SISTER MURCIA. NA HEMED MAYUGU NO. 18 ILIPOISHIA. Sijui nitaishi vipi bila uwepo wake, nitaishi vipi nikimwangalia huku najua wakati wake wa kuniacha ndio huu. Muda wowote tangu sasa ataniacha. Eeeh mungu kwanini umeyaruusu haya yanikute?" Sister murcia alijisemea moyoni. kweli inauma inauma. Ni bora hata wengine wangekuwepo basi kidogo faraja ingekuwemo lakini hatabaki peke yake katika kijiji hicho cha shimo la moto endapo paulo akiondoka. Songa nayo. Siku nzima ilikuwa ni kilio kwa sister murcia. Hata siku iliyofuata alijikaza kutoka ndani kwake kuja kanisani kusali. Kwa bahati mbaya ama nzuri kwake alimkuta paulo yumo ndani ya kanisa akiendeleza maombi. Sister Murcia alishindwa hata kufanya maombi alisimama, akalishika tumbo lake ambalo alitegemea kubeba mimba muda si mrefu, pale pale machozi yakamtoka. Kumbu kumbu zikamrejea akatoka kanisani kurudi chumbani kwake.......Baada ya sister murcia kuondoka paulo naye alitoka nyuma na kumfuata huko huko chumbani kwake. Alipofika akamkuta sister murcia amekaa kitandani machozi tu yakimtoka. "Sister Murcia tafadhali naomba usilie kwani bwana hawezi kukuacha wewe katika mateso. Si wewe tu hata mimi inaniuma tena sana tu kukuacha wewe ukiwa na kizazi changu tumboni mwako bila hata kukiona, lakini kwasababu ni agizo la bwana yanipaswa mimi nife ili huyo azaliwe na huyo atakaye zaliwa yeye ndiye atakaye kikomboa kijiji hiki. Usife moyo na kukata tamaa, usioneshe udhaifu juu ya jambo hili, imani yako itashuka....na imani ikisha shuka tu, tayari shetani anapata nafasi ya kukiingilia hata kile unachokitarajia kutunga tumboni mwako. kitashambuliwa na jeshi la shetani. Nakuomba ujipe Ujasiri twende ukasali. Mungu yu pamoja nasi hawezi kabisa kukuacha ukateseka" Paulo alisema. Baada ya kusema maneno hayo kwa ujasiri kabisa wa hali ya juu paulo alimbusu Sister murcia kwenye paji la uso kisha akamnyanyua kitandani kwake wakaongozana kurudi kanisani kwa ajili ya maombi. Mida kama ya saa mbili ndio walimaliza kuomba. Wakiwa wanatoka ndani ya kanisa kuja inje walikutana na vijana wawili mlangoni mwa kanisa. Vijana wale walikuwa ni miongoni mwa walinzi wa kijiji hicho. Si kwamba walikuwa na mapanga hapana walikuwa wao na miili yao pamoja na miguu na mikono yao huku ikiwa mitupu kabisa. Sister murcia aliogopa sana baada ya kuwaona. Paulo alikuwa tayari kaisha jipanga kwa ajili ya kuwakabiri. Hata kabla paulo hajafanya maamuzi yoyote alishangaa kuwaona vijan wale wakipiga magoti mbele yao kisha wakasema. "Sisi ni wenye dhambi tunaomba tusamehewe dhambi zetu" Hakuna aliyeamini paulo na sister Murcia kila mmoja alimgeukia mwenzake na kumwangalia kwa muda kama wa sekunde thelathini kisha paulo akaawambia vijana wale wanyanyuke kisha akawaruhusu waingie kanisani. Sister murcia alikuwa na wasiwasi nao, alishindwa kuwaamini kwani alilikumbuka tukio la Josephina na Nyamumwi ambaye mpaka kipindi hicho walikuwa tayari washakufa kwa uwezo wa nguvu za bwana. Akiwa mwenye wasiwasi alimuita paulo pembeni na kumwambia. "Paulo umesahau tukio la kutekwa kwangu, mi siwaamini tena watu hawa?" "Si kwa mamlaka yako bali kwa mamlaka ya mungu wako, je mimi ni nani kwako?" Paulo alimuuliza Sister murcia. "Wewe ni mkuu kwangu, umepewa mamlaka na nafasi kubwa moyoni mwangu. Wewe ni mume wangu" Kwa upole Sister murcia alisema. "Basi bwana kakisikiliza kilio chako, wala hutobaki kwa mateso na hii ni dalili za kweli, ya kuwa tayari kile alicho ahidi bwana kimeanza kutunga ndani ya tumbo lako" Paulo alisema. Baada ya paulo kuyasem maneno hayo, sister murcia aliliangalia tumbo lake ambalo mpaka kipindi hicho lilikuwa halioneshi kama kuna kiumbe ndani yake. Alitumia kama dakika moja kuliangalia tumbo lake machozi yakamtoka akamgeukia tena mpenzi wake akamwangalia kisha akamuuliza. "Wanitazama vipi hali yangu kwa sasa?" Swali hilo paulo alilijibu kuwa. "Moyo wako unaonekana una majeraha mengi, majeraha ambayo yanapelekea imani yako kushuka. Mtumainie bwana kwa kila jambo kwani yeye anaujua wakati ulionao" Paulo alisema maneno hayo kisha akamfuta machozi Sister murcia ambaye hata kwa kipindi hicho alisha kuwa npenzi wake kwasababu tu ya kukikamilisha kile kilicho toka kwa bwana. Baada ya Zoezi hilo alimshika wakarudi kanisani na kuanza kuzungumza na wageni wao. Vijana waliokuwa wachawi leo wamejileta wao wenyewe kutubia dhambi zao. Walizungumza nao kwa kina, nao vijana wale wakakiri kwa kina juu ya madhambi yao. "Mmesamehewa dhambi zenu, kwani mungu wetu ni mwepesi wa kusamehe madhambi yetu. Kila anaye muomba kwa imani thabiti mungu umpa kwa muda muafaka, umlinda katika wakati mgumu. Kwa mungu hakuna kinachoshindikanika" paulo alisema. Kisha akawakaribisha wale vijana kuwa nao pamoja. Siku ilikuwa ni siku ya ajabu wao waliita. Kumbe watu waliokuja kutubu dhambi zao waliongezeka hata mwenyekiti wa kijiji hicho, ambaye alikuwa mchawi mkubwa, aliongozana na Familia yake kuja kanisani kuomba kusamehewa dhambi zake. Paulo hakuamini kabisa, kumuona mchawi yule ambaye alikuwa akitisha kabisa, aliyekuwa hapendi masihara, aliyekuwa anauwa, akaifanya ardhi ya kijiji kile kama ya kwake. Kwa hakika lilikuwa ni jambo la kushangaza. Hata kabla hajafanya chochote akiwa kasimama mlangoni mzee yule alisema. "Mungu wako kaniokoa, hakika nalikumbuka tukio langu la mwezi nyuma. Nilikaa nikilitafakari sana. Nimekuwa mshirikina kwa zaidi ya miaka ishirini sikuwahi kuiona nguvu ya ajabu kama ile tena kwa maneno tu. Hakika nitasimulia na kuwafundisha watu wote duniani juu ya nguvu za mungu wako" mzee yule akiwa kabisa na familia yake ya watoto watano alipiga magoti mlangoni mwa kanisa huku machozi yakimtoka. Kila mmoja kanisani alishindwa kuamini. kwakeli lilikuwa ni tukio ambalo hakuna ambaye angelitarajia. Paulo alijinyanyua pale alipokuwa amekaa na kuwafuata watu wale na kuwambiwa. "Hakika mmesamehewa dhambi zenu, mungu wetu ni mwepesi wa kusamehe hata kama ulikuwa na dhambi kama mlima mkubwa" baada ya kusema hivyo paulo aliwambia watu wale wasimame na kuingia kanisani waungane na wenzao ili wamsome bwana mungu wao na kumjua. ***** Hatimaye siku zilienda, miezi ikakatika. Mpaka ikawa hata miezi saba tangu Sister murcia akiwa na mjamzito, bado paulo alikuwepo. Watu walizidi kuongezeka kuja na kuja katika kanisa la bwana. Kipindi hiki kijiji kile cha kichawi kilibadilika na kuwa cha kulitangaza neno la bwana kila sehemu, hakukuweko tena na kuwaponda waliokuwa wanakitangaza neno la bwana. Ingawaje wengi bado waliamini mila zao lakini kiujumla watu wale walikuwa wakilitangaza neno la bwana bila matatizo. ***** Zikiwa zimesalia kama mwezi tu kuzaliwa yule waliyekuwa wanamtarajia kuja kukikomboa kijiji hicho, hapo ndipo siku za paulo zilifika tamati, yule aliyekuwa shujaa wa kijiji hicho cha shimo la moto aliwaacha watu katika maumivu makubwa maumivu ambayo kamwe miyoni mwao haikuwa Rahisi kuyasahau. Ulikuwa ni msiba mzito. Inasemekana kuwa Sister murcia alizimia kwa wiki kwasababu ya uchungu aliokuwa nao. Kweli duniani tunapita, huo ndio ulikuwa mwisho wa mtu mwema, mwenye nguvu aliyepigania uhai wa watu wenye haki na kulipigania neno la mungu liweze kusimama na kuwabadilisha watu wa kijiji kile. Mpaka mazishi ya paulo yanaisha Sister murcia bado alikuwa amezimia. Kipindi hicho kiujumla kilikuwa ni kigumu sana kwa wanafunzi na watu wote waliokuwa katika kijiji hicho. Lakini kilichoacha mshangazo na kusitaajabisha kwa kila mmoja katika msiba wa paulo, ulitokea mng'alo wa ajabu katika jeneza lake mpaka anaenda kuzikwa bado hata kabri lake lilikuwa na mwanagaza au nuru ya pekee, nuru hio iliwatatiza wengi hata baadhi ya wachawi walijaribu kulisogelea karibu lile wakiamini kuwa watapata hata kuichukua nuru hio kiuchawi, walipigwa kwa nguvu na kuanguka huko. Inasemekana kuwa ni zaidi ya wachawi ishirini waliolisogelea kaburi lile wote walitoka pale na majeraha ambayo yalisababisha hata baadhi kufa kwa muda wa siku chache baadaye. Baada ya kifo cha paulo wanafunzi wake waliendelea kulitangaza neno la bwana kwa kushirikina na Sister murcia ambaye kwa kipindi hicho alikuwa anangoja kujifungua mtoto ambaye angekuwa mkombozi wa kijiji hicho. Itaendelea. Usikose sehemu inayofuata na ya mwisho kabisa katika hadithi hii ya kupendeza.

at 4:35 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top