Home → ushauri
→ Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba (kwa
Kiingereza "Fertility Awareness", kifupi FA) unahusu mbinu zinazotumika kutambua wakati
mwanamke anapoweza kushika mimba na asipoweza kushika mimba katika mzunguko wa
hedhi . Mbinu hizo zinaweza kutumika ili kuzuia mimba isiyotamaniwa na vilevile kupata mimba iliyotamaniwa, lakini pia kama njia ya kusimamia afya ya uzazi wa mwanamke.
Mbinu kadhaa za kubaini siku ambazo mwanamke hawezi kupata mimba zinajulikana tangu zamani, lakini ujuzi wa ki sayansi uliopatikana katika karne ya 20 umeongeza sana idadi na hasa usahihi wa mbinu hizo.
Kutoka mwaka 1930 hadi 1980 , utafiti na ukuzaji wa uelewa huo wa masuala ya uzazi ulifanywa hasa na wataalamu wanaohusika na
Kanisa Katoliki kwa lengo la kusaidia kupanga uzazi watu wa ndoa wanaokataa mbinu za
teknolojia kwa msingi wa maadili au kwa kuzingatia ma dhara yake.
Kwa kiasi kikubwa mashirika yanayotafuta na kueneza ufahamu wa uwezo wa kushika mimba yanaendelea kuongozwa na Wakatoliki, lakini baadhi ya mashirika ya kawaida sasa yapo.
Mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutegemea uchunguzi wa mabadiliko ya ishara za msingi yanayoashiria uwezekano wa kutunga mimba (kama vile joto la mwili , ute wa uke , na mkao wa seviksi ) kwa kufuatilia mzunguko wote wa hedhi na hivyo kubaini wakati ambapo inawezekana kushika mimba.
Ishara nyingine pia zinaweza kuzingatiwa: hizo ni pamoja na ulaini wa ma titi na uchungu wakati kijiyai kinapoachiliwa, uchunguzi wa
mkojo kwa vifaa vya kubashiri udondoshwaji wa vijiyai, na uchunguzi wa ki hadubini wa ute au ugiligili wa seviksi (yaani mlango wa kizazi). Isitoshe, ipo njia ya kufuatilia uwezo wa kushika mimba kwa tarakilishi .
Istilahi
Mbinu zinazotegemea dalili zinafuatilia moja au zaidi kati ya ishara tatu za msingi za kuweza kutunga mimba - joto la msingi la mwili, ute wa uke na mkao wa seviksi. [1]
Mbinu zinazotegemea ute wa uke tu ni pamoja na Mbinu ya Billings ya Kutambua Kijiyai Kuachiliwa, The Ovulation Method , Mbinu ya Creighton, na Mbinu ya Siku Mbili.
Mbinu za dalili ya joto la mwili hujumuisha pia uchunguzi wa joto la msingi la mwili (basal body temperature = BBT), ute wa uke, na wakati mwingine mkao wa seviksi.
Mbinu zinazotegemea kalenda hufuatilia mzunguko wa hedhi ya mwanamke na kwa kuzingatia urefu wa mzunguko wake kutambua anapoweza kupata mimba. Mbinu maarufu zaidi kati ya hizo ni Mbinu ya Siku Sanifu.
Mbinu ya Urari-Kalenda pia huhesabiwa njia ya kutegemea kalenda, ingawa haijafafanuliwa vizuri na ina maana nyingi tofauti kwa watu tofauti.
Mbinu hizo za kupanga uzazi zinaweza kuitwa Mbinu za Uzazi Zinazotegemea Ufahamu (wa uwezo wa kuzaa), [2] Jina "Mbinu ya Uelewa wa Uzazi" (kwa Kiingereza Fertility Awareness Method = FAM) linatumika hasa kwa mfumo uliofundishwa na Toni Weschler. Jina "Mbinu Asili ya Uzazi wa Mpango" (kwa Kiingereza natural family planning = NFP) wakati mwingine hutumiwa kutaja mbinu yoyote inayotegemea Ufahamu wa Uzazi. Hata hivyo, msamiati huo ni mahsusi kuhusu mbinu zile zinazokubaliwa na Kanisa Katoliki: mbali ya uwezekano wa kutopata mimba wakati wa kunyonyesha (kwa Kiingereza Lactational amenorrhea method = LAM), ni kutofanya tendo la ndoa siku ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Hapo mbinu za FA zinaweza kutumika ili kutambua nyakati hizo zinazoweza kuleta mimba.
Wanawake ambao wananyonyesha na wanapenda kukwepa mimba wanaweza kutegemea kukatizwa kwa hedhi wakati wa kunyonyesha. Hiyo ni tofauti na ufahamu wa uzazi, lakini kwa sababu haihusishi vifaa wala kemikali, mara nyingi hutajwa pamoja na FA kama njia asili ya uzazi wa mpango.
Historia
Ukuaji wa mbinu zinazotegemea kalenda
Haijulikani kwa hakika lini iligunduliwa kwa mara ya kwanza kuwa wanawake wana vipindi vya kutunga mimba na visivyo vya kutunga mimba vinavyoweza kutabirika. Mwaka 388
Agostino wa Hippo aliandika kuhusu kuepuka mara kwa mara tendo la ndoa ili kuzuia mimba akiwalaumu Wamani kwa kutumia njia hiyo ili kubaki bila watoto. [3]
Kitabu fulani kinasema kuacha ngono kwa muda kulipendekezwa na "watu wachache wasio wa dini tangu katikati ya karne ya 19", [4] lakini katika karne ya 20 ushawishi mkuu uliohamasisha mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulitoka katika Kanisa Katoliki.
Mwaka 1905 Theodoor Hendrik van de Velde,
mwanajinakolojia wa Uholanzi, alionyesha kuwa wanawake hutoa kijiyai mara moja tu kila mzunguko wa hedhi. [5] Miaka ya 1920
Kyusaku Ogino , mwanajinakolojia wa Ujapani , na Hermann Knaus , kutoka Austria , wakifanya kazi bila ushirikiano waligundua kwamba kijiyai hutokea siku kumi na nne hivi kabla ya kipindi cha hedhi kinachofuata. [6] Ogino alitumia uvumbuzi wake kutengeneza hesabu ya kuwasaidia wanawake wasiopata mimba kwa kufanya tendo la ndoa kwa wakati mwafaka kupata mimba. Mwaka 1930 John Smulders , daktari Mkatoliki kutoka Uholanzi, alitumia uvumbuzi huo kuunda mbinu ya kuepuka mimba. Smulders alichapisha kazi yake chini ya Chama cha Matabibu Wakatoliki wa Uholanzi, na hiyo ilikuwa mbinu sanifu ya kwanza ya kuepuka mimba kwa kuacha kujamiiana kwa kipindi fulani - mbinu ya kalenda. [6]
Uanzilishi wa mbinu za dalili za joto na ute wa mlango wa uzazi
Katika miaka ya 1930, Wilhelm Hillebrand , padri Mkatoliki nchini Ujerumani , alitunga mbinu ya kuzuia mimba kwa kutegemea joto la msingi la mwili. [7] Mbinu hiyo ya joto ilionekana kuwa na ufanisi mkubwa zaidi katika kuwasaidia wanawake kuzuia mimba kuliko mbinu ya kutegemea kalenda. Katika miongo michache iliyofuata, mbinu hizo mbili zikawa zinatumika sana miongoni mwa wanawake Wakatoliki. Hotuba mbili zilizotolewa na Papa Pius XII mwaka 1951 zilitoa kibali cha hali ya juu kutoka Kanisa Katoliki kwa mbinu hizo kutumiwa na mume na mke waliohitaji kuzuia mimba. [4][8]
Mwanzo mwa miaka ya 1950 , John Billings aligundua uhusiano kati ya ute wa mlango wa uzazi na uwezekano wa kutunga mimba alipokuwa akifanya kazi katika Shirika Katoliki la Ustawi wa Jamii mjini Melbourne , Australia . Billings na madaktari wengine kadhaa, akiwemo mke wake Evelyn , walifanyia utafiti ishara hiyo kwa miaka kadhaa, na kufikia mwishoni mwa miaka ya 1960 walikuwa wamefanya majaribio ya kitabibu na kuanzisha vituo vya kufundishia mbinu yao duniani kote. [9]
Mashirika ya kwanza ya ufundishaji mbinu zilizozingatia dalili
Japo awali akina Billings walifundisha pamoja mbinu za dalili ya joto na ya ute wa uke, walipata shida katika kufundisha ishara ya joto kwa idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika katika nchi zinazoendelea . Hivyo katika miaka ya 1970 walibadilisha mbinu ili kutegemea ute tu. [7] Taasisi ya kimataifa iliyoanzishwa na Billings sasa inajulikana kama "Shirika la Kimataifa la Mbinu ya Kudondosha Kijiyai ya Billings" (kwa Kiingereza World Organization Ovulation Method Billings = WOOMB).
Shirika la kwanza kufundisha mbinu ya dalili za joto lilianzishwa mwaka 1971 . John na Sheila Kippley , walei Wakatoliki, walijiunga na Konald Prem katika kufundisha mbinu iliyotegemea dalili zote tatu: joto, ute na mkao wa mlango wa uzazi. Taasisi yao sasa inaitwa "Shirika la Kimataifa la Wanandoa kwa Wanandoa" (kwa Kiingereza "Couple to Couple League International"). [7]
Muongo uliofuata ulishuhudia kuanzishwa kwa mashirika mengine ya Kikatoliki ambayo sasa ni makubwa - "Familia ya Amerika" (kwa Kiingereza "Family of the Americas") iliyoundwa mwaka 1977 na kufundisha mbinu ya Billings, [10] halafu "Taasisi ya Papa Paulo VI " ( 1985 ), inayofundisha mbinu mpya ya ute pekee iitwayo Creighton Model. [11]
Hadi miaka ya 1980 , habari kuhusu ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulipatikana tu kutoka vyanzo vya Kikatoliki. [12] Shirika la kwanza lisilo la kidini la kutolea mafundisho hayo ya uzazi lilikuwa Kituo cha Uelewa wa Uzazi cha New York, lililoanzishwa mwaka
1981 . [13] Toni Weschler alianza kufundisha mwaka 1982 na kuchapisha kitabu kilichouzwa sana cha Taking Charge of Your Fertility mwaka
1995 . [14] "Justisse" ilianzishwa mwaka 1987 huko Edmonton, Kanada . [15] Mashirika hayo yote yasiyo ya kidini yanafundisha mbinu ya dalili za joto. Ingawa mashirika ya Kikatoliki yanayoeneza uelewa wa uzazi ni makubwa sana kuliko hayo ya wanaharakati yasiyo ya kidini, walimu wasiotegemea dini wamezidi kuongezeka katika miaka ya 1990 na milenia mpya .
Maendeleo ya sasa
Ustawi wa mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaendelea. Mwishoni mwa miaka ya 1990, "Taasisi ya Afya ya Uzazi " katika Chuo Kikuu cha Georgetown ilianzisha mbinu mbili mpya. [16][17] Mbinu ya Siku Mbili, inayotegemea ute tu, na CycleBeads , ambayo inafuata mbinu ya Siku Sanifu na ina pia toleo la kieletroniki, iCycleBeads), zimeundwa ili kuwa na ufanisi na urahisi mkubwa zaidi katika kufundisha, kujifunza, na kutumia.
Ishara za uwezo wa kushika mimba
Mizunguko mingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kupatikana (muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai), halafu siku ambazo mimba inaweza kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika ( muda wa kutoshika mimba baada ya kijiyai kudondoshwa). Siku ya kwanza ya kuvuja damu inahesabiwa kuwa siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Mbinu mbalimbali za kufahamu uwezo wa kushika mimba huhesabu kwa njia tofauti kidogo kipindi ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba, yaani hutumia ishara za msingi za uwezekano huo, historia ya mzunguko, au zote mbili.
Ishara za msingi za kuweza kupata mimba
Ishara tatu za msingi za uwezekano wa kushika mimba ni joto msingi la mwili, ute wa uke na mkao wa seviksi. Mwanamke anayetumia dalili hizo ili kujua uwezo wake wa kupata mimba anachagua kutumia ishara moja, mbili, au zote tatu pamoja. Wanawake wengi hung'amua pia ishara nyingine za ziada kulingana na mzunguko wa hedhi, kama vile maumivu na uzito tumboni, maumivu mgongoni, ulaini wa matiti na maumivu ya kudondosha kijiyai.
Joto la msingi la mwili
Joto la msingi la mwili ni joto la mwili wa mtu linalopimwa wakati wa kwanza anapoamka asubuhi (au baada ya usingizi wa muda mrefu zaidi katika siku). Miongoni mwa wanawake, kudondoshwa kijiyai husababisha joto kupanda kwa 0.3°C hadi 0.9° C (0.5°F hadi 1.6°F) na kubakia hivyo kipindi chote hadi wakati wa hedhi ijayo. Mabadiliko hayo ya joto yanaweza kutumika kubaini mwanzo wa kipindi cha kutoweza kutungika mimba kabla ya kudodosha kijiyai.
Ute wa uke
Ute wa uke
Kuonekana kwa ute wa uke na mwasho wake ni ishara zinazoelezwa kwa kawaida pamoja kama njia za kubaini ishara hiyohiyo. Ute wa uke huzalishwa na seviksi, ambayo huunganisha mji wa mimba na mfereji wa uke. Ute wa uke wenye uwezo wa kushika mimba hukuza maisha ya manii kwa kupunguza uasidi wa uke, na husaidia kuongoza manii kupitia seviksi na kuelekea ndani ya mji wa mimba. Uzalishaji wa ute wa uke wenye uwezo wa kupata mimba husababishwa na homoni ileile ( istrojeni ) ambayo huandaa mwili wa mwanamke kwa udondoshwaji wa kijiyai . Kwa kuangalia ute wa uke wake, na kuzingatia hisia pindi unapopita ukeni, mwanamke anaweza kubaini wakati mwili wake unapojiandaa kudondosha kijiyai, na wakati ambapo udondoshwaji wa kijiyai umepita. Kijiyai kikidondoshwa, uzalishwaji wa istrojeni hupungua na projesteroni huanza kuongezeka. Kupanda kwa kiwango cha projesteroni husababisha mabadiliko maalumu katika wingi na hali ya ute wa uke. [18]
Mkao wa seviksi
Seviksi hubadilisha mkao kutokana na homoni zilezile zinazosababisha ute wa uke kutolewa na kukauka. Wakati mwanamke yuko katika awamu ya kutoshika mimba katika mzunguko wa hedhi, seviksi hushuka chini katika mfereji wa uke, ikiguswa huwa ngumu (kama ncha ya
pua ya mtu), na upenyu (mlango wa seviksi) unakuwa mdogo ukilinganishwa na wakati mwingine, au umefungika. Kadiri mwanamke anavyozidi kuwa na uwezo wa kushika mimba ndivyo seviksi inavyopanda juu katika mfereji wa uke, inakuwa laini ikiguswa (kama mdomo wa mtu), na upenyu unakuwa wazi zaidi. Baada ya kudondoshwa kwa kijiyai, seviksi itarejea mkao wake wa wakati usio wa kushika mimba.
Historia ya mzunguko
Mbinu zinazotegemea kalenda hubainisha uwezekano wa kutopata mimba kabla na baada ya kudondosha kijiyai kulingana na historia ya mzunguko. Zinapotumika vizuri kuzuia mimba, mbinu hizo si madhubuti kama mbinu zinazotegemea dalili, hata hivyo umadhubuti wake unalingana na mbinu zuizi kama vile
kiwambo na kizibo cha seviksi .
Mbinu za kuepuka mimba zinazotegemea ute wa uke na joto la mwili kubainisha uwezo wa kutunga mimba baada ya kijiyai kudondoshwa, hushindikana mara chache sana zinapotumika vizuri. [19] Hata hivyo, mbinu hizo huwa na upungufu fulani katika kubaini uwezo wa kutotunga mimba kabla ya kudondosha kijiyai. Rekodi ya joto la mwili pekee haitoi mwongozo kuhusu uwezekano wa mimba kutungwa au kutotungwa kabla ya kijiyai kudondoshwa. Kubaini uwezekano wa kutoshika mimba kabla ya tukio hilo kunaweza kufanywa kwa kuchunguza ute wa uke; hata hivyo, njia hii inafanikiwa kwa kiwango cha chini kuliko ule unaoshuhudiwa katika kipindi baada ya kudondosha kijiyai. [20] Kutegemea uchunguzi wa ute pekee pia ina maana kwamba tendo la ndoa haliruhusiwi wakati wa hedhi, kwa sababu ute wowote hautakuwa dhahiri. [21]
Matumizi ya sheria fulani za kalenda katika kutambua urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya kijiyai kudondoshwa huruhusu siku chache za ngono mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi huku kukiwa na kiwango cha chini sana cha uwezekano wa kupata mimba. [22] Kwa kutumia mbinu ya ute pekee, kuna uwezekano wa kukosea kwa kudhani ni hedhi damu inapotoka katikati ya mzunguko wa hedhi au wakati ambapo kijiyai halikudondoshwa. Kuweka chati sahihi ya joto la msingi la mwili huwezesha utambuzi wa hedhi, wakati ambapo sheria za kalenda kuhusu kipindi kabla ya kudondosha kijiyai zinaweza kutumiwa kwa usahihi. [23] Katika mbinu za joto pekee, sheria ya kalenda inaweza kutegemewa pale tu kutambua uwezekano wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai. Katika mbinu za joto na ishara, sheria ya kalenda huthibitishwa na rekodi za ute: uchunguzi wa ute wa uke unaoashiria uwezo wa kupata mimba unapewa kipaumbele kuliko mbinu yoyote ya kalenda ya kubainisha uwezo wa kushika mimba. [22]
Sheria za kalenda zinaweza kuweka idadi mahsusi ya siku, ikibainisha kwamba (kulingana na urefu wa mizunguzo iliyopita ya hedhi ya mhusika) siku tatu hadi sita za kwanza katika kila mzunguko wa hedhi huchukuliwa kuwa hazina uwezo wa kupata mimba. [24] Au, sheria ya kalenda inaweza kuhitaji hesabu, kwa mfano lazima iwe kwamba urefu wa kipindi kisicholeta uzazi kabla ya kudondosha kijiyai ni sawa na urefu wa mzunguko mfupi zaidi wa mwanamke huyo ukiondoa siku ishirini na moja. [25] Badala ya kutegemea urefu wa mzunguko, sheria ya kalenda inaweza kuhakikishwa kutokana na siku ya mzunguko ambapo mwanamke ameshuhudia badiliko la joto la mwili. Mfumo mmoja unasema urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya kudondosha kijiyai unalingana na siku ya kwanza ambapo mwanamke alishuhudia kupanda joto la mwili ondoa siku saba. [26]
Mbinu nyingine
Vifaa vya kubashiri udondoshwaji wa kijiyai (kwa Kiingereza Ovulation predictor kits = OPKs) vinaweza kutambua udondoshwaji unaokaribia kutokea kwa kutegemea wingi wa homoni ya kuandaa ukuta wa chupa ya kizazi (kwa Kiingereza "lutenizing hormone" = LH) katika mkojo wa mwanamke. Kwa kawaida ubashiri wa kufana wa undondoshwaji huo hufuatiwa na udondoshwaji ndani ya saa 12-36.
Uchunguzi wa mate kwa hadubini, ukifanyika kwa usahihi, unaweza kugundua vijidutu maalum katika mate ambavyo hutangulia udondoshwaji wa kijiyai. Vijidutu hivyo kwa kawaida huonekana siku tatu kabla ya udondoshwaji na kuendelea mpaka udondoshwaji utokee. Katika kipindi hiki, vijidutu hivyo hutokea katika ute wa uke pamoja na mate.
Vichunguza uzazi vya kieletroniki vinapatikana kwa majina mbalimbali ya ki biashara . Vichunguzi hivyo vinaweza kutumia mifumo ya Joto la Msingi la Mwili pekee, au kuchambua vitepe vya kupimia mkojo, au kufuatilia dalili mchanganyiko au kuchunguza ukinzani umeme wa mate na ugiligili wa uke, au kwa pamoja baadhi ya mambo hayo mbalimbali .
Manufaa na mapungufu
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba una kiwango fulani cha sifa bainifu:
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika kudhibiti afya ya uzazi. Mabadiliko katika mzunguko wa hedhi yanaweza kumtahadharisha mtumiaji kuhusu kujitokeza kwa matatizo ya kiginakolojia. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba pia unaweza kutumika kusaidia katika kuagua matatizo yanayojulikana ya kijinakolojia kama vile kutoweza kushika mimba.
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ni uwanda mpana: unaweza kutumika kuzuia mimba au kusaidia katika kutunga mimba.
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumiwa na wanawake wote katika kipindi chote cha uzazi, bila kujali ikiwa anakaribia kumaliza kuzaa, ananyonyesha, au anapata mzunguko wa hedhi usio wa kawaida kwa sababu zingine.
Matumizi ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi mwili wa mwanamke unavyofanya kazi, na unaweza kuwaruhusu wanawake kuwa na udhibiti mkubwa wa uzazi wao wenyewe.
Aina fulani ya mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba zinazotegemea dalili ya uzazi zinahitaji uchunguzi au kugusa ute wa uke, matendo ambayo baadhi ya wanawake hawafurahii. Baadhi ya wahudumu wanapendelea kutumia neno "majimaji ya seviksi" badala ya ute wa uke, katika juhudi ya kuwafanya wanawake kama hao kuhisi huru kidogo.
Baadhi ya dawa, kama vile ya kupunguza kupaliwa mapafuni, yanaweza kubadili ute ya kizazi. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi, ishara ya ute huenda isionyeshe kisahihi uwezo wa kutunga mimba . [27]
Baadhi ya mbinu zinazotegemea dalili huhitaji ufuatiliaji wa joto la kimsingi ya mwili. Kwa sababu usingizi usiokuwa na utaratibu unaweza kuvuruga usahihi wa joto la kimsingi la mwili, wafanyakazi wa kubadilisha zamu na walio na watoto wadogo sana, kwa mfano, huenda wasiweze kutumia mbinu hizo. [27]
Kama njia ya kupanga uzazi
Kwa kufanya tendo kamili la ndoa siku zile tu ambapo katika mzunguko wa hedhi mimba haiwezi kutungwa, maharusi wanaweza kuzuia mimba isipatikane. Wakati ambapo katika mzunguko wa hedhi mimba inaweza kutungwa, wanaweza wakaacha ngono ili kuwa na hakika ya kutoitunga. Wengine siku hizo wanatumia mbinu mbadala za kuzuia mimba ingawa pengine hazifai kwa sababu mbalimbali. [28] Kinyume chake maharusi wanaweza kulenga uzazi kwa hakika zaidi wakifanya tendo la ndoa kwa kutumia vizuri siku zinazouwezesha.
Manufaa
Katika kutumia ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hakuna madhara yanayotokana na teknolojia inayotumiwa na mbinu nyingine. Kwa jumla hakuna madhara yoyote ya utumiaji, isipokuwa yanayoweza kutokea kwa kuingiza vidole ndani ya uke ili kuchunguza seviksi (kama inavyopendekezwa na baadhi ya mbinu).
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza ukatumika pamoja na vifaa vya kuzuia mimba ili kuendelea kujamiiana katika kipindi ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Tofauti na utumiaji wa vifaa hivyo bila ufahamu wa uwezo wa kushika mimba, ufahamu huo unawezesha kutumia vizuiamimba siku chache tu, na hivyo kupunguza madhara yanayoletwa navyo.
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hauna gharama au ni nafuu sana. Watumiaji wanaweza wakahitaji kununua chati, kalenda,
kipimajoto , au tarakilishi, au pengine kumlipa
mkufunzi . Kwa vyovyote gharama ni ya chini ikilinganishwa na mbinu nyingine.
Tofauti na mbinu nyingine mbalimbali ambazo zina athari za muda mrefu, ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unawezesha kubadili mara moja kutoka uamuzi wa kuzuia mimba hadi ule wa kuilenga.
Mapungufu
Wasipotumia vifaa vya kizuia mimba katika kipindi ambapo mimba inaweza kutungwa, wanandoa wanalazimika waache ngono. Ila kupunguza uwezekano wa kupata mimba uwe chini ya 1% kwa mwaka, katika kila mzunguko kuna takriban siku 13 ambapo lazima waache ngono. [29] Kwa wanawake wenye mzunguko unaobadilikabadilika sana - kama ilivyo kawaida wakati wa kunyonyesha, karibu na hedhi kwisha kabisa, au kwa wenye magonjwa ya homoni (kama vile Polycystic ovary syndrome = PCOS) kuacha kujamiiana au kutumia vizuizi kunaweza kuhitajika miezi mfululizo. Wengi hawana motisha au nidhamu ya kutosha wafanye hivyo kwa muda mrefu. Wanaposhindwa kufuata masharti, ni rahisi kupata mimba isiyopangwa.
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba haukingi dhidi ya maradhi ya zinaa. [30] Ndiyo maana inafaa zaidi kati ya watu ambao ni waaminifu wao kwa wao, kama watu wa ndoa.
Ufanisi
Ufanisi wa ufahamu ya uzazi, kama ulivyo kwa mbinu nyingi za uzazi wa mpango, unaweza kutathminiwa kwa njia mbili zifuatazo. Kwa kawaida mfumo wa Pearl Index hutumika kukokotoa viwango vya ufanisi, lakini baadhi ya tafiti hutumia majedwali ya mapunguzo. [31]
Kwa kawaida viwango hupimwa katika mwaka wa kwanza wa matumizi. [32] Viwango vya
matumizi kamili ni kwa wale tu wanaofuata sheria zote, wakitambua kwa usahihi kipindi ambapo kuna uwezekano wa kutunga mimba, na wanaacha ngono isiyo na kinga siku walizotambua kuna uwezekano wa kuitunga. Viwango vya matumizi halisi au matumizi ya kawaida ni kwa wale wote wanaotegemea ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ili kuizuia, wakiwa ni pamoja na wasioweza kutimiza vigezo vya "matumizi kamili".
Kiwango cha kufeli kwa ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutofautiana pakubwa kulingana na mbinu iliyotumika kubaini uwezekano wa kupata mimba, njia ya mafundisho, na idadi ya wanaotafitiwa. Baadhi ya tafiti zimekuta viwango halisi vya kufeli vya 25% kwa mwaka au zaidi. [33][34][35] Angalau utafiti mmoja umepata kiwango cha kufeli cha chini ya 1% kwa mwaka kukiwa na mafundisho endelevu na mapitio ya kila mwezi, [36] na tafiti kadhaa zimegundua viwango vya kufeli halisi vya 2-3% kwa mwaka. [29][37][38][39]
Inapotumika kwa usahihi, na kuandamana na mafundisho endelevu ya mara kwa mara, baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mbinu fulani za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba huwa na 99% za ufanisi, [36][40][41][42]
Kitabu Teknolojia ya Uzazi kinaripoti hivi: [43]
Mbinu za baada ya kudondosha kijiyai (yaani kuacha ngono kuanzia wakati wa hedhi mpaka baada ya kudondoshwa) inafeli kwa 1% kwa mwaka.
Mbinu ya dalili na joto la mwili inafeli kwa 2% kwa mwaka.
Mbinu ya ute wa uke pekee inafeli kwa 3% kwa mwaka.
Mbinu ya urari wa kalenda inafeli kwa 9% kwa mwaka.
Mbinu ya Siku Wastani inafeli kwa 5% kwa mwaka.
Sababu za ufanisi mdogo katika matumizi ya kawaida
Sababu kadhaa zinachangia kufanya ufanisi wa matumizi ya kawaida uwe wa chini kuliko ule wa matumizi kamili:
watumiaji kutotii kwa makusudi maelezo (kushiriki ngono bila kinga siku ambapo wanajua mimba inaweza kutungwa): ndiyo sababu ya kawaida zaidi [29][42]
makosa ya watoa maelezo ya jinsi ya kutumia mbinu (mkufunzi kutoa taarifa isiyo sahihi au isiyo kamili)
makosa ya mtumiaji (kutoelewa sheria, kutunza kumbukumbu vibaya)
Kama njia ya kupata mimba
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika pia kwa lengo la kupata mimba kwa urahisi zaidi.
Kupanga wakati wa kujamiiana
Utafiti uliofanywa na Barrett na Marshall umeonyesha kuwa vitendo vya ngono visivyopangwa huwa na uwezekano wa 24% kutungisha mimba katika mzunguko wa hedhi. Utafiti huo pia uligundua kuwa ngono inayolenga wakati maalumu kulingana na ufahamu unaotokana na mbinu ya joto la msingi la mwili pekee huongeza viwango vya mimba hadi 31% -68%.
Utafiti wa mbinu ya ute wa uke umegundua viwango vya mimba vya 67%-81% katika mzunguko wa kwanza ikiwa kujamiiana kutatokea katika Siku ya Kilele cha ishara za ute. [44][45]
Kwa sababu ya viwango vya juu vya mimba kutoka mapema sana (25% za mimba hupotea katika wiki sita za kwanza tangu hedhi ya mwisho ya mwanamke), mbinu zinazotumika kuchunguza uwepo wa mimba zinaweza kusababisha upendeleo katika viwango vya utungaji mimba. Mbinu tofauti na hizo zinaweza kuonyesha viwango vya chini kwa sababu tu huwa zinakosa kugundua mimba zilizotoka mapema. Utafiti mmoja nchini China kati ya wanaoshiriki ngono bila mpangilio ili kutungisha mimba ulitumia mbinu bora za kugundua mimba, ikapata kiwango cha 40% cha kutungwa mimba kwa kila mzunguko katika kipindi cha utafiti cha miezi 12. [46]
Uchunguzi wa tatizo
Mizunguko ya kawaida ya hedhi wakati mwingine huchukuliwa kuwa ushahidi kwamba mwanamke anadondosha vijiyai kawaida, na mizunguko isiyo ya kawaida kuwa ushahidi kuwa udondoshaji wa kijiyai si wa kawaida. [47] Hata hivyo, wanawake wengi ambao mizunguko yao si ya kawaida hudondosha vijiyai kama kawaida, na baadhi ya wenye mizunguko ya kawaida kwa kweli hawadondoshi vijiyai au wana matatizo katika utayarishaji wa ukuta wa chupa cha uzazi. Hasa rekodi za joto la msingi la mwili, lakini pia rekodi za ute wa uke na mkao wake, zinaweza kutumika kwa usahihi kung'amua ikiwa mwanamke anadondosha kijiyai, na kama urefu wa kipindi cha baada ya kudondosha kijiyai cha mzunguko wa hedhi unatosha kwa ujauzito.
Ute wa uke unaoweza kutunga mimba ni muhimu katika kujenga mazingira ambayo yanaruhusu manii kupiti mlango wa uzazi na katika viriba vya falopu ambako husubiri kudondoshwa kwa kijiyai. [48] Chati za uwezo wa kupata mimba zinaweza kusaidia kugundua ute hasimu kwa mimba kutungwa, ambao ni sababu ya kawaida ya kutopata mimba. Ikiwa hali hii itagunduliwa, baadhi wanapendekeza matumizi ya guaifenesini katika siku chache kabla ya udondoshwaji wa kijiyai ili kupunguza uzito wa ute. [49]
Upimaji mimba na umri wa ujauzito
Vipimo vya ujauzito si sahihi mpaka wiki 1-2 baada ya kudondoshwa kijiyai. Kujua tarehe inayokisiwa ambayo kijiyai kitadondoka kunaweza kukamzuia mwanamke asipate matokeo yasiyo sahihi kutokana na upimaji wa mapema mno. Pia, siku 18 mfululizo za joto la juu zinamaanisha mwanamke ni mjamzito karibu bila shaka. [50]
Makadirio ya tarehe ya kudondosha kijiyai kutokana na chati za uwezo wa kuzaa ni njia sahihi zaidi ya kukadiria umri wa ujauzito kuliko mbinu za jadi za kupima mimba au mbinu ya kuchunguza hedhi ya mwisho katika utaratibu wa kufuatilia hedhi. [51]
Kama njia ya kupanga jinsia ya mimba
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika pia kwa lengo la kupata mimba ya jinsia inayotamaniwa zaidi. [52] Maharusi wanaweza kuchagua mtoto wa kiume au wa kike kwa 85% ya hakika wakifanya tendo la ndoa kwa kupanga kulingana na ute wa uke kuwa wa kuvutika na kuteleza au siyo. Ni kwamba jinsia ya mimba inategemea tu kromosomu za mbegu za baba ambazo ni nusunusu: X kwa kuzaa watoto wa kike na Y kwa kuzaa watoto wa kiume. Mbegu zenye kromosomu X ni dhaifu kidogo nazo huogelea polepole, lakini zinaishi muda mrefu. Kumbe zenye kromosomu Y zina nguvu zaidi na kuogelea upesi, lakini hufa upesi.
Ili kupata mtoto wa kiume
Kwa kuzingatia tabia hizo mbili tofauti, maharusi wakitaka mtoto wa kiume wanatakiwa kufanya tendo la ndoa siku ya kwanza baada ya kilele (kujisikia kuteleza) na kuendelea kwa miandamo 6 ya hedhi. Kama mwanamke hajapata mimba baada ya miandamo 6, waanze kuonana siku ya kilele na siku inayofuata. Kama mwanamke amekosa siku ya kilele, yaani kama utelezi wa ute unaendelea siku inayofuata, waonane tena siku inayofuata. Kwa njia hiyo mbegu zenye kromosomu Y tu zitafikia kijiyai kilichochopoka, kwa sababu mbegu zenye kromosomu X zinaogelea polepole tu.
Ili kupata mtoto wa kike
Kinyume chake, wakitaka mtoto wa kike wanatakiwa kufanya tendo la ndoa siku ya kwanza ya ute wa uzazi. Halafu wapumzike mpaka siku ya nne baada ya kilele. Waendelee hivyo kwa miandamo michache. Kama mwanamke hajapata mimba baada ya miezi michache, wafanye tendo la ndoa siku ya kwanza na ya pili ya ute wa uzazi halafu wapumzike mpaka siku ya nne baada ya kilele. Waendelee hivyo kwa miandamo michache. Kama mwanamke hajapata mimba baada ya miezi michache, wafanye tendo la ndoa pia siku ya tatu ya ute wa uzazi halafu wapumzike mpaka siku ya nne baada ya kilele. Waendelee hivyo kwa miandamo michache. Kwa njia hiyo mbegu zenye kromosomu Y zitakufa kabla ya kuweza kuungana na kijiyai, na hivyo zitabaki zenye kromosomu X kuwa na nafasi hiyo. Siku nzuri ya kupata mtoto wa kike ni kufanya tendo la ndoa siku mbili kabla ya kilele.
Tazama pia
Uzazi wa mpango
Uzazi wa mpango kwa njia asilia
Tanbihi
1. ↑ Weschler, Toni (2002). Taking Charge of Your Fertility , Revised, New York: HarperCollins, 52. ISBN 0-06-093764-5 .
2. ↑ Medical Eligibility Criteria for Contraceptive Use:Fertility awareness-based methods . Fourth edition. World Health Organization. 2010. http://www.who.int/reproductivehealth/publications/family_planning/9789241563888/en/index.html . Retrieved 2012-12-11.
3. ↑ Saint, Bishop of Hippo Augustine; Philip Schaff (Editor) (1887). A Select Library of the Nicene and Post-Nicene Fathers of the Christian Church, Volume IV . Grand Rapids, MI: WM. B. Eerdmans Publishing Co., On the Morals of the Manichæans , Chapter 18 .
4. ↑ 4.0 4.1 Yalom, Marilyn (2001). A History of the Wife , First, New York: HarperCollins, 297–8, 307. ISBN 0-06-019338-7 .
5. ↑ A Brief History of Fertility Charting .
FertilityFriend.com . Iliwekwa mnamo 2006-06-18.
6. ↑ 6.0 6.1 Singer, Katie (2004). The Garden of Fertility . New York: Avery, a member of Penguin Group (USA), 226–7. ISBN 1-58333-182-4 .
7. ↑ 7.0 7.1 7.2 Hays, Charlotte. "Solving the Puzzle of Natural Family Planning" . Holy Spirit Interactive. http://www.holyspiritinteractive.net/features/prolife/article_05.asp . Retrieved 2012-02-15.
8. ↑ [18] ^ Moral Questions Affecting Married Life: Addresses given October 29, 1951 to the Italian Catholic Union of midwives 26 Novemba 1951 to the National Congress of the Family Front and the Association of Large Families, National Catholic Welfare Conference, Washington, DC.
9. ↑ Billings, John (Machi 2002). "THE QUEST — leading to the discovery of the Billings Ovulation Method" . Bulletin of Ovulation Method Research and Reference Centre of Australia 29 (1): 18–28. http://www.woomb.org/omrrca/bulletin/vol29/no1/thequest.shtml . Retrieved 2007-03-18.
10. ↑ About us . Family of the Americas (2006). Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
11. ↑ About the Institute . Pope Paul VI Institute (2006). Iliwekwa mnamo 2012-02-21.
12. ↑ Singer (2004), p.xxiii
13. ↑ About us . Fertility Awareness Center (2006). Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
14. ↑ Weschler (2002)
15. ↑ About Us . Justisse (2002). Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-11-16. Iliwekwa mnamo 2007-03-18.
16. ↑ Arévalo M, Jennings V, Sinai I (2002).
"Efficacy of a new method of family planning: the Standard Days Method." (PDF).
Contraception 65 (5): 333–8. doi: 10.1016/S0010-7824(02)00288-3 .
PMID 12057784 . http://pdf.dec.org/pdf_docs/PNACQ416.pdf .
17. ↑ Jennings V, Sinai I (2001). "Further analysis of the theoretical effectiveness of the TwoDay method of family planning".
Contraception 64 (3): 149–53. doi: 10.1016/S0010-7824(01)00251-7 .
PMID 11704093 .
18. ↑ James B. Brown (2005). Physiology of Ovulation . Ovarian Activity and Fertility and the Billings Ovulation Method . Ovulation Method Research and Reference Centre of Australia.
19. ↑ Kippley (2003), uk.121-134, 376-381
20. ↑ Kippley (2003), uk.114
21. ↑ Evelyn, Dr. Billings, Ann Westinore, (1998). The Billings Method: Controlling Fertility Without Drugs or Devices . Toronto: Life Cycle Books, 47. ISBN 0-919225-17-9 .
22. ↑ 22.0 22.1 Kippley (2003), uk.108-113
23. ↑ Kippley (2003), uk.101 sidebar na Weschler (2002), uk.125
24. ↑ Kippley (2003), uk.108-109 na Weschler (2002), uk.125-126
25. ↑ Kippley (2003), uk.110-111
26. ↑ Kippley (2003), uk.112-113
27. ↑ 27.0 27.1 How to Observe and Record Your Fertility Signs . Fertility Friend Handbook . Tamtris Web Services (2004). Iliwekwa mnamo 2005-06-15.
28. ↑ Manhart, MD; Daune, M; Lind, A; Sinai, I; Golden-Tevald, J (January–February 2013).
"Fertility awareness-based methods of family planning: A review of effectiveness for avoiding pregnancy using SORT." . Osteopathic Family Physician 5 (1): 2–8. doi : 10.1016/j.osfp.2012.09.002 . http://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S1877573X12001542 .
29. ↑ 29.0 29.1 29.2 Frank-Herrmann P, Heil J, Gnoth C, et al. (2007). "The effectiveness of a fertility awareness based method to avoid pregnancy in relation to a couple's sexual behaviour during the fertile time: a prospective longitudinal study". Hum. Reprod. 22 (5): 1310–9. doi: 10.1093/humrep/dem003 .
PMID 17314078 .
30. ↑ Fertility Awareness Method . Brown University Health Education Website . Brown University (2012). Iliwekwa mnamo 2012-12-11.
31. ↑ Kippley, John; Sheila Kippley (1996).
The Art of Natural Family Planning , 4th addition, Cincinnati, OH: The Couple to Couple League, 141. ISBN 0-926412-13-2 .
32. ↑ Hatcher, RA; Trussel J, Stewart F, et al. (2000). Contraceptive Technology , 18th, New York: Ardent Media. ISBN 0-9664902-6-6 .
33. ↑ Wade ME, McCarthy P, Braunstein GD, et al. (Oktoba 1981). "A randomized prospective study of the use-effectiveness of two methods of natural family planning".
American journal of obstetrics and gynecology
141 (4): 368–376. PMID 7025639 .
34. ↑ Medina JE, Cifuentes A, Abernathy JR, et al. (Desemba 1980). "Comparative evaluation of two methods of natural family planning in Colombia". American journal of obstetrics and gynecology 138 (8): 1142–1147.
PMID 7446621 .
35. ↑ Marshall J (Agosti 1976). "Cervical-mucus and basal body-temperature method of regulating births: field trial". Lancet 2 (7980): 282–283. doi : 10.1016/S0140-6736(76)90732-7 . PMID 59854 .
36. ↑ 36.0 36.1 Evaluation of the Effectiveness of a Natural Fertility Regulation Programme in China : Shao-Zhen Qian, et al. Reproduction and Contraception (English edition), in press 2000.
37. ↑ Frank-Herrmann P, Freundl G, Baur S, et al. (Desemba 1991). "Effectiveness and acceptability of the sympto-thermal method of natural family planning in Germany". American journal of obstetrics and gynecology 165 (6 Pt 2): 2052–2054. PMID 1755469 .
38. ↑ Clubb EM, Pyper CM, Knight J (1991).
"A pilot study on teaching natural family planning (NFP) in general practice" .
Proceedings of the Conference at Georgetown University, Washington, DC . http://www.fertilityuk.org/nfps822.html .
39. ↑ Frank-Herrmann P, Freundl G, Gnoth C, et al. (Juni-Septemba 1997). "Natural family planning with and without barrier method use in the fertile phase: efficacy in relation to sexual behavior: a German prospective long-term study". Advances in Contraception 13 (2-3): 179–189. doi: 10.1023/A:1006551921219 . PMID 9288336 .
40. ↑ Ecochard, R.; Pinguet, F.; Ecochard, I.; De Gouvello, R.; Guy, M.; Huy, F. (1998). "Analysis of natural family planning failures. In 7007 cycles of use". Fertilite Contraception Sexualite 26 (4): 291–6. PMID 9622963 .
41. ↑ Hilgers, T.W.; Stanford, J.B. (1998). "Creighton Model NaProEducation Technology for avoiding pregnancy. Use effectiveness".
Journal of Reproductive Medicine 43 (6): 495–502. PMID 9653695 .
42. ↑ 42.0 42.1 Howard, M.P.; Stanford, J.B. (1999). "Pregnancy probabilities during use of the Creighton Model Fertility Care System".
Archives of Family Medicine 8 (5): 391–402.
doi : 10.1001/archfami.8.5.391 .
PMID 10500511 .
43. ↑ James Trussell et al. (2000) "Contraceptive effectiveness rates",
Contraceptive Technology - 18 Edition, New York: Ardent Media. On-press.
44. ↑ Ryder R (1993). ""Natural family planning": effective birth control supported by the Catholic Church". BMJ 307 (6906): 723–6.
doi : 10.1136/bmj.307.6906.723 .
PMC 1678728 . PMID 8401097 .
45. ↑ Hilgers T, Daly K, Prebil A, Hilgers S (Oktoba 1992). "Cumulative pregnancy rates in patients with apparently normal fertility and fertility-focused intercourse". J Reprod Med 37 (10): 864–6. PMID 1479570 .
46. ↑ Wang X, Chen C, Wang L, Chen D, Guang W, French J (2003). "Conception, early pregnancy loss, and time to clinical pregnancy: a population-based prospective study". Fertil Steril 79 (3): 577–84. doi: 10.1016/S0015-0282(02)04694-0 .
PMID 12620443 .
47. ↑ "Infertility fact sheet" . womenshealth.gov, U.S. Department of Health and Human Services, Office on Women's Health. http://www.womenshealth.gov/publications/our-publications/fact-sheet/infertility.cfm#f . Retrieved 2012-12-11..
"Some signs that a woman is not ovulating normally include irregular or absent menstrual periods."
"Female Infertility" . Adult Health Advisor . 2012. http://www.ihacares.com/index.cfm/HealthAdvisors/AdultHealthAdvisor/crs-aha-aha_obg_female.infertility/ .. "A woman who is not ovulating normally may have irregular or missed menstrual periods."
"Is Clomid Right For You?" .
JustMommies.com . 2007. http://www.justmommies.com/articles/clomid-and-ovulation.shtml .. "If you have an irregular cycle there is a good chance you are not ovulating normally."
48. ↑ Ellington, Joanna (2004). Sperm Transport to the Fallopian Tubes . Frequently Asked Questions with Dr. E . INGfertility Inc. Iliwekwa mnamo 2008-04-27.
49. ↑ Weschler (2002), uk. 173.
50. ↑ Weschler (2002), uk.316
51. ↑ Weschler (2002), uk.3-4 ,155-156, Insert p.7
52. ↑ Ursula Birgitta Schnell OSB (2011).
Uimarishaji wa Familia - Mpango wa uzazi kwa njia ya asili Billings Ovulation Method , 15th, Ndanda, Tanzania: Benedictine Publication Ndanda-Peramiho. ISBN 9976-63-132-4 .
Marejeo
Kwa Kiswahili
Ursula Birgitta Schnell OSB (2011).
Uimarishaji wa Familia - Mpango wa uzazi kwa njia ya asili Billings Ovulation Method , 15th, Ndanda, Tanzania: Benedictine Publication Ndanda-Peramiho. ISBN 9976-63-132-4 .
Kwa Kiingereza
Toni Weschler (2006). Taking Charge of Your Fertility , 10th Anniversary, New York: Collins.
ISBN 0-06-088190-9 .
John F. Kippley and Sheila K. Kippley (1996). The Art of Natural Family Planning , Fourth, Cincinnati, OH: Couple to Couple League International. ISBN 0-926412-13-2 .
Léonie McSweeney (2006). Love & Life, Billings Method of Natural Family Planning , Ninth, Ibadan, Nigeria: African Universities Press. ISBN 978-148-092-0 .
Nakala inapatikana chini ya Creative Commons Attribution/Share-Alike License ; masuala ya ziada yanaweza kukubalika. Tazama Masharti ya Utumiaji kwa maelezo zaidi. Wikipedia ni nembo iliosajiliwa na Wikimedia Foundation, Inc. , asasi isiyokuwa ya kifaida.
Faragha • Dawati Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba
Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba (kwa Kiingereza "Fertility Awareness", kifupi FA) unahusu mbinu zinazotumika kutambua wakati mwanamke anapoweza kushika mimba na asipoweza kushika mimba katika mzunguko wa hedhi . Mbinu hizo zinaweza kutumika ili kuzuia mimba isiyotamaniwa na vilevile kupata mimba iliyotamaniwa, lakini pia kama njia ya kusimamia afya ya uzazi wa mwanamke. Mbinu kadhaa za kubaini siku ambazo mwanamke hawezi kupata mimba zinajulikana tangu zamani, lakini ujuzi wa ki sayansi uliopatikana katika karne ya 20 umeongeza sana idadi na hasa usahihi wa mbinu hizo. Kutoka mwaka 1930 hadi 1980 , utafiti na ukuzaji wa uelewa huo wa masuala ya uzazi ulifanywa hasa na wataalamu wanaohusika na Kanisa Katoliki kwa lengo la kusaidia kupanga uzazi watu wa ndoa wanaokataa mbinu za teknolojia kwa msingi wa maadili au kwa kuzingatia ma dhara yake. Kwa kiasi kikubwa mashirika yanayotafuta na kueneza ufahamu wa uwezo wa kushika mimba yanaendelea kuongozwa na Wakatoliki, lakini baadhi ya mashirika ya kawaida sasa yapo. Mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutegemea uchunguzi wa mabadiliko ya ishara za msingi yanayoashiria uwezekano wa kutunga mimba (kama vile joto la mwili , ute wa uke , na mkao wa seviksi ) kwa kufuatilia mzunguko wote wa hedhi na hivyo kubaini wakati ambapo inawezekana kushika mimba. Ishara nyingine pia zinaweza kuzingatiwa: hizo ni pamoja na ulaini wa ma titi na uchungu wakati kijiyai kinapoachiliwa, uchunguzi wa mkojo kwa vifaa vya kubashiri udondoshwaji wa vijiyai, na uchunguzi wa ki hadubini wa ute au ugiligili wa seviksi (yaani mlango wa kizazi). Isitoshe, ipo njia ya kufuatilia uwezo wa kushika mimba kwa tarakilishi . Istilahi Mbinu zinazotegemea dalili zinafuatilia moja au zaidi kati ya ishara tatu za msingi za kuweza kutunga mimba - joto la msingi la mwili, ute wa uke na mkao wa seviksi. [1] Mbinu zinazotegemea ute wa uke tu ni pamoja na Mbinu ya Billings ya Kutambua Kijiyai Kuachiliwa, The Ovulation Method , Mbinu ya Creighton, na Mbinu ya Siku Mbili. Mbinu za dalili ya joto la mwili hujumuisha pia uchunguzi wa joto la msingi la mwili (basal body temperature = BBT), ute wa uke, na wakati mwingine mkao wa seviksi. Mbinu zinazotegemea kalenda hufuatilia mzunguko wa hedhi ya mwanamke na kwa kuzingatia urefu wa mzunguko wake kutambua anapoweza kupata mimba. Mbinu maarufu zaidi kati ya hizo ni Mbinu ya Siku Sanifu. Mbinu ya Urari-Kalenda pia huhesabiwa njia ya kutegemea kalenda, ingawa haijafafanuliwa vizuri na ina maana nyingi tofauti kwa watu tofauti. Mbinu hizo za kupanga uzazi zinaweza kuitwa Mbinu za Uzazi Zinazotegemea Ufahamu (wa uwezo wa kuzaa), [2] Jina "Mbinu ya Uelewa wa Uzazi" (kwa Kiingereza Fertility Awareness Method = FAM) linatumika hasa kwa mfumo uliofundishwa na Toni Weschler. Jina "Mbinu Asili ya Uzazi wa Mpango" (kwa Kiingereza natural family planning = NFP) wakati mwingine hutumiwa kutaja mbinu yoyote inayotegemea Ufahamu wa Uzazi. Hata hivyo, msamiati huo ni mahsusi kuhusu mbinu zile zinazokubaliwa na Kanisa Katoliki: mbali ya uwezekano wa kutopata mimba wakati wa kunyonyesha (kwa Kiingereza Lactational amenorrhea method = LAM), ni kutofanya tendo la ndoa siku ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Hapo mbinu za FA zinaweza kutumika ili kutambua nyakati hizo zinazoweza kuleta mimba. Wanawake ambao wananyonyesha na wanapenda kukwepa mimba wanaweza kutegemea kukatizwa kwa hedhi wakati wa kunyonyesha. Hiyo ni tofauti na ufahamu wa uzazi, lakini kwa sababu haihusishi vifaa wala kemikali, mara nyingi hutajwa pamoja na FA kama njia asili ya uzazi wa mpango. Historia Ukuaji wa mbinu zinazotegemea kalenda Haijulikani kwa hakika lini iligunduliwa kwa mara ya kwanza kuwa wanawake wana vipindi vya kutunga mimba na visivyo vya kutunga mimba vinavyoweza kutabirika. Mwaka 388 Agostino wa Hippo aliandika kuhusu kuepuka mara kwa mara tendo la ndoa ili kuzuia mimba akiwalaumu Wamani kwa kutumia njia hiyo ili kubaki bila watoto. [3] Kitabu fulani kinasema kuacha ngono kwa muda kulipendekezwa na "watu wachache wasio wa dini tangu katikati ya karne ya 19", [4] lakini katika karne ya 20 ushawishi mkuu uliohamasisha mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulitoka katika Kanisa Katoliki. Mwaka 1905 Theodoor Hendrik van de Velde, mwanajinakolojia wa Uholanzi, alionyesha kuwa wanawake hutoa kijiyai mara moja tu kila mzunguko wa hedhi. [5] Miaka ya 1920 Kyusaku Ogino , mwanajinakolojia wa Ujapani , na Hermann Knaus , kutoka Austria , wakifanya kazi bila ushirikiano waligundua kwamba kijiyai hutokea siku kumi na nne hivi kabla ya kipindi cha hedhi kinachofuata. [6] Ogino alitumia uvumbuzi wake kutengeneza hesabu ya kuwasaidia wanawake wasiopata mimba kwa kufanya tendo la ndoa kwa wakati mwafaka kupata mimba. Mwaka 1930 John Smulders , daktari Mkatoliki kutoka Uholanzi, alitumia uvumbuzi huo kuunda mbinu ya kuepuka mimba. Smulders alichapisha kazi yake chini ya Chama cha Matabibu Wakatoliki wa Uholanzi, na hiyo ilikuwa mbinu sanifu ya kwanza ya kuepuka mimba kwa kuacha kujamiiana kwa kipindi fulani - mbinu ya kalenda. [6] Uanzilishi wa mbinu za dalili za joto na ute wa mlango wa uzazi Katika miaka ya 1930, Wilhelm Hillebrand , padri Mkatoliki nchini Ujerumani , alitunga mbinu ya kuzuia mimba kwa kutegemea joto la msingi la mwili. [7] Mbinu hiyo ya joto ilionekana kuwa na ufanisi mkubwa zaidi katika kuwasaidia wanawake kuzuia mimba kuliko mbinu ya kutegemea kalenda. Katika miongo michache iliyofuata, mbinu hizo mbili zikawa zinatumika sana miongoni mwa wanawake Wakatoliki. Hotuba mbili zilizotolewa na Papa Pius XII mwaka 1951 zilitoa kibali cha hali ya juu kutoka Kanisa Katoliki kwa mbinu hizo kutumiwa na mume na mke waliohitaji kuzuia mimba. [4][8] Mwanzo mwa miaka ya 1950 , John Billings aligundua uhusiano kati ya ute wa mlango wa uzazi na uwezekano wa kutunga mimba alipokuwa akifanya kazi katika Shirika Katoliki la Ustawi wa Jamii mjini Melbourne , Australia . Billings na madaktari wengine kadhaa, akiwemo mke wake Evelyn , walifanyia utafiti ishara hiyo kwa miaka kadhaa, na kufikia mwishoni mwa miaka ya 1960 walikuwa wamefanya majaribio ya kitabibu na kuanzisha vituo vya kufundishia mbinu yao duniani kote. [9] Mashirika ya kwanza ya ufundishaji mbinu zilizozingatia dalili Japo awali akina Billings walifundisha pamoja mbinu za dalili ya joto na ya ute wa uke, walipata shida katika kufundisha ishara ya joto kwa idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika katika nchi zinazoendelea . Hivyo katika miaka ya 1970 walibadilisha mbinu ili kutegemea ute tu. [7] Taasisi ya kimataifa iliyoanzishwa na Billings sasa inajulikana kama "Shirika la Kimataifa la Mbinu ya Kudondosha Kijiyai ya Billings" (kwa Kiingereza World Organization Ovulation Method Billings = WOOMB). Shirika la kwanza kufundisha mbinu ya dalili za joto lilianzishwa mwaka 1971 . John na Sheila Kippley , walei Wakatoliki, walijiunga na Konald Prem katika kufundisha mbinu iliyotegemea dalili zote tatu: joto, ute na mkao wa mlango wa uzazi. Taasisi yao sasa inaitwa "Shirika la Kimataifa la Wanandoa kwa Wanandoa" (kwa Kiingereza "Couple to Couple League International"). [7] Muongo uliofuata ulishuhudia kuanzishwa kwa mashirika mengine ya Kikatoliki ambayo sasa ni makubwa - "Familia ya Amerika" (kwa Kiingereza "Family of the Americas") iliyoundwa mwaka 1977 na kufundisha mbinu ya Billings, [10] halafu "Taasisi ya Papa Paulo VI " ( 1985 ), inayofundisha mbinu mpya ya ute pekee iitwayo Creighton Model. [11] Hadi miaka ya 1980 , habari kuhusu ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ulipatikana tu kutoka vyanzo vya Kikatoliki. [12] Shirika la kwanza lisilo la kidini la kutolea mafundisho hayo ya uzazi lilikuwa Kituo cha Uelewa wa Uzazi cha New York, lililoanzishwa mwaka 1981 . [13] Toni Weschler alianza kufundisha mwaka 1982 na kuchapisha kitabu kilichouzwa sana cha Taking Charge of Your Fertility mwaka 1995 . [14] "Justisse" ilianzishwa mwaka 1987 huko Edmonton, Kanada . [15] Mashirika hayo yote yasiyo ya kidini yanafundisha mbinu ya dalili za joto. Ingawa mashirika ya Kikatoliki yanayoeneza uelewa wa uzazi ni makubwa sana kuliko hayo ya wanaharakati yasiyo ya kidini, walimu wasiotegemea dini wamezidi kuongezeka katika miaka ya 1990 na milenia mpya . Maendeleo ya sasa Ustawi wa mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaendelea. Mwishoni mwa miaka ya 1990, "Taasisi ya Afya ya Uzazi " katika Chuo Kikuu cha Georgetown ilianzisha mbinu mbili mpya. [16][17] Mbinu ya Siku Mbili, inayotegemea ute tu, na CycleBeads , ambayo inafuata mbinu ya Siku Sanifu na ina pia toleo la kieletroniki, iCycleBeads), zimeundwa ili kuwa na ufanisi na urahisi mkubwa zaidi katika kufundisha, kujifunza, na kutumia. Ishara za uwezo wa kushika mimba Mizunguko mingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kupatikana (muda wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai), halafu siku ambazo mimba inaweza kutungika, na kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika ( muda wa kutoshika mimba baada ya kijiyai kudondoshwa). Siku ya kwanza ya kuvuja damu inahesabiwa kuwa siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Mbinu mbalimbali za kufahamu uwezo wa kushika mimba huhesabu kwa njia tofauti kidogo kipindi ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba, yaani hutumia ishara za msingi za uwezekano huo, historia ya mzunguko, au zote mbili. Ishara za msingi za kuweza kupata mimba Ishara tatu za msingi za uwezekano wa kushika mimba ni joto msingi la mwili, ute wa uke na mkao wa seviksi. Mwanamke anayetumia dalili hizo ili kujua uwezo wake wa kupata mimba anachagua kutumia ishara moja, mbili, au zote tatu pamoja. Wanawake wengi hung'amua pia ishara nyingine za ziada kulingana na mzunguko wa hedhi, kama vile maumivu na uzito tumboni, maumivu mgongoni, ulaini wa matiti na maumivu ya kudondosha kijiyai. Joto la msingi la mwili Joto la msingi la mwili ni joto la mwili wa mtu linalopimwa wakati wa kwanza anapoamka asubuhi (au baada ya usingizi wa muda mrefu zaidi katika siku). Miongoni mwa wanawake, kudondoshwa kijiyai husababisha joto kupanda kwa 0.3°C hadi 0.9° C (0.5°F hadi 1.6°F) na kubakia hivyo kipindi chote hadi wakati wa hedhi ijayo. Mabadiliko hayo ya joto yanaweza kutumika kubaini mwanzo wa kipindi cha kutoweza kutungika mimba kabla ya kudodosha kijiyai. Ute wa uke Ute wa uke Kuonekana kwa ute wa uke na mwasho wake ni ishara zinazoelezwa kwa kawaida pamoja kama njia za kubaini ishara hiyohiyo. Ute wa uke huzalishwa na seviksi, ambayo huunganisha mji wa mimba na mfereji wa uke. Ute wa uke wenye uwezo wa kushika mimba hukuza maisha ya manii kwa kupunguza uasidi wa uke, na husaidia kuongoza manii kupitia seviksi na kuelekea ndani ya mji wa mimba. Uzalishaji wa ute wa uke wenye uwezo wa kupata mimba husababishwa na homoni ileile ( istrojeni ) ambayo huandaa mwili wa mwanamke kwa udondoshwaji wa kijiyai . Kwa kuangalia ute wa uke wake, na kuzingatia hisia pindi unapopita ukeni, mwanamke anaweza kubaini wakati mwili wake unapojiandaa kudondosha kijiyai, na wakati ambapo udondoshwaji wa kijiyai umepita. Kijiyai kikidondoshwa, uzalishwaji wa istrojeni hupungua na projesteroni huanza kuongezeka. Kupanda kwa kiwango cha projesteroni husababisha mabadiliko maalumu katika wingi na hali ya ute wa uke. [18] Mkao wa seviksi Seviksi hubadilisha mkao kutokana na homoni zilezile zinazosababisha ute wa uke kutolewa na kukauka. Wakati mwanamke yuko katika awamu ya kutoshika mimba katika mzunguko wa hedhi, seviksi hushuka chini katika mfereji wa uke, ikiguswa huwa ngumu (kama ncha ya pua ya mtu), na upenyu (mlango wa seviksi) unakuwa mdogo ukilinganishwa na wakati mwingine, au umefungika. Kadiri mwanamke anavyozidi kuwa na uwezo wa kushika mimba ndivyo seviksi inavyopanda juu katika mfereji wa uke, inakuwa laini ikiguswa (kama mdomo wa mtu), na upenyu unakuwa wazi zaidi. Baada ya kudondoshwa kwa kijiyai, seviksi itarejea mkao wake wa wakati usio wa kushika mimba. Historia ya mzunguko Mbinu zinazotegemea kalenda hubainisha uwezekano wa kutopata mimba kabla na baada ya kudondosha kijiyai kulingana na historia ya mzunguko. Zinapotumika vizuri kuzuia mimba, mbinu hizo si madhubuti kama mbinu zinazotegemea dalili, hata hivyo umadhubuti wake unalingana na mbinu zuizi kama vile kiwambo na kizibo cha seviksi . Mbinu za kuepuka mimba zinazotegemea ute wa uke na joto la mwili kubainisha uwezo wa kutunga mimba baada ya kijiyai kudondoshwa, hushindikana mara chache sana zinapotumika vizuri. [19] Hata hivyo, mbinu hizo huwa na upungufu fulani katika kubaini uwezo wa kutotunga mimba kabla ya kudondosha kijiyai. Rekodi ya joto la mwili pekee haitoi mwongozo kuhusu uwezekano wa mimba kutungwa au kutotungwa kabla ya kijiyai kudondoshwa. Kubaini uwezekano wa kutoshika mimba kabla ya tukio hilo kunaweza kufanywa kwa kuchunguza ute wa uke; hata hivyo, njia hii inafanikiwa kwa kiwango cha chini kuliko ule unaoshuhudiwa katika kipindi baada ya kudondosha kijiyai. [20] Kutegemea uchunguzi wa ute pekee pia ina maana kwamba tendo la ndoa haliruhusiwi wakati wa hedhi, kwa sababu ute wowote hautakuwa dhahiri. [21] Matumizi ya sheria fulani za kalenda katika kutambua urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya kijiyai kudondoshwa huruhusu siku chache za ngono mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi huku kukiwa na kiwango cha chini sana cha uwezekano wa kupata mimba. [22] Kwa kutumia mbinu ya ute pekee, kuna uwezekano wa kukosea kwa kudhani ni hedhi damu inapotoka katikati ya mzunguko wa hedhi au wakati ambapo kijiyai halikudondoshwa. Kuweka chati sahihi ya joto la msingi la mwili huwezesha utambuzi wa hedhi, wakati ambapo sheria za kalenda kuhusu kipindi kabla ya kudondosha kijiyai zinaweza kutumiwa kwa usahihi. [23] Katika mbinu za joto pekee, sheria ya kalenda inaweza kutegemewa pale tu kutambua uwezekano wa kutoshika mimba kabla ya kudondosha kijiyai. Katika mbinu za joto na ishara, sheria ya kalenda huthibitishwa na rekodi za ute: uchunguzi wa ute wa uke unaoashiria uwezo wa kupata mimba unapewa kipaumbele kuliko mbinu yoyote ya kalenda ya kubainisha uwezo wa kushika mimba. [22] Sheria za kalenda zinaweza kuweka idadi mahsusi ya siku, ikibainisha kwamba (kulingana na urefu wa mizunguzo iliyopita ya hedhi ya mhusika) siku tatu hadi sita za kwanza katika kila mzunguko wa hedhi huchukuliwa kuwa hazina uwezo wa kupata mimba. [24] Au, sheria ya kalenda inaweza kuhitaji hesabu, kwa mfano lazima iwe kwamba urefu wa kipindi kisicholeta uzazi kabla ya kudondosha kijiyai ni sawa na urefu wa mzunguko mfupi zaidi wa mwanamke huyo ukiondoa siku ishirini na moja. [25] Badala ya kutegemea urefu wa mzunguko, sheria ya kalenda inaweza kuhakikishwa kutokana na siku ya mzunguko ambapo mwanamke ameshuhudia badiliko la joto la mwili. Mfumo mmoja unasema urefu wa kipindi cha kutoweza kutunga mimba kabla ya kudondosha kijiyai unalingana na siku ya kwanza ambapo mwanamke alishuhudia kupanda joto la mwili ondoa siku saba. [26] Mbinu nyingine Vifaa vya kubashiri udondoshwaji wa kijiyai (kwa Kiingereza Ovulation predictor kits = OPKs) vinaweza kutambua udondoshwaji unaokaribia kutokea kwa kutegemea wingi wa homoni ya kuandaa ukuta wa chupa ya kizazi (kwa Kiingereza "lutenizing hormone" = LH) katika mkojo wa mwanamke. Kwa kawaida ubashiri wa kufana wa undondoshwaji huo hufuatiwa na udondoshwaji ndani ya saa 12-36. Uchunguzi wa mate kwa hadubini, ukifanyika kwa usahihi, unaweza kugundua vijidutu maalum katika mate ambavyo hutangulia udondoshwaji wa kijiyai. Vijidutu hivyo kwa kawaida huonekana siku tatu kabla ya udondoshwaji na kuendelea mpaka udondoshwaji utokee. Katika kipindi hiki, vijidutu hivyo hutokea katika ute wa uke pamoja na mate. Vichunguza uzazi vya kieletroniki vinapatikana kwa majina mbalimbali ya ki biashara . Vichunguzi hivyo vinaweza kutumia mifumo ya Joto la Msingi la Mwili pekee, au kuchambua vitepe vya kupimia mkojo, au kufuatilia dalili mchanganyiko au kuchunguza ukinzani umeme wa mate na ugiligili wa uke, au kwa pamoja baadhi ya mambo hayo mbalimbali . Manufaa na mapungufu Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba una kiwango fulani cha sifa bainifu: Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika kudhibiti afya ya uzazi. Mabadiliko katika mzunguko wa hedhi yanaweza kumtahadharisha mtumiaji kuhusu kujitokeza kwa matatizo ya kiginakolojia. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba pia unaweza kutumika kusaidia katika kuagua matatizo yanayojulikana ya kijinakolojia kama vile kutoweza kushika mimba. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ni uwanda mpana: unaweza kutumika kuzuia mimba au kusaidia katika kutunga mimba. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumiwa na wanawake wote katika kipindi chote cha uzazi, bila kujali ikiwa anakaribia kumaliza kuzaa, ananyonyesha, au anapata mzunguko wa hedhi usio wa kawaida kwa sababu zingine. Matumizi ya ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutoa ufahamu kuhusu jinsi mwili wa mwanamke unavyofanya kazi, na unaweza kuwaruhusu wanawake kuwa na udhibiti mkubwa wa uzazi wao wenyewe. Aina fulani ya mbinu za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba zinazotegemea dalili ya uzazi zinahitaji uchunguzi au kugusa ute wa uke, matendo ambayo baadhi ya wanawake hawafurahii. Baadhi ya wahudumu wanapendelea kutumia neno "majimaji ya seviksi" badala ya ute wa uke, katika juhudi ya kuwafanya wanawake kama hao kuhisi huru kidogo. Baadhi ya dawa, kama vile ya kupunguza kupaliwa mapafuni, yanaweza kubadili ute ya kizazi. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi, ishara ya ute huenda isionyeshe kisahihi uwezo wa kutunga mimba . [27] Baadhi ya mbinu zinazotegemea dalili huhitaji ufuatiliaji wa joto la kimsingi ya mwili. Kwa sababu usingizi usiokuwa na utaratibu unaweza kuvuruga usahihi wa joto la kimsingi la mwili, wafanyakazi wa kubadilisha zamu na walio na watoto wadogo sana, kwa mfano, huenda wasiweze kutumia mbinu hizo. [27] Kama njia ya kupanga uzazi Kwa kufanya tendo kamili la ndoa siku zile tu ambapo katika mzunguko wa hedhi mimba haiwezi kutungwa, maharusi wanaweza kuzuia mimba isipatikane. Wakati ambapo katika mzunguko wa hedhi mimba inaweza kutungwa, wanaweza wakaacha ngono ili kuwa na hakika ya kutoitunga. Wengine siku hizo wanatumia mbinu mbadala za kuzuia mimba ingawa pengine hazifai kwa sababu mbalimbali. [28] Kinyume chake maharusi wanaweza kulenga uzazi kwa hakika zaidi wakifanya tendo la ndoa kwa kutumia vizuri siku zinazouwezesha. Manufaa Katika kutumia ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hakuna madhara yanayotokana na teknolojia inayotumiwa na mbinu nyingine. Kwa jumla hakuna madhara yoyote ya utumiaji, isipokuwa yanayoweza kutokea kwa kuingiza vidole ndani ya uke ili kuchunguza seviksi (kama inavyopendekezwa na baadhi ya mbinu). Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza ukatumika pamoja na vifaa vya kuzuia mimba ili kuendelea kujamiiana katika kipindi ambapo kuna uwezekano wa kupata mimba. Tofauti na utumiaji wa vifaa hivyo bila ufahamu wa uwezo wa kushika mimba, ufahamu huo unawezesha kutumia vizuiamimba siku chache tu, na hivyo kupunguza madhara yanayoletwa navyo. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hauna gharama au ni nafuu sana. Watumiaji wanaweza wakahitaji kununua chati, kalenda, kipimajoto , au tarakilishi, au pengine kumlipa mkufunzi . Kwa vyovyote gharama ni ya chini ikilinganishwa na mbinu nyingine. Tofauti na mbinu nyingine mbalimbali ambazo zina athari za muda mrefu, ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unawezesha kubadili mara moja kutoka uamuzi wa kuzuia mimba hadi ule wa kuilenga. Mapungufu Wasipotumia vifaa vya kizuia mimba katika kipindi ambapo mimba inaweza kutungwa, wanandoa wanalazimika waache ngono. Ila kupunguza uwezekano wa kupata mimba uwe chini ya 1% kwa mwaka, katika kila mzunguko kuna takriban siku 13 ambapo lazima waache ngono. [29] Kwa wanawake wenye mzunguko unaobadilikabadilika sana - kama ilivyo kawaida wakati wa kunyonyesha, karibu na hedhi kwisha kabisa, au kwa wenye magonjwa ya homoni (kama vile Polycystic ovary syndrome = PCOS) kuacha kujamiiana au kutumia vizuizi kunaweza kuhitajika miezi mfululizo. Wengi hawana motisha au nidhamu ya kutosha wafanye hivyo kwa muda mrefu. Wanaposhindwa kufuata masharti, ni rahisi kupata mimba isiyopangwa. Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba haukingi dhidi ya maradhi ya zinaa. [30] Ndiyo maana inafaa zaidi kati ya watu ambao ni waaminifu wao kwa wao, kama watu wa ndoa. Ufanisi Ufanisi wa ufahamu ya uzazi, kama ulivyo kwa mbinu nyingi za uzazi wa mpango, unaweza kutathminiwa kwa njia mbili zifuatazo. Kwa kawaida mfumo wa Pearl Index hutumika kukokotoa viwango vya ufanisi, lakini baadhi ya tafiti hutumia majedwali ya mapunguzo. [31] Kwa kawaida viwango hupimwa katika mwaka wa kwanza wa matumizi. [32] Viwango vya matumizi kamili ni kwa wale tu wanaofuata sheria zote, wakitambua kwa usahihi kipindi ambapo kuna uwezekano wa kutunga mimba, na wanaacha ngono isiyo na kinga siku walizotambua kuna uwezekano wa kuitunga. Viwango vya matumizi halisi au matumizi ya kawaida ni kwa wale wote wanaotegemea ufahamu wa uwezo wa kushika mimba ili kuizuia, wakiwa ni pamoja na wasioweza kutimiza vigezo vya "matumizi kamili". Kiwango cha kufeli kwa ufahamu wa uwezo wa kushika mimba hutofautiana pakubwa kulingana na mbinu iliyotumika kubaini uwezekano wa kupata mimba, njia ya mafundisho, na idadi ya wanaotafitiwa. Baadhi ya tafiti zimekuta viwango halisi vya kufeli vya 25% kwa mwaka au zaidi. [33][34][35] Angalau utafiti mmoja umepata kiwango cha kufeli cha chini ya 1% kwa mwaka kukiwa na mafundisho endelevu na mapitio ya kila mwezi, [36] na tafiti kadhaa zimegundua viwango vya kufeli halisi vya 2-3% kwa mwaka. [29][37][38][39] Inapotumika kwa usahihi, na kuandamana na mafundisho endelevu ya mara kwa mara, baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa mbinu fulani za ufahamu wa uwezo wa kushika mimba huwa na 99% za ufanisi, [36][40][41][42] Kitabu Teknolojia ya Uzazi kinaripoti hivi: [43] Mbinu za baada ya kudondosha kijiyai (yaani kuacha ngono kuanzia wakati wa hedhi mpaka baada ya kudondoshwa) inafeli kwa 1% kwa mwaka. Mbinu ya dalili na joto la mwili inafeli kwa 2% kwa mwaka. Mbinu ya ute wa uke pekee inafeli kwa 3% kwa mwaka. Mbinu ya urari wa kalenda inafeli kwa 9% kwa mwaka. Mbinu ya Siku Wastani inafeli kwa 5% kwa mwaka. Sababu za ufanisi mdogo katika matumizi ya kawaida Sababu kadhaa zinachangia kufanya ufanisi wa matumizi ya kawaida uwe wa chini kuliko ule wa matumizi kamili: watumiaji kutotii kwa makusudi maelezo (kushiriki ngono bila kinga siku ambapo wanajua mimba inaweza kutungwa): ndiyo sababu ya kawaida zaidi [29][42] makosa ya watoa maelezo ya jinsi ya kutumia mbinu (mkufunzi kutoa taarifa isiyo sahihi au isiyo kamili) makosa ya mtumiaji (kutoelewa sheria, kutunza kumbukumbu vibaya) Kama njia ya kupata mimba Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika pia kwa lengo la kupata mimba kwa urahisi zaidi. Kupanga wakati wa kujamiiana Utafiti uliofanywa na Barrett na Marshall umeonyesha kuwa vitendo vya ngono visivyopangwa huwa na uwezekano wa 24% kutungisha mimba katika mzunguko wa hedhi. Utafiti huo pia uligundua kuwa ngono inayolenga wakati maalumu kulingana na ufahamu unaotokana na mbinu ya joto la msingi la mwili pekee huongeza viwango vya mimba hadi 31% -68%. Utafiti wa mbinu ya ute wa uke umegundua viwango vya mimba vya 67%-81% katika mzunguko wa kwanza ikiwa kujamiiana kutatokea katika Siku ya Kilele cha ishara za ute. [44][45] Kwa sababu ya viwango vya juu vya mimba kutoka mapema sana (25% za mimba hupotea katika wiki sita za kwanza tangu hedhi ya mwisho ya mwanamke), mbinu zinazotumika kuchunguza uwepo wa mimba zinaweza kusababisha upendeleo katika viwango vya utungaji mimba. Mbinu tofauti na hizo zinaweza kuonyesha viwango vya chini kwa sababu tu huwa zinakosa kugundua mimba zilizotoka mapema. Utafiti mmoja nchini China kati ya wanaoshiriki ngono bila mpangilio ili kutungisha mimba ulitumia mbinu bora za kugundua mimba, ikapata kiwango cha 40% cha kutungwa mimba kwa kila mzunguko katika kipindi cha utafiti cha miezi 12. [46] Uchunguzi wa tatizo Mizunguko ya kawaida ya hedhi wakati mwingine huchukuliwa kuwa ushahidi kwamba mwanamke anadondosha vijiyai kawaida, na mizunguko isiyo ya kawaida kuwa ushahidi kuwa udondoshaji wa kijiyai si wa kawaida. [47] Hata hivyo, wanawake wengi ambao mizunguko yao si ya kawaida hudondosha vijiyai kama kawaida, na baadhi ya wenye mizunguko ya kawaida kwa kweli hawadondoshi vijiyai au wana matatizo katika utayarishaji wa ukuta wa chupa cha uzazi. Hasa rekodi za joto la msingi la mwili, lakini pia rekodi za ute wa uke na mkao wake, zinaweza kutumika kwa usahihi kung'amua ikiwa mwanamke anadondosha kijiyai, na kama urefu wa kipindi cha baada ya kudondosha kijiyai cha mzunguko wa hedhi unatosha kwa ujauzito. Ute wa uke unaoweza kutunga mimba ni muhimu katika kujenga mazingira ambayo yanaruhusu manii kupiti mlango wa uzazi na katika viriba vya falopu ambako husubiri kudondoshwa kwa kijiyai. [48] Chati za uwezo wa kupata mimba zinaweza kusaidia kugundua ute hasimu kwa mimba kutungwa, ambao ni sababu ya kawaida ya kutopata mimba. Ikiwa hali hii itagunduliwa, baadhi wanapendekeza matumizi ya guaifenesini katika siku chache kabla ya udondoshwaji wa kijiyai ili kupunguza uzito wa ute. [49] Upimaji mimba na umri wa ujauzito Vipimo vya ujauzito si sahihi mpaka wiki 1-2 baada ya kudondoshwa kijiyai. Kujua tarehe inayokisiwa ambayo kijiyai kitadondoka kunaweza kukamzuia mwanamke asipate matokeo yasiyo sahihi kutokana na upimaji wa mapema mno. Pia, siku 18 mfululizo za joto la juu zinamaanisha mwanamke ni mjamzito karibu bila shaka. [50] Makadirio ya tarehe ya kudondosha kijiyai kutokana na chati za uwezo wa kuzaa ni njia sahihi zaidi ya kukadiria umri wa ujauzito kuliko mbinu za jadi za kupima mimba au mbinu ya kuchunguza hedhi ya mwisho katika utaratibu wa kufuatilia hedhi. [51] Kama njia ya kupanga jinsia ya mimba Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba unaweza kutumika pia kwa lengo la kupata mimba ya jinsia inayotamaniwa zaidi. [52] Maharusi wanaweza kuchagua mtoto wa kiume au wa kike kwa 85% ya hakika wakifanya tendo la ndoa kwa kupanga kulingana na ute wa uke kuwa wa kuvutika na kuteleza au siyo. Ni kwamba jinsia ya mimba inategemea tu kromosomu za mbegu za baba ambazo ni nusunusu: X kwa kuzaa watoto wa kike na Y kwa kuzaa watoto wa kiume. Mbegu zenye kromosomu X ni dhaifu kidogo nazo huogelea polepole, lakini zinaishi muda mrefu. Kumbe zenye kromosomu Y zina nguvu zaidi na kuogelea upesi, lakini hufa upesi. Ili kupata mtoto wa kiume Kwa kuzingatia tabia hizo mbili tofauti, maharusi wakitaka mtoto wa kiume wanatakiwa kufanya tendo la ndoa siku ya kwanza baada ya kilele (kujisikia kuteleza) na kuendelea kwa miandamo 6 ya hedhi. Kama mwanamke hajapata mimba baada ya miandamo 6, waanze kuonana siku ya kilele na siku inayofuata. Kama mwanamke amekosa siku ya kilele, yaani kama utelezi wa ute unaendelea siku inayofuata, waonane tena siku inayofuata. Kwa njia hiyo mbegu zenye kromosomu Y tu zitafikia kijiyai kilichochopoka, kwa sababu mbegu zenye kromosomu X zinaogelea polepole tu. Ili kupata mtoto wa kike Kinyume chake, wakitaka mtoto wa kike wanatakiwa kufanya tendo la ndoa siku ya kwanza ya ute wa uzazi. Halafu wapumzike mpaka siku ya nne baada ya kilele. Waendelee hivyo kwa miandamo michache. Kama mwanamke hajapata mimba baada ya miezi michache, wafanye tendo la ndoa siku ya kwanza na ya pili ya ute wa uzazi halafu wapumzike mpaka siku ya nne baada ya kilele. Waendelee hivyo kwa miandamo michache. Kama mwanamke hajapata mimba baada ya miezi michache, wafanye tendo la ndoa pia siku ya tatu ya ute wa uzazi halafu wapumzike mpaka siku ya nne baada ya kilele. Waendelee hivyo kwa miandamo michache. Kwa njia hiyo mbegu zenye kromosomu Y zitakufa kabla ya kuweza kuungana na kijiyai, na hivyo zitabaki zenye kromosomu X kuwa na nafasi hiyo. Siku nzuri ya kupata mtoto wa kike ni kufanya tendo la ndoa siku mbili kabla ya kilele. Tazama pia Uzazi wa mpango Uzazi wa mpango kwa njia asilia Tanbihi 1. ↑ Weschler, Toni (2002). Taking Charge of Your Fertility , Revised, New York: HarperCollins, 52. ISBN 0-06-093764-5 . 2. ↑ Medical Eligibility Criteria for Contraceptive Use:Fertility awareness-based methods . Fourth edition. World Health Organization. 2010. http://www.who.int/reproductivehealth/publications/family_planning/9789241563888/en/index.html . Retrieved 2012-12-11. 3. ↑ Saint, Bishop of Hippo Augustine; Philip Schaff (Editor) (1887). A Select Library of the Nicene and Post-Nicene Fathers of the Christian Church, Volume IV . Grand Rapids, MI: WM. B. Eerdmans Publishing Co., On the Morals of the Manichæans , Chapter 18 . 4. ↑ 4.0 4.1 Yalom, Marilyn (2001). A History of the Wife , First, New York: HarperCollins, 297–8, 307. ISBN 0-06-019338-7 . 5. ↑ A Brief History of Fertility Charting . FertilityFriend.com . Iliwekwa mnamo 2006-06-18. 6. ↑ 6.0 6.1 Singer, Katie (2004). The Garden of Fertility . New York: Avery, a member of Penguin Group (USA), 226–7. ISBN 1-58333-182-4 . 7. ↑ 7.0 7.1 7.2 Hays, Charlotte. "Solving the Puzzle of Natural Family Planning" . Holy Spirit Interactive. http://www.holyspiritinteractive.net/features/prolife/article_05.asp . Retrieved 2012-02-15. 8. ↑ [18] ^ Moral Questions Affecting Married Life: Addresses given October 29, 1951 to the Italian Catholic Union of midwives 26 Novemba 1951 to the National Congress of the Family Front and the Association of Large Families, National Catholic Welfare Conference, Washington, DC. 9. ↑ Billings, John (Machi 2002). "THE QUEST — leading to the discovery of the Billings Ovulation Method" . Bulletin of Ovulation Method Research and Reference Centre of Australia 29 (1): 18–28. http://www.woomb.org/omrrca/bulletin/vol29/no1/thequest.shtml . Retrieved 2007-03-18. 10. ↑ About us . Family of the Americas (2006). Iliwekwa mnamo 2007-03-18. 11. ↑ About the Institute . Pope Paul VI Institute (2006). Iliwekwa mnamo 2012-02-21. 12. ↑ Singer (2004), p.xxiii 13. ↑ About us . Fertility Awareness Center (2006). Iliwekwa mnamo 2007-03-18. 14. ↑ Weschler (2002) 15. ↑ About Us . Justisse (2002). Jalada kutoka ya awali juu ya 2006-11-16. Iliwekwa mnamo 2007-03-18. 16. ↑ Arévalo M, Jennings V, Sinai I (2002). "Efficacy of a new method of family planning: the Standard Days Method." (PDF). Contraception 65 (5): 333–8. doi: 10.1016/S0010-7824(02)00288-3 . PMID 12057784 . http://pdf.dec.org/pdf_docs/PNACQ416.pdf . 17. ↑ Jennings V, Sinai I (2001). "Further analysis of the theoretical effectiveness of the TwoDay method of family planning". Contraception 64 (3): 149–53. doi: 10.1016/S0010-7824(01)00251-7 . PMID 11704093 . 18. ↑ James B. Brown (2005). Physiology of Ovulation . Ovarian Activity and Fertility and the Billings Ovulation Method . Ovulation Method Research and Reference Centre of Australia. 19. ↑ Kippley (2003), uk.121-134, 376-381 20. ↑ Kippley (2003), uk.114 21. ↑ Evelyn, Dr. Billings, Ann Westinore, (1998). The Billings Method: Controlling Fertility Without Drugs or Devices . Toronto: Life Cycle Books, 47. ISBN 0-919225-17-9 . 22. ↑ 22.0 22.1 Kippley (2003), uk.108-113 23. ↑ Kippley (2003), uk.101 sidebar na Weschler (2002), uk.125 24. ↑ Kippley (2003), uk.108-109 na Weschler (2002), uk.125-126 25. ↑ Kippley (2003), uk.110-111 26. ↑ Kippley (2003), uk.112-113 27. ↑ 27.0 27.1 How to Observe and Record Your Fertility Signs . Fertility Friend Handbook . Tamtris Web Services (2004). Iliwekwa mnamo 2005-06-15. 28. ↑ Manhart, MD; Daune, M; Lind, A; Sinai, I; Golden-Tevald, J (January–February 2013). "Fertility awareness-based methods of family planning: A review of effectiveness for avoiding pregnancy using SORT." . Osteopathic Family Physician 5 (1): 2–8. doi : 10.1016/j.osfp.2012.09.002 . http://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S1877573X12001542 . 29. ↑ 29.0 29.1 29.2 Frank-Herrmann P, Heil J, Gnoth C, et al. (2007). "The effectiveness of a fertility awareness based method to avoid pregnancy in relation to a couple's sexual behaviour during the fertile time: a prospective longitudinal study". Hum. Reprod. 22 (5): 1310–9. doi: 10.1093/humrep/dem003 . PMID 17314078 . 30. ↑ Fertility Awareness Method . Brown University Health Education Website . Brown University (2012). Iliwekwa mnamo 2012-12-11. 31. ↑ Kippley, John; Sheila Kippley (1996). The Art of Natural Family Planning , 4th addition, Cincinnati, OH: The Couple to Couple League, 141. ISBN 0-926412-13-2 . 32. ↑ Hatcher, RA; Trussel J, Stewart F, et al. (2000). Contraceptive Technology , 18th, New York: Ardent Media. ISBN 0-9664902-6-6 . 33. ↑ Wade ME, McCarthy P, Braunstein GD, et al. (Oktoba 1981). "A randomized prospective study of the use-effectiveness of two methods of natural family planning". American journal of obstetrics and gynecology 141 (4): 368–376. PMID 7025639 . 34. ↑ Medina JE, Cifuentes A, Abernathy JR, et al. (Desemba 1980). "Comparative evaluation of two methods of natural family planning in Colombia". American journal of obstetrics and gynecology 138 (8): 1142–1147. PMID 7446621 . 35. ↑ Marshall J (Agosti 1976). "Cervical-mucus and basal body-temperature method of regulating births: field trial". Lancet 2 (7980): 282–283. doi : 10.1016/S0140-6736(76)90732-7 . PMID 59854 . 36. ↑ 36.0 36.1 Evaluation of the Effectiveness of a Natural Fertility Regulation Programme in China : Shao-Zhen Qian, et al. Reproduction and Contraception (English edition), in press 2000. 37. ↑ Frank-Herrmann P, Freundl G, Baur S, et al. (Desemba 1991). "Effectiveness and acceptability of the sympto-thermal method of natural family planning in Germany". American journal of obstetrics and gynecology 165 (6 Pt 2): 2052–2054. PMID 1755469 . 38. ↑ Clubb EM, Pyper CM, Knight J (1991). "A pilot study on teaching natural family planning (NFP) in general practice" . Proceedings of the Conference at Georgetown University, Washington, DC . http://www.fertilityuk.org/nfps822.html . 39. ↑ Frank-Herrmann P, Freundl G, Gnoth C, et al. (Juni-Septemba 1997). "Natural family planning with and without barrier method use in the fertile phase: efficacy in relation to sexual behavior: a German prospective long-term study". Advances in Contraception 13 (2-3): 179–189. doi: 10.1023/A:1006551921219 . PMID 9288336 . 40. ↑ Ecochard, R.; Pinguet, F.; Ecochard, I.; De Gouvello, R.; Guy, M.; Huy, F. (1998). "Analysis of natural family planning failures. In 7007 cycles of use". Fertilite Contraception Sexualite 26 (4): 291–6. PMID 9622963 . 41. ↑ Hilgers, T.W.; Stanford, J.B. (1998). "Creighton Model NaProEducation Technology for avoiding pregnancy. Use effectiveness". Journal of Reproductive Medicine 43 (6): 495–502. PMID 9653695 . 42. ↑ 42.0 42.1 Howard, M.P.; Stanford, J.B. (1999). "Pregnancy probabilities during use of the Creighton Model Fertility Care System". Archives of Family Medicine 8 (5): 391–402. doi : 10.1001/archfami.8.5.391 . PMID 10500511 . 43. ↑ James Trussell et al. (2000) "Contraceptive effectiveness rates", Contraceptive Technology - 18 Edition, New York: Ardent Media. On-press. 44. ↑ Ryder R (1993). ""Natural family planning": effective birth control supported by the Catholic Church". BMJ 307 (6906): 723–6. doi : 10.1136/bmj.307.6906.723 . PMC 1678728 . PMID 8401097 . 45. ↑ Hilgers T, Daly K, Prebil A, Hilgers S (Oktoba 1992). "Cumulative pregnancy rates in patients with apparently normal fertility and fertility-focused intercourse". J Reprod Med 37 (10): 864–6. PMID 1479570 . 46. ↑ Wang X, Chen C, Wang L, Chen D, Guang W, French J (2003). "Conception, early pregnancy loss, and time to clinical pregnancy: a population-based prospective study". Fertil Steril 79 (3): 577–84. doi: 10.1016/S0015-0282(02)04694-0 . PMID 12620443 . 47. ↑ "Infertility fact sheet" . womenshealth.gov, U.S. Department of Health and Human Services, Office on Women's Health. http://www.womenshealth.gov/publications/our-publications/fact-sheet/infertility.cfm#f . Retrieved 2012-12-11.. "Some signs that a woman is not ovulating normally include irregular or absent menstrual periods." "Female Infertility" . Adult Health Advisor . 2012. http://www.ihacares.com/index.cfm/HealthAdvisors/AdultHealthAdvisor/crs-aha-aha_obg_female.infertility/ .. "A woman who is not ovulating normally may have irregular or missed menstrual periods." "Is Clomid Right For You?" . JustMommies.com . 2007. http://www.justmommies.com/articles/clomid-and-ovulation.shtml .. "If you have an irregular cycle there is a good chance you are not ovulating normally." 48. ↑ Ellington, Joanna (2004). Sperm Transport to the Fallopian Tubes . Frequently Asked Questions with Dr. E . INGfertility Inc. Iliwekwa mnamo 2008-04-27. 49. ↑ Weschler (2002), uk. 173. 50. ↑ Weschler (2002), uk.316 51. ↑ Weschler (2002), uk.3-4 ,155-156, Insert p.7 52. ↑ Ursula Birgitta Schnell OSB (2011). Uimarishaji wa Familia - Mpango wa uzazi kwa njia ya asili Billings Ovulation Method , 15th, Ndanda, Tanzania: Benedictine Publication Ndanda-Peramiho. ISBN 9976-63-132-4 . Marejeo Kwa Kiswahili Ursula Birgitta Schnell OSB (2011). Uimarishaji wa Familia - Mpango wa uzazi kwa njia ya asili Billings Ovulation Method , 15th, Ndanda, Tanzania: Benedictine Publication Ndanda-Peramiho. ISBN 9976-63-132-4 . Kwa Kiingereza Toni Weschler (2006). Taking Charge of Your Fertility , 10th Anniversary, New York: Collins. ISBN 0-06-088190-9 . John F. Kippley and Sheila K. Kippley (1996). The Art of Natural Family Planning , Fourth, Cincinnati, OH: Couple to Couple League International. ISBN 0-926412-13-2 . Léonie McSweeney (2006). Love & Life, Billings Method of Natural Family Planning , Ninth, Ibadan, Nigeria: African Universities Press. ISBN 978-148-092-0 . Nakala inapatikana chini ya Creative Commons Attribution/Share-Alike License ; masuala ya ziada yanaweza kukubalika. Tazama Masharti ya Utumiaji kwa maelezo zaidi. Wikipedia ni nembo iliosajiliwa na Wikimedia Foundation, Inc. , asasi isiyokuwa ya kifaida. Faragha • Dawati Ufahamu wa uwezo wa kushika mimba
Artikel Terkait
NJIA RAHISI 13 ZA KUWA NA FURAHA KILA SIKU  Mabadiliko yalio mepesi kwenye tabia zako za kila siku yatakuweka kwenye mstari wa furaha unayoitaka Umejikuta uko kwenye siku tofauti, story hizo hizo, imekuwa ni kawaida yako? Basi muda huu , sio kesho , sio wiki ijayo, ni wakati wa kubadilisha historia yako. ni za haraka, rahisi na hazina gharama unapofanya hivyo na matokeo yatakupa furaha unayoitaka. 1.Pata masaa 7 mpaka 8 ya kulala usiku. Kulala usingizi wa kutosha unapata furaha, utaweza kuwa na nguvu ya kufanya kazi zako , na utakuwa na mahusiano mazuri. weka simu yako mbali unapoenda kulala, usitumie chakula kingi wakati wa jioni. 2.Amka mapema , dakika 30 kabla . Kama wewe ni mfanya kazi wa kuajiriwa na una tabia ya kuchelewa kazini, jaribu kuamka mapema dakika 15 au 30 kila siku kwa ajili ya kujiandaa vizuri na kukumbuka vitu vyote vya kufanya, kuchukua siku hio. utaona tofauti ya tabia yako. 3.Meditate. Hii ni kubwa. meditate kwa muda wa dakika 10 au 20, utapata faida nyingi zaidi ya furaha, pamoja na kuwa muwazi, kuwa na malengo ya siku nzima. Anza siku yako na meditation. utajiepusha na tress na wasiwasi na hutachanganyikiwa na kazi zako. 4.Jipe nafasi wengi wetu huwa tunajaza vitu nyumbani, ofisini hata vile ambavyo havina kazi, hatuvitumii. inaharibu mfumo mzima wa akili yako, hisia zako, na mwili wako. Ondoa vitu ambavyo huvitumii, tupa nje au gawia watu ambao wanahitaji kuwa navyo, hali yako ya furaha itaboreka. Na hutalemewa na kazi nyingi. 5.Jifunze kitu kipya Jitahidi kujifunza kitu kipya kila siku, kwa sababu hio ndio changamoto itakayokupa furaha, kujifunza kitu kipya inaboresha afya yako ya mwili na akili, kujifunza utajenga ujasiri pia na utakuwa sharp. 6.Tembea mara kwa mara Kutembea kwa dakika 30 kwa siku moyo wako utakuwa unafanya kazi vizuri, utapunguza hasira, hutakuwa na chuki. Kama unaona ni ngumu kwako kutembea , hasa kama una gari , jifunze kupaki gari yako mahali mbali na ofisi , tembea . anza kutumia maji ya kutosha. utapata faida nyingi . 7.Usijihusishe na mambo ya mitandao. Ni rahisi kuingia instagram, facebook na zingine, lakini wachunguzi wanasema kwamba ukizidisha kujihusisha na mitandao unaweza kuharibu afya yako ya akili. badala ya kutumia nusu saa kwenye mitandao, unaweza kufanya kitu kingine unachokipenda, au kusoma kitabu, kujifunza mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kujiboresha mwenyewe kuwa mwenye afya. 8.Kuwa mwema. Ukarimu unakuongoza kwenye furaha yako mwenyewe na utakuwa mwenye afya bora. vitu ambavyo vinavyo chochea furaha ni kutoa , na kuwa mkweli , utapata faida , na utajisikia vizuri kuwa sehemu ya baraka kwa mtu fulani. kujitolea kufanya kitu, au kumwachia mtu kiti kwenye daladala. Sehemu ngumu? lakini nzuri. 9.Kaa na watu wenye furaha. Angalia watu unaoshinda nao, unaofanya nao kazi, ni watu wa aina gani. kwa sababu kuna msemo unasema kuwa ukikaa na ua rose utanukia hata kama ulikuwa hunukii. Fanya hivyo na utaweza kufungua mlango mpya kwa ajili yako maishani. utaiona furaha ikitiririka kama mto. 10.Don’t gossip. Kuseng’enya, umbeya, itakusababishia maradhi ya misongo na kukosa furaha. mtu mmbeya hawezi kusaidia kitu. wakati mwingine jitenge na watu kama hawa, au unapoona kuna kutoelewana na wafanya kazi wenzako, jaribu kutulia kwanza , badilisha negative to positive. Sema kitu kizuri kuhusu mtu. ni vizuri. kwa sababu utajiwekea alama nzuri kwako. 11.Tumia muda wako na watu unaowapenda Unapoongea na familia au marafiki kwenye simu , inatia moyo. mawasiliano hayo yanakupa afya na furaha.Fikiri ilivyo vizuri kama utaenda kula na rafiki yako mahali fulani, au kuamua kupika nyumbani , au kucheza na watoto wako kitu kama game, mpira, inafurahisha. 12.Journal Kuandika vitu vya kufanya kwa siku, au kuandika vitu unavyotaka kuvipata, Lengo hili dogo litaongeza IQ yako na kuleta utulivu wa kuboresha ujasiri wako, ukiwa na tabia hii kila siku , furaha haitakosekana kwako na utapata faida ya akili na hisia zako zitakuwa bora. 13.Jizoeze kujijali. Unapojijali ,Utaona faida zake, pamoja na kuondoa stress na wasiwasi, utakuwa mtu wa kuwaza mazuri na utaboresha immunity.pata muda kila siku kufanya kitu kwa ajili ya furaha, kama vile mazoezi, kupika chakula kizuri, kusoma . utaanza kushangaa jinsi ilivyo rahisi kuwa na furaha unapojijali na utaboresha akili yako na mwili wako, na roho yako. Kama unavyojua , kuna njia nyingi zinazotushambulia kwa siku, Ondoka mahali ambapo panaharibu ratiba yako. sasa, kama kitu kingine chochote,mafanikio ni kufanyia kazi. kwa hio pick one, and let the fun begin! ... Read More
VITU VIZURI 60 VYA KUMWAMBIA MSICHANA UMPENDAE:  Ninamaanisha kuwa maneno matamu.Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza kutumia maneno matamu.Na lazima ujue kuwa sio kila neno unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka,Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza . Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. watu wengi pia huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza. sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unaempenda na unahitaji awe wako milele. 1.Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama. 2,Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili mapenzi yako. 3.Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu. 4.Wewe ni mzuri na ni mrembo naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua. 5.Unapotabasamu huzuni kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha. 6.Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini umenichagua mimi. 7.Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo. 8.Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti. 9.Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu. 10.Siamini , maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi. 11.kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife. 12.Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja. 13.Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia. 14.Kukutana nawe ni kitu ambacho hakijawahi kutokea. 15.Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa. 16.Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi. 17.Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama haitatosha kukupenda. 18.Napata furaha nikiwa na wewe. 19. Napenda kutumia muda na wewe. 20.Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa. 21.Natamani maishsa yangu yote nikuone ukiwa na furaha. 22.Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo. 23.Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto. 24.Napenda nywele zako. 25.Napenda nikukumbatie ninapokuaga. 26.Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako. 27.Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza siku na wewe kwenye ndoto zangu. 28. ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka. 29.Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima ni mtu wa furaha. 30.Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke. 31.Unaponiaga napata shida kukuruhusu uende. 32. Umenielewa vizuri, ni kama unasoma mawazo yangu. 33.Mungu alikupendelea kukuumba, akili na kila ulichonacho. 34.Najivunia kuwa na wewe na ninafurahia. 35.Napenda unavyosema unanipenda. 36.Mapenzi yetu ni kama mawimbi ya bahari, wakati mwingi hutulia, na wakati mwingine huvuma,lakini yanarudi palepale. 37.mapenzi yetu yawe kama ua rose ambalo halina miiba. 38.Najua kwa nini watu wanatutazama , ni kwa sababu wewe ni mzuri kuliko mwezi. 39.Muda utakuwa hauna thamani endapo sitatumia na wewe. 40.kama siku yangu ingeanza na busu lako, nisingehitaji kahawa. 41.Kama ningeambiwa nielezee rangi, basi ningeenda kwenye rangi za rainbow, kwa sababu wewe ni mzuri.ni wa muujiza. 42.Mimi bila wewe ni mbaya, lakini ni mzuri nikiwa na wewe. 43.Tukishikana mikono na mioyo yetu inashikana,na nafsi zetu zinapatana . 44.Siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ipo siku tutakutana tena, na nafurahi imetokea. 45.Nafurahi tumekua pamoja, sina cha kukosa hata kidogo. 46.Moyo wangu unapumua kama ndege, kila unapotabasamu. 47.Kila ninapokuwa nimeshuka moyo, nikikusikia wewe moyo wangu unapata nguvu. 48.Shika mikono yangu nami nitashika moyo wako, tunza kwa maisha yote. 49.Maisha yote , milele yote,isio na mwisho, toka nimekutana na wewe maneno yote yana maana. 50.Siku naona kama mwaka, na siku inapita kama sekunde. 51.Natamani ningekuwa kama pweza mwenye mikono mingi ili nikukumbatie na mikono myote. 52.Siamini katika nafsi mpya, lakini baada ya kukutana na wewe nimeamini, natamani kama ningeweza kurudi nyuma na kutengeneza kitu. 53.Sitaweza kukutoa kwenye mawazo yangu , kwa maana nakuhitaji uwepo. 54.Kuna wakati nahisi upweke, kwa wakati huo, basi huamua kukupigia simu na kusikia sauti yako. 55.Ninapokutizama namuona mungu jinsi alivyokuumba na kukubariki. 56.Unanifanya niwe wa muhimu . 57.Ni siri ambayo inanifanya nikutazame zaidi kwa kila siku. 58.Kuongea na wewe kila siku unanifanya nikufahamu zaidi na zaidi. 59.Moyo wangu nakupa,nipe moyo wako ili tuifungie kwa pamoja, na tutupe ufunguo mbali. 60.Nakuhitaji muda wote, siku , mwaka na hata milele. ... Read More
HESABU YA KUONGEZA Niwapo hisabatini, Hufikiri akilini, Kuongeza umakini, Jawabu kulibaini. Jawabu hilo halani, Hukaa makinikoni, Linafaa maishani, Hapa hapa duniani. Ingawa jana nyumbani, Siku niliyobaini, Hata leo furahani, Nakuweka pongezini. Kijana huyu nyikani, Akiwa hisabatini, Kanuniye mkononi, Kaifikiri kichwani. Ndipo nilipobaini, Kafika hisabatini, Kasogea nyongezani, Hapa hapa duniani. Kafika hisabatini, Kashikilia kanuni, Kuingia umrini, Kakaa makinikoni. Hesabuye kabaini, Kamjalia Manani, Kaingia furahani, Yamfaa maishani. Nyongezaye umrini, Hapa hapa duniani, Ufurahi maishani, Singie ubazazini. Sivutwe hisabatini, Duara kulibaini, Ukaidai kanuni, Ukokotozi pupani. Sivutwe hisabatini, Maumbo kuyabaini, Kuchora karatasini, Ukafika ushenzini. Hari yako maishani, Tuliza kichwa nyumbani, Makinika ubwabwani, Ukishibishe tumboni. Busara zako kichwani, Ziongeze kwa makini, Ufike makinikoni, Utulie furahani. Nyongezayo umrini, Ikufae maishani, Hapa hapa duniani, Sichenge msikitini. Wasalamu tamkoni, Nalitoa mdomoni, Ukae mshawashani, Vilevile moralini. Sijiweke haramuni, Kulazimisha kanuni, Iliyo hisabatini, Ukae makinikoni. Na kwa kheri tamkoni, Naitoa mdomoni, Naenda zangu nyumbani, Nikae pumzikoni. UJUMBE Shamsa Cyprian ... Read More
Hivi unazijua Dalili 5 Za Mwanaume Anayekupenda Kwa Dhati??  Undapo utaona dalili hizi kwa mwezi wako wa kiume basi tambua fika basi, ya kwamba anMapenzi ya kweli. 1. Anakusaidia fedha pale unapokua umekwama kabisa, yuko na jukumu la kukusaidia kiuchumi. Anapenda kukupa kile ambacho amejaaliwa nacho. Hana mkono wa birika, Huyu anakupenda! 2. Anazungumzia future yake na wewe, mipango ya baadae pamoja na wewe, huyu anayo dhamira ya dhati ku Anakupigia simu mara kwa mara na kukuuliza siku yako imeendaje. Anafanya hivi kirafiki na kwa upendo, haigizi. Anakupenda kweli. 3. Anakutembelea mara kwa mara, anakuwa karibu na wewe kipindi unaumwa, hii inamaanisha kwamba yupo tayari kukuvumilia katika shida na raha. Mpende mwanaume huyu. 4. Anawapenda ndugu zako kama ndugu zake. Anaongea nao vizuri na kusaidiana mambo ya hapa na pale. Mtizame kwa jicho la tatu huyu mwanaume! 5. Anaongea na wewe kwa adabu na kwa upole, anakukosoa bila wasiwasi kama kuna mambo unaenenda visivyo. Anakuelekeza njia zilizonyoka..sio wa kumuacha huyu! ... Read More
Mbinu Tata Za Kumfanya Mwanamke Ajigonge Kwako Kirahisi  #1 Mfanye mwanamke ajieleze kwako Unaweza kumuuliza swali kama “Ni kitu gani ambacho kinakufanya unique/tofauti na wengine?” Ama kumwambia, “Wewe unakaa mdogo sana kiumri kwangu. Ni kitu gani ambacho uko nacho ambacho kitaziba pengo hilo?” Ataanza kukupatia sababu ambazo anajiona kuwa yeye ni unique – kiufupi atakuwa akijaribu kujieleza zaidi ili ajipendekeze kwako/ umpende zaidi. Yaani atakuwa anajaribu kuhakikisha kuwa unaridhika na kila kitu ambacho atakwambia. Na uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa kadri mwanamke anavyokuwa mrembo ndivyo zaidi utakavyohitajika kumfanya ajihitimishe kwako, usiogope kumuuliza maswali ambayo yatamlazimu ajihitimize kwako. Muulize maswali mazito. Muulize maswali ambayo itakuwa ngumu kwake kujihitimu kwako. Na kitu cha kufurahisha kuhusu wanawake warembo, ni kuwa wamezoea kufukuziwa na wanaume kiasi cha kuwa ukianza kuuliza maswali na kujihitimu kwako, atafall na wewe zaidi. Hii ni kwa sababu hawajazoea kuulizwa maswali kama hayo. Hawajazoea kuambiwa, “Wewe si mwanamke type yangu.” ama, “Ningekutongoza lakini unanikumbusha ndugu yangu wa kike mdogo.” Pia unapaswa kuhitimisha wanawake kulingana na ladha yako. Labda kwa mfano hupendi wanawake wanaovuta sigara, kunywa pombe nk, basi mhitimishe kwa kutumia mambo haya. Usimfiche. Mwambie ukweli. Kumwambia mambo kama haya kutamfanya ajue vigezo vyako. Unampa challenge na yeye kutaka kutimiza vigezo vyako. Mbinu hii ni rahisi ya kumuwin kirahisi na kumfanya akufukuzie. #2 Tumia Mwili wako Mara ya kwanza unapoongea na mwanamke huwa anaangalia kando. Wewe ndie uko wazi, unaongea na yeye, unamwangalia, lakini yeye ameangalia kando kabisa. Hapo kuna ile hisia ambayo inakuja ndani yako kuwa huyu mwanamke hamakiniki na wewe kabisa. Well, hapa ndipo unatumia mbinu funge ya kuiga vile ambavyo anafanya yeye. Wakati umemuapproach, si lazima umuangalie mzima mzima kwanza, unaweza kuangalia kiupande. Na akiongea kitu ambacho umependezwa nacho, unaweza kutumia mwondoko wazi kwa kuangalia upande wake. Na akisema kitu ambacho hujapenda basi tumia mwondoko funge kwa kuangalia kando. Mbinu hii hufanya kazi kwa kuchukua atenshen na umakinifu wa mwanamke. Atamakinika kwa kila neno ambalo atakwambia. Mwishowe itajeuka kuwa ni yeye ndiye anayekufukuzia na wala si wewe. Mbinu hii pia inampa confidence ya kutamka mambo ambayo si rahisi kutamkwa na mwanamke hivihivi. #3 Ongea Kwa Kujiamini na Amri Ndani yake Katu mwanamke hawezi kukufukuzia kama utatumia toni saidizi kama, “Mambo waendeleaje?” ambapo sentensi kama hii toni ya sauti inapanda mwishoni. Kama vile unauliza swali. Matumizi ya sentensi hizi zitakufanya uonekane mtu mdhaifu, mhitaji, na utafanya wanawake wakukimbie. Lakini ukitumia toni saidizi zilizovunjwa kwa mwanamke kama, “Hey! Njoo hapa! Waendeleaje!” unatoa sauti ya kuamrisha na ya kutoa maelekezo. Na kwa kuwa uasili wa mwanamke ni kufuata amri, atakujibu kwa kutafuta toni saidizi ili aweze kujihitimisha kwako. Atakwambia, “Mmh, jina langu ni Mamito?” huku akitaka umthibitishe. So, ukimwambia, “Sasa, mpangilio wako ni upi!? kwa toni saidizi iliyovunjwa, atakujibu... “Mmh, mimi mwanafunzi nasomea...huu ni mwaka wangu wa...” Kiufupi hapa anajaribu kujieleza zaidi kwako kulingana na vile sauti yako ilivyotoka. [Soma: Jinsi ya kuwa mwanaume bora ya wote] #4 Weka nafasi na Pozi Katika Maongezi yako Unapoongea na mwanamke, hutaki kuona umepalilia maongezi bila mpangilio, badala yake huwa unataka nafasi angalau kurudi nyuma kiasi kuyapa maongezi yenu nafasi ya kupumua. Unaruhusu kuwe na angalau kimya ndani yake. Kimya ambacho kinaenda polepole. Na nafasi ambayo utampa mwanamke nafasi ya kujileta kwako ili kuteka atenshen yako. So mpe mwanamke nafasi ya kujiekeza kwako, na utagundua kuwa mwanamke huyu anakusaidia pakubwa kuyafanya maongezi yenu yanawiri. Atafurahi kukupa namba yake ya simu kwa kuwa anakufukuzia. Atafurahi kukutana na wewe katika deti ya pili. Na hatakutatiza zile nyakati za mwisho mwisho za kumuomba penzi. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Sikuweza kushika mimba kwa miaka 10 kwenye ndoa yangu, nilikuwa kwenye ukingo wa kupoteza ndoa yangu kwa sababu mume wangu alihitaji mtoto wa kumzaa, mwenzangu wa kazi alinielekeza kwa Dr Dawn, Alikubali kunifanyia tambiko la ujauzito, nilifuata maagizo aliyonipa, na pia mshangao wangu, nilipata ujauzito ndani ya wiki 6, mimi na mume wangu tukafanya mtihani na matokeo yakaonyesha mapacha, Lakini sasa nina wavulana wangu 2 warembo, zote namshukuru Mungu Mwenyezi kwa kumtumia Dk Dawn kusaidia ndoa yangu,
Ninampendekeza Dr Dawn, kwa yeyote aliye na masuala ya uhusiano/ndoa au utasa, Dr Dawn hakika atakusaidia, wasiliana naye kwa Whatsapp: +2349046229159