SISTER MURCIA. Sehemu.............(16), Na...........Hemed mayugu. ILIPOISHIA. Najua njaa ipo basi ngoja nikatafute chakula?" "Wapi Paulo utakipata chakula?" "Usijali nitakipata tu" Paulo alisema. Kisha akachukua panga na ngao yake vyote vya ajabu na kutoka mbio kuelekea alikokuwa anaamini angepata chakula. SONGA NAYO. Alikimbia mbio kweli kweli, alipofika umbali kama wa mita amsini kutoka kanisani. Akasogea sehemu iliyokuwa na mti mzuri wenye kivuri kisha akapiga magoti na kusema. "Eee bwana sina hakika na niendako kama nitakipata chakula bali tumaini langu nikipate chakula. Wewe uliyemlezi wa viumbe vyote nifanyie wepesi nikipate, niongoze njia ya kweli ya kukipata chakula hicho" baada ya kusema maneno hayo alimalizia na neno Ameen kuashilia maombi yake yapokelewe. Baada ya kumaliza kusema hivyo paulo alitoka pale kwenye mti akiwa haelewi anaenda wapi. Kilichokuwa kinamuongoza ni njia tu basi. Kwa bahati mbaya alikuwa akiongoza njia ya kuelekea mjini. Njia ambayo wanapita watu waliokuwa wanatoka mjini kuingia katika kijiji hicho cha shimo la moto. Hakiwa mbio hivyo alijikuta akisimama ghafra baada ya kuona kichwa cha Lucas njiani. Paulo alichanganyikiwa kabisa akashindwa kuamini ikambidi akisogelee kichwa hicho. Kabla hajakifikia alitokea mwenyekiti wa kijiji hicho. Ambaye pia alikuwa ndie mchawi mkuu wa kambi ya magharibi. Mzee yule alikuwa ameshikiria kamba iliyokuwa kama bakora. "Najua unajiamini sana na huyo mungu wako, lakini nazani inaweza kuwa ndiyo mwisho wako wa kuishi" paulo alimwangalia mzee yule kwa hasira akamtamani vilivyo. Lakini moyo wake ukamuonya asimsogelee mzee yule mchawi. Moyoni maneno yakamuhijia kuwa sema. "Kwa bahati yako mungu wangu kanikataza kukumaliza lakini utaonywa kwa madhambi yako" haikupita hata sekunde nzee yule mchawi alianguka chini na kujipigiza utafikiri kabwebwa juu kisha akatupwa. Kipindi hicho pauli alikuwa kaisha iendeleza safari yake kuelekea alipokuwa anaongozwa, hata habari za kichwa cha Lucas alizisahau muda huo. Sijui lakini huwenda yote yaliyokuwa yanafanyika kwake yalikuwa yakiongozwa na bwana mungu wake. Alikimbia mpaka mahara pa njia panda, kama ni mwenye kumbu kumbu mahara hapo ndiko kuna kona. Mahara hapo ndipo kuna vibwanga vya hatari na ndipo walikwama na kutekwa wakiwa na Moris kisha wakatekwa na kupelekwa makao makuu ya kichawi iliko kambi ya Mashariki ambayo inaongozwa na padre Joseph. Cha ajabu alipofika hapo alilikuta gari lao liko hapo, kila kitu kikiwemo. Alistaajabu sana kukuta kila kitu kimo kwenye gari, alipo angalia upande mwingine kungalia kama kuna chochote cha kumletea madhara hakuona chochote, swali likabaki ni vipi ataweza kukitoa chakula kile kwenye gari. Alijikuta akijisemea moyoni. "Nitakibeba!" Atakibeba vipi wakati ni kingi? kitu hicho alikisahau, tasimini yake ilikuwa haina maana, labda aliplani kubeba kile ambacho angekiweza. Basi paulo alipiga magoti kisha akasema. "Eee mungu hakika wewe unastahili kushukuliwa sifa njema zikwendee. Hakika wewe ni tegemezi la moyo wangu, milele amina" Ilikuwa kama vile ni maombi ya miujiza maombi yake yalipitiliza moja kwa moja na kupokelewa. Bado hakiwa amepiga magoti huku machozi yakimtoka aliishitukia tu gari inatikisika. Akageuka nyuma kwa mshituko kuangalia nini kimesababisha. Hakuona chochote, bado akiwa anashangaa mala mlango wa gari ulifunguka akawa kama anavutwa kuingia ndani ya gari. Paulo akiwa aelewi ni nini kinafanyika alijikuta akiingia ndani ya gari kisha akakaa sehemu ya Dereva. Akili zake zikamtuma aliendeshe gari, naye akafanya vile, hakika lilikuwa ni tukio la kushangaza sana kwake alijikuta akiliendesha gari lile kutoka pale lilipokuwa kuelekea kanisani. Njia nzima paulo alikuwa akiendesha gari huku aamini kama ni yeye kweli, gari liliongoza njia mpaka kanisani. Halipo fika akapiga honi kuashilia kuwa amefika. Sister Murcia alitoka ndani ya kanisa mbio kuja inje kuangalia. Sister akuamini macho yake baada ya kumkuta paulo akishuka kwenye gari huku akiangalia mikono yake, kwa muda mfupi paulo alijiona chizi, alishindwa kuamini kama ni yeye baada ya kufika pale kanisani. "Paulo ni wewe au hapana?" Sister Murcia aliuliza. "Hata mimi sijui kama ni mimi" paulo alijibu. Wote kwa pamoja walisaidizana kuingiza vitu ndani zoezi liliwachukua kama nusu saa. Tayari mpaka muda huo ilikuwa ishafika mida ya saa nane kasoro. Sister Murcia bado alishindwa kuamini akamwangalia paulo kisha machozi yakamtoka, kumbe katika vitu vile kulikuwemo na matunda. Kama ndizi maparachichi na mapapai lakini kwa uwezo wa roho mtakatifu na nguvu ya bwana hakuna hata kimoja kilichonesha arama ya kubadilika. "Paulo, Naomba unisamehe" Sister murcia alisema. "Nikusamehe kwa lipi sister mbona hakuna chochote ulichonikosea" paulo alisema. Hakiwa na uzuni mkubwa moyoni sister murcia alijisema. "Hakika yapaswa iwe kweli, hakika yapaswa aje mkombozi wa kijiji hiki kutoka katika wewe" Paulo bado alishindwa kuayaelewa tena maneno ya mwalimu wake. Kipindi hicho chote sister murcia alikuwa akitokwa na machozi. "Hakika sitokuwa na mamlaka juu yako, bali wewe ndiwe mwenye mamlaka kwangu toka sasa" sister murcia alisema kisha akajinyanyua alipokuwa amekaa akaingia ndani ya Sakarastia akaja na kitabu alichokabiziwa na Murcia wa kwanza alipofika akayasogelea mazabahu, akapiga magoti kisha akasema. "Mapenzi yako yawe juu yake, mpe ujasiri na umsamehe mazambi yake. Uweke moyo wangu akaye nao moyoni mwake mpaka pale utakapo mchukua. Amiina" baada ya kusema maneno hayo Sister murcia alimsogelea Paulo pale alipokuwa amekaa na kumbusu katika paji lake la uso kisha akamkabizi kitabu kile akisome. Paulo alipokifunua tu kitabu kile cha ajabu kitu cha kwanza alichokutana nacho, alijikuta anakifunika kitabu kile kisha akasema. "Je yapaswa iwe kama maandiko haya yanavyo sema?" Paulo aliuliza. "Bila shaka yapaswa iwe hivyo" sister murcia alisema. Baada ya kusema maneno hayo paulo ambaye alikuwa na njaa aliingia ndani akachukua matunda na kuanza kula. Yote hayo yakiwa yanaendelea sister murcia alikuwa akimtazama tu. "Sister wewe si ndiye uliyekuwa wa kwanza kusema kuwa una njaa?" Paulo aliuliza baada ya kumuona Sister Murcia akimwangalia. Maneno yake yalikuwa kama sumu noyoni mwake, badala ya kujibu sister alianza kutokwa na machozi tena. Tena wakati huu alikuwa akisema. "Tafadhali eee bwana mungu wangu, usiniache nikawa mwenye mateso, mfanye hawepo nami milele" ITAENDELEA. Kuna nini moyoni mwa sister Murcia? Tukutane jumamosi. Share share kwa wingi uwezavyo

at 4:34 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top