Home → ushauri
→ Wanawake: Aina tatu za wanaume wasiostahili muda wako
Utajuaje kuwa tunda moja kati ya mengi limeoza bila kulionja? Tuliongea na wanawake waliokiri kuwa wanaume wazuri wapo, ila kuna wengi wanaofaa kuangaliwa tu bila kuguswa au hata kupewa nafasi ya kujieleza. Hizi ndizo aina tatu za wanaume unaofaa kuwatupilia mbali.
#1. Kasuku
Huyu ni aina ya mwanamume asiyekosa kitu cha kusema, bora tu apate anachokitaka. Wengi kati ya hawa huchukia wanawake na dhamira kuu huwa kuwatumia na kuwaacha. Mwanamke mmoja alisema kuwa aligundua kuwa Mumewe alikuwa na tabia ya kuwaeleza wenzake kuhusu yanayoendelea chumbani mwao ili ajipadishe hadhi.
#2. ‘Mtoto wa Mama’
Wengi kati ya hawa wana shida hata ya kutafuta kazi na wanataka kufanyiwa kila kitu. Usishangae akitaka kulishwa na kunyweshwa kila anapotaka. Wanawake kadhaa tuliowahoji walikiri kuwa wamewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wanaume wa aina hii.
#3. Mjua yote
Habari zote za mjini wanazijua. Jirani akipigwa kofi, ‘mjua yote’ ataiweka kwenye mukhtasari mpaka kitandani.
Unakubaliana na maoni yao?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: