Home → ushauri
→ AINA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA SANA NA WANAUME
WAPENDA USAWAAina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi niwanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu yakifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamiikwa asilimia 50 kwa 50
WANAOJUA MAPENZIWanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwasita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaumebila kujali sifa zao za nje au za ndani
MARAFIKI Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani
WAPENDA UWAZI Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwakisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hiiwamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katikauelewa wa mambo.
WANAOJITEGEMEA Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leohawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza stareheza upande mmoja.
WASIO NA PRESHANikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vituvitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi
MARIDADI Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafina kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano.
WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwawanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzikwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutokajuu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke
WA MMOJA Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kilaaina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziadazaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
AINA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA NA SANA NA WANAUME WAPENDA USAWAAina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi niwanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu yakifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamiikwa asilimia 50 kwa 50 WANAOJUA MAPENZIWanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwasita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaumebila kujali sifa zao za nje au za ndani MARAFIKI Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani WAPENDA UWAZI Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwakisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hiiwamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katikauelewa wa mambo. WANAOJITEGEMEA Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leohawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza stareheza upande mmoja. WASIO NA PRESHANikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vituvitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi MARIDADI Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafina kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. WANAORIDHIKA Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwawanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzikwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutokajuu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke WA MMOJA Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kilaaina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziadazaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.
Artikel Terkait
MAMBO 10 AMBAYO NI SUMU KATIKA MAPENZI  KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi. Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi. 1. WIVU WA KUPINDUKIA Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi. Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu. 2. KUTOMWACHIA NAFASI MPENZI Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi. Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha. 3. KUMWAMULIA MPENZI MAMBO YAKE Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia. Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako. 4. KUMUULIZA MPENZI MASWALI Iwapo utajikuta ukimuuliza mpenzi wako maswali mengi yanayoonesha wasiwasi wako kuhusiana na mwenendo wake, fahamu kuwa kuna tatizo na tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi utakuwa mwanzo wa mwisho wa uhusiano wenu. Mwanamke angependa umuulize maswali ya kawaida kuhusiana na jinsi siku yake ilivyokuwa na kama marafiki zake hawajambo au la, lakini kila jambo lina mpaka wake. Mwanamke hatarajii kuwa kila mnapokutana atakuwa kama ameingia kwenye chumba cha mtihani au usaili wa kazi. 5. KUTOAMINI ANACHOKWELEZA MPENZI Wakati mwingine watu hushindwa kuwaamini wenzao, lakini kwa sababu ambazo ni za msingi, lakini kuna wakati ambapo mtu hushindwa kumwamini mwenzake bila sababu yoyote ya msingi, au kwa sababu zisizo sahihi, kisingizio kikiwa ni mapenzi. Kuna tatizo la kisaikolojia la kujishuku au kuwashuku wenzako. Hili ni jambo ambalo linaweza kukuharibia mustakabali wako katika mapenzi, maana husababisha kujengeka kwa mazingira ya kutokuaminiana. Ili uweze kwenda sanjari na mpenzi wako, amini kila anachokweleza hadi pale utakapokuwa na sababu za msingi za kutokumwamini. Na hata unapokuwa umelithibitisha jambo, endelea kuwa katika uhalisia wako. 6. KUACHA HOBI, MARAFIKI Mahusiano ya kimapenzi mara nyingi huhusisha kila mmoja kuacha baadhi ya mambo yake kwa ajili ya mwenzake. Hata hivyo, lengo ni kuweka tu uwiano wa mahitaji, si kuacha kila kitu ulichokuwa nacho kwa ajili ya mwenzako, ama kwa shinikizo, au kwa kulewa penzi. Iwapo utabaini kuwa marafiki zako sasa wamekuwa ni marafiki zako wa zamani na hobi zako zimebaki tu katika kumbukumbu japo kwa hakika bado unahisi mapenzi katika hobi hizo, basi tambua kuwa huyo mrembo wako amekunywesha sumu ya penzi na sasa huwezi hata kuitumia vema mantiki yako. Mbaya zaidi, iwapo utabaini kuwa marafiki zako wapya ni marafiki wa siku zote wa mpenzi wako na hobi zako ni zile za mpenzi wako, basi tambua kuwa huna tena nafsi yako, bali umejisalimisha mzima mzima kwa mpenzi wako. Lakini msemo mmoja wa hekima unatwambia usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Yamkini unaelewa. 7. KUKUBALI KUPELEKESHWA Pengine unakumbuka kuwa kuna nyakati ambapo ulikuwa na uwezo wa kujikita katika jambo moja na kulifanya kwa umakini, huku ukiwa pia mwerevu, mjanja na unayejisimamia, lakini leo unayeyuka kirahisi tu kama barafu iliyowekwa juani! Hii ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako. Mbaya zaidi ni pale utakapoiacha kazi yako inayokulipa vizuri na kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako. Ukifika hali hii ujue wewe mwenyewe kuwa hapo hakuna mwanamume. 8. UTAYARI WA KUFA KWA AJILI YAKE Umewahi kujisikia kuwa na utayari wa kufa kwa ajili ya mpenzi wako? Kama jibu ni “ndiyo”, basi fahamu kwa hakika kuwa hayo uliyo nayo si mapenzi bali ni upumbavu. Pengine huku ndiko kunywesha sumu ya mapenzi. Kwa hakika, hakuna mwanamke ambaye anastahili kumfanya mwanamume yeyote kufa kwa ajili yake. Yamkini wanaume wanaolengwa katika makala haya si wavulana wanaosoma sekondari, waliobalehe majuzi, ambao wakipenda au kupendwa hujiona kama wako katika sayari yao. Mwanamume aliyepevuka hujiamini na hayaweki maisha yake yote mikononi mwa mwanamke, hata kama mwanamke huyo angekuwa ndiye mrembo wa dunia. Iwapo, ama kwa ujinga au kwa kufahamu umewahi kumwambia mpenzi wako: “Ukiniacha nitajiua,” na ukawa unaamini hivyo kabisa, basi yamkini unahitaji kutafuta msaada wa ushauri nasaha, maana kwa hakika umepotoka. 9. MUDA WOTE UNAWASILIANA NAYE Vijana wa siku hizi ni watumiaji wazuri sana wa simu, lakini iwapo utabaini kuwa asilimia kubwa ya muda wako unautumia ama kwa kuongea au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi na mpenzi wako, basi fahamu kuwa kuna tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka. Kumbuka kuwa mapenzi hayachukui nafasi ya kila kitu. Yamkini huyo mpenzi wako amekukuta unaishi na kuna mambo ya muhimu ya kufanya. Hebu achana na simu kwanza ufanye mambo ya muhimu kuhusiana na maisha yako. Kama mpenzi wako hakwelewi katika hili basi hakufai. 10. NDUGU ZAKE WANAKUFUATILIA Iwapo utabaini kuwa marafiki, ndugu na jamaa za mpenzi wako wanamtonya mpenzi wako kuhusiana na kile wanachokiita mwenendo wako mbaya, usipuuze hali hii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu hawa wanayo sababu ya kuwa na wasiwasi na mwenendo wako, kwa hiyo jichunguze na kuangalia jinsi unavyoenenda. Hata hivyo, jambo hili si ishara njema ya mustakabali mwema wa uhusiano wenu. Iwapo mpenzi wako ataweka watu wake wakufuatilie, maana yake halisi ni kwamba hakuamini. Katika hali kama hii, haitarajiwi kuwa mustakabali wa uhusiano wenu utakuwa mzuri, kwani kutakuwa na uingilizi mwingi wa ndugu, jamaa na marafiki zake. Unaweza kukubali kuendelea kuishi katika hali hii kwa kisingizio cha mapenzi, lakini ukweli ni kwamba hayatakuwa mapenzi bali karaha. KUWA MAKINI Kama unavyoona, hizi ni baadhi tu ya dalili kuwa mapenzi yako kwa mwanamke sasa yanaelekea katika ulevi, mithili ya ule wa dawa za kulevya. Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kweli mapenzi ni kitu kizuri, lakini pia mapenzi yanahitaji kuwa jambo linaloashiria mustakabali mwema kwa wahusika wawili. Yakiwapo mambo haya kumi hauwezi kuwapo mustakabali mwema katika mapenzi. ... Read More
Mimba kuharibika na Sababu zake  Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu. Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba. 1.Mama anapokuwa na matatizo uvimbe (fibroid), huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara. 2. Uzito mkubwa (unene) Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda. 3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika. 4. Utoaji mimba Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba. 5. Matumizi ya Pombe,Sigara Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo. 6. Magonjwa sugu Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia. ... Read More
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu.  Dalili 8 zitakuonyesha kama upo kwenye mahusiano ya kudumu au hapana. Afya. Wote tunafikiria kuhusu hili. hasa kwa kadri tunavyoendelea kukua , tunatembelea madaktari, tunakula vizuri wakati mwingine. Tunatafuta dalili na wakati mwingine matokeo yake yanatuambia kuwa hali zetu sio nzuri. Lakini tunapofikiria afya, tunafanya hivyo katika miili yetu tu. mara nyingi tunasahau kufikiria kuhusu afya ya mahusiano na mapenzi. Tunaangalia zaidi afya ya mwili katika maisha ,lakini kuwa na afya nzuri katika mahusiano ni vitu vinavyoungana. Kwa kurahisisha , mahusiano mabaya hayadumu. au ingawa yanaweza kukaa kwa muda fulani.Na kama yakidumu , atakuwepo mtu wa kuumia. Lakini ni nini hasa afya ya mahusiano? Tutajuaje kama mahusiano yetu yatadumu? Utajuaje kama uko na mtu sio sahihi, mtu ambaye mtaishia kwenye kona fulani tu? Hakuna kipimo halisi cha kujua. Hakuna kipima joto kinaweza kupima kiasi cha muda wa mahusiano kuwa ni ya moto au baridi. Kwa bahati kuna hizi dalili 8 ambazo zinaweza kukusaidia kujua afya iliopo kwenye mahusiano yako. 1.Mchumba wako atakuwa na imani na wewe , na wewe utakuwa na imani naye.  Hataongea kwa ajili yake bali ataongea kwa ajili yenu wote. atakukumbusha pale unapokuwa umesahau au unapokuwa na mashaka kwa jinsi ulivyo. Ana maono ya wazi ya muhimu kwako. atalea hali hio na utaiona. Vilevile na upande wako utakuwa kama yeye. hutamsema vibaya kwa marafiki, hutalalamika kitu bali utaongea mbele yake. Utamwamini kuwa yuko kamili , mtu anayeweza kutatua matatizo na kusimama kwa miguu yake. Hata kama haujamsaidia kitu. 2.Unamwamini. Unamwamini katika ukweli wake wote. ahadi zake ni za kweli. utamkubali alivyo. Anahusika katika majukumu yake. 3.Unakubali mambo yake yaliopita na yeye anakubali ya kwako. Jinsi alivyokuwa, alikuwa na wanawake wangapi, wanaume wangapi. hutajali. utamkubali alivyo ili mkue pamoja. hutafikiria kitu chochote kilichopita, bali utakuwa na hamu ya kutaka kujua jinsi gani huyo mtu alivyo. Mahusiano yako yatakuwa yamekusanya, Msamaha na kuachilia yaliopita. 4.Unashukuru kwa vitu vizuri mlivyonavyo Unakubaliana na vitu vidogo vidogo anavyovifanya kwako. unakuwa na matumaini, husubiri kupata kazi, kwa ajili ya mshahara, kwa ajili ya mambo mengine. unashukuru kwa kile mlichonacho sasa na mwenza wako. Mnafuraha wakati huu. hana mchezo wa kijinga. anatengeneza pesa ya kutosha. anafanya kitu akipendacho. Utakuwa unalenga safari sio mwisho wa ndoa, mtoto, sherehe, vitu vinatokea kwa kawaida. 5.Mawasiliano ni ya wazi na ya kueleweka kwa kila mmoja. Hakuna wa kusubiri ni nani atamtafuta mwenzake. kila mtu anakuwa na jukumu la kufanya hivyo. Na kama itatokea mmoja hakuhusika , hakuna lawama, kwa kuwa mnaelewa . utavaa moyo wake. hutahangaika kuyatawala mahusiano kwa sababu hamfanyi mchezo wa kuigiza. 6.Maisha yenu ya sex yataendelea kuwa mazuri na ya kupendeza. Kwa sababu ya urafiki ambao mnao, maisha yenu ya mahusiano yatakuwa rahisi na ya kimapenzi. Ya ukaribu zaidi. sex itakuwa sio kipaumbele chenu bali ni matokeo ya upendo mlionao. mahitaji yenu ya kimwili yatatosheka kwa pamoja. 7.Utamuheshimu na yeye Atakuheshimu wewe. Kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzake na mnaweza kuhimizana katika kutimiza malengo yenu. kama unapenda kucheza , atakuhimiza kufanya hivyo. hutahitaji kukamilisha hisia zako zote. atakuwa na mahusiano mazuri na watu wengine pia. Ni mtu muhimu kwako. anakufanya ujisikie vizuri. 8.Malengo yenu yanafanana. Hutajaribu kumbadilisha. au kujaribu kuomba kuishi na yeye. hutahitaji awe mtu wa kutengeneza kitu chako. ni mtu ambaye ulimtaka awe wako. thamani yake ni muhimu katika maswali hata. Unataka watoto? Unapenda kusafiri? Una hamu ya kupata uzoefu fulani? unakubaliana katika mambo ya pesa? Una furaha unapokuwa naye? Unataka kuishi naye na kuwa naye chumba kimoja? Afya ya mahusiano yako ni muhimu katika maisha ya ndoa utakayoingia. Lakini hakuna kipimo cha kupimia uzima huo. Ni wewe tu na mwenza wako mnajua kama mahusiano yatadumu au yataishia kwenye kona. yatakuwa na matunda au hapana. Mttajua kama ni mazuri au sio. hizo dalili nane zikusaidie kufahamu kama ni ya afya au sio, yatadumu au hayatadumu. ... Read More
MADHARA YA MWANAMKE KUZAA MFULULIZO BILA KUPUMZIKA.  Ni wazi vifo vya uzazi vimekuwa vikisababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya mwanamke kuzaa mfululizo bila kupumzika hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja kwa wakuu wa mikoa ya kanda ya magharibi, kanda ya ziwa na kwingineko kuongeza juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi wake umuhimu wa kutumia njia ya uzazi wa mpango. Wakuu hao wana kazi ya kuondoa mila na desturi za wananchi wa ukanda huo ili waondokane na mila hizo zilizopitwa na wakati kwa kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango katika kuwezesha taifa kukua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi, Takwimu za nchi zinaonyesha kanda ya magharibi inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kuzaana na kufikiwa asilimia 7.1 ikifuatiwa na kanda ya ya kati na kufuatiwa na kanda ya ziwa hali hii pia inachangia ongezeko la vifo vya uzazi kwa wanawake kutopumzika. Kuna haja wananchi kuelimishwa kuwa matumizi mazuri ya njia ya uzazi hayana madhara mwilini ili waweze kuzaa kwa mpango na kupunguza vifo vya uzazi.  Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alizindua mpango mkakati ulioboreshwa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuwataka watendaji wake katika mikoa yote nchini, ambao ni wakuu wa mikoa kuwa wahakikishe wanapunguza vifo vya watoto na akinamama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: