KIJIJI CHA SHETANI Sehemu Ya Nane Ilipoishia ...... Ni saa 4 mda wa mapumziko Zuma anaamka kutoka usingizini na kukutana na watu wachache darasani ambao walikuwa wamebaki kutokana na wao kutokwenda pumziko. Mara mlangoni ilisikika sauti ya Rama ikisema"Zuma unaitwa ofisini kuna mgeni wako amekuja kaleta taarifa kutoka nyumbani".Alisema Rama na kuuwacha moyo wa Zuma ukilipuka kwa shauku ya kujua ni taarifa gani iliyoletwa. Sasa Endelea .......Huku moyo ukimdunda Zuma aliondoka upesi upesi kuelekea ofisini ili kufahamu ni nani alieleta taarifa na zilikuwa zinahusu nini,taratibu kwa nyuma alifuatiwa na rafiki yake ambae ni Rama. Zuma alifika kwenye mlango wa ofisi na moja kwa moja aligonganisha macho na kijana alieleta taarifa kwake,Kijana alikwenda kwa jina la Mateo,Zuma alikuwa anamjua vema sana Mateo kwa sababu walikuwa wanaishi mtaa mmoja pale kijijini. Taarifa zilizoletwa na Mateo hazikuwa nzuri,Zuma alivutwa na mateo kwa nje kidogo pembeni ya ofisi kisha moja kwa moja Mateo kabla hajaongea alitoa kitambaa mfukoni kisha kufuta kajasho kembamba kalikokuwa kanamtililika kutokana na mwendo wa baiskeli kutoka nyumbani mpaka pale shuleni. "Zuma mama yako yupo hoi sana hivi nimeondoka sijui nini kinaendelea huko nyuma nimeongea na waalimu naitaji nikubebe haraka sana tuelekee nyumbani maana mama yako kila mara anahangaika na kuhema kwa nguvu na kwa uchungu huku akitaja jina lako,chukua mkoba uje tupande baiskeli tuwahi."Aliongea Mateo wakati huo hata kabla hajamaliza maneno ya mwisho Zuma alikuwa ameshaanza kulia huku akianza mwendo kwenda kuchukua mfuko wa Daftari. Aliingia Darasani wakati huo kengere ya mapumziko ilikuwa imeshagonga na wanafunzi walikuwa wameshaingia darasani,Aliona aibu kuingia darasani hivyo alisimama karibu na darasa,Rafiki yake ambae ni Rama yeye alikuwa bado kasimama kushuhudia nini kilichotokea tena nyumbani hivyo hakuingia darasani.Zuma akiwa analia alimuagiza mfuko Rama darasani na Rama taratiibu aliingia kuchukua mfuko wa madaftari wa rafiki yake huku machozi yakiwa yanamlenga kumsitikia rafiki yake. Rama alipochukua tu mfuko wa Zuma wanafunzi walijua moja kwa moja huenda mwanafunzi mwenzao kunakitu kimempata,Baadhi ya wanafunzi walianza kumfuata nyuma nyuma Rama na walipofika mlangoni walimuona Rama anamkabidhi mfuko Zuma na mara moja Zuma akaanza safari ya kuondoka kuelekea nyumbani. * * * * * * Chumba cha Mama Zuma kilizunguukwa na baadhi ya akina Mama ambao ni rafiki zake wa karibu sana na Mama Zuma,Wengine alikuwa anafanya nao biashara ya mgahawa pamoja na wengine ni majirani wa hapa na pale,Mama Zuma alikuwa anahema kwa shida sana,Wakati huo Miriamu na Amos walikuwa wanaendelea kuangusha kilio baada ya kuona hali ya mama yao,Mama Zuma alikuwa akihangaika sana kwa kurusha rusha miguu na mikono huku akionyesha kabisa huenda kifua kilikuwa kimebana sana Moja kati ya akina mama waliokuwemo mle ni Mama yake na Rama,Alichukua bakuri la maji ya baridi na kitambaa kisha kumshusha blauzi Mama Zuma na kuanza kumkanda kifuani na Maji ya Baridi,Mama Rama alijitahidi sana kwa kila jitihada kumkanda kifua Mama Zuma lakini juhudi hazikuzaa matunda,Walianza kupanga mipango ya kumpeleka Mama Zuma kwa mganga huku wakijua moja kwa moja huenda amelogwa,Hii ilikuwa ni imani ya wanakijiji wengi wao hawakupenda kwenda kutibiwa hospitali kwa sababu zahanati ya kijiji iliwekwa mbali sana na mazingira yao,pia ni utaratibu ambao waliukuta wakitumia babu zao na mama zao pindi walipokuwa wakiumwa moja kwa moja waliamini kwamba huenda wanachezeana wao kwa wao,Wengi wao walijikuta wanapoteza kuku,Ng'ombe na mbuzi kwa kupeleka kwa waganga hata pindi walipoumwa mafua. Wakati wazo la kumpeleka kwa mganga Mama Zuma likiendelea ndipo Mama Rama akawaambia akina Mama wenzake kuwa yeye kuna mganga huwa anamtengemea sana hivyo kama wako tayari waagize kijana akaitwe,hatimae wote walikubaliana mganga huyo kuitwa. * * * * * * Mateo aliendesha baiskeli kwa kasi sana kutoka pale shule kuelekea nyumbani,Haikuchukua muda mlefu na hatimae walitia timu nyumbani,moja kwa moja Zuma alikimbilia chumbani kwa Mama yake na kumkuta Mama yake yupo katika hali mbaya sana,Huzuni na vilio vilitawala ndani mle. Muda si mlefu mganga alieendewa aligoma kuja na kusema kwamba Mgonjwa ndio anatakiwa aende kule,taarifa hiyo ililudishwa na kijana alietumwa,Ilikuwa hakuna njia nyingine moja kwa moja taratibu za kumpakia Mama Zuma kwa ajili ya kumpeleka kwa Mganga zilianza. * * * * * * Yapata majira ya saa 7 mchana Mateo akisaidizana na yule kijana alietumwa kumuendea mganga mara ya kwanza walimshusha mama Zuma kuelekea kwenye kibanda cha mganga,Zuma hakuwa nyuma katika kufuatilia hali ya mama yake,Nae alifuata moja kwa moja mpaka ndani ya kile kibada cha mganga,Nyuma yake alifuatiwa na Mama Rama akiwa na akina Mama wenzake watatu. Baada tu ya Mama Zuma kuingia katika kile kibada cha Mganga hali ya hewa pale ilianza kubadilika,Maumivu ya kifua kwa Mama Zuma yalizidi sana kitendo kilichopelekea Mama Zuma kuanza kujipiga piga kifua chake kwa mikono kutokana na maumivu makali na kuhema kwa nguvu. Mganga alichukua dawa moja mkononi mwake na kumpaka Mama Zuma katika paji lake la uso.Taratibu Mama Zuma alianza kupunguza kuhangaika na hatimae akaanza kuhema taratibu. Mambo yalibadilika kwa Mganga kwani alianza kuhangaika na kurusha rusha mikono,Balaa likawa mle ndani,Mganga akaanza kutoa macho makali na makubwa kana kwamba anakabwa,Mara kilisikika kibao kikali sana mle ndani ya kile kibanda cha Mganga,Kibao kile alipigwa Mganga na mtu aliempiga hakuonekana,Zuma na na kundi lake likiongozwa na Mama Rama walishuhudia kuona jicho moja la mganga liling'oka na kwenda kupigizwa ukutani na kupasuka,Walipomuangalia mganga hakua tena mganga bali ni Marehemu,Wakati huo Mama Zuma nae alianza kutupa mikono ya BURIANI KIJIJI CHA SHETANI Sehemu ya 9 Ilipoishia .... Zuma na na kundi lake likiongozwa na Mama Rama walishuhudia kuona jicho moja la mganga liling'oka na kwenda kupigizwa ukutani na kupasuka,Walipomuangalia mganga hakua tena mganga bali ni Marehemu,Wakati huo Mama Zuma nae alianza kutupa mikono ya BURIANI Sasa endelea Povu zito lilianza kutoka mdomoni mwa mama Zuma wakati huo ikiambatana na kitendo cha kurusha rusha mikono na miguu,Ilikuwa ni safari ya mwisho ya mama Zuma katika kile kibanda cha mganga,Kilio na kelele za Zuma kumlilia mama yake zilienea mahali pale pamoja na juhudi za Zuma kulia bado hazikuambua kitu kwani mama Zuma alivuta pumzi ndefu na ya mwisho hatimae umauti ulimfika. Kutokana na kilio kikali alicholia Zuma alijikuta mdomo umefumba huku machozi yakiendelea kumtoka,mwili wake ulianza kutetemeka baada ya kumuona mama yake amekwisha aga dunia,Taratibu Zuma alizimia mahali pale,Matukio yote yale yaliendelea kushuhudiwa na mama Rama akiwa na timu yake,Hawakuwa na cha kufanya zaidi ya kubebelea mwili wa mama Zuma pamoja na kumbeba Zuma aliezimia tayari kwa maandalizi ya msiba. Kilio kilianza na Mama Rama baada ya kukaribia nyumbani kwa mama Zuma huku kikifuatiwa na wenzake,Hatimae panapokuwepo na kelele basi kuna jambo kwani jamaa wa karibu na marafiki walianza kumpokea mama Rama kilio baada ya kujua tukio la Mama Zuma kufariki,Punde si punde nyumbani kwa akina Zuma kukafurika na watu waliolia na kuomboleza kadri kwa kila mmoja alivyomjua mama Zuma. Juhudi za kuenda kumuita mzee Shomary ambae ni baba mzazi wa Mama Zuma zilifanyika lakini hazikuzaa matunda kwani walipofika nyumbani kwake walikutana na kufuri kubwa kuashiria kwamba mzee hayupo.Juhudi za kumtafuta zilifanyika lakini hazikuzaa matunda kwani kila walipouliza majirani hakuna hata mmoja alieagwa kuwa mzee yule anaenda wapi. Yapata saa 2 usiku Zuma akiwa bado amezimia licha ya juhudi za watu kumpepelea lakini ziligonga mwamba,walijitahidi kila njia kumfanya aamke lakini ilishindikana hivyo njia pekee walioifanya ni kumlaza chumbani mwake mpaka pindi atakaporudisha fahamu. Nje taratibu zingine ziliendelea watu waliwasha moto kwenye uwanja kwa ajiri ya kukesha wakimsubiri Mzee Shomary lakini mpaka yapata mda huo alikuwa bado hajatokea,Minong'ono ilisikika kuwa huenda kaenda porini mbali kwenye shughuri zake za uchunaji kamba na uchongaji mipini na hajafanikiwa kurudi,walijipa matumaini na kusema huenda akarudi usiku sana au kesho asubuhi,hapakuwa na muamuzi mwingine juu ya mazishi ya Mama Zuma zaidi ya Mzee Shomary au Zuma mwenyewe hivyo watu waliendelea kuota moto huku simulizi na hadithi za maisha za hapa na pale zikiendelea. * * * * * * Kwa mbali Zuma akiwa kafumba macho alianza kusikia ni kama kelele nyingi sana za shangwe na vigeregere vya fujo,akili yake haikuelewa kuwa ni nini hicho akili yake ilianza kukumbuka ni tendo gani la mwisho lililofanyika ndipo kabla hata hajafumbua macho mahali pale alipokuwa kalala alikuja kugundua kuwa tendo la mwisho ni la mama yake kuaga dunia,Moja kwa moja alijua kelele zile ni za msibani lakini alianza kuwa na mashaka baada ya kusikiliza kwa makini mno,Kelele zile hazikuwa za msibani maana zilikuwa ni kelele za shangwe kana kwamba watu wanashangilia ushindi wa kitu flani,Moyo wake ulianza kumuenda mbio na akajua moja kwa moja kwamba mahali alipokuwepo pale sio msibani au nyumbani,Ndipo alipokuja kufumbua macho na kukutana na uso wa bibi aliekondeana na mwili wake kuzeheka akiwa ameshika kisu na kukielekeza juu ya kifua chake,Alitamani kuvuta mikono ili aweze kukiondoa kile kisu kabla hakijafika vizuri juu ya kifua chake lakini alikuja kugundua kuwa alikuwa amefungwa mikono. Kwa kutumia macho yake haraka haraka aliangalia waliomzunguuka na hatikae alikutana na uso wa mzee Shomary ambae ni babu yake bila kusahau uso wa mzee Kagusa kiongozi mkuu wa uchawi ndani ya Ujiji.Mwili ulianza kumtetemeka sana,wakati huo wachawi wengine waliendelea kuuzunguuka ule mti mkubwa ambapo chini yake alikuwa kalazwa Zuma tayari kwa shughuri lasmi ya kukabidhiwa kijiti cha uchawi. Moja kwa moja yule bibi kwa kutumia kisu alichana ngozi ya juu ya kifuani upande wa moyo wa Zuma kwa kupitia kile kisu, damu nzito ilianza kutililika kutoka katika kifua cha Zuma,huku damu ikiendelea kutililika yule bibi aliemchana kifua Zuma aliludi nyuma kidogo na hatimae mkuu wa msafara wa uchawi wa lile eneo la ujiji alisogea kalibu na alipokuwa amelazwa Zuma. Mkononi mwake alishikilia kikombe kilichoonekana kuchakaa,Taratibu alianza kudondosha matone flani yaliyotoka ndani ya kile kikombe,yalikuwa si matone mengine bali matone ya damu ya mama yake na Zuma aliekwishafariki kwa kutolewa sadaka,Kadri matone ya damu yalivyozidi kudondoka kifuani mwa Zuma ndivyo lile jeraha nalo lilivyozidi kujiziba na hatimae radi zilianza kupiga eneo lile ambalo lilikuwa na giza nene,Mishipa ya mwili wa Zuma ilisimama na kutuna pia mwili wake ulianza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya bluu iliyochanganyikana na nyeusi,Pale pale babu yake ambae ni mzee Shomary alimshika na kumfumbua mdomo,wakati huo Zuma alikuwa akihangaika kujinasuma lakini haikuwezekana,alijitahidi kupiga kelele lakini hazikuzaa matunda,Hatimae mdomo wa Zuma ulifumbuliwa na mzee shomary ambae ni babu yake,Damu nzito ya Mama Zuma iliingia kinywani mwa mwanae ambae ni Zuma. mapigo ya moyo ya Zuma yaliongezeka kasi,Macho yake yalibadilika yakawa kama macho ya simba aliemulikwa na tochi usoni,Radi na ngurumo viliongezeka kasi. JE NINI KITAENDELEA Sehem ya 10 Ilipoishia ..... mapigo ya moyo ya Zuma yaliongezeka kasi,Macho yake yalibadilika yakawa kama macho ya simba aliemulikwa na tochi usoni,Radi na ngurumo viliongezeka kasi. Sasa endelea Shetani mkuu wa anga la ujiji aliingia kupitia mwili wa Zuma aliekuwa amelazwa mahali pale,wakati huo baada ya wafuasi wote wa uchawi wa eneo lile kujua kuwa tayari mkuu wao ameshawasili kupitia mwili wa Zuma wote walilala chini kumwabudu,wakati huo meza kuu ilikuwa tayari imeandaliwa na tayari sadaka ya nyama na damu vilivyotoka katika mwili wa Mama Zuma vilikuwa mezani kwa ajiri ya mkuu wao wa anga kuvitumia,Moja kwa moja mwili wa Zuma huku ukiwa umeingiliwa na Shetani yule ulikata kamba katika kile kitanda alichokuwa amelazwa,radi nyingi zilizidi kuongezeka,wafuasi wa uchawi wote waliohudhulia shughuri mzima ya Zuma kukabidhiwa uchawi walikuwa wamelala kifudi fudi kumwabudu na kumtukuza Mungu wao huku wakiwa wameongonzwa na viongozi wao mzee shomary, Kagusa pamoja na wale wazee wanne. Shetani yule alietumia mwili wa Zuma kuja alinyanyuka moja kwa moja kwa ajili ya kwenda kupata sadaka ya damu na nyama aliyokuwa kaandaliwa,moja kwa moja alielekea katika ile meza bila kupoteza muda alishika vipande vya nyama na kuanza kuvila vikiwa vibichi vinavuja damu,shughuri ya ulaji wa kiumbe yule iliendelea huku wengine wote wakiwa wamelala kifudi fudi kwa ajili ya kuendelea kutoa heshima kwa mkuu wao,hatimae baada ya radi kuwa kubwa mvua ilianza kunyesha taratibu Shetani yule aliemuingia Zuma alianza kuondoka mwilini mwa Zuma,akiwa pale mbele kwenye zile meza Zuma alidondoka na kupoteza fahamu tena,jeraha lake kifuani lilionekana kupona kabisa na hatimae akawa ameachiwa uchawi lasmi hivyo kilichobaki ni kuanza tu mafunzo ya kuimarishwa zaidi,Baada ya tukio hilo sherehe,shangwe na furaha ziliendelea tena maana walilolikusudia lilifanyika kwa muda muafaka. Kiongozi mkuu wa uchawi ambae ni mzee Kagusa alisimama na kwa heshma alienda kuuchukua mwili wa Zuma kisha kuuweka juu ya kitanda tena,kila aliehudhuria mahali pale alipita na kutoa heshima kwa mkuu yule mpya ambae ni Zuma kwa kuwa tayari ameshakubalika na mkuu wa anga,wakati wote huo Zuma alikuwa bado hajitambui. Ni asubuhi na mapema nyumbani kwa akina Zuma taratibu za hapa na pale zikiwa zinaendelea, kwa mbaali Zuma akiwa chumbani kwake huku ki jua chekundu kikiwa kinachomoza na kupenyeza kwenye nyufa za dirisha lake,Zuma alianza kusikia kelele za akina mama wanalia,Muda huo ndio fahamu harisi zinamrudi duniani toka alivyozimia jana pale kwa mganga,Babu yake ambae ni mzee Shomary aliitumia nafasi ile ili kumlisisha mjukuu wake mikoba baada ya kumtoa mwanae kafara ambae ni mama Zuma. Sasa akili ya Zuma ilianza kukumbuka matukio yaliyofanyika,kitu cha kwanza alikumbuka tukio la mwisho la pale kwa mganga la mama ake kuaga dunia,taratibu machozi yalianza kumtoka na kujikuta akianza kufumbua mdomo taratibu ili angalau alie kwa sauti ya kwikwi. Tukio la pili alianza kuhisi kama ilikuwa ni doto,ni tukio la yeye kukabidhiwa uchawi kama wachawi wale walivyokuwa wamepanga,alianza kukumbuka yale yote yaliyotokea usiku ule,Akiwa analia alijifunua kifua baada ya kukumbuka kuwa alichanwa na kisu kifuani,Cha ajabu alikutana na kovu la kidonda kilichopona,kovu hilo lilikuwa jeusi na palikuwa hakuna hata maumivu,Alianza kulia zaidi baada ya kukumbuka kuwa damu waliomlazimisha kunywa usiku ule ilikuwa ni damu ya mama yake,hasira zilimpanda na roho ya kisasi juu ya babu yake ambae ni mzee shomary iliongezeka. Akiwa mle chumbani alizidi kulia zaidi na hatimae watu waliokuwa maeneo ya karibu na kile chumba waliweza kumsikia"Zuma amezinduka jamani"ilikuwa ni sauti mama mmoja aliemsikia kwa ukaribu zaidi,waliingia vijana waliokuwa rafiki zake shule kwa ajiri ya kumbembeleza angalau kumfariji na kumuweka sawa,Mungu akasaidia kwa kiasi kidogo mambo yalienda sawa. Zuma alitoka nje akiwa na rafiki zake,Moja kwa moja alikutana na umati mkubwa wa wanakijiji waliohudhuria katika msiba ule wa mama yake,alipenyeza macho yake katika baraza la wazee walipokuwa wamekaa na moja kwa moja macho yake yalikutana na babu yake ambae ni mzee Shomary,alibaki anajiuliza ni nini kinachoendelea maana mpaka hapo alikuwa hajielewi,kilichomuacha njia panda ni kwamba usiku ndani ya kijiji cha uchawi alimuona babu yake kule na ndio alikuwa mshiriki mkuu sasa huku tena amekuja saa ngapi tena akiwa hana hata roho ya wasiwasi,akiwa anajiuliza hayo maswali ndipo alikuja tena akatupa jicho kwa babu yake,mwili wake ulianza kutetemeka baada ya kuhamisha macho kidogo pembeni ya babu yake na ndipo alipokutana uso kwa uso na mkuu wa uchawi wa eneo lile si mwingine bali ni Mzee kagusa,Jasho jembamba lilimtoka Zuma,uvumilivu ulimshinda mwili ulianza kutetemeka kwa hasira alitaka kunyanyuka na kwenda kuchukua kisu ili aje awachome wale wazee wote wawili lakini akili nyingine ilimzuia asifanye hivyo. Alimsogelea kijana mmoja pembeni na kumuuliza"Babu amefika hapa toka saa ngapi" Zuma aliuliza "Alikuja hapa usiku sana sikumbuki saa ngapi ila walikuja na huyo rafiki yake hapo pembeni walisema kwamba walikuwa wameenda porini kwenye shuguri zao na palikuwa mbali sana"alisema yule kijana. Zuma moja kwa moja akajua kwamba tayari wameshafanikiwa mbinu ile ya usiku ya yeye kurithi mikoba ya uchawi,"Lazima nimuue babu haiwezekani aniulie mama angu".Zuma alijisemea maneno hayo moyoni huku akiwa kainama machozi yakimtoka "Pole sana babu yangu....mipango ya Mungu tu hiyo tumshukuru Mungu kwa kila jambo mjukuu wangu maana yeye ndie muweza wa yote"Ilisikika sauti huku taratibu Zuma akishikwa mkono mahali alipokuwa amekaa,Aliponyanyua macho alikutana moja kwa moja na uso wa babu yake,Maneno yale aliyoyatoa babu kwa kujifanya hajui chochote kinachoendelea yalizidi kumliza sana Zuma na kumpandisha hasira,Bila kumjibu kitu chochote babu yake alinyanyuka na kwenda kulia zaidi chumbani kwake. Babu yake aliishia kutabasamu tu na kumwangalia mjukuu wake wakati anaondoka huku moyoni akijisemea"Tumekuweza huna tena ujanja lazima uwe kiongozi wetu". Zuma akiwa chumbani analia alisikia tangazo la kiongozi wa msiba ule akisema kwamba maiti itazikwa saa nne baada ya chai ya asubuhi,Zuma alipotazama wakati ilikuwa yapata saa mbili asubuhi ikielekea saa tatu,Kwa hasira Zuma alienda sehemu ambayo walikuwa wamewekea vyombo,Alichomoa moja ya kisu kizuri kilichokuwepo katika vile vyombo,Moja kati ya wamama walimuuliza"We Zuma kisu cha nini tena?".Zuma alitoa jibu moja tu"Nimeagizwa barazani"kisha akatokomea kurudi chumbani huku akiwa na hasira kali."lazima niwauwe leo haiwezekani wanichukulie mama yangu"yalikuwa ni maneno ya Zuma kila wakati ndani ya moyo wake. Hatimae Muda wa chai ulifika na watu wakanywa chai na sasa kilichofuata ni mazishi * * * * * * Safari ya kwenda mazishini ilifanywa na wanaume kutokana na taratibu za kidini,Wanawake hawaruhusiwi kwenda kuzika,Mzee shomary na rafiki yake ambae mzee Kagusa hawakuwa mbali,bila kusahau Zuma nae hakucheza nao mbali alihakikisha hapotei hata mmoja machoni pake,hatua za watu zilipigwa huku wakipokezana kubeba mwili ambao ulikuwa sio mwili bali ushetani wa kubadilisha mwili na kuwa mgomba wa ndizi ulikuwa tayari umefanyika,mwili wa Mama Zuma tayari ulikuwa umeshatumika kama chakula katika sherehe za kumuapisha Zuma. Hatimae watu walifika eneo husika kwa ajiri ya safari ya mwisho ya Mama Zuma,Bila kusahau Zuma hakucheza mbali na wazee wake huku akiwa na lengo lake moyoni. Ibada ya mwisho ilifanyika na hatimae mwili ulipumzishwa. Wakati sara ya mwisho ikiendelea ili watu waanze kutawanyika,Kulisikika sauti nzito ya mtu akiungurumia kwa shida,watu wote waligeuka kutazama ni wapi sauti inatokea na ndipo macho yao yalikutana na Zuma akiwa ameshika kisu chenye damu huku tayari babu yake akimwaga damu nzito ikitokea shingoni upande wa nyuma,watu wakiwa bado hawaelewi nini kinaendelea Mzee Shomary alidondoka chini kama mzigo huku akirusha rusha miguu na mikono,Zuma bila kupoteza mda alinyanyua kisu ili ammalize mbaya wake wa pili ambae ni mzee Kagusa,Kitendo tu cha kunyanyua kisu mzee Kagusa alimyooshea kidole Zuma na pale pale kile kisu kililuka pembeni,Zuma bado hakukubali,alikikimbilia kile kisu na kukichukua tena kisha kumfuata Mzee Shomary,watu wakiwa bado wapo na bubuwazi wakimshangaa Zuma anachokifanya ndipo Mzee Shomary aliwahi na kwenda kumshika Zuma na pale pale vumbi kubwa aina ya moshi ilitimka,Watu walifumba macho kwa ajiri ya kuzuia moshi ule usiingie machoni,Moshi ulipoisha walitahamaki kuona Mzee Shomary na Zuma hawapo eneo lile,kwa pembeni ulionekana mwili wa mzee Shomary ukiwa tayari umekauka.Ukawa mwanzo wa msiba mwingine. * * * * * * MIAKA NANE BAADAE MIRIAMU na AMOS wakiwa wamerudi kutoka masomoni ambapo Miriamu alikuwa katika masomo ya juu ngazi ya chuo na pia mdogo wake Amosi akiwa bado yupo masomo ya kidato walifika moja kwa moja kwa mama yao mlezi ambae si mwingine bali ni MAMA RAMA ambae aliyewaombea msaada katika kituo cha kulelea watoto yatima huko mjini mpaka kufanikisha kufikia viwango hivyo vya elimu.Walimkumbatia kwa furaha maana ni miaka mingi sana walikuwa hawajaonana zaidi ya mawasiliano tu,walikaa na kuongea mengi sana na kila mmoja alimuelezea mama yule hali ya ugumu wa elimu waliokutanana nao,zaidi ya yote walimshukuru sana kwa msaada aliowasaidia mpaka kufika mahali pale,na kumuomba sana asichoke kuendelea kuwasaidia maana ni msaada pekee kwao uliobaki Pia waliulizia kama kuna fununu zozote zilizoendelea toka siku ile Zuma na yule mzee ambae ni mzee Shomary wapotee lakini jibu lilikuwa ni kwamba hakuna taarifa au fununu zozote hata dalili za watu wale kuonekana toka wapotee.bila kusahau waliulizia maisha ya Rama ambae alikuwa rafiki kipenzi sana wa Zuma kuwa yuko wapi,Mama Rama aliwajibu kuwa tayari ameshaoa na anamji wake na mtoto mmoja kwani hakufanikiwa kuendelea na masomo Jioni ilipofika Amos na Miriamu walienda kutembelea nyumba waliokuwa wanakaa zamani na kukuta tayari pameshakuwa pori na nyumba ilizunguukwa na majani mengi kutokana na kuwa hakuna anaekaa.Walikaa kwenye jiwe moja liliko kalibu na nyumbani kwao na hatimae walijikuta wanakumbushiana mambo mengi sana enzi wakiwa pamoja na mama yao bila kusahau kaka yao Zuma,Miriamu uvumilivu ulimshinda alijikuta analia kwa kukumbuka yale,Amos alinyanyua sura juu ili kuzuia machozi yaliyokuwa yanakalibia kudondoka.HAKIKA ULIKUWA UCHUNGU MZITO. * * * * * * * * * MWISHO * * * * * * * * * =>Mungu akinijaalia basi tunaweza tukawa na Muendelezo wa hii simulizi msimu wa pili ASANTE KWA KUWA PAMOJA NAMI

at 8:05 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top