SISTER MURCIA, Na; Hemed mayugu, No: 015. ILIPOISHIA. Baada ya kumaliza kazi hio alikata majani ya miti ndani ya msitu huo akausitiri mwili wa Mercia. Sasa swali likabaki. "Wengine wako wapi? au nao washauliwa?" Paulo alijiuliza. Hapana lazima wapo, nitawapata wapo. Pale pale mwanaume alipiga tena kelele nyingine kwa hasira. "Nitawapataaaaaaa!" Kisha akaiyazisha safari kuelekea sehemu ya pango la kafara. SONGA NAYO. Paulo mwanaume wa shoka alitoka mbio kuelekea pango la kafara, kwakuwa haikuwa mbali kweli alipafikia. Baada ya kufika alishituka kuuona mwili wa Alicia uko mtupu halafu umejaa Majeraha kila mahara. "Hapana!..Hapana!...nasema hapanaaaaa! Ilimuuma Paulo ilimuuma sana tena sana. Kwa kujiamini aliusogelea mwili wa Alicia ili auone kama bado yu hai. Akiwa bado anausogelea alipigwa tena na kitu kizito kichwani akaanguka chini. Kipigo hicho kilikuwa kama kimempuliza tu akaanguka hata maumivu Hakuyasikia. Mwanaume akanyanyuka kutoka chini hata bila kutazama ni nani aliye mpiga kisha akasema. " Bwana yu nami, hakika yeye ndiye mwenye mamlaka juu yangu, na kila kitu hutoka kwake yeye aliyemkuu kwetu na ndiye tegemezi langu" baada ya kusema maneno hayo tu aligeuka nyuma. Paulo alistaajabu sana baada ya kugeuka alimkuta Nyamumwi pamoja na Josephina wako kama wameganda huku mikono yao imeunuka juu kama walitaka kumpiga, kwake aliona ni tukio la Ajabu sana. Baada ya kuona hivyo akasema. "Hakika wewe ndiye tumaini langu, wewe ni njia ya uongofu. Nashukuru kwa ulinzi wako juu yangu kwa mashetani hawa, Amina" Alipomaliza kuyasema akainama chini na kuushika mwili wa Alicia, kwakweli hali aliyokuwa nayo Alicia, ulimuumiza sana Paulo. Tayari Alicia naye alikuwa kaisha fariki. Pale pale aliinua mikono yake juu akasema. "Hili ni janga lingine la jeraha kwangu, Eee mungu niepushie hili tena niweze kuwapata hata waliosalia. Usinipe maumivu makubwa mengine moyoni mwangu wewe uliyetegemezi la moyo wangu, amiina" paulo alisema. Kisha akalichukua likitambaa jeusi lilikuwa limepambwa maeneo hayo ya kichawi na kuufunika mwili wa Alicia kisha akaubeba na kuondoka maeneo hayo na kuwaacha wachawi wawili Josephina na Nyamumwi wakiwa wameganda kama wamepigwa Shoti. Hakiwa anatembea huku kaubebea mwili wa Alicia hasira zilimpanda akajikuta anapiga kelele kubwa za kuita jina la Sister Murcia. "Murciaaaaaaaaa! Murciaaaaaaaaa! Murciaaaaaaaaa!" Sauti yake ilijirudia mala tatu. Msitu mzima ukaitika kama alivyo kuwa anasema. Kilichokuwa kinasubiliwa ni majibu ya Msitu huo tu basi, baada ya kulitaja jina hilo Paulo aliisi maumivu makubwa sana moyoni, akaushusha mwili wa Alicia chini kisha akasimama ili kwenda kumtafuta Sister Murcia. Hakiwa anageuka nyuma hakuamini macho yake, baada ya kukutana na Uso wa Sister Murcia akimwangalia kwa hofu huku akihema kwa nguvu, Paulo alishindwa kuvumilia akageuka tena nyuma kuficha macho yake ili asimwangalie Sister Murcia. Aliona haibu kubwa kwani kipindi hicho Sister Murcia alikuwa kama Alivyo zaliwa wala hakuwa hata na nguo yoyote mwilini mwake na haikujulikana amefika vipi alipokuwa amesimama. Kila mmoja Aliona haibu kwa mwenzake hata Sister Murcia naye aligeuka nyuma baada ya kujigundua kuwa yuko mtupu ndani ya msitu tena mbele yake hakiwepo Mwanafunzi wake. Kila mtu akiwa kamtegea mwenzake mgongo Paulo alijiangalia mwilini mwake, amevaa nguo ngapi kwa bahati mbaya alikuwa na Suruali moja, kifuani nguo tayari ulikuwa ishatatuliwa imebaki madaso. Alitamani alitoe likitambaa alilokuwa kaufunikia mwili wa Alicia ampe sister Murcia ajifunge ilimradi astiri mwili wake ili wasiendelee kuangaliana katika hali ya kuogopana. Kulikuwa hakuna namna Paulo alilishika panga lake na kuyakata jamani mengi kisha kwa ushujaa tu akamsogelea Sister Murcia na kumfunga nayo. Hata sister Murcia alishindwa kukataa kwasababu kulikuwa hamna jinsi. Walipolimaliza zoezi hilo, Paulo aliubeba tena mwili wa Alicia hivyo hivyo wote wakiwa na maumivu mpaka sehemu alikokuwa ameuwacha mwili wa Mercia. Sister Murcia hakuamini baada ya kuwaona wanafunzi wake wakike wote wameisha kufa. Alilia sana ndani ya Msitu huo akashindwa kabisa kuamini kama ni kweli. Alilia mpaka akawa anauliza mala mbili mbili kama ni kweli. Paulo yeye machozi tu ndio yalikuwa yakimtoka. Ilimchukua kama nusu Saa sister Murcia kuwalilia wanafunzi wake, Paulo alimuinua na kummtoa eneo hilo. Kilichofuata kilikuwa ni kutoka ndani ya Msitu huo. Walitembea kwa majonzi hivyo hivyo huku wote kwa pamoja wamechoka, kabisa mpaka inje ya msitu. Matumaini ya kuwatafuta Lucas na Morise yalififia Ghafra. Wakiwa inje ya msitu huo wa kutisha sister Murcia alianguka chini na kupoteza fahamu. Paulo alimbeba na kuanza kutembea naye kurudi kanisani. Njiani kote kulikuwa kimya kabisa wala hapakuwa na mtu wala mchawi aliyejitokeza mbele yao. Ilimchukua kama dakika arobaini na tano Paulo akawa amefika ndani ya kanisa. ***** Kanisani Paulo alipakuta kimya kabisa hata hapakuwa na mtu Ambaye alijitokeza hata kuwabuguzi wala wakuongea naye. Kwakuwa alikuwa kamfunga Sister Murcia kwa majani ambayo nayo yalikuwa yashaanza kunyauka aliingia kwenye chumba walichokuwa wanalala wanawake akafikia kitandani akachukua shuka na kurudi kanisani alipokuwa kamuweka sister Murcia na kumfunika shuka. Tayari muda ulikuwa ushaenda sana, ilikuwa kama ni saa tano na nusu za asubuhi. Akiwa anawaza afanye nini kumsaidia Sister Murcia, wazo lilimuijia kuwa lazima itakuwa ni njaa inayomsumbua sister Murcia. Pale pale alijinyanyua akaelekea kwenye chumba walichokuwa wanalala wao, akachukua maji mengi kwenye jagi kisha akarudi kanisani kwa Sister Murcia. Baada ya kufika alimwagia maji kichwani kuona kama ataamka au kushituka. Kweli kama alivyokuwa anawaza, Sister Murcia alitikisa kichwa chake na kuyafumbua macho yake. ingawaje bado alionekana kuwa ni mchovu Paulo alijiskia kidogo nafuu kumuona sister akifumbua macho. Paulo alimnywesha Murcia maji kidogo hili kumuongeza nguvu. Baada ya kinywa maji Yale Sister Murcia aliweza kijinyanyua na kukaa. "Sister unajisikiaje?" Paulo aliuliza. Sister Murcia alikuwa akimwangalia tu Paulo usoni hakuweza hata kulijibu swali aliloulizwa. "Sister Murcia unajisikiaje sasa hivi?" Paulo aliuliza tena. Lakini bado sister Murcia alimwangalia tu bila kumjibu. Bado sister Murcia akiwa anamwangalia mwanafunzi wake aliyekuwa anampenda kuliko wote, machozi yalianza kumtoka. Akajiangalia akakuta kafunikwa shuka halafu ndani kavaa majani ya miti. Sister Murcia aliomba tu Paulo amsaidie kumshika ili asiamame. Paulo naye hakuweza kusita alifanya kama alivyo agizwa. Baada ya kusimama sister Murcia alimwambia Paulo kuwa anaisi uchovu sana anaomba amsaidie maji akaoge. Paulo alitoka mbio ndani ya kanisa akachukua chombo cha kutekea maji ya kuoga, mbio mpaka kisimani na kuteka maji kisha akayapeleka Bafuni akaweka na Sabuni kisha akarudi na kumwambia sister Murcia kuwa tayari kila kitu. Sister Murcia alijikaza kwa kujivuta vuta mpaka bafuni akajimwagia maji. Haikuchukua muda hakawa ametoka huku kajifunga Shuka lake akaelekea chumbani kwake, akavaa nguo nzuri kisha akarudi kanisani. Paulo naye alikuwa mule mule kanisani hakiwa hana habari mawazo yake yakiwa mbali, alishituka kusikia sauti ya Sister murcia akimsemesha. "Paulo wewe husikii njaa?" "Aaaah! Hivi kweli kuna kula, kweli nahisi njaa sana" Paulo alisema huku akishika shika tumbo lake. Majonzi waliyokuwa nayo tayari kwa muda mfupi yalikuwa yashaanza kufutika miyoni mwao. Mpaka kipindi hicho hakuna Ambaye alikumbuka kama Moris na Lucas bado hawajapatikana. Muda wote huo Paulo alikuwa na nguo zile zile, shati lililokuwa limechanika chanika na Suruali yake ambayo pia tayari ilikuwa na Majeraha madogo. Baada ya kujibiwa hivyo sister Murcia alicheka. "Kwani wewe husikii njaa?" Paulo naye aliuliza. "Natamani sana chakula hicho kwasababu lazima kiwe cha kwangu nami pia niwe cha kwake" Murcia alisema. Maneno hayo Paulo hakuyaelewa, alibaki kumwangalia mwalimu wake Ambaye kipindi hicho alikuwa akitabasamu huku akimwangalia yeye usoni. "Najua njaa ipo basi ngoja nikatafute chakula?" "Wapi Paulo utakipata chakula?" "Usijali nitakipata tu" Paulo alisema. Kisha akachukua panga na ngao yake vyote vya ajabu na kutoka mbio kuelekea alikokuwa anaamini angepata chakula. ITAENDELEA. Ni kweli Paulo atakipata chakula? Usikose sehemu nzuri ya hadithi hii. siku ya Jumanne.

at 4:34 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top