Home → ushauri
→ MAMBO AMBAYO HUPASWI KUMFANYIA MWANAMKE ANAEKUPENDA KWA DHATI
1. Usimuumize moyo wake
2. Usi 'pretend' unampenda ili ufanikiwe kufanya yako.
3. Mtukane vyovyote vile ila sio wazazi wake na kumwambia kuwa yeye ni mbaya.
4. Usimfananishe na wanawake zako waliopita.
5. Usimchukulie kirahisirahisi (Never take her love for granted)
6. Usimpige
7. Usimsaliti na kuonyesha kabisa dharau ajue kuwa una 'cheat'
8. Usimvunjie heshima kwa kumgombeza mbele za watu.
9. Usimpotezee muda wake kama hauna mpango wa kumuoa, unamchelewesha kupata mume bora.
10. Usimfanye ajione hapendwi na ana mkosi hapa ulimwenguni, huo ni ujuha.
11. Usimbake
12. Kamwe usisahau kumwambia unampenda na yeye ni mzuri hiyo haipunguzi nguvu za kiume.
13. Usimpe mimba na kumkimbia au kumwambia aitoe, kama huna nia ya kumuoa achana na hayo mambo, nadhani unajua kabisa matokeo ya kufanya ngono.
Sometimes sisi wanaume ni pasua kichwa vilevile, unakuta tunapata mwanamke anaekupenda kwa dhati, mwanamke ambae ni potential, mwanamke ambae hakodoi macho pochi yako, ila masikini ya Mungu anaishia kuumizwa na kulia kila siku na kujilaumu kwanini alikupenda.
Wewe fanya hivyo ukidhani unamkomoa, ila siku na wewe ukibananishwa na mwanamke mjasiriamwili utaisoma namba, nakwambia utauza hadi boxer.
Baadae unakuja kulalamika hapa 'wanawake wanapenda pesa, wanawake wanapenda pesa.' ukishikwa shikamana.
Na kama humpendi usimtongoze!
MAMBO AMBAYO HUPASWI KUMFANYIA MWANAMKE ANAEKUPENDA KWA DHATI 1. Usimuumize moyo wake 2. Usi 'pretend' unampenda ili ufanikiwe kufanya yako. 3. Mtukane vyovyote vile ila sio wazazi wake na kumwambia kuwa yeye ni mbaya. 4. Usimfananishe na wanawake zako waliopita. 5. Usimchukulie kirahisirahisi (Never take her love for granted) 6. Usimpige 7. Usimsaliti na kuonyesha kabisa dharau ajue kuwa una 'cheat' 8. Usimvunjie heshima kwa kumgombeza mbele za watu. 9. Usimpotezee muda wake kama hauna mpango wa kumuoa, unamchelewesha kupata mume bora. 10. Usimfanye ajione hapendwi na ana mkosi hapa ulimwenguni, huo ni ujuha. 11. Usimbake 12. Kamwe usisahau kumwambia unampenda na yeye ni mzuri hiyo haipunguzi nguvu za kiume. 13. Usimpe mimba na kumkimbia au kumwambia aitoe, kama huna nia ya kumuoa achana na hayo mambo, nadhani unajua kabisa matokeo ya kufanya ngono. Sometimes sisi wanaume ni pasua kichwa vilevile, unakuta tunapata mwanamke anaekupenda kwa dhati, mwanamke ambae ni potential, mwanamke ambae hakodoi macho pochi yako, ila masikini ya Mungu anaishia kuumizwa na kulia kila siku na kujilaumu kwanini alikupenda. Wewe fanya hivyo ukidhani unamkomoa, ila siku na wewe ukibananishwa na mwanamke mjasiriamwili utaisoma namba, nakwambia utauza hadi boxer. Baadae unakuja kulalamika hapa 'wanawake wanapenda pesa, wanawake wanapenda pesa.' ukishikwa shikamana. Na kama humpendi usimtongoze!
Artikel Terkait
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
Special kwa Wanawake: Dalili za mwanaume anayekupenda kwa Dhati ANAVYOKUTAZAMA Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda. MIPANGO Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu. ATAONESHA HUZUNI Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. ATAKUAMINI Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake. ATAKUPA NAFASI Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake. UTAKUWA MWANAFAMILIA Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao. ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo. ATAKUSAIDIA Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani. ATAJITOLEA Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati. ATAAMBATANA NAWE Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu. KAMA UMEIPENDA MADA NA KUKUSAIDIA, TUPIA BASI LIKE NIKUPAKULIE NYINGINE!!!! ... Read More
Kufanya Mapenzi Kwa Wiki Mara 3 Kunapunguza Kupata Shambulio La Moyo (Heart Attack) Kwa Asilimia 50%  Utafiti umebainisha kwamba kufanya mapenzi angalau mara tatu kwa wiki kunapunguza uwezekano wa kupatwa Heart Attack (Shambulio la Moyo) kwa 50% ukilinganishwa na yule ambaye anapitisha wiki nzima bila kupiga mambo yetu. Pia utafiti huo unasisitiza ya kwamba mwenye Kufanya Mapenzi killa siku anaondoa uwezekano wa kupata Heart Attack kwa Asilimia 100% ZIJUE FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI Kiafya Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75. Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani. Kuongeza mwendo wa damu Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili. Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol) Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini. Kupunguza maumivu Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa. Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate. Kupunguza mfadhaiko wa moyo Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi. Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen) Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo. Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular). Hupunguza baridi na mafua Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa. NB: Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa HAYA KWA WANA NDOA FANYENI MAPENZI JAPO KWA WIK MARA 3 MUPATE FAIDA ZA TENDO LA MAPENZI NDANI YA NDOA. KWA WALE WASIOWA HAWAPATI HIZI FAIDA SHAURI YENU MSIE OWA OWENI MUPATE FAIDA ZA TENDO LA NDOA ... Read More
Jinsi ya Kuomba Msamaha MACHAGUO YA UPAKUAJI Podikasti Makala Nyinginezo SOMA KATIKA Amkeni! | Septemba 2015 UNAWEZA KUWA NA FAMILIA YENYE FURAHA Fuata Mwongozo wa Mungu ili Uwe na Ndoa Yenye Furaha Kujiuliza maswali mawili rahisi kunaweza kuisaidia ndoa yako. AMKENI! Viwango Vinavyomfaa Kila Mtu, Nyakati Zote—Upendo Upendo unaotajwa mara nyingi katika Biblia si ule wa kimahaba au kimapenzi. HABARI NJEMA KUTOKA KWA MUNGU! Kanuni za Biblia Zinatunufaishaje? Yesu alieleza kwa nini tunahitaji mwongozo na ni kanuni gani mbili za Biblia zina umuhimu mkubwa. Kuwafundisha Watoto Unyenyekevu Je, Inafaa Kujihatarisha Kwa Kusudi la Kujisisimua? Watoto Wanapoondoka Nyumbani Umuhimu wa Kazi za Nyumbani Kuomba msamaha kunaweza kuzuia ugomvi CHANGAMOTO Muda mfupi tu uliopita wewe na mwenzi wako mmetoka kubishana. Kisha unajiambia hivi: ‘Sihitaji kumwomba msamaha. Kwa sababu si mimi niliyeanzisha ugomvi!’ Mmeacha kuzungumzia jambo hilo, lakini hali si shwari. Unafikiria kuomba msamaha lakini unaona huwezi kusema, “samahani.” KWA NINI HILO HUTUKIA Kiburi. “Wakati mwingine si rahisi kusema ‘samahani’ kwa sababu sitaki kujishushia heshima,” anakiri mume anayeitwa Charles. * Kiburi kinaweza kukufanya uone aibu kukubali kwamba umechangia tatizo. Mtazamo. Unaweza kuhisi kwamba kuomba msamaha kunahitajika tu pale unapokosea. Mke anayeitwa Jill anasema hivi: “Ni rahisi kwangu kusema ‘samahani’ ninapojua kwamba nimesababisha tatizo. Lakini, ikiwa sote tulisema mambo yasiyofaa, ni vigumu kufanya hivyo. Kwa nini niombe msamaha ikiwa sote tuna makosa?” Unaweza kujitetea ikiwa unahisi kwamba mwenzi wako ndiye mwenye makosa. “Unapoamini kabisa kwamba hujafanya kosa lolote, unaonyesha huna hatia kwa kukataa kuomba msamaha,” anasema mume anayeitwa Joseph. Malezi. Huenda ulilelewa katika familia ambayo halikuwa jambo la kawaida kuomba msamaha. Ikiwa ndivyo, huenda hukujifunza kukubali makosa yako. Kwa kuwa hukuzoea kufanya hivyo tangu utotoni, ni vigumu kwako kuomba msamaha ukiwa mtu mzima. MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA Mfikirie mwenzi wako. Jaribu kukumbuka jinsi ulivyohisi vizuri ulipoombwa msamaha na mtu fulani. Kwa nini basi usimfanye mwenzi wako ahisi hivyo? Hata ikiwa huamini kwamba ulikosea, unaweza kuomba msamaha kwa ajili ya maumivu ambayo mwenzi wako amepata au kwa sababu ya usumbufu wowote uliotokana na matendo yako. Maneno hayo yanaweza kumsaidia mwenzi wako ahisi vizuri.— Kanuni ya Biblia: Luka 6:31 . Zingatia ndoa yako. Ona kuomba msamaha kuwa ushindi katika ndoa yako na si kushindwa. Zaidi ya yote, mtu anayeendelea kukasirika ni “mgumu kuliko mji wenye nguvu,” inasema Methali 18:19 . Inaweza kuwa vigumu kurudisha amani katika hali hiyo. Pia, unapoomba msamaha unazuia kosa kuwa kikwazo. Ukifanya hivyo, unatanguliza ndoa yako badala ya hisia zako.— Kanuni ya Biblia: Wafilipi 2:3 . Uwe mwepesi kuomba msamaha. Ni kweli kwamba ni vigumu kuomba msamaha ikiwa hujakosea. Lakini makosa ya mwenzi wako hayapaswi kuwa kisingizio cha kuendelea kuwa na tabia mbaya. Hivyo, usisite kuomba msamaha ukifikiri kwamba muda ukipita kosa hilo litasahaulika. Unapoomba msamaha unafanya iwe rahisi pia kwa mwenzi wako kuomba msamaha. Na kadiri unavyoomba msamaha ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kufanya hivyo tena wakati mwingine.— Kanuni ya Biblia: Mathayo 5:25 . Onyesha kwamba unajali hisia za mwenzi wako. Kutetea kosa lako si sawa na kuomba msamaha. Kusema kwa kejeli, “samahani kwa kuwa naona unakwazika haraka kwa sababu ya jambo hili,” si njia ya kuomba msamaha hata kidogo! Kubali makosa yako na utambue kwamba umemuumiza mwenzi wako, hata kama unaona hakuwa na sababu ya kukwazika. Tambua ukweli. Kubali kwamba utafanya makosa. Kwa kweli, kila mtu hukosea! Hata kama unafikiri huna hatia, tambua kwamba kuna uwezekano umechangia jambo hilo. Biblia inasema hivi: “Mtu wa kwanza katika kesi yake ni mwadilifu, mwenzake huingia naye hakika humchunguza kwa undani.” ( Methali 18:17 ) Itakuwa rahisi kwako kuomba msamaha ikiwa una maoni yaliyosawazika kuhusu mapungufu yako ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: