Home → simulizi
→ RIWAYA………………………. ALL OF ME
MTUNZI…………………………….HAZRAT HUSSEIN
SEHEMU YA …………………………….. (01 )
EMAIL……………………………….. hazrahussein@gmail.com
Nyota njema huonekana asubuhi, hivyo ndivyo waungwana wanavyosema. Hata mimi nasadiki maneno hayo. Maana Kila siku niamkapo asubuhi huwa naijua kua siku hiyo huwa na furaha kwangu au huwa ya kawaida kulingana na kipato changu nikiingizacho baada ya kufanya kazi usiku kucha.
Wengi huniita Shamira, au Shammy. Ila mimi hupenda kujiita Queen kutokana na muonekano wangu na jinsi ninavyojikubali.
Zamani nilikua naishi temeke mikoroshi, ila kwa sasa nimepangiwa upande mzima na mwanaume anayenimiliki ambaye ni mume wa mtu.
Mbali na ufadhil huo niliofadhiliwa, lakini mimi ni mmoja kati ya ndege aina ya kunguru. Huwezi kunifuga. Hivyo siku zote niliamini kuwa jasiri haachi asili na mimi niliona vigumu kuacha asili yangu iliyonifanya nipate kile ninachokihitaji kwa haraka.
Sijui Idadi ya wanaume niliolala nao mpaka sasa, ila ninachojua kua hakuna mwanaume ambaye aliugusa mwili wangu na kuacha kuurudia. Na hakuna mwanaume ambaye aliijutia laki mbili yake aliyoitoa kwangu kwa usiku mmoja aliolala na mimi.
Kuna waliokua wanalia na kunipigia magoti na kuniambia kua wapo tayari kunioa. Niliwaangalia na kuwacheka. Maana ndani ya moyo wangu sikua na chembe hata ya ukubwa wa mchele ya upendo juu ya mwanaume yoyote.
Bali pesa ndio alikua bwana wangu wa ukweli na nilimpa moyo wangu wote. Na daima nilimuabudu na kumfuata popote pale alipo.
Rangi yangu ya ung`aavu ndio iliokua inawachanganya wanaume wengi. Pia uteke wa kifua changu na umri ndio kumefanya niwafanye watu waathirike kisaikolojia pindi wanionapo kwenye anga zangu.
Hakuna mtu yoyote mtaani kwetu ambaye alikua anijua kazi niifanyayo, zaidi waliniona tu nikibadilisha nguo kila toleo na chumba changu kilitimia kila aina ya urembo unaotakiwa kuwepo kwenye chumba cha mtoto wa kike.
Mtaani sikua na story na mtu wala kumpa nafasi mtu yeyote kunizoea. Hata wanaume waliokuja kunipigia misele, niliwaagalia kwa dharau na sikuwajibu chochote.
Binti maringo ndio jina nililotungwa huko Temeke na mimi nililipokea kwakua ni kweli nilikua na maringo zaidi ya twiga mbugani.
Mpaka nahama huko temeke na kuhamia hapa kijitonyama ambapo ndio naishi wa sasa, sikuwahi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu yoyote. Ila huyu jamaa ambaye anamiliki maduka ya nguo hapa mjini, niliamua kumpa nafasi nje ya moyo wangu ili mradi tu aweze kunilipia mahitaji yangu niyatakayo bila kuchukua hata senti tano kutoka kwenywe account yangu.
Kwakua nafasi yake yeye ya kuja kwangu ilikua ni mchana pele yake, hivyo hakuweza kunibana kufanya yangu usiku.
Kwakua mchana huwa nautumia kwa kulala, basi kila akija hunikuta nimetulia ndani mtoto wa kike wala sina dalili za kutoka.
Basi moyo wake huburudika na kujiona amepata tulizo la moyo bila kujua kua alipata gume gume lililoshindikana na wazazi mpaka mabazazi.
Mvuto wangu uliwatosha kuwapa darasa masister doo wa mtaa huo niliohamia kwa jinsi nilivyokua nawakimbiza kwa kila kitu.
Kioo changu cha kujiona mwili mzima kiliniambia kua mimi nilikua na umbo jembamba. Lakini kuanzia kiunoni, nilikua na shape ya kibantu na iliyokua pana na kutengeneza hipsi zilitengeneza namba nane ya ukweli. Kibinda cha wastani nilichojaaliwa na Mungu na sio maujanja ya wachina ndicho kilichowaua wanaume wote waliojaribu kuyageuza macho yao kuniangalia.
ITAENDELEA
RIWAYA………………………. ALL OF ME
MTUNZI…………………………….HAZRAT HUSSEIN
SEHEMU YA …………………………….. (02 )
EMAIL……………………………….. hazrahussein@gmail.com
Kioo changu cha kujiona mwili mzima kiliniambia kua mimi nilikua na umbo jembamba. Lakini kuanzia kiunoni, nilikua na shape ya kibantu na iliyokua pana na kutengeneza hipsi zilitengeneza namba nane ya ukweli. Kibinda cha wastani nilichojaaliwa na Mungu na sio maujanja ya wachina ndicho kilichowaua wanaume wote waliojaribu kuyageuza macho yao kuniangalia
Nilijua ni jinsi gani nilivyoweza kuwatesa wanaume wenye uchu wa watoto wazuri kama mimi. Wakati mwengine nilikua nafanya makusudi, ili mradi tu kuwachengua wakwara na walozi wa kufanya mapenzi na mabinti waliokua na hadhi ya nyota tano.
Siku moja wakati nipo kwenye shughuli zangu za usiku. Nilimuona mtu akiwa ana chechemea na kuja upande wetu. Mkononi alikua ameshika fimbo Fulani nyeupe huku akiwa haitumii. Alikua amevaa nguo iliyokua imechafuka na matope karibia suruali yote.
Nillimsogelea na kumkuta akiwa ameanguka chini.
“pole,.. umepatwa na nini kaka yangu.” Nilimuuliza baada ya kuingiwa na imani
Baada ya kumuona amelowana na damu mguuni.
“nimepigwa na wezi waliokua wantaka kuiba visenti vyangu.” Aliongea huku akiushikilia mguu wake huku akionyesha wazi kua alikua anaumia.
“pole.. subiri kidogo.” Niliongea hivyo na kumfuata dereva wa bajaji alikua anakesha maeneo hayo na kwenda nae hadi kwa Yule mtu ambaye nilimkuta amekaa pale pale.
“mpeleke hospitali “ nilliongea baada ya kusaidiana na Yule dereva wa bajaji kumuingiza Yule kaka kwenye bajaji hiyo.
Nilimpa huyo kaka shilingi elfu thelathini kama pocket money kama ikilazimika atoe pesa huko hospitalini, kisha nikamlipa shilingi elfu kumi huyo dereva wa bajaji kama nauli yake ya kumpeleka mgonjwa huyo hospitali.
Mimi sikwenda kutokana na kua na miadi na mshefa wangu wa serikalini muda huo ambaye dakika ishirini baadae alinipitia na kwenda kupumzika nae mpaka asubuhi.
Nilirudi nyumbani na kujifungia ndani kama kawaida yangu baada ya kuoga na kujilaza kitandani ili kupunguza usingizi na uchovu niliokua nao. Ilipofika saa saba mchana,alikuja mpenzi wangu na kuingia ndani. Alinikuta nimetulia sebuleni nikifuatilia moja ya tamthilia niipendayo.
“karibu mpenzi wangu.” Nilimpokea kwa bashasha huku nikijiangusha kifuani kwake baada ya kumbusu.
“ahsante… nina njaa, umeandaa nini?” aliniuliza baada ya kuungana na mimi sebuleni.
“hata sijapika mume wangu, leo hii nilivyochoka. Utanisamehe tu wangu.” Niliongea kwa sauti ya kudeka
“sasa wewe ndio unashindia hizo pop cone?” aliniuliza baada ya kuliona bakuli kubwa la pop cone kwenye meza huku pembeni kukiwa na glass kubwa ya maziwa.
“hii ndio nitolee tena, mimi nikiwa peke yangu huwa nakula vitu simple tu kama hivi . hasa mchana.” Nilimjibu na umfanya atabasamu.
“poa, wacha niende hotelini, kisha nitarudi ofisini . nafikiri tutaonana tena kesho.” Alongea na kunyanyuka.
Alitoa wallet yake mfukoni na kukata kiasi cha fedha bila ya kuhesabu na kunikabidhi.
“take care baby.” Nilimuaga na yeye akaondoka zake.
Baada ya tamthilia hiyo kuisha, nilikumbuka kua nilikua na mgonjwa hospitaini. Nilijiandaa na kwenda kwenye hospitali aliyopelekwa Yule kaka. Nilifika na nikaelezea mapokezi juuya mgonjwa aliyeletwa saa saba usiku.
Baada ya kuelekezwa ward aliyolazwa, nilienda na kumkuta akiwa amefungwa ogo mguuni. Ghafla nilishtuka baada ya kuona uzuri wa mwanaume huyo aliyekua kama ananiangalia bila ya kupepesa macho yake juu yangu.
Nilijikuta mapigo ya moyo wangu yamebadilika ghafla. Na hata ile confidence yangu niliyokuja nayo ilipotea kabisa na kujikuta sina usemo juu ya mwanaume huyo.
ITAENDELEA
RIWAYA………………………. ALL OF ME
MTUNZI…………………………….HAZRAT HUSSEIN
SEHEMU YA …………………………….. (03)
EMAIL……………………………….. hazrahussein@gmail.com
Baada ya kuelekezwa ward aliyolazwa, nilienda na kumkuta akiwa amefungwa ogo mguuni. Ghafla nilishtuka baada ya kuona uzuri wa mwanaume huyo aliyekua kama ananiangalia bila ya kupepesa macho yake juu yangu.
Nilijikuta mapigo ya moyo wangu yamebadilika ghafla. Na hata ile confidence yangu niliyokuja nayo ilipotea kabisa na kujikuta sina usemo juu ya mwanaume huyo.
Alikua aniangalia muda wote na kunifanya nianze kuona aibu. Mara daktari akaingia na kunikuta mimi pale.
“habari yako binti “ alinisalimia Yule daktari baada ya kuingia pale.
“salama tu .” niliitikia na kumuangalia Yule daktari usoni.
“mgonjwa wako amevunjika mguu…. Ila nyinyi ndio mnapaswa kulaumiwa kwa kumuacha mlemavu wa macho kama huyu kutembea usiku peke yake.” Aliongea daktari maneno yaliyonifanya nigeuze shingo yangu haraka na kumuangalia Yule mtu ambaye macho yake hayakunijulisha haraka kama alikua haoni.
“huyu ni kipofu?” niliuliza kwa mshangao
“si umesema ndugu yako, vipi hujui kama haoni?” alingea daktari na kunifanya niumbuke.
“kusema ukweli dokta, mimi sina undugu nae huyu mtu, ila nilimuona tu kama alikua anahitaji msaada pale alipokua ndio maana nikaamua kuchukua uamuzi wa kuhakikisha anafika hospitali.” Niliongea na kumuangalia Yule daktari ambaye alitabasamu na kunionyesha ishara za kufurahia uamuzi wangu.
“basi ndio hivyo, huyu haoni hapo alipo, ila ukimuangalia ni kama mtu ambaye hana madhara yoyote ya macho… pia alikua anaulizia fimbo yake, umebahatika kuiona?” aliniuliza swali hilo Yule Daktari na kunifanya nishindwe jinsi ya kujibu kwakua sikua na kumbu kumbu za uwepo wa hiyo fimbo.
Baada ya kuongea na daktari huyo, nilitajiwa gharama nilizotakiwa kulipa. Kuanzia vipimo ,tiba pamoja na dawa, ilifikia laki moja na thamanini elfu.
Nilitoka nje na kumpigia mshefa wangu na kumuomba kiasi hicho cha fedha, hazikupita hata dakika kumi, shilingi laki tatu ziliingia kwenye accounti yangu ya simu. Nilitoka na kwenda kweye kibanda cha Tigo pesa na kuitoa hiyo hela.
Nilirudi hospitalini na kuilipa hiyo bili. Baada ya kupewa maelezo ya kutosha kutoka kwa daktari, nilimchukua mgonjwa wangu na kumpeleka nyumbani kwangu ninapoishi.
Nilimshika mkono na kumuweka kwenye moja ya sofa yaliyokuwemo ndani kwangu.
“karibu…. Na pole sana.” Niliongea na kumuangalia mvulana huyo aliyekua mzuri wa sura na umbo pia. Lakini sikujua hata kama alikua anajijua kama alikua na uzuri huo kutokana na tatizo alilokua nalo la kutokuona.
“ahsante… pia nashukuru sana kwa yote uliyoyatenda juu yangu.” Aliongea Yule kaka na kunifanya nitabasamu.
“usijali, kwa hali kama ile uliyokua nayo, niliumia sana na nikajikuta automatically nimeingiwa na imani na kuamua kukusaidia. Ila cha kushukuru Mungu hawajakupa tu ulemavu mwengine.” Niliongea huku nikimuangalia mwanaume huyo kwa saura iliyojaa imani na huruma juu yake.
“ni kweli.. mungu atakulipa dada yangu.” Aliongea na yule kaka.
“unaishi wapi hapa dar?” nilimuuliza swali baada ya kurudi kuchukua kisu na kuanza kukata machungwa yaliyokwisha menywa na muuza machungwa huko barabarani nilipo yanunua.
“nilikua naishi Temeke. Ila kwa sasa sina pa kuishi. Maana toka nilipopoteza macho yangu, bado sijaonana na mtu yeyote anaye nijua. Kiufupi maisha yangu nahisi yamefika mwisho. Maana nimepoteza dira ya maisha yangu na sina msaada toka nilipokua na macho yangu. Nahisi hiki kilema ndio sababu iliyonifanya nikate tamaa ya maisha.” Aliongea huyo kaka na kunifanya nizidi kumuonea huruma.
“kwa hiyo unataka kuniambia kua hukuzaliwa na ulemavu wa macho?” niliuliza kwa mshangao.
“ndiio,.. nimepata huu ulemavu wa macho miezi miwili iliyopita..” Aliongea na kunifanya nihuzunike.
“pole sana… imekua haraka mpaka tumeshindwa kufahamiana kwa majina. Mimi naitwa Shamira, au Shammy. Sijui wewe unaitwa nani?”
“naitwa AMOUR.” Alinijibu kiufupi.
“jina zuri kama wewe mwenyewe.” Nilimsifia na kumfanya atabasamu. Nilijikuta nainjoy kuuona mwanya mdogo wa mvulana huyo uliopambwa na ma dim pose yiliyobonyea mashavuni kwake.
“ahsante.” Alishukuru huku akiendelea kutabasamu.
“unaweza kunihadithia ilikuaje mpaka ukapoteza macho yako?” niliuliza baada ya kuona nahitaji kumjua zaidi ili nijue ni jinsi gani naweza kumsaidia.
“huwa naumia sana pindi niikumbukapo siku niliyopoteza macho yangu. Ila kwakua unahitaji kufahamu ilikuwaje, sina budi kukuhadithia kila kitu…….”
ITAENDELEA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: