KIJIJI CHA SHETANI Sehemu ya Kwanza .....NI mida ya jioni kijua chekundu kikielekea kuzama magharibi mwa kigoma katika mtaa wa Ujiji. Zuma aliludi kutoka kisimani akiwa na mdogo wake wa kike aliekwenda kwa jina la Miriamu,Walikuwa wakisaidizana kukokota baiskeli iliyobeba madumu ya maji.Hatimae safari ilifika nyumbani na kumkuta mama yao akimalizia kutwanga mpunga kwa ajiri ya ubwabwa wa jioni. ZUMA alishusha madumu huku akipokelewa na mdogo wao wa mwisho wa kiume alieitwa Amos.Shughuri ya kushusha madumu ilipoisha Zuma alichukua jukumu la kumsaidia mama yake kutwanga mpunga,Miriamu aliingia jikoni kuwasha moto kwa ajiri ya maandalizi ya kupika chakula,Shughuri ya kutwanga mpunga ilipoisha mama Zuma alipepeta kisha akaingia ndani na kutoka na kikombe kidogo na mfuko wa rambo,Alichota vikombe viwili vya mchele kisha akaweka kwenye rambo. "Zumaaa"Sauti ya mama iliita wakati huo Zuma alikuwa ndani,Hivyo ilimbidi atoke kumsikiliza mama anasema nini."Chukua huu mchele wapelekee babu na bibi yako sawa mwanangu".Mama alisema na kumpatia mwanae ule mfuko wa mchele kwa ajili ya kuupeleka alipoagizwa.Zuma aliuchukua kisha kuanza safari.Babu yake Zuma ni babu maarufu sana pale kijijini ndani ya Ujiji katika mkoa wa Kigoma,Watu wengi walisikika wakisema"Huyu mzee sio kabisa anamambo ya ajabu sana".Licha ya kuwa taarifa hizo zilikuwaga zinamfikia Zuma kuwa babu yake anamambo ya kishirikina lakini Zuma hakuwahi kuona tabia hiyo kwa babu yake hata siku moja.Pia babu yake alimuona ni mtu mwenye roho nzuri sana na kwa ukweli alikuwa na upendo sana kwa Zuma. ZUMA alifika kwa babu yake na bibi yake.Babu yake alijulikana kwa jina la Mzee Shomary na bibi yake aliitwa Bi Hindu,Wazee hawa walibahatika kupata watoto takribani sita lakini cha ajabu ni mama yake Zuma tu ndie aliesalia maana wengine wote walikuwa wameshafariki,Zuma aliwakabidhi mchele wakati huo aliwakuta wamewasha moto wanaota wakiwa wamekaa wawili huku wakiongea mambo ya hapa na pale."Asante sana mjukuu wangu kwa mzigo huu mwambie mama babu na bibi wanashukuru sana"Aliongea Bi hindu kutoa shukrani kwa Zuma na mama yake kwa mzigo ule. "Vipi za masomo mjukuu wangu...Chukua kiti ukae tuongee mawili matatu"Alisema mzee shomary. "Za masomo nzuri..ila babu mi leo sikai kesho tunamtihani si unajua tena ndio tupo mwishoni kumaliza kidato cha nne hivyo mitihani ni mingi sana na nikisema tu nisisome basi wataninyan'ganya nafasi yangu ya kuwa wakwanza kama nilivyozoea,Ngoja niwahi nikajisomee kesho ntakuja tupige story vizuri"Alisema Zuma akimwambia babu yake. "Sawa mjukuu wangu wahi ukasome maana ni wewe pekee ndio tunakutegemea".Asante babu,Bibi mimi naenda Usiku mwema."Alisema Zuma kisha kuaga na kuanza safari ya kurudi nyumbani ALILUDI nyumbani na kukuta tayari wamepika,alienda kuoga kisha haraka haraka akatayarisha vitabu vyake mezani,Mama yake alikuwa anampenda sana Zuma aliingia chumbani kwake na kutikisa kama kibatari kina mafuta na kukuta kimepungua,Aliitwa Amos afuate mafuta ili kuja kujazilishia mafuta kwenye kibatari.Baada ya hapo mama alisema"Miriamu mpakulie kaka yako chakula ili awahi kula aanze kujisomea".Bila kupoteza muda Miriamu alifanya kama alivyoagizwa na Zuma alianza kula akiwa sebureni huku mama yake amekaa anaweka sawa vitu vyake kwenye kapu ambalo huwa anabebea kwa ajiri ya biashara yake ya umama ntilie(Mama lishe) katika kibada kimoja kilichopo barabarani ndani ya Ujiji. Mama pia alitumia mwanya huo kumpa maneno yenye nguvu mwanae yatakayomfanya asome kwa uchungu"Soma mwanangu,Tangu baba yako afariki wewe ndie umebaki kuwa baba katika huu mji soma kwa uchungu uje ukomboe wadogo zako,Mimi mama yenu huwezi jua leo mzima je kesho ntakuwaje wadogo zako pia wanahitaji kufika mbali katika elimu,Wote wanakuangalia wewe uwaongoze jitahidi sana mwanangu mimi ntajitahidi kila njia kukupigania ufike mbali."Mama Zuma alisema maneno yale kwa mwanae ili yampe nguvu ya kusonga mbele. MAFUTA yaliletwa na sasa Zuma alivuta koroboi kwa ukaribu zaidi na daftari kisha kuanza kukomaa na maandishi kuyaweka kichwani kwa ajiri ya mtihani wa kesho,Sebureni mama na wadogo zake wawili walipata chakula kisha wakamtakia masomo mema na wao wakaingia kulala. NI mida ya saa sita usiku Zuma bado yupo mezani,ghafla kichwa kilianza kumuuma kwa mbali na mwili ulianza kutoa jasho,Alivumilia kusema kwamba hakusikia maumivu yale badala yake aliendelea kukomaa na kitabu ili asije akaaibika kwenye ubao wa matangazo shule ikishuhudia kinara anaeshika namba moja katika shule ya pale Ujiji sasa wamemtoa. Lakini kila akijitahidi kusoma mambo yalizidi kuwa mabaya mwili ulizidi kutoa jasho na kichwa kuuma,Hakutaka amwamshe mtu yoyote yule badala yake alichukua panadol za akiba alizokuwa nazo mle ndani na kunywa kisha kumwachia Mungu siku ya kesho katika mtihani wake,Aliingia kulala huku mwili wake ukiendelea kutoa jasho.Kilichokuja kumshangaza zaidi richa ya kuwa anatoa jasho na joto kali kuwemo mle ndani lakini cha ajabu mwili wake ulikuwa unatetemeka kama mtu anaesikia baridi.Alijilaza kitandani na hatimae usingizi ulimpitia ZUMA ghafla alikuja kushtuka kutoka usingizini na kabla hajafumbua macho alisikia kelele za watu ni kama kundi kubwa la watu likiimba nyimbo zisizojulikana,Alifumbua macho haraka na hapo ndipo alikuja kujikuta yupo porini ndani ya msitu mnene sana.Alikuwa amefungwa kwenye kitanda cha ngozi na huku akiwa amezunguukwa na watu asiowafahamu,Giza nene lilikuwepo pale licha ya kuwepo mienge ya moto kuwashwa kwa pembeni na mingine kushikiriwa na watu walioimba huku wakizinguuka eneo lile,Kwa macho ya kupepesa huku akitaka kupiga kelele ndipo mzee mmoja alipomnyooshea kidole mdomoni na kujikuta Zuma hawezi kutoa sauti yoyote ile ya kupiga kelele,Alibaki akitoa macho kwa kuwaangalia wale watu huenda labda atamtambua hata mmoja na hapo ndipo hakuamini macho yake kuona yule mzee aliemnyooshea kidole alikuwa ni babu yake mzee Shomary,Kuita babu alishindwa kutokana na kuzibwa na uchawi kutokuongea kabla hajamaliza kushangaa uwepo wa babu yake ghafla pia alimuona mzee maarufu sana pale kijijini aliejulikana kwa jina la Mzee Kagusa.Mzee alijulikana kama ni mtu mshirikina sana pale kijijini na aliogopwa sana na wanakijiji,Mzee yule alikuwa ameshikilia kisu pia na pembe la mnyama ambae hakujulikana. MZEE Kagusa aliamlisha"Haya ile siku tuliyoingojea ya mjukuu wetu Zuma kukabidhiwa uongozi wa kundi letu hatimae umefika,Pongezi ziende kwa babu yake kwa kumteua Zuma kuwa kiongozi wetu na sisi tuko tayari atuongoze,Tujitolee kumfundisha kama sisi tulivyofundishwa na mababu zetu anghari tukiwa bado wadogo"Alisema Mzee Kagusa kisha pembe kupulizwa na sherehe kuanza. KAZI iliyokuwepo pale ilikuwa ni kumlisha uchawi Zuma ili awe miongoni mwa wachawi,Tena sio miongoni mwa wachawi bali ni kiongozi mkuu.Zuma alishindwa la kufanya alibaki akijitikisa kitandani napo hakuweza alijitahidi kupiga kelele alishindwa.Wakati nyimbo zikiendelea na wachawi wengine wakiendelea kuzunguuka na kuimba pia ngoma zikipigwa ndipo sasa Mzee kagusa na mzee Shomary wakiwa na wabibi kama wanne waliozeheka kweli walimsogelea Zuma mahali alipo kwa ajili ya kukabidhiwa mikoba. ZUMA alianza kutetemeka sana aliona siku zake za uhai zimekwisha,mkojo mwembamba ulimtoka akiwa pale kwenye kitanda cha ngozi,Hatimae wazee wale walimsogelea na kumzunguuka,Mzee Kagusa alimkabidhi moja kati ya wale wabibi wanne kisu bibi huyo alikuwa kazeheka kuliko wote pale.Alipewa kisu ili aongoze shughuri rasmi. KISU kilinyanyuliwa juu kwa ajiri ya kumchana Zuma kifuani ili dawa iwekwe ya kichawi itakayomfanya awe mchawi bila kubisha.Mara ghafla yule bibi alipotaka kutelemsha kisu alianza kutetemeka,Kila akijitahidi kukishusha kisu kiligoma,Ilibidi aahilishe zoezi na kushusha kisu kisha kufumba macho kama dakika tano.Baada ya dakika tano Bibi yule alifumbua macho na kusema"mungu wetu amekataa...anasema ili kumpa uongozi huyu ni lazima damu ya mama yake imwagike kama sadaka kwa hiyo ametupa wiki moja tumpelekee nyama na damu ya mama yake kama sadaka kisha ndio tumkabidhi uongozi"Alisema Bibi yule na kurudisha kisu kwa Mzee Kagusa. ZUMA aliyasikia yale maneno vizuri,Alianza kutetemeka na kuita Mamaaaa.....Mamaaaaa.....ndani ya moyo wake bila kutoa sauti.Alikuja babu yake na kumgusa katika paji la uso na hapo Zuma alitoweka maeneo yale. SAA kumi na mbili Alfajili Zuma akiwa chumbani kwake kalala anashtuka kwa kusikia sauti ya mama yake chumbani kwake inamuita"Zumaaaaaa.........Zumaaaaa.....Njoo mwanangu....njooooo nakufa mimi mama yako".Ni sauti hafifu aliyokuwa akiitoa mama yake kule chumbani kuonyesha ni kama mtu aliekuwa akielekea kufa kweli. Zuma pale pale akiwa kitandani alikumbuka kilichotokea usiku ule porini.Mwanzo alivyoshituka kutoka usingizini alijua ni ndoto kama ndoto za kawaida ila kwa sauti na maneno ya mama yake kule chumbani akiitwa alijua hiyo haikuwa ndoto tena bali alichokiona kilikuwa ni kweli kikiendelea katika ulimwengu wa kishetani.Alikurupuka kutoka kitandani mbio akielekea chumbani kwa mama yake.Hofu ya kumpoteza mama yake ambae ni nguzo katika masomo yake ilimtanda...... JE NINI KITAENDELEA ...Naam usikose katika sehemu ya pili ya story hii ya KIJIJI CHA USHETANI itakayokufunza mengi zaidi yanayotokea katika maisha. Usisahau pia ku-Like,Na kukomenti ili kutoa maoni juu ya Simulizi hii PIA nikiwa kama mtunzi wako ninaombi moja tu....Nisaidie kusambaza simulizi hii kwa kushare katika magroup mbalimbali na pia sehemu zingine. Ukifanya hivyo hii itakuwa ni kama shukrani yako kwangu na malipo yako kwangu juu ya simulizi hii.Pia utakuwa umenipa nguvu zaidi ya kusonga mbele na kutenga muda wangu ili nizidi kuiandika zaidi nawe uisome ujifunze.Pia MUNGU ATAKUBARIKI SANA ASANTENI SANA.

at 8:02 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top