Home → simulizi
→ SISTER MURCIA,
NO. (10).
ALICIA WA KICHAWI AFIKA AONEKANA MWENYE KUFUNGAMANA NA BWANA. AJA TENA BINT MWINGINE WA KICHAWI KWA AJILI YA KUMMALIZA SISTER MURCIA. NAYE AMPOKEA BILA KUJUA.
ILIPOISHIA.
ndani ya kijiji hicho kuna wasomi wakubwa wanaokitumia kijiji hicho kwa manufaa yao, ndivyo hivyo hivyo. Wachawi wale waliwachoma Paulo na Moris Sindano za kupunguza nguvu na kuwafanya walegee kabisa na kukosa nguvu.
SONGA NAYO.
Muda huo huo walilala usingizi mzito kabisa na kusahau kila kitu kilichoendelea duniani. Usiku huo ulikuwa ni shangwe na vigerere kwa wachawi wakisheherekea sikukuu ya kuipata kafara kuu kwa ajili ya Rusifa.
********
Siku iliyofuata asubuhi na mapema kabisa sister murcia akiwa na mawazo ya kupotelewa na Mwanafunzi wake, tena bado hana taarifa kuusu akina Moris na Paulo ambao walienda mjini toka asubuhi na mapema ya siku iliyopita na aliwatarajia wafike siku hio hio ya jana lakini hawakufika. hivyo vyote vilimpa mawazo sana Sister murcia, Sister ambaye alikuwa na upako mkubwa kutoka kwa bwana, lakini kipindi hicho alikuwa kwenye wakati mgumu sana. Hata maombi yake kwa bwana yalikuwa kama hayapokelewi katika uzito wake.
Hivyo hivyo na mawazo yake, alitoka ndani akachukua maji kwenda kuoga kuondoa uchafu mwilini mwake. Baada ya kumaliza kuoga alijifunga na kuvaa nguo zake, kisha akaelekea kanisani kufanya maombi.
Ilikuwa ni mapema sana, kama mida ya saa kumi na moja za asubuhi. Sister murcia aliushika mlango wa kanisa ambao ulikuwa hujafungwa bali Umeegeshwa na kuufungua, cha kwanza kuingia ndani ya kanisa ulikuwa ni mguu wake wa kulia kwa maombi maalum aliyo yatanguliza, kisha uso wake ukafuata. Sister murcia akuamini kabisa alipomuona Alicia fake kapiga magoti mbele ya sanamu ya Bikra maria akiomba. Sister Murcia akiamini kabisa kuwa aliyeko mbele yake ni Alicia aliyemzoea aliinua mikono yake juu kwanza akamshukuru Bwana mungu kwa shukurani kubwa. Baada ya kumshukuru bwana mungu aliye hai, Murcia aliita Alicia, Bila hata uwoga Alicia fake, alicia wa kichawi au Nyamumwi aliyejigeuza na kuwa Alicia aliitika na kusema.
"Bwana mungu awe nasi Daima milele, hakika nimeokoka kutoka katika jeshi la Shetani kwa msaada wa bwana. Mungu anapaswa ashukuliwe kwa ukubwa milele amina"
Alicia fake akionekana kabisa kuwa ni mwenye imani kubwa na Mungu aliye hai, mungu wa kweli, mungu mwenye mamlaka na kila kilichomo ardhini, alisema maneno mazuuri yaliyopokelewa kwa "EMEE" kubwa kutoka kwa Sister Murcia.
"Alicia ni wewe kweli?"
"Sister mulcia aliuliza kwa shauku ya kujua.
"Ndiyo mimi sister Murcia, kwani uamini kuwa bwana mungu ameniokoa kutoka katika mikono mibaya ya Shetani?"
Alicia fake isema huku akitabasamu.
"Hapana! Nikwasababu jana....!Tukio la jana liliniweka kwenye wakati mgumu sana. Sijalala usiku kucha nikikuwaza!"
Sister Murcia alisema.
"Kwani sister? we hukufanya maombi kwa ajili yangu?"
Alicia aliuliza.
"Nilifanya lakini maombi yangu asaiv yana...........!" Sister murcia akutaka kuimalizia Kauli yake.
"Yana nini sister?"
Alicia fake, Alicia wa kichawi au nyamumwi aliuliza kwa lengo la kuthibitisha kuwa alichokuwa anakisem padre joseph kuusu sister Murcia ni cha kweli.
"Hapana! Naomba unambie ni nini ambacho kilikukuta huko?"
Badala ya kujibu Murcia naye aliuliza na kubadili mada pale pale.
"Baada ya kupotea katika kile kimbunga cha jana, nilijikuta niko kwenye pori kubwa, huko palikuwa panatisha sana, nilianza kuogopa nilipofika huko, nilikuwa peke yangu tu. Baada ya muda kama dakika tano niliisi kama sauti ya Shetani ikiniita. Pale pale namimi nikapiga magoti na kuanza kuomba halafu nikiliita jina la yesu, yesu! yesu! huku nimefumba macho, sikujua nilipotea vipi maeneo yale nikajikuta niko humu kanisani"
Alicia wa kichawi alisema kwa kujiamini kabisa.
"Mh! Pole sana. Mimi huwa nawambia mnapaswa muwe na imani kama hio. mungu ni wa ajabu anamuokoa na kumlinda kila mwenye kumtumainia"
Sister Murcia alisema. Mbele ya shetani mkubwa, mchawi aliyebobea katika fani ya kuwanga na kuwaloga watu, Aliyejulikana kwa jina la Nyamumwi.
Moyoni mchawi yule alikuwa akimcheka na kumzomea Murcia huku akijisemea.
"Subiri uje uone na ujue ni nini maana ya kijiji cha shimo la moto, lazima ufe iwe isiwe lazima ufe"
Akiwa kaisha gundua kabisa kuwa alichokisema padre joseph kuusu sister murcia ni cha kweli, ya kwamba kuwa Maombi yake hayapokelewi ipaswavyo mbele ya Bwana kutokana na kuwa katika hali mbaya, hali chafu, hali ambayo kila mwanamke huwa inamkuta. Nyamumwi kwa ulimi wake alimwambia sister Murcia.
"Sister naomba tuwafanyie maombi Akina Paulo na Moris ili mungu awape wepesi wa kurudi haraka, au kama kuna tatizo limewakuta, basi wapate kuokolewa"
Sister Murcia akuamini kabisa alichokisiakia kutoka kwa mwanafunzi wake ambaye alikuwa na imani haba kuweza kusema maneno ya kuwaombea watu walioko mjini.
"Alicia naona umebadilika unapenda kusali na kumuomba mungu ipasavyo sasa. Basi naomba wewe ndiye uwe muombaji mkuu wa maombi haya kwakuwa wewe u msafi"
Sister murcia alizidi kujiweka wazi kwa mchawi yule nyamumwi. Bibi mchawi kabisa aliyekuwa kajigeuza na kuichukua sura ya Alicia na wakati kipindi hicho Alicia alikuwa mikononi mwa jeshi la shetani akiwa ajitambui kabisa.
Maombi yasiyokuwa na faida kutoka kwa watu wawili sister Murcia na mchawi yalianza ndani ya kanisa. Ndicho kipindi hicho hicho Mercia naye alifika na kuendelea na maombi hakutaka kuwasumbuwa wenzake ijapo kuwa alishikwa na butwaa alipomkuta Alicia yumo kanisani akiomba na Sister Murcia. Bado wakiwa wanaendelea kuomba Lucas naye alifika na kuunganisha nao katika kuomba.
Maombi yaliwachukua kama lisaa limoja kisha wakamaliza. Baada ya kumaliza Mercia na Lucas nao walimuuliza Alicia kuusu alipokuwa. Alicia huyo mchawi kabisa bila hata aibu naye aliwasimulia habari za uongo wake nao pia wakawa wenye kuamini.
Kweli wasemavyo waswahili kuwa kumjua mchawi huwa ni vigumu wakati wa mchana hata usiku labda akutokee akiwa katika hali yake ya kishirikina, na hata wale wasemao kuwa hata mchawi umtegemea mungu ili afanikishe maswala yake basi huwenda ni kweli. Mchawi yule aliyekuwa kajibadilisha kafanana kabisa kila kitu na Alicia alifanya kazi kwa bidii sana, tena yeye ndiye aliyebadilika na kuwa muamasishaji wa wenzake kusali kuisoma Biblia takatifu. Mpenzi msomaji zingatia kabisa kuwa yaliyomo ndani ya Biblia au kwenye Kitabu chochote cha Mungu hayana msaada kwako usipokuwa na imani nayo, hata ufanyaje hayawezi kukusaidia. Shetani anayatumia akiwa na Tahadhari kubwa akijua kabisa akienda nayo ovyo yatamwangamiza na kumuua lakini Sisi binadamu wenye imani haba ndio tunayachukulia kawida.
Mchawi yule Nyamumwi aliweza kuwaingia akilini wote ndani ya siku moja tu, kila mmoja pale akaamini kabisa kweli Alicia kabadilika kawa mtu wa kumtumikia bwana na mwenye imani kubwa. Kumbe walikuwa wanamuwazia kiumbe ambaye amekuja kuwangamiza na akuwa Alicia waliyekuwa wakimzani.
********
Masaa yalizidi kwenda, hatimaye ikatimu mida ya saa kumi jioni, hazikuonekana hata dalili za kufika kwa Moris na Paulo kurudi kutoka mjini sister murcia na wanafunzi wake hapo ndipo walizidi kuchanganikiwa kabisa.
"Oooh! Mungu wangu hawa wanekamatwa na kikundi cha wachawi, mbona hawarudi?"
Sister Murcia alijisemea huku wasiwasi ukiwa umemtanda, alishindwa kuvumilia machozi yakamdondoka kabisa. kuingia ndani ya Sakarasitia kuomba kwake ilikuwa ngumu.
"Jamani msiwe na hofu, mungu atawalinda na kuwaokoa, si tunamtegemea mungu kwa kila jambo kwanini tusimwamini mungu wetu"
Alicia mchawi alisema.
Bibi huyo wa kichawi aliyekuwa kajigeuza kwa sura ya Alicia alizungumza upuuzi tena kwa kuweka kejeli za ajabu kabisa. Maneno hayo yalimkasirisha kila mmoja pale na kumkemea.
"Sister naomba mnisamehe sitarudia kusema hivyo tena"
Baada ya kusena hivyo mchawi yule alijifanya kuzira na kukaa pembeni kuona wenzake watasema nini.
Lakini napo pia hawakumjali mawazo ya Sister Murcia yaliishia kwa Paulo na Moris.
"Chakula kimetuishia hata usiku hakitoshi, sijui tutaishi vipi hapa, mungu wangu Eee! kipokee kilio chetu tunateseka waja wako"
Sister Murcia alisema.
Maneno yake yakisikika moja kwa moja masikioni mwa mchawi Alicia. Kumbe kipindi hicho naye alikuwa anapokea taarifa kutoka kwa mkuu wake taarifa ambazo zilikuwa zinasikika moja kwa moja masikioni mwake kupitia cheni aliyokuwa ameivaa shingoni.
Alipomaliza kuzisikiliza taarifa kutoka kwa mkuu wake, mchawi yule ambaye pia maneno ya murcia aliyasikia vizuri alisema.
"Naomba mwalimu wangu, naomba leo tukajaribu kwenda kukitembelea kijiji hiki, mi ninaamini kabisa watu watatusaidia hata chakula cha kula usiku huu Halafu kesho tuaweza kutafuta namna nyingine au huwenda kesho paulo na Moris watarudi"
Mchawi yule aliutoa ushauri mzuuri ambao tayari yeye alikuwa anajua ni nini madhara yake.
"Hapana Alicia aiwezekani kabisa hiki kijiji mimi nakijua watu wa hapa si binadamu ni watoto wa shetani kabisa hawaoni wala awaelewi"
Sister murcia alisema.
"Murcia mimi nipo nitajitoa sadaka kwa hawa ndugu zangu, naomba wao wabaki tuongozane na wewe, au kama hata wewe hutaki ngoja mimi niende pekee, nina hakika ninaweza kuja na chakula kutoka kwa watu hao"
Wakiwa bado wanazungumza alikuja bint mmoja mzuri kavalia nguo nzuri kabisa. Bint yule kila mmoja pale alimshangaa, alikuwa ni bint wa aina yake. kwa mazingira ya kijiji kile akuna ambaye alikuwa anauwezo wa kumfikia hata kimvuto kwa jinsi alivyokuwa akionekana.
Bint yule kumbe naye alikuwa shetani, kambi moja na Alicia fake aliyetumwa na padre joseph aje kusaidizana na Nyamumwi kummaliza sister murcia.
Baada ya kufika bint yule alijitambulisha kwa jina la Josephina, alisema kuwa yeye ni mwenyeji wa kijiji hicho cha zima moto lakini siku ni nyingi toka aondoke karibu miaka mitatu, alikua kaja kumuona mama yake, lakini alipofika akaambiwa kuwa siku nyingi mama yake kaisha fariki na alipokuwa anaishi kiwanja washauza na hakuna tena ndugu wa kwenda kumfikia kwahio aliomba alale hapo kanisani kwa siku moja tu ili kesho yake aamke akawatafute ndugu zake.
Maelezo ya bint huyo yalimuingia kila mmoja, lakini bado wote walikuwa na wasiwasi huwenda jeshi la shetani limewavaa.
"Wewe! watu wa hapa wote, huwa hawaji katika kanisa hili, wote wanalichukia kanisa la bwana, Au umetumwa?"
Aliyekuwa wa kwanza kuuliza alikuwa Alicia mchawi, yote hayo kutaka kuyatengeneza mazingira ya kumkaribisha mchawi mwenzake.
"Jamani kweli ndio hivyo basi ngoja nikalale kichakani tu!"
"Sisi hatujakataa kukusaidia lakini kwanini usiwambie hao wanakijiji wakakusaidia?"
Mercia aliuliza.
"Mimi ni mtoto wa kike, mazingira ya watu wa hapa kijijini sijayazoea kwanza nilikuwa nimemuijia mama yangu kesho tu nianze safari ya kurudi naye mjini"
Bint yule alisema kwa unyenyekevu kabisa, kipindi hicho sister murcia yeye alikuwa akiwaza mbali, mawazo yakawa yanajirudia kichwani mwake kuusu alivyoambiwa na Murcia wa kwanza kuusu kikombolewa kwa kijiji hicho cha shimo la moto.
"Sister murcia ebu sema kuusu mtu huyu?"
Lucas alisema.
Maneno ya Lucas ndio yalimrudisha sister Murcia katika hali ya kawaida.
Apite akaye bwana katufungulia njia"
Maneno ya sister murcia ndiyo yalikuwa kama ruhusa wa kuingia ndani ya kanisa kwa bint yule.
Bint yule mchawi aliingia ndani ya kanisa huku kashikili begi yake ya kisasa yaliyoshonwa mfumo wa kigunia halafu begani kauvaa mkoba wa kung'aa kabisa aliyafurahia mapokezi ya kuingia ndani ya kanisa.
ITAENDELEA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: