Home → simulizi
→ KIJIJI CHA SHETANI
Sehemu ya Pili
Ilipoishia
.... Alikurupuka kutoka kitandani mbio akielekea chumbani kwa mama yake.Hofu ya kumpoteza mama yake ambae ni nguzo katika masomo yake ilimtanda......
Sasa Endelea
......Aliingia chumbani kwa mama yake na kumkuta akitetemeka kwa baridi kali,Zuma alianza kulia huku akiita mamaaa....mamaa....Wakati huo mama yake alikuwa akiweweseka na kutetemeka kiasi kwamba mpaka kitanda nacho kilikuwa kinatetemeka.Punde si punde wadogo zake waliamka na wao kuelekea chumbani kuangalia mama yao amepatwa na nini.Miriamu alipomuona mama yake yupo katika ile hali nae alianza kudondosha kilio pale pale,Kitendo hichi kilisababisha pia hata mdogo wao wa mwisho Amos nae aanze kulia.Walianza kumfunika mama yao shuka ili baridi lipungue lakini kadri walivyokuwa wakiongeza shuka ndivyo pia na mama yule alizidi kutetemeka.Hatimae pia alipata wazo na kuona njia pekee ni kuelekea kwa babu yake Mzee Shomary ili hata akamuombe wasiweze kumfanyia chochote mama yake kile walochokusudia.
ALITIMUA mbio za wakimbiaji wa Kenya kuelekea kwa babu yake ili aweze kuinusuru roho ya mama yake,Alipofika kwa babu yake alimkuta bibi yake akifagia uwanja asuhuhi hiyo na mapema,Zuma alifika na kumwamkia bibi yake na swali lililofuata aliuliza"Bibi nimemkuta babu??".Bibi huyu kwanza kabla hajajibu alishangaa sana ujio wa Zuma pale nyumbani Asubuhi yote ile na wakati haikuwahi kutokea,"Babu yako hayupo kaamka Asubuhi kaelekea porini"Bibi alimjibu Zuma na kumuuliza kwani kuna nini.
ZUMA alikaa kwanza kama dakika moja hivi kabla hajajibu lile swali.Alikuwa akijiuliza maswali kichwani mwake"Inamaana bibi hakuwepo usiku ule kwenye lile swala la mimi kupewa ukuu wa uchawi?,Inamaana bibi yeye si mchawi na haelewi chochote kinachoendelea".Wakati Zuma akijiuliza maswali hayo alikumbuka wakati anapepeza macho kuangalia watu waliohudhuria katika ile sherehe hakuona sura ya bibi yake.Zuma baada ya kufikiria hayo kichwani aliamua kutoa jibu kwa bibi yake huku analia"Mama anaumwa na yupo kitandani anatetemeka".Zuma aliposema maneno haya mbele bibi yake, Bi Hindu huyu alishikwa na bubuwazi kitendo kilichosababisha aachie ufagio.Bila hata kuuliza chochote alianza kukimbia kuelekea nyumbani kwa akina Zuma huku akijiongelea"Mwanangu......Mwananguuu mama Zumaaaa Mwanangu wa mwisho"...Yaani akimaanisha mama yake Zuma ndie aliekuwa mwanae wa mwisho katika watoto 6 aliozaa
* * * * * * * * * * * *
BI Hindu mke wa mzee Shomary alibahatika kupata watoto 6 akiwa na mumewe yule yaani Mzee Shomary lakini watoto watano wote walipokuwa na umri mkubwa walianza kufariki mmoja baada ya mwingine na hatimae aliekuwa amesalia alikuwa ni mama Zuma tu,Mzee Shomary alianza maswala ya uchawi akiwa toka mdogo sana baada ya kurithishwa na babu yake kipindi hicho walipokuwa wanakaa kibondo,Maisha yake yote ameishi ya ujana na mpaka amekuwa mzee ni ya uchawi tu,Ni Mzee ambaye tayari ameshaua watu wengi sana walio ndugu na wengine sio ndugu kutokana na uchawi hivyo jukumu alilokuwa nalo lilikuwa ni kumuua pia mwanae huyo wa mwisho kwa ajiri ya mjukuu wake kurithi kiti chake,Ukweli ni kwamba hata wale watoto watano wote mzee aliwatoa kama sadaka na mpaka kubakia na mtoto mmoja.Mzee shomary kuuwa kwake au kupoteza ndugu yake wa damu haikuwa shida kwake,Harufu ya damu za watu wanamlilia ilikuwa ni nyingi sana katika mwili wake,Roho hii ya kishetani aliipata toka siku ile alipopewa uchawi na babu yake kibondo na kwa mara ya kwanza alijikuta ameua wazazi wake kwa amri ya uchawi na pia kula nyama zao na damu akiwa na wachawi wenzake,Toka siku hiyo roho ya kishetani na uuwaji ilikaa ndani yake hivyo hakuona shida yoyote katika maisha yake kuua mtu yoyote hata kama ni ndugu yake ili mladi tu kuupigania uchawi.
Mzee Shomary alimuoa Bi Hindu wakati huo Bi Hindu alikuwa sio mchawi,Na mwanzo wa maish Mzee Shomary alifanya shughuri zake za uchawi kwa siri bila ya Bi hindu kujua lakini aliona atakaa mpaka lini akimficha mkewe kama yeye ni mchawi,Hivyo siku moja aliamua kumweleza Bi hindu kila kitu,Bi hindu alimpenda sana Mzee Shomary hivyo hata alipojua kuwa ni mchawi hakuona sababu ya yeye kuachana nae.Waliendeleza maisha pamoja na taratiibu Bi hindu alijikuta nae anatambulishwa katika kundi la uchawi na kujikuta anaanza kujifunza maswala ya kishirikina,Licha ya kuingizwa kundini na kujifunza maswala ya kishirikina Bi hindu alikuwa bado hapendi hayo maswala,Hakuwahi kuua wala kufanya tukio lolote baya.
MAISHA aliyoishi Bi hindu alikuwa kama vile mtu asiejihusisha na ushirikina japo aliujua vizuri hivyo mara nyingi hakuambatana na mumewe katika kazi zake.Ukweli ni kwamba asubuhi ile Mumewe hakuwa ameenda porini bali tangu aondoke usiku ule kwenda huko uchawini hakurudi nyumbani,Bi hindu aliujuaga mpango wa mumewe kutaka kumtoa kafara mwanao huyo wa mwisho kama wengine,Waliishi wakigombana kila siku na Mzee shomary kwa sababu Bi hindu hakutaka kuona anampoteza mwanae huyo wa mwisho,Hivyo Mzee shomary aliamua aifanye kazi hiyo ya kumpoteza kimya kimya Mama Zuma bila ya kushirikiana na Mkewe Bi Hindu na ndio maana Bi Hindu alipoletewa taarifa na Zuma Moyo wake ulianza kumuenda mbio akijua sasa anampoteza mwanae
* * * * *
MOJA KWA MOJA Bi Hindu aliingia ndani chumbani kwa mwanae huyo Mama Zuma na kumkuta anahali mbaya kiasi kwamba wangechelewa kama dakika 20 wangemkuta tayari marehemu,Aliwakuta Miriamu na Amos wamelia mpaka machozi yamekauka,Pia mwili wa Mama Zuma ulikuwa umeshaanza kukunjamana tayari kwa kipenga cha mwisho.Bi Hindu aliingia pale na kuanza kulia huku akisema"Haiwezekani mwanangu wakuchukue bora wanichukue mimi....Haiwezekani".Haraka sana alimsogelea mwanae pale kitandani na kwa sekunde tano alifikilia cha kufanya,Alichokifanya alinyoosha kidole chake kile kidogo cha mwisho cha mkono wa kulia kilichokuwa na kucha ndefu na kukiweka katika kitovu cha mtoto wake huyo ambae ni Mama Zuma.Alikiweka huku kafumba macho na kuongea maneno yenye lugha isiyoeleweka ndani ya kama dakika tano.
Kadri alivyokuwa anazidi kukiweka ndivyo Mama Zuma alipunguza kutetemeka na mwili ulianza kukaa sawa,Hatimae kutetemeka kukaisha na mwili ukakaa sawa kisha mama Zuma alipiga chafya kuashiria uhai upo.
PALE PALE katika mamlaka na falme ya kitawala ya kichawi aliyopo Mme wake ambae ni mzee Shomary taarifa zilifika kuwa kuna mtu kaaribu kazi ya kuutoa mwili na Damu ya mama Zuma kama sadaka.Wazee wa kichawi walikasirika sana na amri ilitolewa alieharibu kazi ile atafutwe na auwawe na pia kabla wiki haijaisha pia Mama Zuma nae anatakiwa Auwawe na sasa zilikuwa zimebakia siku sita.Bi Hindu akawa amenunua kesi na mara moja wakawa tayari wamemtambua kupitia Mitambo yao ya kichawi.Mzee Shomary alikasirika sana Kuona mkewe kaingilia kazi.
JE NINI KITAENDELEA
....JE nini hatima ya Bi hindu?
....Je nini hatima ya Mama Zuma?
....Na vipi kuhusu Zuma kurithishwa uchawi??
ASANTE SANA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: