Home → simulizi
→ Chombezo fupi: Kitamu Kinaliwa na Wengi
Sehemu: 04
👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼
Ilipoishia jana...
...baada ya kumpata mpenzi mpya aliyekuwa amemuacha mbali mpenzi wangu aliyenisaliti na rafiki yangu. Kuanzia siku ile mimi na Anna tulikutana jioni na kuachana asubuhi.
Songa nayo sasa...
Anna alinieleza yeye ni mfanyabiashara mkubwa jiji, kutokana na vito vya thamani alivyokuwa akivaa na uwezo wa kifedha kwa kulipia hoteli kila tupokutana pia kunipa fedha ya nauli. Mara nyingi jioni alikuwa akinipeleka sehemu na kuniacha kwenye baa kabla ya kuondoka alinunulia pombe ya kutosha kisha unieleza anakwenda kumuaga mjomba wake na aliporudi baada ya saa nzima siku nyingine saa mbili akiwa amebadili nguo na kuondoka naye mpaka hotelini ambayo tuligeuza kama yetu.
Kutokana na uwezo wangu mdogo kimaisha Anna alinitafutia sehemu katikati ya jiji na kulipia fedha nyingi kwa ajili ya kunifungulia duka kubwa la spear pia alinieleza baada ya mwezi mmoja na nusu gari langu la kutembelea lingeingia hapo ndipo tungepanga mipango ya ndoa.
Kama kawaida yetu kila jioni lazima apitie kwa mjomba kwanza kumuaga kisha alinipitia na kuondoka. Siku moja baada ya Anna kwenda kwa mpenzi wake aliniacha nikipata kinywaji, mara walitokea jamaa wawili ambao niliungana nao katika meza yangu na kuanza kupiga stori.
Mmoja aliniuliza swali ambalo lilinishtua kidogo.
“Eti mkubwa yule ni dada yako au mtu wake wa karibu?”
“Kwa nini?”
“Kila siku huwa anakuacha hapa na kukupitia kisha huwa mnaondoka kama wapenzi vile.”
“Ni mpenzi wangu.”
“Mpenzi wako au unatania maana siku hizi kuna wapambe wa kiume kumsindikiza demu kwa mpenzi wake kisha kupewa posho kidogo.”
”Hivi mnanionaje?”
“Samahani usituelewe vibaya wewe kijana mwenzetu lazima tukueleze ukweli juu ya huyo demu.”
“Ana nini?” Wasiwasi wangu huenda ameathirika.
“Kwani akikuacha hapa anasema anakwenda wapi?”
“Kwa Anko wake.”
“Ni kweli mpenzi wako?”
“Na muda si mrefu tutafunga ndoa.”
“Mmh! Basi tuyaache kama yalivyo tusije kukuhalibia bure.”
“Naomba mniambie kuna nini?”
“Lazima uwe na moyo wa kiume, huko anapokwenda demu wako si kwa mjomba wake bali kwa jamaa yake mmoja TX mmoja ndiye anayemlinda mjini makeke yote ni kwa ajili ya huyo jamaa.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa.’
”Sasa huko anakwenda kufanya nini?” niliuliza swali la kijinga.
“Wewe mtu mzima swali gani hilo.”
”Nitapataje ukweli kuwa yule si mjomba wake bali mpenzi wake.”
“Tunaweza kukupeleka, mwanzoni tulikuwa tukipiga chabo lakini baada ya kuona jamaa mchovu tuliachana nayo.”
Kwa kutaka uhakika niliongozana na wale jamaa hadi kwenye jumba moja la kifahari na kunielekeza niwafuate taratibu hadi kwa nyuma kisha walinisogeza kwenye dirisha moja na kuchungulia ndani. Sikuamini mpenzi mwangu Anna alikuwa mtupu pembeni ya kipisi cha jamaa mmoja mzungu ambaye naye alikuwa mtupu.
Nilimsikia yule mzungu akilalamika:
“Sasa mpenzi milioni mia tatu ndogo?”
“Unaziona nyingi hivi kila siku unauchezea mwili wangu unaona raha eeh?”
“Basi kesho nitakuongezea zingine mbili.”
“Kama kesho utanipa mia tatu.”
“Sawa mpenzi.”
Nilitaka kupiga kelele baada ya kujua Anna naye hakufaa kuwa mke wangu kwani ilionesha ni kahaba mzoefu anayefanya biashara ya mwili. Niliamini kabisa hakuwa na bwana mmoja, kabla sijapiga kelele jamaa na kunieleza:
****
Je nini kitaendelea??
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: