Home → ushauri
→ HII NI KWA NDUGU ZANGU WANAUME VITASA! MFANYE AJIHISI MWANAMKE!
Iko hivi mwanamke kutaka umhudumie haina uhusiano na pesa wala shida. Hapana ili mwanamke ajihisi anapendwa nilazima awe na mwanaume ambaye anajali mahitaji yake, mwanaume ambaye anafahamu kuwa ana mahitaji na anamhudumia.
Ndiyo nazungumzia kuhudumia kwani ni wanaume wachache ambao wanaweza kuhonga (kuhonga ni kama kumnunulia gari, ukamjengea, shopping dubai, ukatoa laki tano za kusuka na vitu kama hivi) sisi wengine tunahudumia kama kununua vichupi chupi na vi braa, kununua chakula na vocha, kumtoa out ya elfu ishirini.
Ndiyo mwanamke hata kama ana hela vipi lakini ni mwanamke anahitaji mwanaume wa kumhudumia, hata kama si wa kumnunulia gari na kumlipia kodi lakini angalau ajue kua nayeye ana siku zake ampe hata hela ya Pedi!
Sasa wewe ndugu yangu hata hujiongezi, ukatuma hata vocha, unaona anabadilisha tu underwear hujiongezi hata ukatafuta ka dazeni kamoja ukampelekea, ukajipinda na vimanukato kidogo.
Yaani hembu mpe kitu cha kuringishia kwa marafiki zake. Kwamba wakimsifu unanukia vizuri hii perfyume umenunulia wapi ajishaue hata kama anajua aseme hii kaniletea Baby hata sijui kanunulia wapi!
Tena unajisifia kabis ayule ni “Demu Wangu” wakati underwear aliyovaa kanunuliwa na Mzee wa umri wa Baba yako! Acha kujisemea kua yule anafanya kazi anajiweza ndugu yangu mbona wewe bafu lipo unaweza maliza mambo yako lakini unamfuata yeye?
#BADILIKA #SHARE
HII NI KWA NDUGU ZANGU WANAUME VITASA! MFANYE AJIHISI MWANAMKE! Iko hivi mwanamke kutaka umhudumie haina uhusiano na pesa wala shida. Hapana ili mwanamke ajihisi anapendwa nilazima awe na mwanaume ambaye anajali mahitaji yake, mwanaume ambaye anafahamu kuwa ana mahitaji na anamhudumia. Ndiyo nazungumzia kuhudumia kwani ni wanaume wachache ambao wanaweza kuhonga (kuhonga ni kama kumnunulia gari, ukamjengea, shopping dubai, ukatoa laki tano za kusuka na vitu kama hivi) sisi wengine tunahudumia kama kununua vichupi chupi na vi braa, kununua chakula na vocha, kumtoa out ya elfu ishirini. Ndiyo mwanamke hata kama ana hela vipi lakini ni mwanamke anahitaji mwanaume wa kumhudumia, hata kama si wa kumnunulia gari na kumlipia kodi lakini angalau ajue kua nayeye ana siku zake ampe hata hela ya Pedi! Sasa wewe ndugu yangu hata hujiongezi, ukatuma hata vocha, unaona anabadilisha tu underwear hujiongezi hata ukatafuta ka dazeni kamoja ukampelekea, ukajipinda na vimanukato kidogo. Yaani hembu mpe kitu cha kuringishia kwa marafiki zake. Kwamba wakimsifu unanukia vizuri hii perfyume umenunulia wapi ajishaue hata kama anajua aseme hii kaniletea Baby hata sijui kanunulia wapi! Tena unajisifia kabis ayule ni “Demu Wangu” wakati underwear aliyovaa kanunuliwa na Mzee wa umri wa Baba yako! Acha kujisemea kua yule anafanya kazi anajiweza ndugu yangu mbona wewe bafu lipo unaweza maliza mambo yako lakini unamfuata yeye? #BADILIKA #SHARE
Artikel Terkait
KAMA NI MUOGA WA KUKUTANA NA MWANAMKE MPYA SOMA HAPA  1. Zifahamu sehemu nzuri za kukutana na wanawake Sehemu za kujivinjari kama vilabu na baa ni sehemu nzuri za kukutana na wanawake lakini kama unataka mahusiano marefu na mwanamke basi sehemu hizo si nzuri kwako. Iwapo unataka mchepuko wa haraka basi unaweza kuenda kutafuta katika hizo sehemu. Iwapo wewe ndio umeingia katika dunia ya kutongoza kwa sasa, basi ningekushauri utafute sehemu mbadala kwa sababu kutakufungua macho na ufahamu mpango mzima kuhusiana na maswala ya mahusiano na mapenzi. Sehemu nzuri za kukutana na wanawake ni: Supermarket Mkahawa Bustani Vituo vya mabasi Chuoni 2. Jaribu mitandao ya kutafuta wachumba, wapenzi Hii inaweza kuonekana kama utata kwako lakini kulingana na utafiti ni kuwa wanaume wengi hupata wachumba wao kupitia mitandao ya kutafuta wachumba. Uzuri wa mitandao hii ni kuwa haina stress ya kujisumbua kuzunguka, unatafuta mchumba ukiwa nyumbani kwako ukiwa umetulia. Pia mitandao hii inakupa fursa ya kupata mchumba ambaye mnagawa maslahi na tabia moja. Lakini chunga iwapo utatafuta mchumba kwa mtandao kwa sababu kuna wengi wamefanyiwa ufidhuli huko na kuporwa pesa zao. Unaweza kuangalia mitandao ya kutafuta wachumba bora zaidi Afrika ambayo tumekuchagulia. 3.Usishushe hadhi yako Iwapo unataka kutongoza mwanamke sehemu yeyote ile, usijaribu kushusha hadhi yako. Iwapo unaamini ya kuwa wewe ni mzuri zaidi kwa mwanamke basi pia yeye ataamini hivyo hivyo. Pia iwapo unaona hauna uwezo wa kumvutia mwanamke, elewa ya kuwa vivyo hivyo wanawake watakuona kama mwanaume usiyejiamini ambaye huna confidence ya kuwaaproach ama kuwatongoza. Wanawake hupenda wanaume ambao wana confidence na wanaopenda kuchukua misimamo ya haraka. 4. Kuwa na mipango Kama iwapo unataka kukutana na mwanamke mara ya kwanza ama wakati mwingine, hakikisha ya kuwa unaweka mpango unaoeleweka ili usipate tatizo mbeleni. Mfano unamtoa out mwanamke, hakikisha ya kuwa unaifahamu vyema sehemu unapanga kumtoa out ili usianze kupapatika kuhusu wapi na nini la kufanya wakati mmetoka sehemu hizo. Wanawake hupenda wanaume ambao huwa na mwongozo wa mambo ambayo hufanya. Sehemu nzuri za kukutana na mwanamke ni katika mkahawa, gym, na baa. Hakikisha ya kuwa sehemu unayoichagua inapendeza. 5. Uwe unapendeza kila wakati Iwapo unataka kuwa na mahusiano mazuri na wanawake basi unafaa uwe unapendeza kimuonekano. Hakikisha ya kuwa unauboresha mwonekano wako na pia umaintain kila wakati. Kuvalia nguo nzuri mara kwa mara ni muhimu lakini usivuke mipaka. Ni muhimu kufanya hivi kwa sababu huwezi kujua lini ama wapi unaweza ukakutana na mwanamke utakaye mzimia. 6. Fanya mazoezi ya ujamiifu wako Ujamiifu ni socialization na wengine. Iwapo unataka kukutana na wanawake wengi katika maisha yako, basi kigezo cha kujamiiana na wengine ni muhimu. Kutembea sehemu za vilabu, baa, sehemu ambazo kuna matukio flani ni muhimu ili kunoa kipawa chako cha kutangamana na wengine. Tumia fujo wakati ambapo unatangamana na wanawake ili uboreshe ubabe wako. Kama ni kuenda kwa kilabu, hakikisha ya kuwa unadensi na wanawake tofauti tofauti. Hii inakupa confidence kwa mwanamke. Pia hakikisha ya kuwa unaenda wakati ufaao sehemu kama hizi. Mfano nenda kwa klabu wakati watu wamekuwa wengi. Pia usijifiche wala kuogopa yeyote yule. 7. Usibabaikie kutemwa Kila mtu katika maisha yake ashapitia wakati flani ambapo amekataliwa na mtu flani, so kukataliwa ni jambo la kawaida na halifai kusumbua mtu akili. Kando na hivyo, kukataliwa hakumaanishi ya kuwa unafanya makosa. Wakati mwingine huwa ni kuwa wanawake wengine hawataki kuwa katika mahusiano, washachumbiwa ama sababu nyingine kama hizi. Kumalizia ni kuwa kuna mbinu tofauti tofauti na sehemu tofati za kutafuta mchumba hivyo woga la kutemwa halifai kuwa swala kuu. 8. Pata ujuzi kutoka kwa wanaume wengine Ukweli usemwe, hakuna mwanaume hapa duniani yuko sawa asilimia 100. Hivyo ni vizuri kupata ujuzi kwa kuwauliza wenzako ni vipi waliweza kutongoza ama kupata windo fulani. Ingawa ni vizuri kupata ushauri kutoka kwa marafiki zako, mimi naona ushauri wa mtu huwa tofauti na mwingine hivyo mara nyingi ushauri kutoka kwa mwanaume mwingine unaweza kukupotosha ama kuegemea upande mmoja. Hapa NESIMAPENZI tumekulekea post tofauti tofauti za kukufunza wewe na hatujaegemea upande wowote. ... Read More
HIVI UNAIJUA MAANA YA MAPENZI VIZURI AMA.......???  Jina mapenzi limeweza kupewa maana nyingi kulingana na maongezi yanayozunguka jina hilo. Mapenzi yaweza kusemwa kwamba ni jina linaloonyesha hisia za mtu iwe mahaba, pendo kwa mtu ama upendo wa Mungu. Mara nyingi watu wengi hukosea kwa kuchambua mapenzi katika mahaba pekee. Watu wengi hudhania mapenzi huwa yanahusisha moyo wa binadamu, lakini hakika ni kwamba huhusisha ubongo wa mwanadamu. Kuna aina nyingi za mapenzi ambazo binadamu huonyesha katika maisha yao wanapoendelea na shughuli zao za kila siku. Kama binadamu sisi husahau aina nyingine za mapenzi kwani wengi wetu hawajui neno mapenzi lina maana nyingi. Kwa kufafanua mapenzi yapo na aina zifuatazo Mapenzi ya kimwili (Eros) Aina hii ya mapenzi ni ya kimahaba. Kwa mfano mwanamume kumtamani mwanamke ama vile vile mwanamke kumtamani mwanamume kwa hamu ya ngono. Hapa mapenzi huwa yanayoendelezwa na hisia za kumtaka yule mwingine kimapenzi. Hii ndio aina ambayo watu wengi duniani hudhani ndio maelezo kamili ya mapenzi ill hali hii ni moja yapo ya zingine nyingi. Aina hii ya mapenzi ni muhimu kwa watu wanaoanza kutongozana ama watu wanaofikiri kuwa katika uhusiano. Mapenzi ya Urafiki (Philia) Aina hii ni ambayo inavutiwa na mtu kukufanyia kitendo kizuri ama kukusaidia ama ni mtu mzuri kwa ujumla. Mapenzi hapa yaweza kuwa kwa ndugu ama rafiki yako mzuri. Mapenzi haya huwa sana ambapo mtu wanashiriki maadili sawa na mwenzake na kwamba hisia zao sinaambatana ama mmoja anapokea matendo sawia na yale anamwelekezea yule mwenzake. Mapenzi ya aina hii yanaenziwa sana duniani. Wataaluma huamini kwamba mapenzi ya urafiki husaidia kutoa tamaa ya mwili na kuzingatia kufahamiana zaidi kwa marafiki na dunia kwa jumla. Mapenzi ya Familia(Storge) Aina hii ya mapenzi ni inayoonekana na wazazi kwa watoto wao na pia kutoka kwa watoto kwa wazazi. Aina hii hutofautiana na ya urafiki kwani haizingatii kile mtu anachokutendea bali uhusiano wa kidamu na vile wazazi na watoto wao wanavyotegemeana. Sifa za binafsi hazizingatiwi hapa ili wazazi waonyeshe wanao hisia hizi. Uhusiano wao huchangia kwa mapenzi haya. Mapenzi haya huhusishwa na mtu kujiskia yuko huru na salama. Mapenzi ya Kujitolea(Agape) Aina hii ya mapenzi inazingatia asili, mapenzi kwa Mungu au miungu na mapenzi kwa usiowajua. Hii ni mapenzi ya kujitolea kwa ubinafsi ama mapenzi ya ubinadamu. Aina hii inahusishwa na kuto tarajia malipo au kitu chochote kwa matendo unayoyafanya. Yaani ni mapenzi yakujitolea mhanga. Aina hii ya mapenzi hutusaidia kuwapenda watu tusiowajua na kusaidiana kibinadamu kwa hali yoyote ile. Dunia yastahili kuwa na aina hii kwa wingi ili tukaweza kukaa kwa amani na furaha. Mapenzi kwa Mungu ama niungu pia huwa katika aina hii. Kumwabudu Mungu aliye binguni ni mfano mmoja wa kueleza aina hii. Mapenzi Changamfu (Ludus) Aina hii ya mapenzi ni mapenzi yasio na dhamira yoyote na ma mzaha tu. Mapenzi haya hayana masharti hata kidogo. Mfano wa aina hii ya mapenzi ni kama mtu anovyomtongoza mwingine, kupinga densi na kucheza. Aina hii ya mapenzi haina mambo mengi kwani huwa ni kawaida tu. Aina hii huwa sawa kwa watu wanaojitosheleza kimaisha. Aina hii ya mapenzi huwa gumu wakati mtu mmoja hufasiri kwamba mwingine ana hamu ya kimwili. Inafaa watu waweze kuelewa kama wanahamu zaidi na raha na kufurahi tu. Mapenzi Madhubuti(Pragma) Aina hii ni mapenzi ambayo yako na msingi wa wajibu wako kwa mwingine na wa kuzingatia maslahi ya mwingine ya siku za usoni. Mfano mwema ni kwa wapenzi ambao wako katika ndoa. Aina hii inahusishwa na uvumulivu na maelewano kati ya walio katika ndoa. Aina hii ya mapenzi hukuzwa kwa muda wa miaka kadha na ndio maana yaitwa madhubuti ya ka kudumu. Mvuto wa kimwili sana hauzingatiwi katika aina hii ya mapenzi bali kujengana kimawazo na kufanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kinyume na aina zingine za mapenzi mapenzi madhubuti huzingatia pande zote mbili za wapenzi wawili. Lazima wewe wanapendana ama kuwa na mafikira na dhamira sawia. Mapenzi ya Kibinafsi (Philautia) Mapenzi haya ni ya mtu binafsi. Aina hii ya mapenzi huwa ina matokeo mawili, yaweza kuwa nzuri ama ya kudhuru. Upande mbaya wa aina hii huwa kwa ile hali ya ubinafi, kutafuta umaarufu na kutafuta utajiri na hufanya mtu kujiona ana dhamana kuliko mtu mwingine yeyote. Upande huu hufanya mtu akajiona yuko mkubwa kuliko mungu. Pia kuna upande mzuri wa aina hii ya mapenzi ambao inahusiana na mtu kujijua, kwa kufahamu uwezo wako na kujidhamini kwa uzuri wako na unachoweza kufanya. Kwa uhusiano wowote, huwezi kumpenda mwingine kama wewe mwenyewe hauna mapezi ya kibinafsi. Kwa kujipenda kwanza ndio tunaweza kupenda wengine na kuwatunza vizuri maishani. Aina hii ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu. Mapenzi ya kibinafi humsaidia mtu kujua mazuri na mabaya na kupanga maisha yake kwa nji inayostahili. Mapenzi ya kibinafsi humwongezea mtu hali ya kujiamini na kujidhamini. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi huweza kuelewana sana na watu wengi kwa vile kwa kujidhamini watu pia hukudhamini. Hii husaidia kwa vile mnaelewana na watu kazini, nyumbani na mahali pengine ambapo mnapatana. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi hawahitaji kujigamba ili watu wawajue ama kujionyesha kwa watu. Uzuriwao hujionyesha kwa wanayofanya na wanavyoongea. Watu wanaojipenda kibinafsi huwa wako huru kwa mambo mapya na uwazi. Uchambuzi na ufahamu wa mapenzi ni nini husaidia kila mwanadamu kutambua aina gani anafaa kuwapa watu kwa kila wakati na aina gani ya mapenzi kutupilia mbali. Mwanadamu anaweza penda ila kwa hiari yake. Haina maana lazima mtu akupende ndio umpende nawe. Kila mwanadamu anauwezo wa kumpenda mwingine ama kitu anachotaka hata kama yeye mwenyewe hajapatiwa mapenzi hayo. Lazima kama mwanadamu kufanya mapenzi kama kitu cha kawaida kwa kila tunachofanya maishani. Iweke iwe sehemu ya maisha yako na utu wako. Pia ni muhimu kuwa na aina hizi zote za mapenzi kwa uhusiano kwa kila siku na watu wengine ilituweze kuishi maisha marefu. Kama binadamu, mapenzi ya muhimu sana ni yale ya kujitolea na yale ya kibinafsi. Unapokuwa na mapenzi yasiyo tarajia kitu chochote na mapenzi yako mwenyewe ndio utaweza kuwapa watu mapenzi hayo mengine. Tukiweza kushikilia aina zote zingine za mapenzi kwa mahusiano yetu basi tutakuwa na maisha marefu na yenye kufana. Mapenzi ni kitu muhimu maishani na ni sharti yaenziwe na kila mwanadamu. ... Read More
NJIA RAHISI 13 ZA KUWA NA FURAHA KILA SIKU  Mabadiliko yalio mepesi kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka Umejikuta uko kwenye siku tofauti, story hizo hizo, imekuwa ni kawaida yako? Basi muda huu , sio kesho , sio wiki ijayo, ni wakati wa kubadilisha historia yako. ni za haraka, rahisi na hazina gharama unapofanya hivyo na matokeo yatakupa furaha unayoitaka. 1.Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku. Kulala usingizi wa kutosha unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala, usitumie chakula kingi wakati wa jioni. 2.Amka mapema , dakika 30 kabla . Kama wewe ni mfanya kazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako. 3.Meditate. Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na hutachanganyikiwa na kazi zako. 4.Jipe nafasi wengi wetu huwa tunajaza vitu nyumbani, ofisini hata vile ambavyo havina kazi, hatuvitumii. inaharibu mfumo mzima wa akili yako, hisia zako, na mwili wako. Ondoa vitu ambavyo huvitumii, tupa nje au gawia watu ambao wanahitaji kuwa navyo, hali yako ya furaha itaboreka. Na hutalemewa na kazi nyingi. 5.Jifunze kitu kipya Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hio ndio changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa sharp. 6.Tembea mara kwa mara Kutembea kwa dakika 30 kwa siku moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira, hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi . 7.Usijihusishe na mambo ya mitandao. Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya. 8.Kuwa mwema. Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri. 9.Kaa na watu wenye furaha. Angalia watu unaoshinda nao, unaofanya nao kazi, ni watu wa aina gani. kwa sababu kuna msemo unasema kuwa ukikaa na ua rose utanukia hata kama ulikuwa hunukii. Fanya hivyo na utaweza kufungua mlango mpya kwa ajili yako maishani. utaiona furaha ikitiririka kama mto. 10.Don’t gossip. Kuseng’enya, umbeya, itakusababishia maradhi ya misongo na kukosa furaha. mtu mmbeya hawezi kusaidia kitu. wakati mwingine jitenge na watu kama hawa, au unapoona kuna kutoelewana na wafanya kazi wenzako, jaribu kutulia kwanza , badilisha negative to positive. Sema kitu kizuri kuhusu mtu. ni vizuri. kwa sababu utajiwekea alama nzuri kwako. 11.Tumia muda wako na watu unaowapenda Unapoongea na familia au marafiki kwenye simu , inatia moyo. mawasiliano hayo yanakupa afya na furaha.Fikiri ilivyo vizuri kama utaenda kula na rafiki yako mahali fulani, au kuamua kupika nyumbani , au kucheza na watoto wako kitu kama game, mpira, inafurahisha. 12.Journal Kuandika vitu vya kufanya kwa siku, au kuandika vitu unavyotaka kuvipata, Lengo hili dogo litaongeza IQ yako na kuleta utulivu wa kuboresha ujasiri wako, ukiwa na tabia hii kila siku , furaha haitakosekana kwako na utapata faida ya akili na hisia zako zitakuwa bora. 13.Jizoeze kujijali. Unapojijali ,Utaona faida zake, pamoja na kuondoa stress na wasiwasi, utakuwa mtu wa kuwaza mazuri na utaboresha immunity.pata muda kila siku kufanya kitu kwa ajili ya furaha, kama vile mazoezi, kupika chakula kizuri, kusoma . utaanza kushangaa jinsi ilivyo rahisi kuwa na furaha unapojijali na utaboresha akili yako na mwili wako, na roho yako. Kama unavyojua , kuna njia nyingi zinazotushambulia kwa siku, Ondoka mahali ambapo panaharibu ratiba yako. sasa, kama kitu kingine chochote,mafanikio ni kufanyia kazi. kwa hio pick one, and let the fun begin! ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
Mimba kuharibika na Sababu zake  Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu. Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba. 1.Mama anapokuwa na matatizo uvimbe (fibroid), huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara. 2. Uzito mkubwa (unene) Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda. 3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika. 4. Utoaji mimba Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba. 5. Matumizi ya Pombe,Sigara Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo. 6. Magonjwa sugu Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: