Home → ushauri
→ Mara kadhaa amejitahidi kukwambia "Nakupenda, usiniache please", ila sasa hawezi kusema tena. Ametaka kusema "Kwanini hauelewi jinsi navyoumia moyoni", ila amejua kwamba hawezi kukulazimisha umpende.
Ametaka kujaribu kusema "sijali tena", ila ametambua haitasaidia tena kukurudisha kwake. Ametaka kusema "samahani" ila amejua kwamba hajakutendea kosa lolote kupelekea usimpende tena!k
Ametaka kusema, "Mbona umebadilika, haukua hivi", ila ametambua kwamba hawezi kukuomba au kukulazimisha ubadilike. Ametaka kusema "tujaribu kukaa chini, tujadiliane na kurudisha mapenzi yetu", ila ametambua hataweza kwani wewe hauko serious hata kidogo.
Amejitahidi kuonesha kila aina ya upendo, ila wewe umeshindwa kumpenda. Amekupigia simu mara kwa mara hupokei. Amefikiria labda utakuwa busy, lakini siku nzima inapita wala hupati call yake kuonyesha aliona missed call zako!
Amekupigia simu usiku, amekukuta busy ukiongea na simu, na ulipomaliza kuongea wala hukumpigia tena simu.
Amekutumia messages watsapp zinaonesha kabisa tick ya blue lakini hukuhangaika hata kumjibu, busy ukichati na watu wengine!
Mapenzi yanauma asikwambie mtu, hufika hatua ukachukia kila mtu na kila kitu. Ukatamani Dunia ikumeze japo kwa dakika chache usahau maumivu unayopitia.
Mtu hutamani uwe na uwezo wa kuteka mawazo ya mpenzi wako na kujua nini anachokiwaza kichwani mwake. Watu wengi wanapitia magumu katika mapenzi, sio masikini, tajiri au wa daraja la kati. Mahusiano yameteka akili za binadamu.
Badili gia angani, kubaliana na hali halisi, mwaka mzima mtu habadiliki, utakumbatia mti wenye miba mpaka lini? Mtu akikupenda ni vigumu sana kukusababishia maumivu moyoni! Labda hilo halikuwa fungu lako. Moyo ukipenda ni vigumu sana kubishana nao, ila utafanya nini sasa?
Najua maumivu ni makali, moyo unauma, akili haifanyi kazi, inauma zaidi ukikumbuka nyakati zile zilizo njema, kipindi mapenzi yakiwa mapenzi kweli! Nyakati alipokuwa mtu wa kweli kwako...ila sasa mambo yamebadilika, ni kama kibatari kilichozimika ghafla katika kiza kinene penye uhitaji wa mwanga.
Busara yangu, "one of the happiest moments in life is when you find the courage to let go of what u can not change"
Tuache masihara mapenzi yanauma asikwambie mtu, Mungu wangu aliye muaminifu akakuvushe katika gumu unalopitia, akakusaidie kurudisha furaha yako uliyoipoteza. Ukiona ugumu nitafute unishirikishe tuliite jina la Mungu wetu aliye mkuu teso hilo litaondoka na mungu atakurehemu mahali ulipokosea.
Mara kadhaa amejitahidi kukwambia "Nakupenda, usiniache please", ila sasa hawezi kusema tena. Ametaka kusema "Kwanini hauelewi jinsi navyoumia moyoni", ila amejua kwamba hawezi kukulazimisha umpende. Ametaka kujaribu kusema "sijali tena", ila ametambua haitasaidia tena kukurudisha kwake. Ametaka kusema "samahani" ila amejua kwamba hajakutendea kosa lolote kupelekea usimpende tena!k Ametaka kusema, "Mbona umebadilika, haukua hivi", ila ametambua kwamba hawezi kukuomba au kukulazimisha ubadilike. Ametaka kusema "tujaribu kukaa chini, tujadiliane na kurudisha mapenzi yetu", ila ametambua hataweza kwani wewe hauko serious hata kidogo. Amejitahidi kuonesha kila aina ya upendo, ila wewe umeshindwa kumpenda. Amekupigia simu mara kwa mara hupokei. Amefikiria labda utakuwa busy, lakini siku nzima inapita wala hupati call yake kuonyesha aliona missed call zako! Amekupigia simu usiku, amekukuta busy ukiongea na simu, na ulipomaliza kuongea wala hukumpigia tena simu. Amekutumia messages watsapp zinaonesha kabisa tick ya blue lakini hukuhangaika hata kumjibu, busy ukichati na watu wengine! Mapenzi yanauma asikwambie mtu, hufika hatua ukachukia kila mtu na kila kitu. Ukatamani Dunia ikumeze japo kwa dakika chache usahau maumivu unayopitia. Mtu hutamani uwe na uwezo wa kuteka mawazo ya mpenzi wako na kujua nini anachokiwaza kichwani mwake. Watu wengi wanapitia magumu katika mapenzi, sio masikini, tajiri au wa daraja la kati. Mahusiano yameteka akili za binadamu. Badili gia angani, kubaliana na hali halisi, mwaka mzima mtu habadiliki, utakumbatia mti wenye miba mpaka lini? Mtu akikupenda ni vigumu sana kukusababishia maumivu moyoni! Labda hilo halikuwa fungu lako. Moyo ukipenda ni vigumu sana kubishana nao, ila utafanya nini sasa? Najua maumivu ni makali, moyo unauma, akili haifanyi kazi, inauma zaidi ukikumbuka nyakati zile zilizo njema, kipindi mapenzi yakiwa mapenzi kweli! Nyakati alipokuwa mtu wa kweli kwako...ila sasa mambo yamebadilika, ni kama kibatari kilichozimika ghafla katika kiza kinene penye uhitaji wa mwanga. Busara yangu, "one of the happiest moments in life is when you find the courage to let go of what u can not change" Tuache masihara mapenzi yanauma asikwambie mtu, Mungu wangu aliye muaminifu akakuvushe katika gumu unalopitia, akakusaidie kurudisha furaha yako uliyoipoteza. Ukiona ugumu nitafute unishirikishe tuliite jina la Mungu wetu aliye mkuu teso hilo litaondoka na mungu atakurehemu mahali ulipokosea.
Artikel Terkait
AINA 10 ZA WANAUME AMBAO WANAWAKE HUJUTIA WAKIWA NAO  1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband). HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea. 2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake. 3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband). Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke. 4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband). Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida. 5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband). Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao. 6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband). Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena. 7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband). Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa. 8. Mume Mtalii (Visiting Husband). Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto. 9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke. 10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband). Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake. ... Read More
KWA WANAWAKE TU! NJIA 14 ZA KUJIWEKA ILI WANAUME WATAMANI KUKUTONGOZA  Je umekuwa ukijiuliza kwa nini haukuwi approached na wanawaume kama unavyotaka? Mtandao wa Sayari ya Mapenzi umeamua kukuandalia mbinu na maujanja ya kutumia ili uonekane mwanamke ambaye anaweza kufukuziwa na mwanaume kwa urahisi. Owk.... Kando na itikadi ambazo umekuwa ukifikiria, kuapproachiwa ama kufukuziwa na mwanaume si gemu ya bahati nasimu ambayo mtu anaingojea ijitokezee. Na pia kando na itikadi nyingi za wanawake wanazozifikia, si lazima ufanye kitendo kikubwa ama cha inadi ili mwanaume aweze kukutongoza. Ukweli ni kuwa, kama unaielewa akili ya mwanaume na jinsi inavyofanya kazi kabla ya kuapproach mwanamke, unaweza kumfanya mwanaume yeyote kutaka kuongea na wewe dakika tano atakapokuja katika himaya yako. So mbinu zenyewe ndizo zipi? Zama nami... Njia za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukutongoza Kwanza jiweke nadhifu Hii ni muhimu katika yote kama wataka mwanaume akutambue. Mwanaume kitu cha kwanza anachokiangalia huwa ni mwonekano wa mwanamke. Mwanaume anapoingia katika chumba, inamchukua sekunde ndogo zana kuamua iwapo anataka kuapproach mwanamke mfani au la. Kama umevalia vizuri na unapendeza, itarahisisha kazi yako sana. Pili usionekane kama una shughli Usijishughlishe sana na simu yako, ama kitabu chako, ama kitu kingine. Unaweza kuwa umeboeka na unajaribu kujiweka buzy, lakini fursa iweza kuwa hivi, kufanya hivyo kunaweza kumfanya mwanaume anayetaka kukuapproach kuona ya kuwa uko buzy sana kiasi cha kuwa atashindwa kukufuata kwanu unaweza usiwe interested na maongezi yake. Tatu ni kuwa mko ligi moja? Hii inakinzana na hatua ya kwanza, lakini inaweza kuwa na tatizo iwapo unaoneka kama uko ligi tofauti na mwanaume. Kama utaoneka amakujiweka mtu wa hadhi ya juu wanawake watapenda kukuangalia lakini hawatakuaproach. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hawapendi kudhalilishwa wakati wanapoamua kukuapproach....kiufupi ni kuwa ukiwa unavutia kupindukia wanaume watakuogopa. Lakini tena, kuna wale wanaume ambao wanajiamini kupindukia ambao wanajua thamani ya kukuapproach, nao ni wanaume alfa, wanaume diriki, na pia wale wanaume mapleya. Kama wataka kuteka atenshen ya mwanaume mzuri wa kawaida lakini anayeogopa kukuapproach, jaribu kutumia mbinu ya kuwa jamili na watu wanaokuzunguka. Huwa inasaidia. Ujanja wa kumfanya mwanaume aweze kukuakuaproach 1. Jinsi utakavyovalia Usivalie kana kwamba huna kitu cha kuficha. Utapata atenshen ya kila mtu lakini wanaume ambao wataamua kukuapproach ni wale ambao wanataka kulala nawe kwa usiku mmoja pekee. Enyewe kuvalia kwa kutamanisha kunasaidia kuteka atenshen ya mwanaume, lakini usivuke mipaka ya kawaida. Kumbuka kuwa si lazima uonyeshe viungo vyako vyote vya mwili ili uweze kuteka macho ya mwanaume. Kama unavutia inatosha kumfanya mwanaume akugundue. 2. Unavyomuangalia Mchungulie mara moja na nyingine, halafu mwangalie mara kwa mara. Hakikisha ya kuwa haujisahau ukamwangalia sana kupindukia ama atakuona kama wewe ni rahisi wa kuapproach na anaweza kukupuuza. 3. Mitindo ya kumwangalia Kuna mitindo miwili mikuu ya kumwangalia mwanaume ili kumuonyesha ya kuwa umevutiwa naye. Unaweza kutumia mbinu zote mbili kulingana na vile unataka. i) Kumwangalia polepole - wakati ambapo unaangalia pande zote, angalia upande wake na uyaangalie macho yake kwa sekunde kadhaa huku ukiweka tabasamu. Halafu pole pole zungusha kichwa chako uangalie kwingine. Mbinu hii ni ya kijasiri ya kumwonyesha mwanaume umevutiwa kwake. ii) Kumwangalia kwa uharaka - hii ni mbinu ya kumwangalia kwa uharaka. Anza kumuangalia, ukiona kama anataka kukuangalia, ghafla angalia kando halafu utoe tabasamu ukiangalia chini. Mbinu hii inampa confidence na kukuona wewe ukipendeza. 4.Mfanyie kazi iwe rahisi Inakuwa vigumu kwa mwanaume kumuapproach mwanamke sehemu ambapo yuko kundini na marafiki zake. Kama mawazo yako ni kufuatwa na mwanaume, hakikisha ya kuwa wakati mwingine unajipa time ukiwa pekeako ama zaidi uwe na rafiki yako wa kike mmoja. 5. Sehemu zifaazo Si kila sehemu ni nzuri kufanya maongezi na mtu. Kama unataka mwanaume akuapproach, chagua sehemu ambayo si kila mtu ataanza kujeuza kichwa chake kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yenu. Sehemu za mkawahawa, supermarket, ama bookshop ni sehemu nzuri zaidi za kukutana na mwanaume kupiga stori. 6. Mpatie nafasi aongee na wewe Hata kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe, unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume huyu kuzungumza na wewe. 7. Tabasamu Onekana jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka macho ya mwanaume yamwone. 8. Usiboe Kuwa mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua. Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo na mwanga. 9. Usiwe mjeuri Kama wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa. 10. Usitangamane na wanaume Hii ni muhimu kwa mwanamke yeyote aelewe. Usiwahi kamwe kutangamana na marafiki zako wa kiume kama unataka kukuwa approached na mwanaume. Haitafanya kazi kamwe. 11. Mwoneshe kuwa uko intrested Mwonyeshe kuwa uko interested kwake kwa kutaka kumjulia hali zaidi. Hata kama uko na marafiki zako mnaongea halafu amekaa karibu na wewe, mwangalie iwapo anakuangalia hata kama unawajibu rafiki zako. 12. Onyesha uanawake wako Mwangalie mara kwa mara, halafu ukishika macho yake, peta nywele zako nyuma ya sikio lako. Inaweza kuonekana kama jambo dogo kwako, lakini kwa mwanaume ni kama kugonga ndipo. 13. Mtege Pita mbele yake halafu mwangalie machoni mwake wakati unapompita. Mtese kihisia, ataipenda kuona atenshen yake. 14. Usilazimishe Utakuwa unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia mara moja na nyingine ama kuwatabamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa. Ok hizi ni mbinu ambazo unafaa kuzitumia kama unataka mwanaume yeyote yule akunotice ama akufukuzie. ... Read More
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
Kwa wanawake tu! Jinsi ya kujisafisha uke  Naomba kufahamishwa na wanawake jinsi ya kujisafisha kwenye papuchi(mwanaume atakaye shauri naomba awe doctor au mwenyewe experience ya kutosha kuhusu maumbile ya mwanamke) Mimi huwa nikienda kuoga natumia sabuni ya jamaa kusafisha juu kabisa ya papuchi yaani kwenye mapaja na pale juu kwenye nyw**le...then natumia maji mengi kujisuuza na kuingiza kidole ndani kidogo ya K kutoa uchafu either wa period kama niko P na sometimes nakuta kuna ule uchafu mweupe wanaita(utoko) but huo uchafu huwa ni mweupe kama barafu na pia haunuki kabisaa..... Sasa swali ni kwamba kuna watu wanadai hatupaswi kutoa huo uchafu eti ni bacteria wa kukinga K isipate madhra so hupaswi kuingiza kidole kabisa.... tuoshe juujuu tu...... Second wengine wanasema tusinawe na sabuni kabisaa(japo kama nilivyosema mimi sabuni napitisha kwa juu kabisa tena nikiwa nimesimama ili isiweze kuingia kwenye K coz siamin kama kujisafisha bila sabuni harufu ya mkojo, harufu ya P na jasho itaisha kwa kunawa na maji tu.....na situmii sabuni zenye chemical). Naomba wanake wenzangu mnipe experience zenu juu ya hili ... Read More
Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu.  Dalili 8 zitakuonyesha kama upo kwenye mahusiano ya kudumu au hapana. Afya. Wote tunafikiria kuhusu hili. hasa kwa kadri tunavyoendelea kukua , tunatembelea madaktari, tunakula vizuri wakati mwingine. Tunatafuta dalili na wakati mwingine matokeo yake yanatuambia kuwa hali zetu sio nzuri. Lakini tunapofikiria afya, tunafanya hivyo katika miili yetu tu. mara nyingi tunasahau kufikiria kuhusu afya ya mahusiano na mapenzi. Tunaangalia zaidi afya ya mwili katika maisha ,lakini kuwa na afya nzuri katika mahusiano ni vitu vinavyoungana. Kwa kurahisisha , mahusiano mabaya hayadumu. au ingawa yanaweza kukaa kwa muda fulani.Na kama yakidumu , atakuwepo mtu wa kuumia. Lakini ni nini hasa afya ya mahusiano? Tutajuaje kama mahusiano yetu yatadumu? Utajuaje kama uko na mtu sio sahihi, mtu ambaye mtaishia kwenye kona fulani tu? Hakuna kipimo halisi cha kujua. Hakuna kipima joto kinaweza kupima kiasi cha muda wa mahusiano kuwa ni ya moto au baridi. Kwa bahati kuna hizi dalili 8 ambazo zinaweza kukusaidia kujua afya iliopo kwenye mahusiano yako. 1.Mchumba wako atakuwa na imani na wewe , na wewe utakuwa na imani naye.  Hataongea kwa ajili yake bali ataongea kwa ajili yenu wote. atakukumbusha pale unapokuwa umesahau au unapokuwa na mashaka kwa jinsi ulivyo. Ana maono ya wazi ya muhimu kwako. atalea hali hio na utaiona. Vilevile na upande wako utakuwa kama yeye. hutamsema vibaya kwa marafiki, hutalalamika kitu bali utaongea mbele yake. Utamwamini kuwa yuko kamili , mtu anayeweza kutatua matatizo na kusimama kwa miguu yake. Hata kama haujamsaidia kitu. 2.Unamwamini. Unamwamini katika ukweli wake wote. ahadi zake ni za kweli. utamkubali alivyo. Anahusika katika majukumu yake. 3.Unakubali mambo yake yaliopita na yeye anakubali ya kwako. Jinsi alivyokuwa, alikuwa na wanawake wangapi, wanaume wangapi. hutajali. utamkubali alivyo ili mkue pamoja. hutafikiria kitu chochote kilichopita, bali utakuwa na hamu ya kutaka kujua jinsi gani huyo mtu alivyo. Mahusiano yako yatakuwa yamekusanya, Msamaha na kuachilia yaliopita. 4.Unashukuru kwa vitu vizuri mlivyonavyo Unakubaliana na vitu vidogo vidogo anavyovifanya kwako. unakuwa na matumaini, husubiri kupata kazi, kwa ajili ya mshahara, kwa ajili ya mambo mengine. unashukuru kwa kile mlichonacho sasa na mwenza wako. Mnafuraha wakati huu. hana mchezo wa kijinga. anatengeneza pesa ya kutosha. anafanya kitu akipendacho. Utakuwa unalenga safari sio mwisho wa ndoa, mtoto, sherehe, vitu vinatokea kwa kawaida. 5.Mawasiliano ni ya wazi na ya kueleweka kwa kila mmoja. Hakuna wa kusubiri ni nani atamtafuta mwenzake. kila mtu anakuwa na jukumu la kufanya hivyo. Na kama itatokea mmoja hakuhusika , hakuna lawama, kwa kuwa mnaelewa . utavaa moyo wake. hutahangaika kuyatawala mahusiano kwa sababu hamfanyi mchezo wa kuigiza. 6.Maisha yenu ya sex yataendelea kuwa mazuri na ya kupendeza. Kwa sababu ya urafiki ambao mnao, maisha yenu ya mahusiano yatakuwa rahisi na ya kimapenzi. Ya ukaribu zaidi. sex itakuwa sio kipaumbele chenu bali ni matokeo ya upendo mlionao. mahitaji yenu ya kimwili yatatosheka kwa pamoja. 7.Utamuheshimu na yeye Atakuheshimu wewe. Kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzake na mnaweza kuhimizana katika kutimiza malengo yenu. kama unapenda kucheza , atakuhimiza kufanya hivyo. hutahitaji kukamilisha hisia zako zote. atakuwa na mahusiano mazuri na watu wengine pia. Ni mtu muhimu kwako. anakufanya ujisikie vizuri. 8.Malengo yenu yanafanana. Hutajaribu kumbadilisha. au kujaribu kuomba kuishi na yeye. hutahitaji awe mtu wa kutengeneza kitu chako. ni mtu ambaye ulimtaka awe wako. thamani yake ni muhimu katika maswali hata. Unataka watoto? Unapenda kusafiri? Una hamu ya kupata uzoefu fulani? unakubaliana katika mambo ya pesa? Una furaha unapokuwa naye? Unataka kuishi naye na kuwa naye chumba kimoja? Afya ya mahusiano yako ni muhimu katika maisha ya ndoa utakayoingia. Lakini hakuna kipimo cha kupimia uzima huo. Ni wewe tu na mwenza wako mnajua kama mahusiano yatadumu au yataishia kwenye kona. yatakuwa na matunda au hapana. Mttajua kama ni mazuri au sio. hizo dalili nane zikusaidie kufahamu kama ni ya afya au sio, yatadumu au hayatadumu. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: