikuta unaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hatakujali vya kutosha kwakuwa labda humfokei au kumpiga anapokukosea – au utajikuta ameshakupanda kichwani na kuanza kukudai mambo ambayo huwezi kuyatimiza lakini ukajikuta unajitutumua kumtimizia kwa sababu unataka kumfurahisha mpenzi wako na analijua jambo hilo. Kwa sababu baadhi ya wanaume wanapenda kulinda siri na kuwaachia uhuru wapenzi wao, wanajikuta wakiwapa ruhusa wanawake zao kwenda popote wanapojisikia bila kuwafatilia wanachofanya. Nini kinafata baada ya hapo? Mwanamke anatoka, anatafuta mchepuko na kukusaliti. Mwisho inakufanya wewe mwanaume uonekane mjinga mbele ya wengine. Tatizo ni kwamba tabia hii inaibuka kutokana na mazoea ya watu kuingia kwenye uhusiano wakiwa wameficha tabia zao halisi na kuja kufungua makucha yao baada ya kuona ameshaishi na wewe kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi tena kumuacha. Hii inasababisha wanaume walioathirika kutokana na tabia kama hizi kutoka kwa waliokuwa wapenzi wao wasiweze kuwaamini wanawake wengine tena kwa kuona kwamba wote ni sawa na wale waliowaumiza na kusababisha wasiweze kuwaonesha wenza wao wapya mapenzi kwa kiwango cha juu wakihofia kuumizwa tena. Kuwa mpole, mkarimu na mwenye upendo wa hali ya juu kwa mpenzi wako ndio jambo linalotarajiwa kwenye uhusiano. Mtu hatakiwi kufanywa ajisikie vibaya kwa kumuonesha mapenzi ya kweli mwenza wake. Kama wewe unakuwa muaminifu na mwema kwa mpenzi wako lakini umekuwa unadharauliwa au ukaachwa kutokana na tabia hiyo, kaa ukiwa na amani kabisa kwamba lawama za kuvunjika kwa uhusiano huo hazikuhusu wewe – lawama ni za mpenzi wako aliyeshindwa kujua wewe umekuwa mwema kiasi gani kwake. ... Read More
NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?  Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu. Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile. Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…...... Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo. Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani. Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish. Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye. Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni? Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala . Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu. Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali. Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake? Ushauri tafadhali........... ... Read More
Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa njia 10 muhimu  Mwanamke ni kiumbe anayependa kuonyeshwa mapenzi kila wakati. Kumtongoza mwanamke kunaweza kuwa kazi ngumu sana usipozingatia mambo kadhaa muhimu. Ukitaka kuweza kumtongoza mwanamke lazima ujue anachotaka yeye. Waweza kushangaa kwamba wanachotaka wanawake ni vitu vidogo ambavyo waweza timiza ili kuweza kumfanya akukubali hata kuzungumza na wewe. Waweza kumtongoza mwanamke ukizingatia mambo yafuatayo Msikilize mwanamke unayemtongoza Wanawake hupenda mtu ambaye anawasikiliza kwa kila jambo wanachosema. Ni muhimu unapopatana na mwanamke sharti uwe makini na anacho simulia. Kuwa mtu ambaye anauliza maswali na anaye taka kujua zaidi juu ya huyu mwanamke. Muulize kazi anayofanya, anakoishi, na mwonyeshe kwamba unamsikiliza kwa kuuliza swali unapotaka ufafanuzi. Mwanamke huskia ako huru kwa mwanamme ambaye anamsikiliza kwa maana hii huonyesha mwanamume anamdhamini huyo mwanamke. Kwa kumwonyesha kwamba wewe una nia ya kujua mahitaji yake, kwa matendo yako, si maneno yako, kutakusaidia kumwonyesha kwamba wewe ni mtu anayeweza kuwa naye maishani mwake. Kuweka kipaumbele mahitaji yake na kumsikiza kutakusaidia kwa kumtongoza mwanamke huyo. Mwanamke hupenda mtu mwenye kujiamini Unapomwongelesha mwanamke lazima uwe mtu mwenye kujiamini. Ujasiri na kujiamini ni kitengo kikubwa kinachofafanua mwanamume. Unapomwongelesha mwanamke lazimi uonyeshe ujasiri mbele yake. Kama Warren Farrell, Ph.D., anavyosema “Jambo linalomvutia mwanamke kwa mwanamume ni mwanamume mwenye ujasisiri”. Ujasiri utamvutia mwanamke kwa kujua mwanamume anazungumza na kujibeba kwa ujasiri. Mwanamke hupenda kuwa karibu na mwanamume anayevutia Kuvutia kwa mwanamume huja kwa njia kadhaa. Mwanamke hupenda mwanamume ambaye hachoshi kwa hadithi zake, ni mcheshi, anachangia kwa mazungumzo kati yao na anaye hakikisha kwamba mwanamke anajiskia huru kwa maongezi. Kama mwanamume, hakikisha unatoa mifano inayoendana na maongezi mliyo nayo. Hakikisha mnayoyaongelea yanachangiwa na nyinyi wawili. Mwanamume aliemcheshi na mwenye kumvutia mwanamke kwa anavyoendeleza mazungumzo ndie aliye na nafasi kubwa ya kumpata mwanamke anayetarajia ama aliye na hamu naye. Kumbuka kwamba usiwe ni wewe pekee unayeongea, mwachie pia mwanamke achangie pia. Ukizingatia haya, mwanamke hujiskia yuko huru nawe na anaweza ongelea chochote. Mwanamke hapendi mtu mwenye haraka Haraka hapa ina maana, kwa kutongoza mwanamke lazima uwe mtu mwenye subra sana. Kinachomfanya mtu awe na hamu ya kuwa na mwingine ni matarajio anayopata rohoni. Unapopatana na mwanamke kwa wakati wa kwanza, usimwonyeshe kwa umbele unachotaka, lakini taka kumsikiliza, mjue jina, anachofanya kazini, na mambo mengine kwanza. Kwa kufanya haya mwanamke ataona kwamba unahamu naye na kwamba atajiskia wa maana kwako. Jambo hili litakusaidia sana kwa kutongoza huyo mwanamke. Kitu cha muhimi ni kwanza upate kuwa marafiki na mwanamke yule ili uweze kupata nafasi nzuri ya kumtongoza. Ubinafsi wa kipekee Mwanamke hupenda vitu vya kipekee sio vitu vinavyoigwa kwingine. Usije ukafanya ama ukanena kama mwanamume mwingine ili kumshinda huyo binti. Kuwa na ubinafsi wako, fanya mambo yako kwa kipekee. Kuiga wengine hakutakusaidia kwani mwanamke atakuona kama mtu asiyejiamini. Mwanamke hupenda manamume ambaye ni tofauti na wanaume wengine ambao amewahi kutana nao hapo mwanzo. Ni vizuri kuwa na vitu ambavyo ni vya kipekee kwako. Kama sauti yako, vile wacheka vile wamtizama mwanamke yule, vile wavaa, vile umejipaka manukato mazuri. Upekee huu hukupa nafasi ya mbele kwa mpango wako wa kumtongoza mwanamke yule. Mavazi na usafi Mwanamke hupenda usafi sana. Ukitaka mwanamke aweze kuvutiwa nawe lazima uvae vizuri na uwe safi. Kuvaa vizuri, nguo zinazokufanya upendeze huwa njia moja ya kuvutia wanawake. Pia kuwa makini na usafi. Kuoga vizuri, kujipaka manukato yanayo vutia, kuweka nywele, nguo safi husaidia sana kwa kukupa ujasiri wa kumwendea mwanamke uliye na hamu naye. Sio lazima uvae mavazi ghali, lakini valia kwa kupendeza. Mwanamke hupenda mtu anayejiamini katika alichovalia. Muziki Kwa miaka mingi muziki umejulikana kuwa chombo cha kuonyesha mapenzi ama kama namna ya kumtongoza mwanamke. Mwanamke hupenda kuonyeshwa kwamba ni mtu wa thamani kwa mwanamume. Muziki waweza kukusaidia kuweka mazingira yenye utulivu na yenye riwaya ya mahaba. Kumbuka kumzingatia wakati unaweka muziki ule, jua mbeleni muziki anaopenda na fanya hima kwamba unamtumbuiza na aina hizo kwa kikamilifu. Ukifanya hivyo, mwanamke ataoona kwamba unathamini. Weka muziki wenye utulivu, wenye mahaba na wenye kumsifu mtu wa kike na uzuri wake kwa kumwonyesha mapenzi. Bidii ya kuwa makini kwa mwanamke na kumpa pongezi wakati wowote Mwanamke ni kiumbe anayependa kusifiwa na kupongezwa sana. Kwa mwanamume ni muhimu kwamba kwa kumtongoza mwanamke, kumbuka kila wakati kumpongeza kwa kuvaa kwake, nywele, viatu, anavyong’aa. Ni muhimu kumwonyesha kwamba umefurahia bidii yake ya kuvaa vyema na kuhakikisha anakaa vyema mnapokutana. Mwanamke hujiskia mwenye thamana sana kwa kujua kwamba kuna mwanamume amemwona anakaa sawa. Mwambie wapenda alivyosongwa, anavyotoa busu, anavyocheka, na kila kidogo anachofanya. Utashangaa kwamba yaweza onekana ni mambo madogo lakini huchangia katika kutongoza mwanamke. Mpikie chajio mwanamke unayemtongoza Kama mwanamume hakuna kitu cha muhimu kama kumpikia mwanamke uliye na macho kwake. Mwanamume ajuaye kupika huwa anawavutia wanawake sana. Unaweza kumwalika mwanamke kwako ka chajio. Fanya hima ukajua chakula anachopenda binti unaye mtarajia, ukahakikisha umepika chakula kitamu na kinachovutia kwa kuangalia na harufu tamu. Mwandalie mezani pamoja na kinyuaji. Kuwa umehakikisha kuna mazingira yenye utulivu na pia weka mziki wenye mahaba. Mwanamke hujihisi mwenye thamani sana. Hapa utakuwa umejiongezea pointi kadhaa kwa mpango wako wa kumtongoza binti yule. Zawadi Kila mwanamke hupenda kupata zawadi wakati wowote. Kama mwanamume itakusaidia pakubwa kwa mpango wako wa kumtogoza binti yeyote. Zawadi zaweza kuwa tofauti. Waweza mtumia maua ya waridi kazini, ukakumbuka kumtumia chokoleti wakati wa wapendanao, ukamtumania kahawa asubuhi akiingia kazini. Kwa kufanya vile, mwanamke hujiskia wa dhamana na anayependwa. Wanawake pia hupenda kupelekwa mahali pa zuri ambapo anaweza kujibinjari. Mpeleke densi, mpeleke mahali mkala chajio, mpeleke mbugani kwa wanyama ama kwa safari. Kufanya vile kutakupatia pointi nyingi kwa mtazamo wako wa kumtongoza mwanamke yule. Kama kawaida wanawake na wanaume huwa na hamu ya kujuana na kuishi maisha pamoja. Katika kumtongoza mwanamke lazima kwanza mwanamume afahamu nini mwanamke yule anachopenda. Pia inabidi mwanamume pia kumpa sikio binti yule wakati wowote wanapozungumza na kuuliza mwaswali asipoelewa kitu. Mpe wanamke pongezi wakati wowote mnapopatana, mpe pongezi kwa kusukwa vizuri, kupaka kucha vizuri, kuvaa nguo vizuri, tabasamu lake na anavyocheka. Mara kwa mara mpe zawadi za hapa na pale. La muhimu sana ni mwanamke huvutiwa na mwanamume anaye jiamini. Ukiwa mwanamume ambaye anajiamini, itamfanya mwanamke yule kujiskia huru kuwa karibu nawe na hio itakusaidia katika hali ya kumtongoza. ... Read More
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: