Home → simulizi
→ KIJIJI CHA SHETANI.
Sehemu ya Sita
ILIPOISHIA.........
.... Zuma moja kwa moja akiwa amejaa hasira alimuangalia babu yake,na hapo ndipo walipogonganisha macho yao wote wawili.Balaaaa....
SASA ENDELEA........
.....ZUMA akiwa amepandwa na hasira juu ya Babu yake na kile walichotaka kumfanyia usiku alijikuta anataka kutoka pale alipokuwa kasimama kwenye mlango wa chumba cha wazee wake hao ili akamkute babu yake,Alipotaka kujalibu kufanya hivyo Mzee Shomary alimkazia macho mjukuu wake na kumpiga na uchawi wa chini kwa chini kwa kutumia macho,ghafla Zuma mwili wake uliishiwa nguvu na hatimae akiwa pale mlangoni alizimia,Mzee shomary alifanya hivyo kwa mjukuu wake ili kumzuia asitoe siri kwa kile anachokifahamu
Msiba ulitengwa na watu karibuni kijiji kizima cha Ujiji walihudhuria pale kwa ajiri ya kutoa heshima za mwisho,wakati huo msiba unaendelea pia baadhi ya watu walikuwa wakihangaika kumpepelea Zuma ili aludishe fahamu,Watu walijua huenda amezimia kwa sababu ya mshituko wa tukio la kufariki kwa Bibi yake ambae ni Bi Hindu.
Mama Zuma nae alikuwa ni mtu wa kulia na kuzimia kisha anazinduka na kuendelea kulia tena kutokana na kifo hicho cha mama yake cha bila kutarajia,Hakuamini mama yake yule ambae ameonyesha msaada wa mwisho kwake hatimae ameaga dunia.
Walishindwa kuzika siku hiyo hiyo kutokana na kuwa muda umeenda sana hivyo taratibu za mazishi zilipangwa kesho yake saa nne asubuhi.
Mnamo saa mbili usiku baada ya Zuma kupepelewa sana pia kumwagiwa maji ya baridi hatimae alizinduka,Cha ajabu pamoja na kwa Zuma alizinduka lakini tayari babu yake alikuwa amevuluga akili za Zuma hivyo Zuma alizinduka kama mtu aliepoteza kumbukumbu na akili pia zikiwa zimechanganyikiwa kidogo,Zuma alijikuta akiwa pale msibani alikuwa anauliza watu waliokuwa wanampepelea kuwa hapo kunanini.Licha watu kumueleza kuwa kuna msiba wa bibi yake lakini Zuma hakuonekana kushtuka na kitu chochote au kulia kama awali,Badala yake alibaki kimya akiwaangalia watu tu na kuwashangaa,Hakuwa anakumbuka chochote kinachoendelea na kila kitu alichokiona pale kilionekana kigeni kwake.
Waliamua kumpa chakula kisha kumpa maji ya kuoga baada ya kuona hali aliokuwa nayo haikuwa nzuri kutokana na yeye kuwa amepoteza kumbukumbu na pia akili yake haijakaa vizuri,Baada ya hapo Zuma walimpatia sehemu ya kulala kwa ajili ya mazishi ya Bibi yake kesho,Hatimae wengine wa kulala msibani walilala na pia wegine wa kukesha pale nje wakiwa wamewasha moto walikesha.
Kesho yake asubuhi na mapema maandalizi yaliendelea kwa ajili ya heshima za mwisho na pia kwa ajili ya kumuita shekhe atakaeweza kusoma Dua ya mwisho kwa ajili ya marehemu.Ibada ya Dua ya kumuaga Bi hindu iliandaliwa isimwe saa 4 asubuhi kisha baada ya hapo ni mazishi.
Ukweli ni kuwa ndani hapakuwa na Bi Hindu bali palikuwa na Mgomba uliowekwa kwa mfano wa Bi Himdu maana Bi Hindu alikuwa tayari ameshageuzwa sadaka na kafara kwa ajili yao.
Shamla shamla za uandaaji wa chai kwa ajili ya waliohudhuria kwenye msiba ule ziliendelea n hatimae saa tatu kamili watu walianza kupata chai.
Masikini Zuma hali ya kupoteza kumbukumbu na akili yake kuharibiwa na babu yake bado ilimtawala kichwani,alikuwa bado ni mtu asieelewa chochote kinachoendelea hivyo hata alipoabiwa kuwa bibi yako amefariki na penyewe hakuelewa chochote,Walimpatia pia na yeye chai kisha kumuweka tayari kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho za Bibi yake.
Saa Nne Asubuhi ndani ya alama kila kitu kilikuwa tayari,Mwili ulitolewa nje kwa ajili ya kuswaliwa na watu walishika Udhu kwa ajili ya ibada ya kuuaga mwili.
SHEKHE aliehudhulia pale kwa ajili ya kuongoza ibada ile ya kumuaga Bi Hindu alikuwa si mwingine bali mwite Shekhe Kagusa yaani Mzee Kagusa kiongozi mkuu wa uchawi eneo la ujiji.Ni mtu mnafiki alieonekana kujishirikisha na mambo ya Mungu lakini ndani yake ni mchawi wa kutupa.
Pia kuna sababu za Mzee Shomary kumuweka Mzee Kagusa yeye aongoze ibada ile kwa sababu laiti wangechagua Shekhe mwingine mwenye nguvu za Mungu za rohoni walihofia huenda akagundua upuuzi walioufanya wa kugeuza mwili wa Bi Hindu kama mgomba na wakati Bi Hindu wakati huo alikuwa tayari kwenye matumbo yao pamoja na damu yake.Hivyo ndio maana walimpanga Mzee Kagusa kwa sababu wote lao ni moja.
IBADA ilianza na kama kawaida ibada za kuombea mwili wa marehemu katika Uislamu huwa sio ndefu za kuchoshana hatimae wanaume walinyayuka kwa ajili ya kwenda kumpumzisha Bi Hindu japo hakuwa Bi Hindu.Waliondoka na kubeba mgomba ule wenye sura ya Bi Hindu huku nyuma wakiacha vilio vya wakina mama kutokana na wao kwa sheria ya Dini kutokuruhusiwa kwenda kuzika.Hatimae wanaume walifika mahali ambapo waliandaa kwa ajili ya makazi ya milele ya Bi Hindu na taratibu zikafuata za kuutua mzigo ule kwa ajili ya Mzee Kagusa kumalizia DUA za hapa na pale kabla na baada ya mazishi.HUO NDIO UKAWA MWISHO WA BI HINDU.R.I.P
* * * * * * *
HALI ilikuwa bado tete kwa Zuma,kutokana na kutokujitambua na wakati huo msiba ulikuwa umeisha na waliokuwa wamebaki eneo hilo la msiba ni majirani wa kawaida na pia Mama Zuma,Zuma pamoja na wadogo zake,muda wote Zuma alikuwa hajielewi wala haelewi kinachoendelea,Walikaa pale mpaka mida ya usiku na hatimae Mama Zuma aliamua kuwachukuwa wanawe na kwenda kumuaga baba yake ambae ni Mzee Shomary kuwa anaenda nyumbani kwake na kumuahidi kesho atakuja Asubuhi kumsaidia majukumu ya hapa na pale.Baada ya hayo Mama Zuma aliondoka akiambatana na Zuma pamoja na wanawe.
Ilikuwa mida ya saa moja na nusu usiku ambapo Zuma na mama yake pamoja na wadogo zake wamelejea nyumbani,Moja kwa moja Zuma aliingia kulala.
Mama Zuma alifikia jikoni na kuanza kupika chakula cha usiku huku akisaidiwa na Miriamu mdogo wa pili wa Zuma.
Mida ya saa tatu usiku ikielekea saa nne Zuma alishtuka kutoka usingizini,alipokelewa na giza zito lililokuwa chumbani mwake,kitu cha kwanza alichojiuliza kichwani ni"Hivi hapa nipo wapi".Alitulia pale kitandani kwake kama sekunde kadhaa akiendelea kujiuliza yupo sehemu gani.Alivuta kumbukumbu na kukumbuka tukio la mara ya mwisho pale mlangoni kwa babu yake yeye na babu yake na ndipo akakumbuka kuwa alikuwa msibani kwa bibi yake.Kumbukumbu na akili ya Zuma sasa zilikuwa zimeachiliwa na babu yake baada ya kupigwa na uchawi pale msibani ili asiweze kufanya chochote.Zuma bado alikuwa anajiuliza pale kitandani kuwa kwa sasa hivi yupo eneo gani?,alikuwa bado yupo njia panda je yupo bado msibani kwa bibi yake au yupo sehemu nyingine,Wasiwasi ulianza kumuingiana hofu kuwa asije akawa yupo tena mikononi mwa babu yake na watu wake.
Hapo ndipo Zuma alipoamua kujitikisa kitandani na kupokelewa na mlio wa kitanda chake kile kilichokuwa na ubovu katika nati kikilia "Nyweeeeeeeh" pindi mtu akikitikisa.
Zuma alitabasamu baada ya kusikia mlio ule na kujua moja kwa moja kuwa sasa yupo nyumbani.
Mara sauti ya mama yake ilisikika ikimwambia miriamu nje"Nenda ndani kamlete kaka yako aje ale".Miriamu aliagizwa na mama yake akijua kabisa Zuma bado akili hazijalejea hivyo ni ngumu kumuita aje mwenyewe.Wakati huo walikuwa wametandika mkeka nje na chakula kilikuwa kimewekwa kwa ajili ya kuliwa.
miriamu alianza kupiga hatua za kumfuata Zuma chumbani kwake ili aje ale.Ghafla mama Zuma alishangaa kumuona miriamu akirudi kinyume nyume mara baada ya kutaka kuingia mlangoni ili aingie kuelekea chumbani kwa kaka yake akamuite.Mama Zuma moyo ulimlipuka baada ya kuona kitendo kile cha miriamu kurudi kinyume nyume akirudi alikotoka.
JE NINI KITAENDELEA
Kwanini Miriamu analudi kinyume nyume badala ya kwenda kumuita kaka yake....?
Usikose sehemu ya saba ya Simulizi hii ya kusisimua
KIJIJI CHA SHETANI
Sehemu ya saba
Ilipoishia
...... Ghafla mama Zuma alishangaa kumuona miriamu akirudi kinyume nyume mara baada ya kutaka kuingia mlangoni ili aingie kuelekea chumbani kwa kaka yake akamuite.Mama Zuma moyo ulimlipuka baada ya kuona kitendo kile cha miriamu kurudi kinyume nyume akirudi alikotoka.
Sasa endelea
.....Kilichomfanya Mariamu arudi nyuma ni baada ya kukutana na Zuma mlangoni akiwa amesimama,Zuma wakati huo alikuwa amesimama huku mawazo mengi sana yakipita kichwani mwake,alikuwa akiwaza mengi juu ya msiba wa bibi yake na pia kile alichokifanya babu yake,Kilichomtoa kutoka kule chumbani mpaka pale mlangoni ni kwasababu tayari fahamu na uelewa wake ulikuwa umelejea na alisikia sauti ya mama yake ikimuagiza Miriamu aje amuite hivyo kabla Miriamu hajaja kumuita aliamua aamke mwenyewe aende.
Miriamu aliludi nyuma na kuogopa kwa sababu toka kaka yake apoteze akili zake na uelewa wake alimuona ni hatari hivyo aliogopa hata kukaa nae karibu huenda hata akamdhuru hivyo alivyomuona pale mlangoni kasimama alihisi kiama chake kimefika,Mama Zuma alinyanyuka na kwenda kushuhudia ni kwanini Miriamu alipatwa na wasiwasi kiasi kile mpaka kurudi nyuma,alitembea haraka haraka ili akashuhudie kuna nini mle ndani kinachoendelea,Alipofika eneo la mlango alikutana na Zuma ambae nae alikuwa anataka kuanza kupiga hatua za kutoka nje baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa pale mlangoni.
Zuma alipomuona mama yake alimuamkia"Shikamoo mama".Kabla hata Mama zuma hajaitikia salamu ile alianza kudondosha machozi ya furaha kwa kumuona mwanae amelejea katika hali yake,Hakutarajia kama kuona atapona tena alijua ndio alishakuwa wa hivyo hivyo.Wakati mama Zuma akilia kwa furaha juu ya kurejea kwa uzima kwa mwanae Zuma nae alijikuta analia kwa uchungu kila akifikilia yale yatakayotokea mbeleni juu ya mama yake kutokana na Bi Hindu ambae alikuwa msaada mkubwa kuwa amefariki,Hivyo walijikuta wote mtu na mama yake wamekubatiana huku wakilia kila mmoja akilia na la kwake.
Baada ya Vilio vile vya mtu na mwanae sasa familia ilikaa mkekani kupata chakula,Walikuwepo wote yaani Mama yao,Miriamu,Amos pamoja na Zuma mwenyewe,Zuma mda wote akili haikuwepo pale nyumbani bali ilichukuliwa mbali sana na mawazo mazito kutokana na mambo mazito yanayoendelea ambayo hata mama hajui chochote,Hii ilimpelekea hata chakula ale kwa kusitasita kama vile mtu ambae hajapendezwa na chakula.Zuma ilifika kipindi akafikilia hata kuchukua panga na kwenda kumuua babu yake lakini alipokumbula ule uchawi ambao aliofanyiwa siku ile na kumfanya apoteze kumbukumbu aliogopa na kuwa mpole.
Hatimae walimaliza kula na baada ya hapo kukawa na mazungumzo ya hapa na pale kama familia kisha kila mmoja alielekea kulala,Zuma alifika chumbani mwake na sasa zimepita takribani siku kama mbili hajagusa hata daftari,Aliingia moja kwa moja kulala japo usingizi wenyewe haukupita mawazo mengi sana yalikuwa yakipita kichwani mwake kitendo kilichopelekea kichwa chake kuuma usiku ule.Hatimae Mungu si athumani usingizi ulimpitia.
* * * * * *
...NI alfajiri na mapema yapata saa 11 hivi sauti ya adhanaa msikitini kupitia kipaza sauti ilipenya masikioni mwa Zuma,Bila kupoteza muda na wakati Zuma alijisemea moyoni"Lazima leo niende shule hata kama jana nilikuwa na msiba nipo kidato cha nne mwishoni nikizubaa ntafeli,Moja kwa moja aliamka na kisha kuanza taratibu za kujiandaa kuwahi shule,Mama yake nae alikuwa ni fundi pia wa kuitumia sauti ile iliyowaamsha na kuwahimiza ibada waislamu kama sauti ya yeye kuanza pia kufungasha na kujiweka tayari katika biashara yake ya mgahawa lakini kwa siku ile Mama Zuma ilikuwa ya tofauti kwake kwani alishtuka tu na badala ya kuweka vitu sawa alifumbua tu macho na kumsikiliza mwanae akiwa katika maandalizi"Mh mtoto huyu anavyopenda shule hata kusema akae nyumbani hata siku mbili aomboleze msiba wa bibi yake hakuna"Alijisemea mama Zuma huku akiendelea kumsikiliza Zuma na purukushani zake kule chumbani,alijua hana uwezo wa kumzuia asiende shule kwa sababu hata njaa yenyewe ilishindwa kupambana ma Zuma.Hata hivyo japo kuwa shule ilikuwa mbali kiasi kwamba ilimlazimu aamke saa 11 lakini bado Zuma hakuwahi kuonyesha udhaifu wa kutokwenda shule kitendo kilichomfanya aonekane kuwa na bidii katika masomo.
Ndani ya nusu saa purukushani za Zuma kujiandaa kwa ajiri ya kwenda shule ziliisha na sasa alimuita mama yake kwa ajiri ya kumsalimia na kumuaga huku tayari wenzake aliokuwa anasoma nao walikuwa wameshampitia kwa ajiri ya kuianza safari.
Yapata saa moja na nusu baada ya mwendo mrefu na sasa safari ilifikia kikomo katika darasa lililoandikwa kwa maandishi makubwa mlangoni KIDATO CHA NNE "A".Lilikuwa ni darasa la wanafunzi wa sayansi na wakati huo walikuwepo tayari wameingia darasani,ilikuwa ni kawaida kwa Zuma na wenzake kuchelewa kutokana na umbali mrefu kitendo kilichosababisha waalimu kuwapa ruhusa ya wao kuwa wanafika pale shule saa moja na nusu hadi saa mbili asubuhi wakati huo muda wa paredi unakuwa umeisha na sasa unakuwa ni muda wa kipindi cha kwanza darasani.
Darasa lilikuwa limetulia lakini baada tu ya kuingia Zuma darasa lilianza kujawa na mazungumzo huku kila mwanafunzi akienda katika dawati la Zuma kumpa mkono wa pole kutokana na kufiwa na bibi yake.Zuma alipendwa sana na wenzake kutokana na tabia ya kumsaidia kila mtu katika masomo hivyo hakuwa na mtu wa kumchukia kwa mabaya hivyo dawati lake lilijaa watu waliotoa pole kwake.
Baada ya mlima mrefu wa pole za wanafunzi uliojaa katika dawati la Zuma hatimae darasa lilitulia na wanafunzi kuendelea kujisomea.Kwa Zuma ilikuwa tofauti sana kwani kila akishika daftari ajisomee mambo yaligoma na kujikuta anafikilia hatima ya maisha yanayoendelea katika familia yake.
RAMA rafiki yake kipenzi aliekuwa akikaa nae kwenye dawati aliona rafiki yake yupo katika hali ya tofauti sana.Rama ilibidi awe mfariji wa rafiki yake akijua kuwa kilichomsubua Zuma ni kuondokewa na Bibi yake ambae ni Bi Hindu.Kumbe kwa Zuma ilikuwa tofauti yeye hakuwa anawaza msiba bali aliwaza juu ya familia yake na uchawi wa babu yake unaoendelea.Mawazo mengi na sauti ya maneno ya kuriwaza kutoka kwa Rama yalitengeneza usingizi kwa Zuma na kujikuta anapiga usingizi mzito darasani.Rama baada ya kuona rafiki yake amelala hakutaka kumuamsha bali kumuacha apumzishe kichwa labda itokee dharura ya mwalimu kuingia darasani kufundisha
Ni saa 4 mda wa mapumziko Zuma anaamka kutoka usingizini na kukutana na watu wachache darasani ambao walikuwa wamebaki kutokana na wao kutokwenda pumziko.
Mara mlangoni ilisikika sauti ya Rama ikisema"Zuma unaitwa ofisini kuna mgeni wako amekuja kaleta taarifa kutoka nyumbani".Alisema Rama na kuuwacha moyo wa Zuma ukilipuka kwa shauku ya kujua ni taarifa gani iliyoletwa.
JE NINI KITAENDELEA
..Tukutane śaa 2usiku hap hap team b professional love
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: