Home → ushauri
→ MWANAMKE NI NANI (SIYO MSICHANA TAFADHALI)
Mwanamke ni binadamu wa pili kuumbwa na Mungu kutokana na ubavu wa Adamu.
-: Mwanamke ni yule ambae huijua thamani yake angali bado mdogo aidha kwa kufundishwa na wazazi wake au kwa utashi wake binafsi.
-: Mwanamke ameumbiwa mwanaume mmoja tu, mwanamke hatakiwi kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, hutulia na mwanaume mmoja hata pale mahusiano yake yasipoenda sawia, husubiri muda muafaka wa kupata mwanaume atakaempenda na sio kuwapanga foleni.
-: Hujua thamani ya mume wake na nafasi yake ya usaidizi kwa mwanaume wake.
-: Tumbo lake la uzazi li tayari kubeba mimba, nyonga zake zi tayari kupokea kashikashi za uchungu na kujifungua, Mikono yake na moyo wake u tayari kulea uzao wake.
-: Humnyonyesha mwanae na si kumpa maziwa ya kopo akihofia kuharibu maziwa yake.
-: Hufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo na kumhudumia mumewe.
-: Kwake tendo la ndoa ni hisia zaidi na hulifurahia afanyapo na yule anae mpenda na sio zawadi kwa vile amefanyiwa jambo fulani na mwanaume yeyote.
WASICHANA HUWA HIVI....
-: Wamewapanga foleni wanaume, wanaume za watu pamoja na wavulana mithili ya enzi za kupokea mishahara dirishani au kudraw pesa ATM mara baada ya kutoka.
-: Hawana muda wa kuwaza future, wao ni kuponda raha kufa kwaja.
-: Kucha zao zina thamani, kuliko hata nguo zao za ndani.
-: Kwao mwanaume ni kitega uchumi swadakta kabisa, ambacho kinahitaji ili kupata wakitakacho ni kuwekeza miili yao.
-: Hufanya ngono kwa kutegemea mrejesho wa pesa, kitu au ahadi walizopewa na watu wao..!
-: Hutumia muda wa dakika mbili kuoga lakini hutumia lisaa lizima katika kujiremba na kujipiga picha nzuri za kuweka Instagramu, facebook, Snapchat huku wakilembua macho na kutoa ndimi zao nje mithili ya nyoka aonae kitu au mwenye kiu...!
-: Miaka ikikatika na akifikisha umri wa miaka 30+ na bado bila bila, husema anahitaji mtoto tu na hana haja ya mume, lakini akiwa mwenyewe chumbani kwake, anajijua na nafsi yake jinsi anavyotamani maisha mema ya ndoa.
-: Utetezi wao mkubwa wao husema ndoa kitu gani, watu wanaoana leo na wanaachana kesho, pasina kujua kwamba Ndoa inahitaji msingi imara ikiwemo na uvumilivu na Mungu juu ya vyote.
NDUGU YANGU TAMBUA KUWA:-
Ni vigumu sana kushindana na asili, kuna wakati utafika na kusema bora ningefanya hivi. Amua njia ile iliyo sahihi ambayo kwayo unajiona hutakua na majuto nayo hapo baadae.
Siku zote kuna manufaa katika kusubiri, ila kuna majuto mengi katika kukurupuka.
Mungu awabariki 'wanawake' wote katika magumu yote mnayopitia akawafanyie wepesi, na pia awabariki 'wasichana' watambue ni nini wanapaswa kufanya, kwa wakati walionao na wajitambue na waweze huko waendako....!
KWA JINSIA YA KIKE...!
VIPI WEW NI MSICHINA AU MWANAMKE.......!?
PRINCE NAAHJUM ALSINA
MWANAMKE NI NANI (SIYO MSICHANA TAFADHALI) Mwanamke ni binadamu wa pili kuumbwa na Mungu kutokana na ubavu wa Adamu. -: Mwanamke ni yule ambae huijua thamani yake angali bado mdogo aidha kwa kufundishwa na wazazi wake au kwa utashi wake binafsi. -: Mwanamke ameumbiwa mwanaume mmoja tu, mwanamke hatakiwi kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja, hutulia na mwanaume mmoja hata pale mahusiano yake yasipoenda sawia, husubiri muda muafaka wa kupata mwanaume atakaempenda na sio kuwapanga foleni. -: Hujua thamani ya mume wake na nafasi yake ya usaidizi kwa mwanaume wake. -: Tumbo lake la uzazi li tayari kubeba mimba, nyonga zake zi tayari kupokea kashikashi za uchungu na kujifungua, Mikono yake na moyo wake u tayari kulea uzao wake. -: Humnyonyesha mwanae na si kumpa maziwa ya kopo akihofia kuharibu maziwa yake. -: Hufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo na kumhudumia mumewe. -: Kwake tendo la ndoa ni hisia zaidi na hulifurahia afanyapo na yule anae mpenda na sio zawadi kwa vile amefanyiwa jambo fulani na mwanaume yeyote. WASICHANA HUWA HIVI.... -: Wamewapanga foleni wanaume, wanaume za watu pamoja na wavulana mithili ya enzi za kupokea mishahara dirishani au kudraw pesa ATM mara baada ya kutoka. -: Hawana muda wa kuwaza future, wao ni kuponda raha kufa kwaja. -: Kucha zao zina thamani, kuliko hata nguo zao za ndani. -: Kwao mwanaume ni kitega uchumi swadakta kabisa, ambacho kinahitaji ili kupata wakitakacho ni kuwekeza miili yao. -: Hufanya ngono kwa kutegemea mrejesho wa pesa, kitu au ahadi walizopewa na watu wao..! -: Hutumia muda wa dakika mbili kuoga lakini hutumia lisaa lizima katika kujiremba na kujipiga picha nzuri za kuweka Instagramu, facebook, Snapchat huku wakilembua macho na kutoa ndimi zao nje mithili ya nyoka aonae kitu au mwenye kiu...! -: Miaka ikikatika na akifikisha umri wa miaka 30+ na bado bila bila, husema anahitaji mtoto tu na hana haja ya mume, lakini akiwa mwenyewe chumbani kwake, anajijua na nafsi yake jinsi anavyotamani maisha mema ya ndoa. -: Utetezi wao mkubwa wao husema ndoa kitu gani, watu wanaoana leo na wanaachana kesho, pasina kujua kwamba Ndoa inahitaji msingi imara ikiwemo na uvumilivu na Mungu juu ya vyote. NDUGU YANGU TAMBUA KUWA:- Ni vigumu sana kushindana na asili, kuna wakati utafika na kusema bora ningefanya hivi. Amua njia ile iliyo sahihi ambayo kwayo unajiona hutakua na majuto nayo hapo baadae. Siku zote kuna manufaa katika kusubiri, ila kuna majuto mengi katika kukurupuka. Mungu awabariki 'wanawake' wote katika magumu yote mnayopitia akawafanyie wepesi, na pia awabariki 'wasichana' watambue ni nini wanapaswa kufanya, kwa wakati walionao na wajitambue na waweze huko waendako....! KWA JINSIA YA KIKE...! VIPI WEW NI MSICHINA AU MWANAMKE.......!? PRINCE NAAHJUM ALSINA
Artikel Terkait
Mbinu za kufufua penzi lenu 1. Badilisha mavazi yako . Ikiwa bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako. Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo. Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile. 2. Hamia nyumba mpya Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako. Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja. 3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala. Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako. Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo. 4. Omba msamaha nawe umsamehe. Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa. Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu. Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa. 5. Endeni mjivinjari kwa tarehe Endeni likizo au tokeni nje pamoja. Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja. 6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana. Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana. Jiulize mbona watu huangalia picha hizi? Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?. Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe. Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua? Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu. Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi. Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake. 7. Jisalimishe upya Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu. Je unampenda kama awali? Je unanipenda kweli? Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu. Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao. 8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba. Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee . Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika. 9. Epuka kuumiza mwenzako Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako. Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda. 10. Mbusu mpenzi wako zaidi. Mabusu huleta watu pamoja. Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi. 11. Omba Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu. Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu. 12. Tenga wakati wa Faragha Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako. Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda . Ni muhimu sana. 13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani. Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe. Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako. 14. Weka teknolijia mbali Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo . Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ? Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe . Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ? Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia . 15. Chezeni pamoja Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba. Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani ! Chezeni miili yenu ikigusana! 16 Kaeni msemezane Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ? Unamwambia nini kitandani ? Unazungumzia kuhusu madeni yako? Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye . 17. Andikianeni barua za kimapenzi. Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako. 18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja. Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!! Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu. Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu 19.Nunua marashi mapya Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe. 20.Jiachilie Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba Mchezee shere Mtanie mpenzi wako ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
Wanawake: Mumeo akikukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana  Usiku kama mumeo kakukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana, hata malaika baraka hawawezi shuka kwenu. Huyo ulionae amezaliwa kwao kaja na tabia zake na wewe umezaliwa kwenu una tabia zako. Sasa ukitaka kila kitu kiwe wewe unavyotaka atakuwa mwanao tena huyo sio mumeo samehaneni kwa kila mnalofanyiana. Usiweke vinyongo tena ukajua unamkomoa mana unavyonuna ndo mchepuko unavopata chance ya kuwasiliana na si kila mwanaume anamchepuko wengine washkaji tu sasa ukijitia umenuna kisa umemuona kachat, sijui umekuta meseji sijui nini utakonda uzikwe na presha na unavyotiwa kaburini tu huku wenzio wanamtext pole kazi ya Mungu mpenzi. Gangamala mtoto wa kike sio kidogo kununa kama unga wa ngano ulokosa amira. Tabasamu njia nzuri na sahihi ya kumuua mtu akikosea ukatabasamu ataanza kutafuta mchawi kumbe mchawi mwenyewe, ataanza kutoka kujua kwanini hujakasirika atatulia tu akiamini anakuvizia kumbe anajivizia. ... Read More
SABABU YA KWELI WANAWAKE KUENDELEA KUTEMBEA NA WANAUME WALIO OA  Jane ni mwanamke mwenye mafanikio, anamiliki kampuni ya kutengeneza mifuko ya plastic, ana studio. Ana akili , anavutia na ni mwenye ujasiri. Pia anatembea na mume wa mtu. Amekuwa akiwauliza rafiki , familia yake ambao wanafahamu kuwa kitu gani kinamfanya mwanamke mwenye mafanikio, akili na ujasiri kutembea na mume wa mtu kwa miaka zaidi ya mitatu? Hamu ndio Inayoanza Mwanaume ambaye ameoa anapomkaribia mwanamke , anakuwa na hatari— hatari ambayo inaonyesha kumuhitaji zaidi. Kuwa na muda naye. Huenda kwa meseji au kupata chakula pamoja kwa siri, au kulala nae kwa siri. Huonyesha kuwa na majukumu kama mwanaume single. Lakini mwanaume single huandaa date. Huwa na sababu nyingi za kufanya hivyo, na ukiri wao huwa ni wa makini na huonyesha kuwa hawako interested. Hujikuta wameingia kwenye majukumu ambayo hakuwa amejiandaa. Kwa ushindani, kazi ya mwanaume aliyeoa Inamlinda kutokana na nia yake kwa mwanamke single ili kuonyesha hamu yake. Kama hataweza kuonyesha hisia zake kwa kumtazama macho yake, sauti yake, kumsugua mwanamke mgongo wake, kumfanyia massage kwenye mabega, mwanamke atajuaje kama anamtaka? Na ataendeleaje kubaki nae kama hamtimizii haja zake? Kwa kufanya hayo anaweza kumuwekea ulinzi, mahusiano yao kukomaa na kuwa mazuri na kuwa ya kawaida. Lakini akili Itakuja. Marafiki aliowaambia watamkumbusha.Ni mume wa mtu. Familia watamuuliza , bado yuko na mke wake? Wakati anapoanza kujiuliza ndani yake , mume alienae, Ataanza kuwa na njia mbili. Kwa wanawake wengi, hio imepitwa na wakati. Kwa wengine mchezo utaendelea—kwa kufahamu maamuzi haya…tuangalie sasa 1.Wakati mwanaume anapotoka nje, uwezekano mkubwa hana furaha ndani ya nyumba yake. 2Talaka zinaongezeka . ndoa zinafikia mwisho, na wanaume wanaoa tena. 3.Uzinzi unaongezeka kwa wanaume. Huenda kuishi muda mrefu peke yao sio mpango mzuri. Kwa mtu kama Jane kuishi maisha kama hayo, huenda ni katika kumpata mtu sahihi na kumuondoa kwa mke wake hata kama kutakuwepo hatari katika hisia zake. Mwanamke kama Jane ni wepesi wa kujifunza zaidi kuhusu tabia za wanaume ambao wanacheat kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano ya kudumu. Wengi wa wanaume wanasema , sababu kubwa ya kucheat ni kukosa sex Ni kiasi kidogo sana cha wanaume ambao hupotea katika mapenzi ya nje Baadhi ya wanaume wanaocheat walitoa taarifa kuwa wanafanya hivyo kwa wenza wengi karibu miaka yote Kwa kulinganisha wanawake na wanaume. Wanawake wao huingia kwenye mahusiano kwa mwanaume aliyeoa kwa sababu ya kuwapenda. Lakini sio nzuri kama mtu ameoa ni bora kujiheshimu na kumuheshimu mke wake , Na kama kuna tatizo ni vizuri kurekebisha kuliko kwenda kutafuta majibu ya tatizo lako nje.Kwa nini nasema hivi , ni kwa sababu ipo siku mwanamke huyo atahitaji kuwekwa wazi , utafanyaje na wewe ulikuwa ni mwizi. kwa upande wa mwanamke Utavunjika moyo, inapofika wakati kama huo.Maumivu ya kuachwa na mwanaume aliyeoa ni makubwa kuliko ya kuachwa na mwenza ambaye ni wako kabisa. Black woman hugging her knees 1.Utajisikia kama mkosaji mara mbili. Kwamba hukuweza kumpata mtu ambaye tayari kwanza alikuwa ameoa na amekuacha baada ya kuridhika kwake. 2.Wasaliti wanaokatiza mahusiano huwa wanaonyesha kabisa kuwa hawana hisiana za kutosha kwako. Wanakuchukulia kama wewe ni msichana mkubwa, na unaelewa kitu gani unachokifanya. 4.Mfumo unaompa support unaweza ukawa upo gizani. HUenda ni aibu au hamu ya kumlinda msaliti au vyote. Hakuna mtu ambaye anafahamu. Kama wapo basi ni wa katibu sana. Kwa hio watu kama Jane wataepuka vipi hatari inayotokana na aina hii ya mahusiano? Ukweli ni kwamba, ufahamu una nguvu.Kama msomaji unahusika na mume wa mtu, rudia tena kusoma makala hii kwa makini kabla hujaendelea zaidi. Maisha ni mafupi.Muda wa kumsaidia mume wa mtu ambaye amekosa kitu fulani kwa mwenza wake umekwisha. Mwache akatengeneze kwa mwenza wake. Wanaume Single wako wengi wanakusubiri na hawana hatari kama hizo. Hata kama atakuonyesha kuwa wako cool mwanzoni usidanganyike. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: