Home → simulizi
→ SISTER MURCIA,
NA HEMED MAYUGU,
NO. 012.
ILIPOISHIA.
Kundi la wachawi linafanikiwa kumchukua sister Murcia kutoka kanisani na kutoweka naye ikiwa ni baada tu ya kumpulizia dawa yao ya kichawi kazi iliyofanywa na Nyamumwi au Alicia wa kichawi pamoja na Josephina Bint ambaye pia alitumwa na hao hao wachawi kwa ajili ya kumsaidia nyamumwi kumteka Murcia; kweli kama zoezi lao lilivyo kuwa limepangwa wamefanikiwa kutoweka naye. Kipindi hicho hicho Paulo naye anafanikiwa kufika kanisani baada ya kutoroka katika mikono ya wachawi, Baada ya kufika kanisani Paulo anamkosa Sister Murcia anawakuta Mercia pamoja na Lucas lakini wote wakiwa hawajitambui ikiwa tu ni baada ya kula sumu ya kichawi iliyokuwa kwenye mikate. Akiwa kashindwa kuwaamsha Paulo anaingia ndani ya Sakarastia. Baada ya Paulo kuingia ndani ya Sakarastia anaanguka na kupoteza fahamu na mlango wa Sakarastia unajifunga.
SONGA NAYO.
hatimaye usiku ulikucha. kanisani Mercia na Lucas wote kwa pamoja wanaamka lakini wakiwa na njaa pamoja na kiu isiyo na kifani. wote kwa pamoja waliangaliana kwa muda kama wa dakika tano bila kusemeshana, hapo walikuwa wakijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu. baada ya dakika hizo kupita, Mercia alimuuliza mwenzake.
"Lucas kwanini tuko humu kanisani, kwanini hatukulala Vyumbani?"
"Hata Mimi sijui labda tukamuulize Sister Murcia anaweza kutueleza!"
"Halafu naisi njaa, na kiu utafikiri nilikuwa shambani sijui kwanini, hivi Jana tulikula kweli?"
Mercia aliuliza tena.
"Hapana, hata Mimi ni kama wewe na sikumbuki kama tulikula"
Majawabu ya Lucas yalimtosha kabisa Mercia kuendelea kuuliza. Kumbe wote kwa pamoja walisahau kuwa jana usiku walikula. Hivyo hivyo Wote kwa pamoja wakiwa na njaa zao walitoka inje ya kanisa kwa ajili ya kwenda kumuona Sister Murcia, mungu wangu, vichwani mwao hakukuwa hata na wazo lolote wala hawakuju kama kipindi hicho kanisani hapo walikuwa wamebaki peke yao tu, na wala hakukuwa na mwingine zaidi ya Paulo ambaye naye alikuwa yumo ndani ya Sakarastia akiwa hajitambui kabisa. Vijana wale wote wawili walikisogelea chumba ambacho alichokuwa anakitumia Sister Murcia pamoja na Mabint wakike kulala ili wamuulize kwanini wao wamelala kanisani. Waliufikia mlango na kuugonga wakisubili wafunguliwe mlango huo, waligonga mlango mala nyingi bila kufunguliwa wala kuitikiwa karibu. baada ya kuona kimya Mercia aliamua ausukume, mlango na kuufungua mwenyewe, Mercia bila kuogopa aliingia ndani ya chumba hicho kangalia kama kuna mtu lakini hawakumkuta Sister Murcia, wala Alicia wala Mgeni wao(josephina) lakini taa ya chumba hicho bado ilikuwa inawaka. Hali hio iliwafanya kujipa matumaini kuwa huwenda sister Murcia atakuwa kanisani ndani ya Sakarastia akisali.
baada ya kuona hivyo wote kwa pamoja wakasemeshana kuwa bila Shaka Sister na Alicia watakuwa kanisani kwenye Sakarastia. Basi wote wawili waliamua waongozane kurudi kanisani kwa ajili ya kumwangalia Sister Murcia wakizani kabisa kuwa yumo ndani ya Sakarastia, waliongozana mpaka ulipokuwa mlango wa Sakarastia, lakini walipofika mlangoni walijaribu kuufungua mlango ule, lakini mlango haukufunguka uligoma kabisa kufunguka. Hali hio iliwanyima Furaha Lucas na Mercia. Baada ya kuwakosa wenzao kanisani waliamua wote watoke inje, wazunguke nyuma ya kanisa wakiamini labda huwenda wakawaona, Nako huko waliwakosa hawakuwaona.
"Sasa hawa wameenda wapi?"
"Hata Mimi sijui"
"Labda watakuwa, wametoka na yule mgeni wa Jana"
"Mgeni!?"
Alicia aliuliza kwa mshangao. Kwani alikuwa amesahau kama Jana walikuwa na mgeni.
"Ndiyo! Umesahau kama Jana kuna mgeni wa kike alikuja hapa?"
Lucas alisema.
"Sawa lakini Sister Murcia hawezi kuondoka hapa bila kutushilikisha sisi"
Mercia alisema.
"Sawa Mercia wewe unaamini si unakumbuka kabisa hapa kuna uhaba wa chakula, huwenda wameongozana kwenda kutafuta chakula"
Lucas alisema.
Baada ya kuzungumza hivyo, wote kwa pamoja bado wakiwa wamesimama, nyuma ya Kanisa walianza kuulizana usiku ilikuwa vipi mpaka wakalala ndani ya Kanisa. Baada ya kuulizana maswali machache wakakumbuka kuwa Jana usiku wao walikula mkate kutoka kwa Josephina. Mkate huo ndio huwenda umewafanya kulala ndani ya kanisa.
hapo ndipo Akili ziliwaingia wakajikuta wanaamini kuwa Wenzao huwenda, wametekwa. Mawazo yao yakawapeleka kwa Josephina, fikira zao zikawambia kuwa Josephina hakuwa mtu mzuri huwenda alikuwa ni miongoni mwa watu wabaya aliyekuwa ametumwa kuja kuwaangamiza. Kitendo cha kukumbuka machozi yalianza kuwatoka wote kwa pamoja wakajua kabisa wamempoteza sister Murcia. Bado wakiwa wanaendelea kulia nyuma ya Kanisa, mala Josephina alitokea mbele yao akiwa katika sura ya kutisha Sura ya kishetani, Sura ya kichawi. Lucas na Mercia baada ya kuona hivyo kila mmoja alikimbia kujificha mgongoni kwa mwenzake, walikuwa kama wanapigana ili kila mmoja kuutafuta mgongo wa mwenzake kwa ajili ya kujificha. Kitendo hicho kilimfurahisha sana Josephina, Akacheka kwa nguvu kisha akasema.
"Yeyote akija huku huwa arudi alikotoka, wala hakuna taarifa ambazo huwa zinarudi mliko toka, ni wakati wenu wa kufaaaaaa Ha ha ha ha haaa!"
Josephina alisema
Maneno yaliyokuwa yanatisha huku akimalizia kwa kicheko cha nguvu, maneno hayo yaliwaingia Lucas na Mercia yakawa yanazikwangua nyoyo zao. huwezi amini wote kwa pamoja wakavikumbuka vitendo na mafunzo ya Sister Murcia, alivyokuwa anawaambia kuwa wanapaswa wawe na imani kubwa miyoni mwao ili kulishinda jeshi la shetani.
Hata hawakuwa na namna na njaa zao walianza kulia kuomba msamaha kwa Josephina asiwauwe, walishindwa hata kumuomba na kuziweka imani zao kwa Bwana mungu wao labda wangeokolewa, wao walikuwa wakupiga makelele ya kuomba msamaha kwa shetani hawasamehe.
"Hivi unaweza kumuomba shetani msamaha halafu baadaye umshinde. Basi jueni kuwa Shetani kazi yake ni kuwangamiza, haijarishi ni kwa njia gani ila yeye huwa anaangamiza tu, hata nikikusameeni nitakuwa sijawasaidia. kawaida nikipata chasi ya kuuwa na kunywa Damu huwa siiachi hata kama ni mtoto mchanga"
Josephina alisema.
Maneno hayo yaliwashitua sana, hapo ndipo Lucas na Mercia wakajua kuwa wasipomtumainia bwana watakufa kweli, hapo wakajikakamua kuanza kumuomba mungu huwenda akawasaidia kutoka katika janga hilo. Ilikuwa kama ni kujisumbua, Imani zao zilikuwa bado kabisa. Ilikuwa ni rahisi kwa Josephina kuwasogelea karibu yao. Ndicho kipindi hicho hicho Nyamumwi naye alitokea akiwa bado katika sura ya Alicia. bila kujua wala kutambua Mercia na Lucas wakamsogelea kumuomba msaada wakizani kuwa ni Alicia. Kabla hawajamfikia walishitushwa baada ya kuiona ni Sura ya Bibi mwingine kabisa Ambaye hawajawahi kumuona toka wanafika kijijini hapo. Kitendo cha kuona Alicia kugeuka kuwa bibi tena mwenye kutisha, mdomono amejaa mapengo na makucha ya kutisha, waliogopa na kurudi nyuma kwa kasi kumuepuka yule Bibi mchawi, Bibi Ambaye alikuwa kajigeuza katika Sura ya Alicia.
"Ha ha ha ha! Mwanzo mlikuwa vichwa mpaka mkapelekea wenzetu kujeruhiwa na kupoteza sehemu katika mihili yao, Leo mmepatikana. Lazima tuwale, ha ha ha ha ha"
Yule Bibi alisema na kucheka.
Tayari muda huo Mercia alikuwa kaisha zima. Lucas alijitahidi kukimbia kurudi ndani ya kanisa akizani labda kuna kupona lakini napo haikusaidia kikundi kile cha wachawi wawili, kilimtokea huko huko. Bila Kupoteza muda, Josephina alimpiga pigo moja Lucas naye akazimika kisha wakatoweka naye pomoja na Mercia.
Itaendelea.
Je sister Murcia atapatikana?
Vipi Lucas na Mercia watabakwa na kukatwa sehemu zao za Siri kama ilivyo desturi ya watu wa kijiji hicho?
Tukutane jumatatu. SHARE SHARE KWA WINGI NA INVITE RAFIKI ZAKO KU-LIKE PAGE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: