Chombezo fupi: Kitamu Kinaliwa na Wengi Sehemu: 01 Simu: 0658247651 *Yote (1500)*Tu Mmh kweli harua haina makombo lakini yataka moyo kula kile ambacho umekiona kimeliwa na mwenzako muda mfupi. Sweet mama Sukari siamini, lakini bado nampenda na msaada wake kwangu mkubwa..Lakini kwa hili mmmh we acha tu...Kafanya nini kwa nini uumie kichwa? Endelea sasa uone utamu wake.... *************** Niliyafumbua macho yangu na kujikuta sehemu niliyolala ni ngeni machoni mwangu. Hali ile ilinishtua sana na kufanya ninyanyuke na kukaa kitako, kilichonishtua zaidi hali niliyojikutana nayo ya kuwa mtupu bila nguo kuonyesha nimelala bila nguo. Pembeni yangu kwenye kioo kikubwa kulikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa akijipaka mafuta akiwa amenipa mgongo. Kwa haraka haraka kila nilivyo muweka akilini mwangu alikuwa mgeni kwangu. Nilijiuliza huyu ni nani msichana aliyeonekana mbichi tena aliyependelewa mandhari ya nyuma na Mwenyezi. Hakuna na wasiwasi alichukua nguo yake ya ndani na kuivaa akiwa bado amenipa mgongo. Swali lilikuwa nilifanya naye mapenzi? Kama tulifanya mapenzi tulitumia kinga au ndiyo yaleyale ya mlevi hukumbuka mpira baada ya tendo. Kwa haraka nilijikumbusha mara ya mwisho jana yake nilikuwa wapi? Mmh! Nilikumbuka jana ilikuwa siku mbaya sana kwangu pale nilipomfumania mpenzi wangu na rafiki yangu wa damu kitu kilichonichanganya akili. Kutokana na kuchanganyikiwa nilijikuta nimekwenda Billicanas na kuamua kunywa sana....Mmh! Nakumbuka kuna mrembo alikuja na kuomba tujumuike meza moja..Ooh! Sawa kweli kabisa naye akaanza kutembeza ofa. Kuanzia hapo kilichoendelea sikujua mpaka nilipojikuta pale. Wakati nikiwa kwenye lindi la mawazo nlishtushwa na sauti tamu na laini ya yule mrembo ambaye wakati huo alikuwa amegeuka akiwa amejifunga mtandio mwepesi na ndani alikuwa amevaa bikini nyekundu. "Vipi mpenzi mbona upo katika hali hiyo?" nilishtuka na kujikuta nikisimama kitandani bila kujielewa kama sina nguo mwilini na kunifanya niwe kichekesho cha kusimama nikiwa mtupu. Niliichukua shuka na kujifunga kisha nilimfuata yule msichana ambaye alionyesha ni mtu wa gharama kutokana na maskioni na kifuani kuwa na vito vya gharama. Nilijikuta nimemfuata na kumkunja kwa kuushika ule mtandio ambao ulitoka mwilini mwake na kumbakiza na nguo ya ndani tu. "We ni nani na hapa nipo wapi?" "Taratibu mpenzi mwanamke hatumiwi nguvu hivyo." "Nani mpenzi wako malaya mkubwa?" nilimkata kauli "Asante nashukuru, hiyo ndiyo asante yako kwa wema niliokutendea. Nimepoteza muda wangu kwa ajili yako, leo hii shukurani yako ni kuniita mimi malaya asante...asante.. nashukuru." Baada ya kusema vile yule binti mrembo alianza kulia huku akikaa kitandani bila kuokota mtandio wake. Kauli ile ilinifanya nijione mjinga kwa kurupuka kutukana bila kujua nimefikaje pale. *** ***Mwambie na mwenzako kuwa Uwanja wa Simulizi tumerudi upya na kivingine kabisa.. *** *Ni chombezo mpya na fupi, litakuwa likitoka kila siku hapa hapa team 🅱professional love .*

at 5:57 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top