SISTER MURCIA, NA HEMED MAYUGU, NO (013). ILIPOISHIA. Lucas alijitahidi kukimbia kurudi ndani ya kanisa akizani labda kuna kupona lakini napo haikusaidia kikundi kile cha wachawi wawili, kilimtokea huko huko. Bila Kupoteza muda, Josephina alimpiga pigo moja Lucas naye akazimika kisha wakatoweka naye pomoja na Mercia. SONGA NAYO. Bado ilikuwa ni mapema sana za asubuhi. Baada ya Mercia na Lucas kuchukuliwa na kikundi kile cha wachawi yaani Nyamumwi na Josephina. Sister Murcia alikuwa ndani ya msitu mkubwa uliokuwemo ndani yake pango kubwa. muda huo alikuwa ajitambui kabisa, alikuwa amelala kama maiti. Ni muda huo huo sister Murcia akiwa amelala hapo hapo, kilitokea kikundi cha vijana wengine saba wakiwa na mwanamke mmoja mzee, Bibi kabisa, Ambaye alikuwa akiwaongoza vijana wale. Lakini vijana wale hawakuwa peke yao Bali walikuwa wamebeba mwili wa mtu uliokuwa umefunikwa kwa likitambaa jeusi, nao pia wakiusogeza Mahara alipokuwa amelala sister Murcia. Vijana wale walisimama pale pale alipokuwa amelala Sister Murcia, kisha yule Bibi akawaambia wauweke mwili waliokuwa wameubeba pale pale chini mkabala na alipokuwa amelala sister Murcia, baada ya kuuweka mwili huo, Bibi yule alikiondoa kitambaa kile cheusi walichokuwa wameufunikia mwili ule. La hasha! Kumbe mwili ule haukuwa wa mwingine, bali ulikuwa wa Alicia, mwili wa Alicia ulikuwa ujastiliwa hata chembe ya nguo, ulikuwa mtupu kama alivyo zaliwa, mwli mzima ulitapakaa Damu; mwili huo ulikuwa ukionekana kama umechanjwa na visu. baada ya kufanya Yale yote, Bibi yule aliwaamrisha vijana wake wauvue mwili wa sister Murcia nguo alizokuwa kazivaa. Bila kuchelewa walimvua nguo zake. Walipomvua nguo zake bibi yule mchawi alichukua fimbo yake kisha akauchapa mwili wa Sister Murcia mala tatu, yote hayo yalikuwa yakifanyika Sister Murcia alikuwa ajitambui kabisa. Alikuwa kama maiti aliyekuwa anangoja kuoshwa akafanyiwe maziko. Bibi yule akuishia kuupiga mwili wa Sister Murcia Bakora, aliendelea na jambo lingine la ajabu. Alichukua Dawa nyeusi kabisa iliyokuwa kwenye ungo ulio kuwa eneo hilo na kuanza kuimimina kuuzunguka mwili wa Sister Murcia. Bibi aliiuzunguka mwili pia mala tatu. Baada ya kulimaliza zoezi lake, Sister Murcia aliamka mwenyewe mzima mzima. Alikuwa ajielewi bado alikuwa Zezeta tena zezeta. Baada ya kuamka bibi yule alikuwa akimfanya alivyojisikia kumfanya. "Sasa Mimi Naondoka naombeni mkamfanye kama ambavyo huwa tunafanya, kisha mkamtupe kwenye kiota cha joka" Bibi yule alisema. Destuli ya kijiji hicho wanawake walikuwa wakibakwa na wanaume walikuwa wakikatwa sehemu zao za siri kisha nao wanatupwa. Zoezi lililokuwa linaenda kufanyika kwa Sister Murcia lilikuwa ni zoezi la kubwakwa. Bibi yule mchawi aliondoka na kuwaacha vijana wale pamoja na Sister Murcia, akiwa mtupu vile vile hata atambui kama yupo mtupu. Kwani mpaka muda huo alikuwa ni zezeta. Baada ya yule Bibi kutoweka tu, wale vijana wakaanza kumuongoza sister Murcia kutoka karibu na pango lile na kuelekea mahara walipokuwa wanapataka wao. Yote hayo alikuwa yanafanyika ndani ya msistu huo huo. Vijana pamoja na Sister Murcia waliondoka na kuuwacha mwili wa Alicia uko pale chini ujitambui. ***** Ni muda huo huo, ndani ya Sakarastia, Paulo alikuwa akiota ndoto kama maono ya kwamba kijiji cha Shimo la moto kinapata ukombozi Mkubwa na ukombozi huo mkubwa unafanywa na mtoto mdogo yapata miaka kumi mpaka kumi na miwili. Ndoto au maono hayo hayakuishia hapo, bali yalimpeleka mpaka akaona watu wa kijiji hicho wakiruka ruka kwa Shangwe huku wakicheza ngoma zao za Asiri, ngoma za kichawi, ngoma ambazo zikichezwa ujue ndani ya kijiji hicho kuna jambo zito, jambo la kumtolea mungu wao zawadi tena zawaidi yenyewe ni mwanamke Bikra kabisa. Baada ya maono hayo Paulo alishituka akashindwa kutambua ndoto zile mbili zilimaanisha nini. Akaanza kuitafakari ndoto ya kwanza akalipata jibu ya kuwa Sister Murcia yapaswa hapate mtoto na mtoto huyo ndiye tu mwenye kukikomboa kijiji hicho cha Shimo la moto, na mtoto atakaye zaliwa lazima atoke katika tumbo la mama mwema na Baba mwema. Hakukuwa na Baba mwema katika kijiji hicho kama si Paulo. Ndoto ya pili hiyo bado alishindwa kuielewa, si kwamba alishindwa kuelewa kwakuwa alikuwa ajui hapana alikuwa anajua ilimaanisha nini. alichokuwa akijiuliza ni vipi kijiji kikombolewe kisha kirudi kuwa katika hali ya kishetani. Bado akiwa katika wimbi zito la mawazo, wazo lilimuhijia akajikuta anajiuliza; Sister Murcia yuko wapi? Kitendo cha kuwaza vile alishituka Sana, akanyanyuka haraka na kusisamama kutoka inje ya Sakarastia. Lakini kabla hajatoka halishangaa sana baada ya kuona panga pamoja na Ngao, vyote ni vifaa vya kivita. Vitu hivyo kwa pamoja vilikuwa vimesimamishwa, vikiwa vimeugemea Malango. bila kujiuliza, Paulo alilishika panga lile pamoja na ngao yake, pale pale nguvu za ajabu zikamuingia mwilini akajikuta ni mtu anayewaza kupambana na jeshi la Shetani. Bila kuchelewa mlango wa Sakarastia ulijifungua wenyewe naye akatoka. Alivyo toka ndani ya Sakarastia alipitiliza moja kwa moja kutoka inje ya kanisa, hakukumbuka tena kama siku aliyoingia ndani ya kanisa kutoka katika mikono ya mateka, yakishetani aliwakuta Mercia na Lucas wamelala huku hawajitambui. akiwa Bado yupo mlangoni mwa kanisa Paulo alitamka maneno haya. "Kwako wewe baba, jina lako litukuzwe, ufalme wako utukuzwe, hapa duniani na mbinguni. Nifanye mshindi katika vita hii ya kupambana na jeshi la watu waovu, nifungulie njia nyepesi kila nitakapo pita ili kuifanikisha dhamila yangu ya ukombozi katika kijiji hiki. Amina" Baada ya kuyasema maneno hayo mazito kabisa, Paulo alizunguka nyuma ya kanisa, akakitazama kijiji cha Shimo la moto jinsi kinavyo onekana. Alichokiona kwenye maono ya ndoto kilikuwa cha kweli. watu wa kijiji kile walikuwa wakishangilia na kupiga vigelele. Bado Paulo hakuamini akaamua akisogelee kijiji kile vizuri aone. kila hatua aliyokuwa akiipiga tena akikimbia kwa kasi ndipo nguvu ziliongezeka kwake. Hata njaa ya siku mbili yeye alikuwa aisikii kabisa. Usipitwe na sehemu ya 14. Je Sister Murcia hatabakwa? Paulo hatafanikiwa kuwapata wenzake? Vipi kuusu Mercia na Lucas pamoja na Moris. Je Alicia Amekufa au hapana? Tukutane Jumamos./

at 4:33 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top