Home → simulizi
→ SISTER MURCIA,
NA.......Hemed mayugu,
No.............(017).
ILIPOISHIA.
Maneno yake yalikuwa kama sumu moyoni mwake, badala ya kujibu sister alianza kutokwa na machozi tena. Tena wakati huu alikuwa akisema.
"Tafadhali eee bwana mungu wangu, usiniache nikawa mwenye mateso, mfanye hawepo nami milele"
Songa nayo.
Sister murcia alipo maliza kuisoma sala yake akamgeukia Paulo kisha akasema.
"Niamuru basi nami nitatii kwakuwa una mamlaka makuu kwangu Toka sasa"
Paulo alimwangalia sister murcia kwa aibu, alishindwa afanye nini kwasababu tu agizo la mungu lilipaswa litimizwe. Bado akiwa anaendelea kumwangalia Sister Murcia alitokwa tena machozi. Paulo alishindwa kuelewa kwanini mwalimu wake kila alipokuwa anamwangalia alikuwa akilia. ingawaje alidai ananjaa lakini tayari chakula cha kutosha kipo. Baada ya kushindwa kuelewa ilimbidi aulize.
"Sister mbona unalia kila ukinitazama?"
Swali hilo sister murcia bado akulijibu zaidi alizidi kulia. Baada ya kuona hivyo paulo alimsogelea akamshika kichwa akakilaza kifuani kwake kisha akamuuliza tena.
"Je kuna mauzi ambayo nimekufanyia?"
"Hapana, naogopa kusema" sister murcia alisema.
"Je ni kuusu swala la mtoto mwema, mwenye kukikomboa kijiji hiki?"
"Hapana hilo hata si lenye kiniumiza"
Kwa sauti ya upole iliyokuwa imejaa unyenyekevu sister murcia alikuwa akiongea. Paulo alishindwa kuelewa mwalimu wake alimaanisha nini ilimbidi amuulize tena kwa mala nyingine.
"Je kama si hicho ni nini? Au kupotea kwa wanafunzi wenzangu?"
"Hapana paulo wewe ni moyo wa faraja kwa moyo wangu, wale hawakuwa na imani na mungu wao, labda ndio maana imekuwa hivyo" sister murcia alisema.
"Kama si hivyo nambie ni nini kilichomo moyoni mwako?"
"Naogopa kubaki peke yangu" sister murcia alisema.
"Unaogopa kubaki peke yako! Mbona mi nipo nawe wakati wote?" Paulo aliuliza kwa mshangao baada ya kauli ya sister murcia kumshangaza.
"Paulo.....lazima......lazima mtoto apatikane baina yangu na wewe kwani wewe ndiye uliye mwema katika kijiji hiki, lakini nilikuwa ndani ya Sakarastia nikaona kuwa wewe lazima ufe pale tu mimi nitakapokuwa na mjamzito"
Sister murcia alisema, machozi yakimtoka huku kichwa chake kimeegeshwa kifuani kwa paulo. Maneno hayo yalimshitua paulo na ndio ulikuwa ukweli kuwa sister murcia akipata mimba ya mtoto atakaye kikomboa kijiji cha shimo la moto yeye yapaswa afe. Hayo yalikuwa ni maono ya kweli aliyooneshwa sister murcia.
Kwa upole na kwa unyonge paulo alimshika sister murcia kichwani akasema.
"Hakika ni katika wema, na kitokacho kwa bwana mungu wetu hakipaswi kukataliwa au kukimbiwa ni dhambi kubwa kwetu kupingana na agizo la bwana mungu wetu. Yapaswa litimizwe ili ufalme wake utimie na ukamilike. Hakika bwana mungu wetu yeye aujua ukweli wa nyoyo zetu na maisha yetu, yeye ndiye mwanzo na mwisho wetu yapaswa tutii na kutekeleza maamrisho yake, ili ufalme wake utimie"
Paulo alitamka maneno yaliyomjaza imani sister murcia akakiinua kichwa chake kutoka katika kifua cha paulo na kumtazama tena usoni. Akilia kwa kwikwi sister alimkumbatia paulo na kusema.
"Naomba unisanehe kwa maneno hayo"
"Ujanikosea hakika moyo wangu unakwamini na kukusikiliza, basi yanipaswa niyatii na kuyapokea yatokayo kwako" paulo alisema.
Baada ya kusema hivyo paulo alimshika murcia begani na kumpa ndizi ale kwani toka watoke msituni alikuwa ajala chochote. Sister murcia aliipokea na kuila, lakini bado alikuwa akimwangalia paulo machozi yakimtoka. Paulo alijinyanyua kutoka kanisani akaingia jikoni akaliwasha jiko lao la gesi akachemsha chai haraka kisha akachukua mkate akarejea navyo kanisa na kumtengea sister murcia ale ili apate nguvu maswala mengine yaendelee.
*****
Siku zilipita mwezi ukakatika wote wakiwa wanaishi wawili katika eneo hilo la kanisa, hakukuwa na usumbufu wowote. Walidumisha maombi na kusari kwa nguvu hata kukumbuka kuwa kuna kuzaliwa mtoto walisahau mbali na hilo walisahau pia kuwa siku za kufa paulo zinasogea.
Ilikuwa ni siku mpya ndani ya mwezi huo huo. Sister murcia aliisi mabadiliko ambayo ni ya lazima kwa mwanamke yoyote kumkuta katika maisha yake. Kiujumla zilikuwa ni siku katika siku za hesabu. Siku hizo ndizo huwa siku za kupata mtoto. siku hio
Toka mchana mpaka jioni wote walikuwa wakiangalina kwa kuogopana, hakuna aliweza kumwangalia mwenzake kwa muda kwani hali ya kufanya tendo la ndoa kwa ajili ya mtoto ilikuwa ishawaingia miyoni mwao. Hata usiku ulipita siku nyingine ikaingia kama ilivyokuwa kawaida ya Sister murcia alikuwa akiamka mapema na kuanza maombi yake, siku hio hata paulo naye aliamka mapema na kuingia ndani ya Sakarastia kwa ajili ya kufanya maombi. Ndani ya sakarastia alikuwemo Sister murcia naye akifanya maombi. Walikaa mule kila mmoja akiomba maombi yake. Hatimaye saa ya kutoka ilifika, walipojaribu kuufungua malango mlango uligoma kufunguka, haukufunguka hata walipotumia nguvu mlango wa chumba kile chema ulishindikanika kufunguka.
"Bila shaka ni wakati wenyewe aliouchagua bwana, wakukitafuta kile kizazi chema kwa ajili ya kukikomboa kijiji hiki" paulo alitamka.
Baada ya kuyatamka maneno hayo mlango ulifunguka. Sister murcia akuamini akamwangalia tena paulo macho yake yakakutana na ya paulo ambaye kipindi hicho yeye alikuwa amejawa na tabasamu, waliangaliana kwa muda kama dakika tano Kisha paulo akamshika sister murcia na kuongozana naye kutoka ndani ya Sakarastia kisha inje ya kanisa na kuelekea katika chumba alichokuwa anakitumia sister murcia. Lilikuwa ni zoezi gumu sana kwao lakini ilikuwa amna jinsi iliwapaswa walifanye ili litimizwe agizo la bwana mungu wao. Baada ya kukifanya kutendo kile siku hio ndio ilikuwa ni ngumu kwao kwani hakuna hata ambaye alitamani kuwa karibu na mwenzake. Sister murcia alipomaliza kuoga alirudi chumbani kwake akakaa, paulo yeye kidogo alikuwa na ujasiri alifanya maandalizi ya chakula na kumpelekea sister chumbani kwake kisha yeye akarudi kanisani na kuendelea na maombi. Moyoni mwake paulo ilikuwa ni kukiombea kizazi kitacho zaliwa kiwe chini ya namlaka ya bwana. Paulo akusahahu kwakuwa alijua kabisa wakati wake wa kufa unamkaribia kama alivyo sema sister murcia, aliomba maombi ili ikifika siku hio apokelewe salama. Alizikumbuka dhambi zake, machozi yakiwa yanamtoka paulo aliomba sana toka mida ya asubuhi kama saa nne mpaka jioni hakuweza kula chochote alikuwa akiomba tu.
Hali hio haikuwa kwake tu Sister murcia naye alikuwa na wakati mgumu, mawazo yalikuwa hayamuishii alitambua kabisa baada ya kukifanya kitendo hicho, zimebakia siku chache tu za kuwa na paulo siku za kumtazama katika macho yake, machozi tu ndio yalikuwa yakimtoka.
"Sijui nitaishi vipi bila uwepo wake, nitaishi vipi nikimwangalia huku najua wakati wake wa kuniacha ndio huu. Muda wowote tangu sasa ataniacha. Eeeh mungu kwanini umeyaruusu haya yanikute?" Sister murcia alijisemea moyoni. kweli inauma inauma. Ni bora hata wengine wangekuwepo basi kidogo faraja ingekuwemo lakini atabaki peke yake katika kijiji hicho cha shimo la moto endapo paulo akiondoka.
ITAENDELEA.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA. HAPA HAPA NDANI YA SIMULIZI ZA HEMED. KESHO KUTWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: