SISTER MURCIA, Na. Hemed mayugu, NO. 014. ILIPOISHIA. Alichokiona kwenye maono ya ndoto kilikuwa cha kweli. watu wa kijiji kile walikuwa wakishangilia na kupiga vigelele. Bado Paulo hakuamini akaamua akisogelee kijiji kile vizuri aone. kila hatua aliyokuwa akiipiga tena akikimbia kwa kasi ndipo nguvu ziliongezeka kwake. Hata njaa ya siku mbili yeye alikuwa aisikii kabisa. Songa nayo. Paulo alikimbia mpaka karibu na nyumba za wanakijiji, akaona vizuri walivyokuwa wanacheza, kwa hasira alitoka mbio kuelekea msituni wanakotelea watu kafara zao, alijua tu tayari Sister Murcia kaisha kamatwa kama si yeye basi ni Alicia kwani toka mwanzo walikuwa wamemuahidi kuwa Alicia atatolewa kafara siku zikifika. Alikuwa mbio zisizo za kawaida. Upanga wake pamoja na ngao yake akiwa navyo mikononi alikimbia mpaka karibu na msitu ambao huwa wanatolea kafara wachawi wa kijiji hicho cha kichawi. Kabla ajaingia ndani alisimama, kisha akapiga magoti, kisha akasema. "Eee mungu, hakika wewe ndiye tumaini la kila mwanadamu, wewe ndiye ngao ya kweli ndani ya nyoyo zetu, wewe ndiye ulinzi na ukombozi wa milele wa maisha yetu. Nilinde Mimi, nioneshe wapi panafaa kuanzia na wapi panafaa kimalizia, nipe nguvu za kukishinda kikosi hiki cha shetani. Amina" baada ya kumaliza kuyasema maneno hayo, ambayo yalikuwa ni maombi kwa bwana mungu wake, alisimama. Akavishika tena vifaa vyake vya kazi. Ni muda huo huo alikuwa kama anasubuliwa amalize kusali, kilitokea kikosi cha kutisha maeneo hayo, kikosi hicho kilikuwa cha vijana wa kichawi, vijana waliokuwa wamevalia mailizi mazito mashingoni mwao, nao pia wakiwa na mapanga yao. Paulo hakuogopa wala kutetereka yeye alivishika vifaa vyake kwa nguvu na kuwasogelea vijana wale ambao walikuwa wamesimama mbele yake. Alichokifanya aliinua panga lake juu. panga lile alilokuwa la ajabu lilitoa miale ya mwanga kama ya jua, kisha likabadilika likawa la moto. Kilichofuata pale hata wale vijana wa kichawi walianza kuogopa kumsogelea. Paulo akulijali hilo aliona kama wanamchelewesha, alitoka mbio huku akipiga kelele za hasira huku kaliweka panga lake la moto tayari kwa ajili ya kukata kichwa cha mtu Ambaye angejitanguliza kimbelembele. Bado vijana wale wa kichawi wakijiuliza wafanye nini, walishangaa vichwa vya wenzao watatu vipo chini, tena Paulo akijiandaa kumkata mwingine wa nne, wote kwa pamoja walikuwa waoga Ghafra na kutoweka maeneo hayo. Baada ya tukio hilo Paulo mwenyewe alijishangaa nguvu zote zile zimetoka wapi? Hata matukio aliyokuwa akiyafanya alishindwa kutambua kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiyafanya. "Bila shaka nguvu ya bwana iko nami" Paulo alisema pale pale akainza safari ya kuingia msituni. Msitu wa ajabu msitu ambao umemlea, ukamfundisha taratibu zote za kishirikina. Kwa ushujaa aliokuwa nao ndani ya kikosi cha wachawi hapo kabla, ukasababisha apewe uongozi wa kikosi cha kudumisha ulinzi wa kijiji kwa wageni wanaoingia ndani ya kijiji hicho. Akiwa ndani ya msitu Paulo alikuwa anatembea huku akilitaja jina la bwana, kimoyo moyo alikuwa akimuomba mungu amsaidie haweze kutoka salama ndani ya msitu huo wa kutisha. Yeye mwenyewe alikuwa anaujua maajabu yake. Akiwa anatembea huku akigeuka geuka kuangalia kila upande ndani ya msitu huo wa kichawi mala lilitanda Giza nene, Giza ambalo alikuwa haoni mbele wala nyuma. Akiwa bado anastaajabu hicho alishituswa na Sauti ya Mtu ikimsemesha. "Nashukuru kwa kurudi nyumbani ingawa si kwenu tena" sauti hio haikuwa ya mwingine Bali ilikuwa ya kiongozi wa wachawi wa kijiji cha Shimo la moto, kiongozi wa upande wa Mashariki akina nyamumwi, Ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kijiji hicho. Kitendo cha kuisikia sauti hio Paulo alijiweka tayari kwa mapambano ingawa alikuwa amuoni Adui yake. Akiwa bado anageuka gauka kuangalia alishangaa tu anapigwa na kitu kizito ambacho hata yeye alishindwa kukitambua ni nini, kipigo hicho kizito kabisa kilimpeleka Paulo chini moja kwa moja. Richa ya kuanguka chini mwanaume alijikusanya tena na panga lake mkononi akasimama tena. Kama vile kulikuwa na maneno yanamuongoza, alizungusha panga lake kwa nguvu upande wa nyuma, kilicho sikika ni sauti ya kilio cha mtu. Hakuishia hapo alilinyoosha panga lake juu kisha likatoa mwanga mkali; mwanga ambao ulisababisha ndani ya msitu huo kuwe kweupe nakusababisha kila kitu kionekane. Kumbe ndani ya msitu hakukuwa na mtu mmoja kilikuwa ni kikosi cha vijana wale wale waliopotea baada ya kushindwa vita ya mala ya kwanza. Kipindi hichi hata wale vijana walionesha okomavu, wakayashika mapanga yao kwa ajili ya kupambana na Paulo. Wote kwa pamoja walimsogelea kwa kasi ili kumvaa. Paulo aliliona akainama chini huku kainua ngao yake juu, kilichofuata ni vijana wale kuanguka chini huku wakipiga makelele ya maumivu, huku miguu yao ikiwa vibutu tayari ishakatwa. Zoezi hilo lilimchukua kama dakika tatu tu kwa uwezo wa bwana akawa amelimaliza. Alipolimaliza zoezi hilo Paulo alimtafuta mkuu wa wachawi wa kijiji hicho hakumuona, kumbe tayari hakuwepo. Kwa mwendo wa tahadhali Paulo aliendelea kusogelea upande liliko panga la siri la kutolea kafara ya kijiji kwa mungu wao ili kuwaokoa watu wake. ***** Ulikuwa ni umbali kama mita amsini kutoka liliko pango la kutolea kafara, Paulo kwa tahadhali na umakini wa hali ya juu huku matumaini yake yakiwa kwa bwana, mapigo ya moyo yalimlipuka baada ya kumkuta Mercia yupo amefungwa kamba kwenye mikono na miguu yuku chini akiwa kama alivyo zaliwa. Kamba zile zilikuwa zimekaa kila moja upande wake, ikiwa kama vile anataka kuvutwa kila kipande cha mguu na mkono upande wake. Kitendo hicho Paulo ilikijua kabisa kuwa ni kawaida ya watu wa kijiji hicho. Kwa hasira akijua kabisa Mercia bado mzima alikimbia kuziwai kamba kabla azijavutwa kumgawanyisha Mercia vipande vinne. Ilikuwa kama anangojewa yeye ili wamchane vipande vipande yeye akiona. Kabla hata hajazifikia kamba zile zote kwa pamoja zilivutika ili kumchana Mercia vipande vinne. Kwa bahati nzuri aliwahi akafanikiwa kuzikata kamba zote nne hata kabla azijaleta madhara kwenye mwili wa Mercia. Richa ya kumuokoa Bint yule mwanafunzi mwenzake lakini tayari alikuwa kaisha fariki, hakuwa tena Mercia Ambaye alikuwa amemzoea ulikuwa mwili wa Mercia. Ilimuuma sana paulo kumpoteza mwanafunzi mwenzake Ambaye alikuwa akifundishwa naye mafundisho mema ya kumjua na kumtumikia bwana. Hata matumaini ya kumpata sister Murcia akiwa mzima yalififia, akachoka na kuchoka. Akiwa pale pale chini huku kapiga magoti, kichwa cha Mercia kikiwa viganjani mwake juu ya malaja yake, machozi yamkitoka, kilitokea kipepeo kikatua kwenye mkono wake wa kulia, kitendo cha kukiona kipepeo kile kilichokuwa na langi nyeupe, Paulo akayakumbuka maono ya ndoto kuwa kijiji cha Shimo la moto kitakombolewa na Mtoto mwema kutoka katika kizazi cha watu wema. Yaani Baba mwema na mama mwema, kitendo hicho kilimrudisha Paulo katika hamasa na nguvu za ajabu, akasimama kisha akapiga kelele zisizo za kawaida; kelele ambazo hata msitu nao uliitikia wito kwa nguvu, kisha ukatulia tulii tayari kwa kuzipokea taarifa za kilichokuwa kinafuata. Akiwa hapo hapo kikosi kingine kilitokea, kikosi hicho alikuwa anakijua vizuri, kilikuwa ni kikosi maalumu kwa ajili ya kubaka na kukata sehemu za siri kwa wanaume na ndicho hicho hicho kilicho kuwa kinataka kuuchana mwili wa Mercia. Kwa kipindi hicho watu wale wangejua basi wasingejisumbua hata kumsogelea Paulo. Mwanaume alikuwa kaisha vimba kwa uchungu wa hasira, hasira ambazo hata mate yake tu ya kinywa yalikuwa yashakuwa sumu hatari sana. Kwa hesabu ya haraka haraka kikosi hicho kilikuwa cha vijana au vidume kama kumi na sita. Kwani unajua hata kikosi kizima kilivyo kwisha, vichwa tu ndivyo vilivyokuwa vinadundadunda chini kama mpila umekoswa wa kuupiga. "Nguvu ya Bwana ipo nami" Paulo alisema tena. Mwanaume kila alipokuwa analisema neno hilo alijiisi kama ndiye mwanaume mwenye nguvu na uwezo wa kupigana kuliko wote Duniani. Na haikuwa uongo kweli nguvu ya Bwana ilikuwa naye. Baada ya kumaliza kazi hio alikata majani ya miti ndani ya msitu huo akausitiri mwili wa Mercia. Sasa swali likabaki. "Wengine wako wapi? au nao washauliwa?" Paulo alijiuliza. Hapana lazima wapo, nitawapata wapo. Pale pale mwanaume alipiga tena kelele nyingine kwa hasira. "Nitawapataaaaaaa!" Kisha akaiyazisha safari kuelekea sehemu ya pango la kafara. ITAENDELEA. ni kweli Paulo atawapata wengine? Itakuwaje, au maono hayatatimia ya kukikomboa kijiji cha Shimo la moto? Tukutane ijumatano ndugu zangu hapa hapa ndani ya SIMULIZI ZA HEMED. SHARE NA SHARE UWEZAVYO.

at 4:34 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top