SISTER MURCIA, NA HEMED MAYUGU, NO. (11). ILIPOISHIA. Bint yule mchawi aliingia ndani ya kanisa huku kashikili begi yake ya kisasa yaliyoshonwa mfumo wa kigunia halafu begani kauvaa mkoba wa kung'aa kabisa, aliyafurahia mapokezi ya kuingia ndani ya kanisa. SONGA NAYO. Ilikuwa ni furaha moyoni mwa Bint yule mchawi na Alicia wa kichawi. Walikaa wakaongea kwa pamoja, wakisimuliana matukio ya kijiji hicho na kufundishana mafundisho ya Mungu, jioni hio kwao ilikuwa yenye furaha kwa watu wawili Alicia na bint Josephina. Kwa sister Murcia ilikuwa ni majonzi moyoni, mawazo yake yaliishia kwa Moris na paulo. Mazingira ya mawasiliano kwa kijiji hicho hayakuwepo kabisa labda angefanya utaratibu wa mawasiliano. Muda wote alikuwa anawaza. ********* Usiku mida ya saa moja walitaka kuandaa chakula lakini hawakuwa nacho cha kutosha, walifikiri watafanya nini, hata basi wangemuomba bwana labda angefanya muujiza wake hawasaidie lakini haikuwezekena au hata wavumilie mpaka kesho waone kitatokea nini, hilo tu ndilo lilikuwa wazo lao. "Sister Murcia mimi nina mikate mitatu hii tunaweza kula kwa pamoja tukashiba usiku huu" Bint yule wa kichawi alisema baada ya kuona kuwa watu wale wanauliza kuusu chakula. Baada ya Murcia kusikia yule bint anamikate akawambia waitenge wale wao wote lakini yeye hakuwa na hamu ya chakula. Kukataa kwa sister Murcia kulikuwa ni pigo kwa wachawi wale, wao walitaka Sister Murcia ale chakula chao kilichokuwa na sumu ya kuwafanya wote wapatwe na gonjwa la kuzimia halafu wajue namna ya kuwabeba kutoka eneo lile la Kanisa mpaka kwao uchawini. Baada ya sister murcia kugoma wachawi wale walijitahidi kumshawishi aweze hata kula kidogo. "Sister Tafadhali jua kesho ni mbali na uwezekano wa watu wale kufika haupo kwasababu hatuna taarifa nao!" Alicia wa kichawi au Nyamumwi kama alivyokuwa anaitwa uchawini kwao alisema. "Hapana Alicia hata ningalifanya nini! Hamu na kula kwangu haipo kabisa kabisa haipo!" Sister murcia alisema. Baada ya kuona kuwa Sister Murcia kagoma kula wachawi wale waliamua kuwapa mkate uliokuwa na madawa yao ya kichawi Mercia na Lucas wao wakabaki na mkate mmoja ambao ulikuwa hauna kitu ndani yake na mmoja wakasema wautunze wakidai kesho Sister Murcia anaweza kuamka akiwa na njaa akala, lakini moyoni walikuwa na jipya badala ya kutumia mkate waliamua waplani njia nyingine ya kumukamata sister Murcia. Sister Murcia aliwaacha watu wale wanakula chakula/mikate yao yeye akaenda kuoga kwa ajili ya maombi ya usiku. Hio ndio ilionekana nafasi nzuri na muwafaka kwa wachawi kumfanyia kile walichotaka kukifanya kwa sister murcia. Lucas na Mercia walikula mkate kwa dakika Tano tu wote wakaanza kulewa kisha wakasisinzia hoi kabisa usingizi mzito hawakujua nini tena kilipaswa kuendelea Duniani. Baada ya kuona kuwa huku kanisani wamewaacha Mercia na Lucas wamezimia, wao moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa Sister Murcia wakimngoja atoke bafuni wamfanyie kile walichokuwa wamepanga kumfanyia. Haikuchukua muda dakika mbili tu toka waingie Sister murcia aliingia ndani kutoka bafuni kuoga. Kitandani alimkuta Alicia wa kichawi au Nyamumwi amekaa, kipindi hicho Josephina alikuwa kajificha nyuma ya mlango. Sister murcia alimwangalia Alicia na kumuomba ampishe avae, Alicia yule wa kichawi alisiamama, kumbe mkononi alikuwa kakumbatia madawa ya kichawi yakiwa ya unga. Sister Murcia hakiwa hana hili wala lile alishitukia anapuliziwa unga ule usoni, ukamtapakaa uso mzima, mwingine ukamwingia machoni akashindwa kuona, mwingine ukamwingia puani na hata mdomoni, haikupita hata dakika mbili sister Murcia alianza kulewa akaanza kuona kizunguzungu, akawa aoni vizuri kabisa. Mambo yalimuwia magumu Sister nguvu zikawa zinamuishia mwilini huku anayakumbuka maneno ya Murcia wa kwanza jinsi yeye alivyotaka kuuliwa bahati mbaya akaponea chupu chupu kwa nguvu za Mungu. Muda huo huo Murcia alianguka chini puuuu! wachawi wale wawili walicheka na kufurahi kwa mafanikio yao ya kuweza kumkamata Sister murcia na kumuweka katika Imaya yao. Baada ya kumaliza zoezi lao wachawi wale Nyamumwi aliyekuwa kajigeuza umbo la Alicia na Josephina Bint ambaye alikuwa kaja kumsaidia Nyamumwi waliwasiliana na Kikosi chao kikuu kuwapa taarifa kuwa wamekamilisha kazi yao. Haikuchukua muda kikatokea kikundi cha vijana watatu wa kiume pamoja na Padre joseph mwenywe, walipofika wote kwa pamoja walipotea na mwili wa sisiter Murcia pekee na kuwaacha Lucas na Mercia ndani ya kanisa hawajielewi kabisa. ******* Ikiwa ndio siku ya kwanza toka kupigwa dawa ya kupoteza fahamu na kundi la wachawi, Usiku huo mida ya saa nne na nusu uwezi amini kwa uwezo wa mungu paulo alijikuta anapata nguvu na kuamka kutoka katika kupoteza fahamu na kuamka, baada ya yeye kuamka katika janga hilo huku hakiwa na njaa kabisa alijaribu kumwamsha Moris ili naye aamke wapate kuondoka eneo hilo hata kwa kutoroka tu, lakini kila alivyokuwa anaangaika kumwamsha Moris hakuweza kuamka, ilikuwa kama kusujisumbua tu, baada ya kuona mwenzake aamki Paulo akajua moja kwa moja kuwa kaisha kufa. Kilichofuata yeye mwenyewe alianza kutafuta namna ya kutoka ndani ya jumba lile la kichawi. Bahati nzuri chumba hicho kilikuwa hakina mlango lakini kila alipokuwa akijaribu kutoka ikawa kama vile anazunguka mule mule ndani ya chumba hicho. "Eee mungu, niondoe na unilinde katika jumba hili la shetani" Maneno hayo tu yalitosha kumfungulia Paulo mlango wa shetani na kutoka mdani ya chumba cha Shetani, aliweza kutoka kirahisi sana ndani ya jumba lile kama vile alikuwa aonekani, aliweza kutoka pale kwenye jumba lile la wachawi na kutembea, hakukua na dalili kabisa za kufukuzwa wala kufuatiliwa na Wachawi. Paulo alikuwa akitembea kwa kulitaja jina la Bwana ndani moyoni mwake, njia nzima alikuwa akimuomba mungu amuongoze afike haraka sana kanisani. Muujiza wa mungu ulifanyika kwake, akalifikia kanisa. Alipofika kanisani cha kwanza alikisogelea chumba alichokuwa analala sister murcia na wanafunzi wa kike na kukigonga chumba hicho. Paulo alijitahidi sana kuugonga huku akiita majina ya watu wote lakini haikusikika hata sauti ya mtu kuitika, baada ya kuona kimya aligundua kuwa hakuna mtu ndani ya chumba hicho japo kuwa taa ilikuwa inawaka, Paulo aliamua aende kanisani. Alipofika kanisani alisitushwa na alichokikuta ndani ya Kanisa, aliwakuta Mercia na Lucas wamelala fo fo fo hawajitambui kabisa. Alichokifanya nikuwamsha huku akiwafanyia maombi lakini ilishindikana kuamka, sumu waliyokuwa wameila kwenye mikate ilikuwa ni sumu kali sana, sumu ya Mchawi. Baada ya kuona Lucas na Mercia hawaamki Paulo aliamua kwenda ndani ya Sakarastia kutazama labda angemkuta sister murcia, alipo ukaribia mlango ukajifungua na kuingia, alipoingia tu mlango ukajifunga naye akaanguka chini na kupoteza fahamu. Sisiter murcia atapatikana? Share tafadhali. Tukutane JUMAMOSI.

at 4:32 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top