SISTER MURCIA, NO.(09). ALICIA APOTEA NA KUCHUKULIWA NA KIKOSI CHA SHETANI, SISTER MURCIA ASHINDWA KULA, AOGOPA KUINGIA NDANI YA SAKARASTIA. PAULO NA MORIS WATEKWA NA KUNDI LA WACHAWI. ILIPOISHIA Wakiwa inje ya kanisa wakifanya shughuri ya usafi mida ya saa 4 za asubuhi. Ghafra upepo mkari ulitokea giza nene likatanda kila mahara katika kijiji hicho, upepo ulikuwa mkari, vumbi likatibuka sehemu hio ya kanisa, hakuna aliyeweza kumuona mwenzake. Ilikuwa ni jambo la kushitukiza kwao. SONGA NAYO. Upepo huo ulichukua muda kama robo saa ndio ukatulia, ulikuwa ni upepo ambao kila mmoja akuutegemea kabisa. Baada ya upepo huo kutulia Sister Murcia alikuwa kabaki peke yake eneo hilo la kanisa, hapo aliisi kuchanganyikiwa akaanza kuita majina ya Wanafunzi wake watatu, Lucas, Mercia na Alicia. Lakini hakuna aliyeitika. Sister Murcia alichoka na kuchoka. "He baba najua hata manabii wako walipata misukosuko kama hii basi nilinde juu ya ili janga zito!" Murcia alisema akiwa ameunua macho yake juu. Baada ya kusema hivyo akili zake zilimtuma azunguke nyuma ya kanisa, bila kuchelewa naye alifanya hivyo. Baada ya kufika nyuma ya kanisa Sister Murcia alisitaajabu baada ya kuwakuta Mercia na Lucas kila mmoja ameanguka upande wake. Bado Murcia aliizidi kuangaza kama angemuona Alicia lakini hakuweza kumuona. Ndipo sister Murcia alipo waamsha wanafunzi wake wawili yaani mercia na Lucas ambao aliwakuta nyuma ya kanisa, Wote wawaili hakutumia nguvu kubwa kuwaamsha , aliwagusa tu mala moja nao wakaamka. Baada ya kuwaamsha wanafunzi hao wawili, Murcia aliwaomba wasaidizane kumtafuta Alicia wote kwa pamoja. Walitafuta maeneo hayo ya kanisa nyuma na mbele hawakuweza kumuona, waliamua wasogee mbele tena ya hapo, napo pia hawakuweza kumuona. Walitafuta sana bila mafanikio, walisogea mpaka katika nyumba za wanakijiji hicho, ambazo zilikuwa umbali kama umbali wa viwanja vitatu vya michezo kutoka lilipokanisa. Huko ndiko kulikuwa kama wanajisumbua, hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa anazungumza nao wengine walikuwa wanawakimbia, wengine walikuwa wanawasotea vidore na kuwaponda wasijaribu kuzisogelea nyumba zao Karibu. Wakiwa wametafuta bila mafanikio kabisa, Murcia alichoka akashindwa afanye nini, kuomba allijaribu mala nyingi eiza mwenyezi mungu amsaidie kumuona mwanafunzi wake, maombi yake yalikuwa kama hayapokelewi. Siku hio mchana ilipita tu, hata kula walishindwa kwasababu ya kumkosa mwenzao. *******. Ni mida ya saa moja za jioni tu, katika nyumba kubwa ndani ya kijiji hicho cha Shimo la moto, jumba hilo lilionekana linaukumbi mkubwa na lipo katikati ya pori, kulikuwa na kundi kubwa la watu wamekusanyika, mmoja akiwa amekaa kwenye kiti kikubwa kama mfalme, mtu huyo alionekana ndiye mkubwa na kongozi wa wengine wote. Watu wengine walikuwa wakiinama na kuinuka. Kwa maana walikuwa wanasujudu na kuinuka mbele ya Mtu huyo. Ndani ya jumba la mtu huyo kulikuwa na misalaba kama ya kanisani. "Ha ha ha ha. Tumefanikiwa Ha ha ha ha!" Mtu aliyekaa kwenye kiti alicheka kwanguvu na kutamka neno hilo moja tu. "Sasa namuomba mtu mmoja mwnamke mwenye ujasiri ajitokeze hapa tumpe kazi!" Mkuu yule wa kundi hilo la wachawi alisema. Baada ya kusema hivyo tu, alijitokeza Bibi mmoja. "Mkuu ni mimi Nyamumwi, nimetumwa na mkuu wangu nije nikusaidie kazi hii" Baada ya bibi yule kusama hivyo, Yule mkuu wa wachawi alicheka sana akasema. Hii ndio faida yetu sisi wachawi tukishindwa jambo huwa tunashirikiana, tukimaliza ndio tunarudi pale pale" "Kweli mkuu! Bibi yule alisema. Hawa wachawi wa upande huu walikuwa wamevaa nguo nyeusi tupu ispokuwa mkubwa wao alikuwa amevalia nguo jekundu likiwa na misaraba. Baada ya Bibi yule kujitokeza, yule mkubwa wa wachawi alinyoosha fimbo aliyokuwa kaishikilia mkononi mwake kwenye kitambaa cheupe kilichokuwa mbele yao. Mala moja ikatokea video kwenye kitambaa hicho; video hio ilimuonesha Sister Murcia akiwa anafanya maombi, mkuu yule wa wachawi alicheke sana, kisha akasema. "We ni mwanamke tu, uwezi kuwa na mamlaka makubwa ya kutushinda sisi, kwani uliona wapi mungu akamleta nabii mwanamke katika Dunia hii, Hata mariam Mwanamke aliyekuwa Mwema kuliko wote yeye hakupewa upeo wa kuwaongoza na kuwafundisha watu habari za mungu wangeanzia wapi kumwelewa, zaidi wangemponda mawe na kumuua. Mimi ndio Joseph padre mkubwa makanisani huko wananijua Ha ha ha ha ha!" Mkuu yule alisema na kumalizia kwa kucheka. "Je mkuu wataka tumfanye nini mtu huyu?" Mmoja wa watu katika wachawi wale alisema. "Muda wake wa kuishi umefikia tamati. " mkuu yule si ndiye miongoni mwa watu wakuogopwa na wanamamlaka makubwa mbele za bwana mungu?" Mtu yule tena aliuliza, mtu huyo alionekana ni msomi kabisa kimawazo. "Ha ha ha ha ha ha! Huyo hana mamlaka makubwa na msaada mbele za mungu kwa sasa, kwani yupo katika wakati mmbaya, malaika wadumisha ulinzi wa bwana hawawezi kumsogelea kwani wao si wakumsogelea aliye mchafu, na ndio maana mwanamke ajapewa mamlaka ya kuwaongoza watu katika maswala ya kiimani labda kwa dharula sana" Baada ya kusema vile mtu yule aliyejiita Joseph ambaye ni padre aliita "Nyambi!" "Nipo mbele zako wewe upaswaye kuwabudiwa!" Nyambi, kijana mmoja wa kiume alijitokeza. "Niletee kafara ya Rusifa" Bila kuchelewa nyamba alitoka na kuingia chumba cha pembeni akamtoa Alicia akiwa hoi kabisa ajitambui, Nyambi alikuwa amembeba mikononi mwake. "Mlaze mbele ya mazabahu ya kuitoleya kafara kuu ya mkuu katika wakuu wa Ulemwengu" Mkuu wao alisema. Baada ya mkuu yule kumaliza vile akasema. Huwa tunatoa kafara moja ya mwanamke Bikra kwa mwaka, mwaka huu tayari kafara tumeisha ipata" Kila mtu alipiga makelele kushangilia alichokisema mkuu wao. "Sasa mkuu mimi nitafanya nini?" Yule Bibi Nyamumwi aliuliza. "Wewe nataka ujigeuze uwe kama huyu bint, kesho asubuhi na mapema kabla hawajaamka ufike pale kanisani wakukute umelala ndani ya kanisa. Taarifa ya jinsi gani tutafanya kuusu kumkamata na kummaliza huyo Murcia tutakuwa tunawasilina" Kama vile ilikuwa umeme baada ya padre joseph kusema vile, yule Bibi Nyamumwi Bibi aliyekuwa emtoka upande wa magharibi kuongeza nguvu katika upande wa Mashariki, alijigeuza na kufanana kama Alicia. Kitendo hicho kila mmoja alikipongeza na kumshangilia. Wakiwa wanamshangilia mala aliingia kijana mmoja wa kiume. "Mkuu wale watu, wawili waliokuwa wameenda mjini tayari washakaribia kufika katika makutano ya njia mbili" Baada ya kijana yule kusema. Padre joseph alimwambia watoke vijana kumi wenye nguvu waende wakawakamate. Baada ya Agizo hilo hakukuwa na kuchelewa vijana wale walijikusanya kisha wakachukua Misumari mikubwa kabisa kama nondo iliyokuwa imechongwa vizuri na kuondoka nayo. ******** Ikiwa ndio inatimu mida ya saa mbili kama na robo Paulo na Moris wakiwa ndani ya Gari la kanisa kutoka mjini, ndani ya gari kukiwa kumesheheni vyakula na mafuta ya kupikia pamoja na mitungi mitatu ya Gas walifika eneo la njia panda sehemu ambayo ilikuwa na kona na sehemu hiyo ndio ilikuwa inapendwa na wachawi kufanyia madawa na wengine kutolea kafara yao, na ndio sehemu ambayo kikundi kilichoagizwa na joseph kilikuwa kwa ajili ya kufanya yao. Wakiwa hawana hili wala lile vijana wale wawili kwenye gari walishsitukia tu tairi ya mbele imelia Pa! Hicho kilikuwa kiashilia tosha kuwa tyre ya mbele ya Gari imepasuka. Kila mmoja ndani ya Gari alishituka, tayari walianza kujitayarisha kwa mapambano, eneo hilo hakuna ambaye alikuwa halijui kati ya wale wawili. Chaka au paulo yeye alikuwa anajua kabisa hapo ilikuwa ni sehemu ya wachawi kuchezea na kufanyia madawa yao, kwani hap kabla hata yeye alikuwa ni miongoni mwao. Moris anapakimbuka kwasababu siku ya kwanza kuja kwenye kijiji hicho cha zima moto ni hapo hapo Gari ilikwama akatokea kiumbe wa ajabu. Wakiwa bado vijana wale wanajiuliza mala kikosi kilichokuwa kimeagizwa na kikundi cha padre joseph kilijitokeza kutoka mafichoni. Chaka kwa ujasiri tena kwa kumtumainia Bwana na imani Thabiti alitoka ndani ya Gari na panga aina ya jambia alikuwa kalichukua mjini kwa ajili ya ulinzi kwa wenzake pale kanisani, alishuka ndani ya Gari kupambana nao. Hata Moris naye alipoona hivyo naye akachukua lake kama kijana wa kiume kwa ujasiri akaungana na mwenzake kupambana na jeshi la Shetani. Ilikuwa ni vita ya kifo timu ya vijana wawili wamtumikiawo bwana na timu ya watu kumi imtumikiayo shetani. Kabla awajalianzisha chaka/,paulo alisema. "Eee! Bwana Nipe nguvu na ujasili wa kuliangusha ili kundi la watu waovu, wamtumikiawo shetani bila kujua?" Usiku huo huo na mwanga wa mbala mwezi mapanga yalianza kulia, kweli Paulo alikuwa ni jasiri. aliweza kupigana na vijana wale na kuwajeruhi vibaya pale pale wote, kundi zima la shetani likakimbia na kutoweka. Ingawa Paulo naye alipatwa na majeraha kidogo lakini yeye Alilishinda kundi la shetani. kipindi hicho Moris yeye alikuwa kajificha chini ya uvungu wa Gari baada ya kuona vita ile sio ya mchezo. Kazi ilibaki ni kutoka hapo, uwezekano haukuwepo tena, ingawa tairi walikuwa nayo lakini Moris aliogopa kutoka inje ya Gari kwa hofu ya watu wale kurudi, Paulo alimng'ang'aniza na kumuomba ili aweze kutoa na kubadili tairi ya gari kwa kusadizana wawili, Moris aliogopa kabisa na kugoma. Ni muda huo huo Kilitokea kikosi kingine hicho kikiongozwa na Mwenywe padre Joseph pamoja na kiongozi wa upande wa Nagharibi pale pale kwenye gari. Hawakuweza kujua jinsi padri Joseph alivyoingia ndani ya Gari na kuwatoa kisha kufungwa kamba na kuondokana nao wakaliacha gari hapo hapo. Waliongozana nao huku wakipigwa mijeredi mpaka katika jumba au kanisa la Shetani alikokuwa kaweka kambi yake Padre joseph. Huko walifika, wakaoneshwa kila ambacho tayari washakifanyakwa Waliokuwa wamebaki katika kanisa la bwana, waliwaonesha Sister Murcia akiwa hoi kabisa kalala kanisani usiku huo hakiwa hana matumaini. Wachawi hawo hawakuishia hapo walimuonesha Alicia jins alivyokuwa anataka kutolewa kafara. "Bado siku tatu tatamtoa kafara" Padre joseph aliwambia Paulo na Moris. "Baada ya yeye nyinyi Mtakaa hapa mteseke na njaa halafu siku ya Tano tutawafanya kama ambavyo wanaume huwa tunawafanya" Padre joseph alisema tena. Paulo na Moris wakiwa wamepigishwa magoti mbele ya Wachawi wote. Kipindi hicho wachawi wale walikuwa wakicheka sana. "Mkuu mimi huyu ungenipa tu, nimtafune mzima mzima yeye kajifanya kumfuata huyo sijui bwana; mbona hatuuoni msaada wake huyo bwana!" Nyamumwi alisema akiwa anamshika shika chaka mabegani. Baada ya hapo walitolewa na kuwekwa katika chumba kilichokuwa na harufu kali kama za uvundo wa vitu vilivyokufa. Huwezi kuamini kumbe wachawi huwa hawatumii uchawi tu, hata njia za kawaida za kumdhoofisha mtu huwa wanatumia wakiona wameshindwa kwa uchawi. Kama alivyo ongea Murcia wa kwanza kumwambia sister Murcia kuwa, ndani ya kijiji hicho kuna wasomi wakubwa wanaokitumia kijiji hicho kwa manufaa yao, ndivyo hivyo hivyo. Wachawi wale waliwachoma Paulo na Moris Sindano za kupunguza nguvu na kuwafanya walegee kabisa na kukosa nguvu. SHARE TAFADHALI. UNAOMBWA TENA UNAOMBWA KUSHARE KAZII HII NA PAGE ILI ITAMBULIKE HARAKA.

at 4:31 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top