SISTER MURCIA. NA. HEMED MAYUGU. NO. (19). ILIPOISHIA. Baada ya kifo cha paulo wanafunzi wake waliendelea kulitangaza neno la bwana kwa kushirikiana na Sister murcia ambaye kwa kipindi hicho alikuwa anangoja kujifungua mtoto ambaye angekuwa mkombozi wa kijiji hicho. SONGA NAYO. kijiji kiliendelea kuwa na amani, mpaka muda huo hakukuwa na dalili za kuwa kuna wachawi wanaoishi, ingawa walikuwepo lakini hawakuweza kufanya chochote. Kipindi hicho kumbe hata wao walikuwa wakifanya mipango yao. Baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho kujitoa katika kikundi hicho cha kishirikina wachawi wa pande zote mbili waliamua kuungana na kuwa kitu kimoja. Wakiwa chini ya uongozi wa padre joseph. Hapo ndipo walipoamua kujipanga upya kwa ajili ya kukifanya kijiji kile kirudi katika mikono ya kishetani. Wachawi walijipanga vya kutosha. tageti yao kubwa ilikuwa siku akizaliwa mtoto ambaye alikuwa tumboni mwa sister murcia ndio na wao walianzieshe. Kwa imani zao waliamini kabisa kuzaliwa kwa mtoto huyo, ambaye hata wao tayari walikuwa washapata taarifa kuwa ndiye atakaye kikomboa kabisa kijiji hicho na kuwa kijiji cha kumtumikia bwana, hapo walijua siku akizaliwa watu wote watakuwa wazubaifu na kujisahau kisha watawafanyia mbinu zao za kichawi. Safari yao ya maandalizi ilianza, kwakuwa walikuwa wanajua kabisa hata mwezi hutoisha Sister Murcia atajifungua mtoto huyo, wachawi walianza kujichomeka katika kundi la watu waliokuwa wanamtumikia bwana. Walifanya hivyo kwa taratibu kabisa bila kugundulika, hata watu wiliokuwa wanawaona waliamini ni miongoni mwao, kwani tayari watu walikuwa washaokoka na kumtumikia bwana mungu wao walikuwa ni zaidi ya mia tatu. Hao ni wale ambao walikuwa wakilitumikia kanisa la bwana. Mamia mengine ya watu bado yaliendelea kuamini katika ushirikina, wakiamini kabisa kuwa bila uchawi na miungu yao maisha hayawezi kwenda, mizimu itawaangamiza. Mpaka zinasalia kama siku mbili Sister murcia kujifungua wachawi zaidi ya amsini walikuwa waisha jichomeka katika watu wa mungu. ***** Siku iliyokuwa imengojwa kwa hamu siku ya kumpokea mtoto wa kiume ambaye ameandikwa kwenye kitabu kuwa yapaswa azaliwe kwa ajili ya kukikomboa kijiji cha Shimo la moto ilifika. Usiku mida ya saa saba Sister Murcia alijisikia mabadiliko mwilini mwake. Alikuwa akisikia maumivu makubwa mwilini mwake, maumivu ambayo hakuwahi kuyasikia, alikuwa kalishikilia tumbo lake huku akiihemea juu juu na miguno ya maumivu ikiwa imkatiki. Kwa bahati mbaya kwenye chumba chake alikuwa amelala peke yake. Toka kupotea kwa wanafunzi wake wa mwanzo wa kike sister murcia aligoma kabisa kulala na watu chumbani kwake. Kwa kujing'ang'aniza alitoka inje na kwenda kwenye nyumba nyingine kubwa iliyojengwa kwa ajili ya wageni na watumishi wengine wa kanisa. Ndani ya nyumba hio walikuwemo watumishi wa kike na wakiume tofauti iliyokuwa ikiwatenganisha vilikuwa ni vyumba. Baada ya kugonga mlango, mlango ulifunguliwa. Mtu wa kwanza kuufungua mlango alikuwa bint mzuuri, bint huyo baada ya kuufungua mlango na kuiona hali ya Sister murcia, aligundua kuwa ndio wakati ambao waliungoja. Bila kuchelewa bint yule aligeuka huku na kule kuangalia kama kuna mtu. Alipoona kuwa hakuna mtu, bint yule aliurudisha mlango na kumwambia sister murcia Waongozane kurudi chumbani kwake. Kwa kujikaza huku bint huyo akimsaidia, sister Murcia alikubali kurudi chumbani kwake. Akiwa anaomba kabisa kimoyo moyo baada ya kufikishwa chumbani kwake Sister murcia alikarishwa chini yule bint akamwambia. "Ndio wakati wenyewe sasa, unaenda kujifungua, kwahio jikaze na kusukuma kwa nguvu ili upate kujifungua. Lakini ghafura ndani ya muda mfupi upepo mkari uliokuwa umeambatana na kimbunga ulivuma. Upepo huo ulisababisha hata madilisha ya chumba cha Sister murcia kufunguka. Bint yule kwa kujifanya kuwa naye anashangaa aliisogelea Switch ya taa yao ya sorah na kuizima. Ndani ya chumba lilibaki giza nene limetanda. Sister murcia alijaribu kuomba msaada taa iwashwe bila mafanikio hakajikaza kuelekea ilikokuwa taa ili awashe, kabla hajafanya chochote alishitushwa na mianga mingi ya mishumaa imetanda, tena yumo ndani ya poli kubwa, poli ambalo lilikuwa linepakana na msitu wa kutisha wa kutolea kafara. Yeye akiwa katikati huku kundi kubwa la watu zaidi ya mia mbili likiwa limemzunguka. Sister murcia aliogopa sana, kilichokuwa kimebaki kwake ni imani yake tu kumkomboa. Alijitahidi kuomba labda mungu wake angeweza kumtoa katikati ya kundi hilo lakini haikuwezekana. Muda huo uchungu uliongezeka sana. Wachawi walipoona hivyo wakacheka sana, kisha mkuu wao akasimama, akawatolea salamu yao ya kichawi kisha akasema. "Yule aliyekuwa akingojwa kwa hamu tunaye. Bila shaka atakuwa miongoni mwetu wala hatokuwa upande wa mungu wao" Mchawi yule alisema, huyo ndiye alikuwa padre joseph. Padre ambaye sister murcia alisimuliwa habari zake na Murcia wa kwanza. "Tunangoja kula nyama ya mama na mtoto. Wote wawili inasemekana kuwa ni watu wa bwana mungu wao, lakini sisi ni wakubwa na tunanguvu nyingi kuliko hata huyo mungu wao, ndio maana kashindwa kuwaokoa kutoka katika mikono yetu" Padre joseph aliendelea kuropoka. Wachawi wenzake walikuwa wakimshangilia sana na vigerere kwa juu. Kumbe muda huo Sister Murcia alikuwa anajisukuma kujifungua. Wachawi wakiwa wanapiga makelele walishitukia kelele za mtoto akilia. Lakini walipo tazama hawakuona kitu, hakukuwa mtoto wala sister murcia, zaidi walikuwa wakisiki kelele za mtoto tu akilia. Ghafra bado wakiwa wanashangaa ulizuka tena upepo mkali pale pale ikatokea kitu kama ukuta umewazunguka, hapo ndipo wachawi walijawa na uhoga wa ajabu, akuna aliyejiamini kwa uchawi wake, hata padre joseph naye alitafuta njia ya kutokea lakini hakuiona. Kila walipokuwa wanajaribu kukimbilia walikutana na ukuta huo. Bado wakiwa wanaangaika, ilitokea nuru kama taa iliyokuwa ikimulika alipokuwa Sister murcia na mwanaye, akiwa kampakata mwanaye kwenye miguu yake huku akimwangalia kwa furaha ya ajabu, wachawi nao walibaki kushangaa. "Imekuwa vipi ndani ya dakika mbili mtoto kazaliwa kawa mchangamfu" kila mchawi aliyekuwa anaona kitendo kile alikuwa anajiuliza hivyo hivyo, ilikuwa ni ajabu kubwa sana kwao. Si kawaida hata kwa maisha ya kawaida haijawahi kutokea. Kweli mtoto yule alionekana kama ni mtoto wa miezi saba. Jinsi alivyokuwa anafanya fanya mikono yake huku yupo mapajani mwa mama yake. Ni muda huo huo wachawi wale wakiwa wanashangaa kitendo kile ilisikika sauti ikiwasemesha. "Hakika ufalme wa bwana utukuzwe, mbinguni na Duniani. Huu ni uthibitisho tosha kwenu nyinyi wanadamu mliokuwa na imani haba kuwa bwana mungu wenu yupo na anafanya kazi usiku na mchana. Hakuna mwenye nguvu wala mwenye mamlaka kama si yeye. Basi yapaswa kumtukuza yeye na kufuata mamlisho yake mpaka pale atakapo uchukua uhai wako" Maneno hayo yalikuwa ya sauti ambayo ilikuwa ikisikika kwa wachawi wale. Kwakuwa wao walikuwa hawajui lakini yule alikuwa ni malaika mwema wa bwana. Muda huo tayari padre mchafu, ambaye aliyatumia mamlaka ya bwana kwa ubaya alikuwa kaisha kufa. Japo Sauti ile walikuwa wakiiogopa lakini wachawi walijikaza na kusogea alipokuwa Sister Murcia na mtoto wake ili kumshika. Mpaka muda huo kila aliyekuwepo pale aliamini kabisa kuwa uchawi si chochote mbele za mungu. Baada ya kuona wachawi wale wakimsogelea sister Murcia alisimama ilikuwa kama vile anajua nini kinaenda kutokea kwa muda huo. Bila fujo wachawi wale walijikuta wanapanga mstari wao na kuanza mmoja mmoja akimsogelea Sister Murcia pale alipokuwa na kumshika mtoto yule mkono, kisha wanainamisha vichwa vyao chini kuonesha ishara ya Eshima na kuondoka. Uwezi amini mpenzi msomaji kila watu walivyokuwa wanaongezeka kumsogelea, mtoto yule alikuwa akitabasamu, kisha akaanza kuwapa mkono yeye mwenyewe hata alikuwa angoji kuguswa. Hayo ndiyo yalikuwa maajabu ya siku hio mpaka usiku kucha. ****** Kanisani watu, walipoamka walifanya kama kawaida yao, wenye kuingia kanisani na kusali walifanya hivyo. Wengine walikuwa wanaendelea na Shughuri zingine. Lakini nao pia walianza kushikwa na wasiwasi baada ya kutomuona Sister Murcia. Hio ilikuwa ni mida kama ya saa mbili asubuhi. "Jamani sister murcia mbona haonekani au kachukuliwa na wachawi?" Kijana mmoja aliuliza. Bado wakiwa wanajiuliza walishangaa kuona kundi kubwa la watu kuzidi hata wale ambao tayari, walikuwa washabadilika na kumfuata bwana mungu wao. Kwakuwa kundi lile la watu lilikuwa limevaa mavazi ya kichawi chawi. Moja kwa moja watu kanisani wakajua wanavamiwa, waliokuwepo wote wakakimbilia mapanga yao tayari kwa kupambana. Bila kutegemea watu wote kanisani walistaajabu baada ya kumuona Sister murcia kabebwa juu mfano wa watu wa pwani kwa machifu wao. Hali hio iliwafanya kujua kabisa kuwa mkombozi waliyekuwa wakimngoja kaisha zaliwa. Nao pia waliamua kwenda kuwapokea watu wale. Toka muda huo kijiji kizima cha zima moto kilizizima kwa kufurika watu katika viwanja vya kanisa lao, lengo kumtazama mwana aliye zaliwa. Huo ndio ulikuwa ukombozi wa watu wale. Baada ya mwezi mmoja tangu Kujifungua Sister murcia naye alifariki na kumwacha mtoto wake ambaye bado alikuwa mchanga katika mikono salama ya watu wa kanisani. Mtoto yule alilelewa lakini alikuwa wa ajabu. Kiujumla alikuwa mtenda miujiza, wagonjwa waliokuwa na imani ya bwana mungu wao, waliweza kupona kwa kushika mikono yake. Toka hapo kijiji cha shimo la moto kiligeuka kikawa shamba la Mungu. Mwisho. Mwisho wa hadithi hii ni sawa na mwanzo wa hadithi nyingine. Naomba share nyingi hizo zitanipa hamasa ya kuiandaa hadith nzuri ya TAIFA LA MOYO WA SHETANI.

at 4:35 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top