Home → simulizi
→ KIJIJI CHA SHETANI
Sehemu ya Nne
Ilipoishia
... Bi Hindu pamoja na kuishi kwake maisha ya kichawi hakuwahi kuonana na shetani wa namna ile wenye kutisha vile,Hakuwa na chakufanya zaidi ya kutetemeka.
Akiwa anatetemeka na vitu ndani kuvurugika mara nje hodi iligongwa"Bibi hodiiii"Ilikuwa si sauti nyingine bali ni sauti ya ZUMA.
Sasa Endelea.
....ZUMA akiwa pale nje alihisi mambo yanayoendelea mle ndani mwa bibi yake hayakuwa ya kawaida.alianza kusikia kama upepo wa ajabu ajabu ukipuliza na kupepelusha vitu mle ndani,alipiga tena hodi na hali ilikuwa ile ile ya ukimya.
Mle ndani yale mashetani mawili yaliyotumwa yalizidi kumsogelea Bi Hindu hatimae yakamfikia karibu yake,wakati huo Bi hindu alikuwa hana sehemu ya kukimbilia alikuwa ameshafika kwenye ukuta,Bi Hindu alisikia vema sana hodi zilizobishwa na mjukuu wake kule nje lakini kila alikuwa akijalibu kutoa sauti ilikuwa haitoki,alijalibu kupiga kelele lakini pia nayo haikutoa sauti hivyo alishindwa kufanya chochote kile.
Zuma nje alisubiri na hatimae uvumilivu wa zile fujo mle ndani ulimshindwa alianza kuhisi tayari bibi yake atakuwa kwenye matatizo,Jukumu aliloamua kulichukua ni kuingia ndani bila hodi ili kuona nini kinajiri.Zuma alisukuma mlango na kuingia ndani kwa Bibi yake,pia moja kwa moja alipitiliza mpaka chumbani kwa bibi yake,Kitu alichokutana nacho kilimfanya Zuma atoke nje mbio na kuanza kukimbia kuelekea kwao.
Aliona zile nyuso za mashetani wale zikiwa kwenye pembe ya ukuta wa chumba zikiwa zimemshikilia Bibi yake ambae wakati huo alionekana kama mtu ambae tayari amekufa au amezimia.Na Zuma alipoingia tu chumbani sehemu ile ya ukuta ilifunguka kama mlango na wale mashetani mawili walipotea kama upepo kupitia ule mlango.Zuma alikuwa amekuja kwa Bibi yake kumshukuru na pia kumuelezea yale yote aliyoyaona ndotoni lakini kwa bahati mbaya ndio alikutana na bibi yake anatoweka.
Kitendo kile kilimfanya Zuma akimbie kwenda nyumbani huku analia kwa ajiri ya kwenda kutoa taarifa kwa mama yake kwa kile alichokiona."Mamaaa..nyumbani kwa bibi....nyumbani kwa bibi'Zuma alifika nyumbani ambapo alimkuta mama yake tayari yuko vizuri na mwenye afya nzuri akiwa kakaa nje,Zuma alishindwa kutoa taarifa lasmi na badala yake kuishia kusema tu hilo neno la Mama nyumbani kwa bibi,Aliwa analia alimshika mkono mama yake na kuanza kuelekea nyumbani kwa bibi yake akiwa na Mama yake,Mama Zuma nae tumbo lilianza kumkata akitaka kujua je nyumbani kwa mama yake kuna nini hivyo walijikuta wakitembea haraka kwenda kuwahi kujua kuna nini,Wakati wote huo Zuma haongei zaidi ya kulia.
Walifika nyumbani kwa Bi Hindu na moja kwa moja waliingia hadi ndani,Zuma hakuamini macho yake baada ya kuingia mle ndani ambapo alipaacha pamevulugika kila kitu kikiwa hovyo hovyo kutokana na upepo mkali wa yale mapepo alikuta pamepangika vizuri na mpaka kitanda kimetandikwa vizuri,Palikuwa hamna hata karatasi wala nguo iliyokuwa imekaa vibaya au kudondoka chini,Zuma aliishiwa la kusema na hata kulia kukaisha.Mama yake alimuuliza"Ulikuwa usema nyumbani kwa bibi kwani kuna nini?,Na mbona bibi yako alisema akifika nyumbani anaondoka kwenda kutafuta kuni sasa kwani amepatwa na nini?,Na mbona sasa hayupo,?"Kwa maswali yale Zuma aliishiwa la kusema,Alitamani amsimulie mama yake mkasa mzima wa kuanzia kwenye ndoto lakini alishindwa.
Taratiibu bila hata kuongea Zuma alianza kuondoka kuelekea nyumbani,Kijasho chembamba kilimtoka hakika akaamini kweli kazi anayo,Na walidhamiria kweli kumtoa mama yake kafara kwa ajili yake,Akiwa njiani huku akilejea nyumbani Zuma alijikuta analia kilio cha kwikwi hasa akifikilia kumpoteza mama yake na hakuna msaada mwingine zaidi ya Bibi.
* * * * * *
Katika Falme na tawala ya kishetani,Ndani ya msitu mnene wa hifadhi ya Gombe katika mti mkubwa aina ya mbuyu,Paliandaliwa eneo maalumu la kutolea sadaka kwa ajili ya Shetani mkuu wa eneo lile,Palitengenezwa kichanja maalumu cha kutolea sadaka kwa ajiki ya Shetani wao,Ikiwa ni katikati ya msitu ule wa Gombe uliosongamana na miti mingi na kutengeneza kiza totolo eneo lile,palikuwepo pia na wachawi wadogo wadogo wakike na wakiume ambao walikuwa uchi wa mnyama huku wamejipaka aina flani ya unga mweupe mwili mzima,Mikononi mwao walikuwa wameshika pembe za ng'ombe wakipuliza na kuimba huku wameshikilia mioto inayowaka kuashilia zoezi la sadaka limekalibia,Japo ilikuwa ni mda wa kama mchana mchana hivi lakini walitengeneza mazingira ya uchawi na eleo lile likawa giza la usiku,Waliokuwa wanaimba na kuuzunguuka mbuyu ni wafuasi wa kichawi wa eneo la Ujiji zima,Haijalishi ulifuatana na mama yako au baba yako lakini sharti la zoezi hilo ni kuwa uchi wa mnyama kuimba nyimbo za ajabu huku mkizunguuka ule mbuyu mkubwa na mnene ulioonekana kuishi miaka mingi sana.
Walikuwa wakisubiri kafara ambae ni Bi Hindu aletwe kwa ajili ya Zoezi zima la utoaji kafara na sasa hatimae zile Shetani mbili zilizotumwa kumfuata Bi Hindu zilitia timu.Wazee na wakuu wa uchawi katika ule mji walikuwa wakiangalia ngoma zilivyokuwa zikiendelea pale huku wakifurahi sasa walisimama kwa ajili ya kuanzisha zoezi zima.Na wazee hao si wengine bali ni Mzee Kagusa kama kiongozi akifuatiwa na Mzee Shomary pia na wale Bibi vizee Wanne.
Pia uimbaji wa ngoma ulibadilika eneo lile na hatimae zikaanza ngoma za kutoa mwili wa mtu kafara,Mashetani yale mawili yalifika na kuulaza mwili wa Bi Hindu ambae tayari alikuwa kaishanyang'anywa uchawi na nguvu za giza alizokuwanazo pia pamoja na kuzimishwa wala asiweze kujitambua au kufanya kitu chochote.Chini ya Uchanja ule paliwekwa mabakuli mengi na makubwa kwa ajili ya kazi maalumu ya kudaka damu,Mzee Shomary kama Muhusika na pia kama ndie mwenye mke alikabidhiwa kisu kwa ajili ya kwenda kutoa Moyo wa mkewe ambae ni Bi Hindu ili mungu wao ashuke kupitia mbuyu aweze kupewa kama sadaka na sasa Mzee Shomary alinyanyuka na kukipokea kisu.Wakati huo shangwe ziliendelea ngoma zilipigwa na furaha iliongezeka.Mzee Shomary alikishika kisu kwanza kabla ya kuendelea na zoezi la utoaji moyo,Alimuangalia mkewe aliekuwa kalala pale kwenye uchanja,ni kama tayari ameshakufa,Alikumbuka siku ya kwanza katika maisha yake kukutana nae na kumpenda angali akiwa bado kijana,Alikumbuka maisha yao yalivyokuwa na walivyofanya mengi wakiwa pamoja,Alimwangalia usoni mkewe na kusogeza mwanga wa moto karibu na kugundua ni kama mkewe alikuwa amelala huku akionyesha tabasamu la kilio.
Kwa mara ya kwanza Mzee Shomary alidondosha chozi jingine kama siku ile aliyodondosha akiwa mdogo alipowauwa wazazi wake.
JE NINI KITAENDELEA
...Je Mzee Shomary atamuua mkewe?
...Je nani atamsaidia tena Mama Zuma?
.....Watafanikiwa kumuunganisha Zuma uchawini?
Usikose Sehemu ya Tano ya simulizi hii kesho saa 5 Asubuhi.Pia Samahani kwa kuwacheleweshea kama siku mbili hivi.
ASANTE SANA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: