KIJIJI CHA SHETANI Sehemu ya Tano Ilipoishia ....Kwa mara ya kwanza Mzee Shomary alidondosha chozi jingine kama siku ile aliyodondosha akiwa mdogo alipowauwa wazazi wake. Sasa Endelea ...Kitendo cha kukumbuka siku aliouwa wazazi wake kiliingiza roho ya ukatili ndani yake,Alijisemea moyoni"Nilipoteza wazazi wangu ambao niliwapenda kuliko kitu chochote duniani,Na siku hiyo niliapa mbele ya Mungu wangu kuwa sintarudi nyuma katika maamuzi ya mauwaji....Nisamehe sana mpenzi wangu thamani ya kukupoteza wewe bado haijafikia thamani ya wazazi wngu,nitakukumbuka daima kama mke wangu kwaheri".Mzee Shomary alisema maneno hayo kisha akamtazama Bi Hindu ambae wakati ule alikuwa kama amelala kutokana na kupewa uchawi mzito ndani yake,Mzee Shomary alionyesha tabasamu la mwisho kwa mkewe kisha akanyanyua kisu juu,baada ya kukinyanyua juu huku akiwa ameshika kwa mikono miwili alikirudisha kwa kasi zaidi moja kwa moja mpaka kifuani kwa Bi Hindu sehemu ya moyo,Maskini Bi Hindu alifumbua macho na kutaka kunyanyua kichwa lakini ilishindikana,Radi na ngurumo kali zilianza kupiga eneo lile wakati huo Bi Hindu alishika mikono ya Mzee Shomary iliyokuwa imeshikilia kisu pale kwenye kifua eneo la upande wa moyo,Alitamani kunyanyua kichwa na kusema neno kwa mumewe lakini haikuwezekana kutokana na uchawi aliokuwa tayari kamezeshwa,damu nzito ilitililika kutoka sehemu ile ya moyo na kumwagika kwa chini ya kichanja ambapo tayari kulikuwa na bakuri kubwa la kuipokea damu ile. Hatimae baada ya kutapatapa sana Bi Hindu aliaga Dunia na mwili wake ukawa wa baridi,Mzee Shomary aliuchimbua moyo kutoka kifuani kwa Bi Hindu na kuutoa wote kisha kuuweka kwenye bakuri,Wakati huo radi ziliendelea kupiga huku shangwe za nyimbo nazo zikipamba moto zaidi. Baada ya Mzee Shomary kumaliza ile shughuri aliondoka eneo lile na kuuacha mwili wa mke wake ukiwa na shimo kubwa sehemu ambapo moyo umetolewa,Habari za Bi Hindu zikawa zimefika mwisho wake.Na sasa alinyanyuka kiongozi mkuu ambae ni Mzee Kagusa kwa ajiri ya kwenda kuukabidhi moyo kwa shetani wao mkuu wa anga lile,alifika eneo lile la ule mbuyu ambapo kuna mwili wa Bi Hindu na lile bakuri la moyo,aliita watu wanne waje waushughurikie mwili wa Bi Hindu kuuondoa pale na kwenda kuuandaa kwa ajiri ya sherehe nzima inayofuata,Baada ya Mwili wa Bi Hindu kuondolewa pale na sasa alikamata Bakuri lililokuwa na moyo na kulinyanyua juu huku kapiga magoti,alianza kuongea maneno na lugha isiyojulikana huku bakuri kalielekeza juu,ngurumo na radi viliongezeka kwa kasi sana eneo lile na hatimae tetemeko likaanza kutikisa ardhi ya eneo lile,wachawi wale waliokuwa wakiimba na kucheza walilala chini kifudifudi kusujudu huku wameziba masikio yao kutokana na kelele nyingi zilizokuwepo eneo lile,wakati huo mzee Shomary macho yake yalibadilika na kuwa mekundu huku pia akendelea kuongeza kasi ya kuingea lugha ile isiyojulikana. GHAFLA eneo lile radi kali zenye miale ya moto zilianza kushuka katika lile bakuli lililokuwa na moyo,zilipiga radi kama tatu kali na nzito na hatimae hali ya pale ilitulia,tukio lile halikuwa la kimchezo maana kila mtu alibaki hoi sana kutokana na balaa lile,Mzee Shomary aliookuja kushusha chombo hapakuwepo mle hata tone la damu,pia moyo nao haukuwepo,tayari sadaka ila ilikuwa imeshachukuliwa na shetani wao wa eneo lile na kafara ilikuwa tayari imekamilika.Sasa sherehe ziliendelea pia ngoma na shangwe kuwa jambo limefanikiwa NI ukweli usiopingika na wazi kuwa unaposikia mtu ametolewa kafara ni kwamba mwili wake na damu yake vimeenda kutumika katika eneo la uchawi kama chakula,hivyo kafara huwa ni kama sadaka juu ya jambo fulani.Mwili wa Bi Hindu siku hiyo ulikuwa kafara mbele ya wachawi wale,Wakati sherehe zinaendelea bakuri lile la damu liliwekwa meza kuu ambapo walikuwa wamekaa Mzee Shomary,Mzee kagusa pamoja na wale Bibi Vizee wanne,Walikuwa kama wanasubiria kitu flani ili waendelee na jambo.Na kitu hicho walichokuwa wanasubiri si kingine bali ni nyama ya mwili wa Bi Hindu uliochukuliwa pale kwenye uchanja na kwenda kukatwa katwa vipande vipande kwa ajili ya chakula.Kwao chakula yaani nyama ya binaadamu na damu huwasaidia kuwatia nguvu katika mambo yao ya uchawi. Hatimae Sinia kubwa lililetwa mezani lililokuwa limesheheni vipande vya myama vilivyokatwa katwa,hapo ndipo sherehe ilizidi kunoga zaidi na amri ilitolewa kuwa sasa zamu ya kupata chakula imefika."Kama ilivyokawaida yetu tutoapo kafara,kila mmoja atapita hapa kupata kipande kimoja cha nyama na damu hii kidogo ili tuendelee kuwa na nguvu na tudumu zaidi na zaidi.Tawala yetu ni lazima itadumu milele,na eneo hili lazima tutatawala milele na wala hakuna mtu yeyote atakaetuzuia"Maneno haya aliyasema Mzee Kagusa na kusababisha furaha kubwa kwa wafuasi wa uchawi waliokuwepo eneo lile.Walianza kupita mmoja mmoja eneo la meza kuu na kulishwa kipande cha nyama pamoja na damu,Nyama ile ilikuwa mbichi kabisa ambayo bado inadamu,cha ajabu ni kuwa kila mmoja aliifurahia sana huku sherehe ya ngoma iliendelea na hatimae wafuasi wote waliisha na wakaendelea kucheza huku wakiunzunguuka mbuyu wakiwa wameshika mienge ya moto na pembe za ng'ombe wakipuliza. Sasa ilikuwa zamu ya meza kuu kupata chakula huku wakiendelea kushehereka kwa kutazama ngoma zinavyoendelea.Sherehe ile iliisha majira ya saa 10 jioni siku hiyo.Mzee Shomary pamoja na wachawi wenzake walikuwa hawajarejea majumbani kwao toka usiku ule kwenye tukio la Zuma na sasa ilikuwa saa 10 jioni ambapo sherehe ilifungwa. * * * * * * ZUMA siku hiyo alijikuta ameipoteza kwa kutokwenda shule toka asubuhi yake baada ya mama yake kuamka akiwa na hali ile,Jalibio la mtihani ule lilimpita siku hiyo japo kuwa alikuwa kidato cha nne akielekea kumaliza,bado alikuwa akitamani kumwabia mama yake yote anayoyajua lakini alishindwa,Alikuwa amekaa peke yake kwenye msingi wa nyumba yao jioni ile akiendelea kuwaza hapa na pale yale yote yaliyotokea.Mama yake alikuwa na wadogo zake eneo la jikoni muda huo wakiandaa andaa maswala ya chakula cha usiku maana ilikuwa yapata majira ya jioni saa kumi na moja hivi. ZUMA akiwa amekaa kwenye msingi akitafakari yaliyotokea pia na aliyoyaona kwa bibi yake ghafla Mmama mmoja ambae ni jirani yao na Bibi na Babu yake Zuma alikuja akiwa analia nyumbani kwa akina Zuma,Alifika hata bila ya salamu moja kwa moja alitoa ujumbe kwa Mama Zuma"Mama Zuma Bi Hindu mama yako amefariki....Jamani Bi Hindu jilani yangu mweee nilikuzoea sana kwanini umeondoka wakati ulikuwa bado na nguvu za kutosha"Mama yule aliendelea kulia huku akiongea maneno yale.Pale pale Mama Zuma bila hata kusema kitu alianza kudondosha kilio huku akikimbia kuelekea nyumbani kwa mama yake kuhakikisha kama kweli amefariki.Mama Zuma alikimbia kama mwehu huku khanga alizokuwa amejifunga zikiwa zinadondoka,Hakujali hilo bali aliendelea kukimbia huku akilia sana. ZUMA alisikia taarifa hizo akiwa amekaa pale nyuma ya nyumba kwenye msingi,hakuchelewa na yeye aliunga msafara moja kwa moja kwenda kushuhudia kama kweli,Wakati anakimbia alikuwa akiwaza kichwani mwake kuwa huyo ni babu yake ndio amefanya yote hayo kwa sababu bibi yake amehusika kumsaidia mama yake ambae alitakiwa afe. Moja kwa Moja bila hata hodi Mama Zuma na Zuma walitua chumbani kwa Mzee Shomary kuona kama kweli,Walifunua shuka na kukuta ni kweli mwili wa Bi Hindu ukiwa umelala.Zuma aliendelea kuukagua zaidi ajabu ni kwamba hapakuwa na hata jeraha moja katika mwili,kubwa zaidi hata ile sehemu ambayo moyo ulichomolewa napo palikuwa pako kama kawaida hapakuonekana na shimo lolote. Zuma akiwa mle chumbani alisikia babu yake akiongea na majirani akiwaadithia ilikuwaje mpaka Bi Hindu amefariki,Alisema"Mimi niliamka asubuhi sana nikamwambia kuwa naenda porini kwenye ukataji wangu wa nyasi na kamba nae akasema baadae kidogo kwenye mida ya saa nne nae ataelekea porini akatafuta angalau kuni za kupikia sasa nimeludi hapa jioni hii nakuta yeye bado hajarudi nimekaa kaa kidogo nashangaa hawa hapa vijana wawili wanamleta wakisema wamemkuta kando kando ya barabara porini akiwa amelala kumtikisa wakagundua tayari amefariki hivyo jukumu walilofanya ni kumleta hapa"Alisema mzee Shomary. Zuma alitoka mle chumbani ili kuwashuhudia hao vijana ni akina nani walioleta mwili wa Bibi yake.Alipowatazama tu moja kwa moja akakumbuka ni kama hizo sura aliziona siku ile usiku kwenye lile tukio la yeye kutaka kukabidhiwa uchawi.Hivyo babu yake alidanganya.Ukweli ni kwamba aliekuwa kalala mle ndani kwa macho ya nyama alionekana Bi Hindu lakini kwa Macho ya kishetani na kiroho ulikuwa ni mgomba wa ndizi uliovaa sura ya Bi Hindu.Maana Bi Hindu habari zake zilikuwa tayari zimeisha na tayari walikuwa wameshamtafuna. Zuma moja kwa moja akiwa amejaa hasira alimuangalia babu yake,na hapo ndipo walipogonganisha macho yao wote wawili.Balaaaa.... JE NINI KITAENDELEA Usikose sehemu ya Sita ya simulizi hii ya kusisimua ASANTENI SANA

at 8:03 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top