SISTER MURCIA. NO.(08) ILIPOISHIA. Murcia aliwakusanya ili awaulize nini kimefanywa kwao na watu wale walikuwepo na mapanga. Wanafunzi wote kwanza walikuwa awaamini kumuona chaka/paulo yupo katika hali ya uzima kabisa. SONGA NAYO. Hapo kila mmoja moyoni akaanza kujua kuwa imani yake kweli ni ndogo. "Tangu sasa huyu mtamuita paulo" Murcia alisema. "Sawa" Hio ndio ilikuwa kauli ya kwanza kutoka kinywani mwa sister Murcia katika kikao chake, akimtambulisha chaka kwa jina jipya la paulo. "Hebu naombeni mnambie ni nini watu wale walifanya kwenu?" Murcia aliwauliza wanafunzi wake. "Walikuja kwa ajili yako walivyo dai!" Mercia alimjibu. "Kwanini ninyi msinge wazuia mkapambana nao?" "Sisi hatukua wenye huwezo wa kupambana nao, hata chaka aliyewazoea yeye alijaribu kupigana nao lakini wakamwangusha mala moja tu na kumjeruhi. Tulivyo ona hivyo hatukuwa tena wakukaa ikabidi tukajifiche humu, tukiwa humu wakasema hawakuja hata kwetu bali kwako!" Alicia alisem. Kipindi hicho chote Moris na Lucas wao walikuwa wamenyamaza wakiona aibu hata kuongea. "Tazameni ninyi watu. Mbona nwamuuzi bwana, tazama ninyi mmechaguliwa kwa ajili ya kukipambania kijiji hiki ili kukibadilisha. lakini ninyi mnafanya vyenye kumuuzi bwana mnakosa imani kabisa mnazidiwa na Paulo/chaka, ambaye hata kusoma na kuandika hajui. Je amna imani na bwana mungu wenu?" Murcia alizungumza kwa kufoka mbele ya wanafunzi wake. "Eeee! Murcia hakika wewe ndiye kiongozi wetu. Tusamehe na utufundishe yaliyomema, hakika imani yetu ni haba!" Mercia kwa kuwawakilisha wenzake alisema. Sister murcia alisikitika sana, akuamini kabisa kilichokuwa kinatoka vinywani mwa watu wale. "Hata wiki mbili hatujamaliza, bado hata kuanza kuwatembelea watu kwa ajili ya kuwapa fundisho la bwana sijui itakuwa vipi" Murcia alisema. Lilikuwa ni jambo la kumsikitisha sana Murcia. hakuweza kuamini, akaanza kujutia kwanini alichukua maamuzi ya kuongozana na watu wasiyokuwa na faida kwake. Usiku mzima hakuweza hata kusema nao tena mpaka kunakucha. Siku iliyofuata Murcia alimchukua chaka na kuingia naye kwenye sakarastia na kuanza kumfundisha kusoma na mafunzo mengine ya dini ya ukristo. Zoezi lilikuwa endelevu wanafunzi wengine aliwapa zoezi la kuisoma biblia na kuomba Mungu ili wapate kuzikuza imani zao. Zoezi la kumfundisha chaka lilimchukua wiki tu, mwanaume yule akaweza kusoma. Jambo hilo lilimshangaza sana Sister nurcia, hakuweza hata kuamini, imekuwaje mtu yule aliyekua na imani haba apate wepesi wa kujua kusoma mapema. Ikiwa ndio wamemaliza wiki ya Tatu pale kijijini, Murcia aliwakusanya wanafunzi wake wote ili kuzungumza nao na kupeana darasa juu ya uwepo wa Bwana. Wanafunzi wote walikusanyika wakakaa pamoja ili kumsikiliza mwalimu wao. Murcia aliwaomba kwanza chaka awambie ni nini siri yake ya kuweza kukisoma kitabu kitakatifu ndani ya wiki. Wakiwa makini kabisa wote kumsikiliza, chaka alisema. "Hakika haya sio mamlaka yangu kuja kwenu bali tu yeye yule aliyembingini!" Maneno hayo tu, yaliwafanya wote mpaka sister Murcia kumgeukia na kumtazama. "Ebu ninyi ndugu zangu tazameni. Kwani hata lile neno alilolisema bwana amkuliona?" Paulo/chaka aliuliza. Kila mmoja alibaki kumshangaa, wote hata sister murcia wakauliza "Neno gani hilo paulo?" "Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho." Chaka alisema. Neno hilo liliwashangaza wote, hakuna aliyeweza kuamini kama chaka anauwezo wa kuisoma biblia na kuyatambua yaliyomo kwa siku chache. "Ninyi; mimi nawambieni pia nawakumbusheni. Kwani siku ile ya kwanza kuja kwangu, Sister murcia aliwambieni nini kuusu mimi?" Hapo kila mmoja alinyamaza hakuna ambaye aliweza kulijibu swali la chaka. "Basi alisema. Huyu ni mwenzetu, bwana kamleta kwetu ili awe njia kwetu! Je hakusema neno hilo?" Wote kwa pamoja wakaitikia alisema. "Mimi nayajua mengi hata msiyoyajua ninyi. Na ninyi amjui kwasababu imani zetu ni haba. Tizama maneno ya Bwana juu ya watu wenye imani na wasiyo na imani. Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo" Chaka/paulo alisema. Alicia, Mercia, Lucas na Moris walibaki kumshangaa chaka/paulo. Kila mmoja alitamani kujua chaka kawezaje kuisoma na kuyasema yaliyomo kwenye biblia bila hata kusoma. Uwezo wa chaka ukuwashangaza wenzake tu hata Murcia naye ulimshangaza. "Chaka unaweza kusema, umewezaje kuyajua hayo?" Murcia aliuliza. "Hakika imani ni ukombozi wa kila moyo katika ardhi ya bwana. Ndio maana Bwana akasema. " Mngekuwa na imani kama chembe ya Haradali basi mngeweza kuuwamuru huu mti wa Mkorosai ung'oke na ukajitose baharini, basi nao ungetii" Chaka alisema maneno ambayo kila mmoja yalimuingia. Chaka/paulo anasema kuwa walipokuwa anamaliza kufundishwa na Sister Murcia jioni. Muda wa kulala usiku yeye alikua akiomba ikifika muda wa saa saba za usiku bwana mungu haweze kumwamsha ili asome. Anasema kuwa "Mida hio nilikuwa natoka chumbani kwetu naenda ndani ya Sakarastia. muda huo nilikuwa naamini kuwa sister Murcia alikuwa kaisha toka ndani ya Sakarastia. Nilikuwa nikifika pale mlango unafunguka wenyewe, nami niliingia na kusoma, nilifanya hivyo katika siku tano nikawa nimeweza kuisoma biblia" Huyo ndio ukweli kuusu kijua biblia. Mazungumzo yao yalichukua muda kama saa zima yakamalizika. Baada ya kumaliza kikao hicho chaka/paulo alimuomba sister Murcia wazungumze kwa usiri. Wote kwa pamoja wakaongozana kuelekea kwenye Sakarastia. Walipofika ndani ya Sakarastia Paulo alimwambia Sister Murcia. "Je waonaje juu ya hili jambo la mtoto mwema atokaye kwa bwana kwa ajili ya kukiokoa kijiji hiki?" Maneno hayo kutoka kwa chaka yalimshangaza sana, Murcia hakuamini kama paulo/chaka naye analijua swala hilo. "We umejua vipi?" Sister murcia aliuluza. "Nikiwa nimelala usiku humu ndani ya Sakarastia nimepatwa na ndoto, kutoka kwa mtu aliyekuwa kashikilia kitabu akanambia. Yupo mtoto mwema mwenye kuzaliwa kwa ajili ya kijiji hiki kutoka katika kizazi cha watu wema. Huyo ndiye mwenye mamlaka ya kukikomboa kijiji hiki. Nilipoambiwa hivyo nilishituka kutoka usingizini na kurudi chumbani kwangu" Paulo/chaka alimwambia sister murcia. "Mala ya tatu nalisikia neno hili, tena nimeoneshwa mtoto akiniita mama huku akinikomboa kutoka katika kundi la shetani" Sister murcia alijisemea kimoyo moyo. Kisha akamuomba chaka atoke inje yeye angelifanyia kazi. ******** Basi masaa yalienda sister murcia akaona tayari kuwa kipimo cha imani kwa wanafunzi kimekuwa Imara. Usiku huo wa siku hio aliwambia wanafunzi wake kuwa kesho wataanza kutembea ndani ya kijiji ili kulitangaza neno la bwana kwa watu wa kijiji cha shimo la moto. Kwakuwa kipindi hicho walikuwa salama kabisa awasumbuliwi na kundi la Shetani kesho kulikucha salama na safari ya maandalizi yao ya kutembelea miji ya wakazi wa kijiji hicho cha shimo la moto ikaanza. Walikitembelea, walijitahidi kupita kila nyumba waliyokuwa wanakutana nayo, muongozo wa msafara alikuwa ni chaka/paulo. Ilikuwa ni safari ya kusumbuka kwao, nyumba zingine walijaribiwa kwa uchawi lakini waliweza kupambana nao na kuushinda. walijitahidi kuubili sana kwa watu wa kijiji hicho. lakini kwao ilikuwa ni ngumu kueleweka. Siku ilipita lakini hawakupata hata mtu wa kuongozana nao. Kesho yake tena walikwenda hivyo hivyo, lakini bado hawakupata mtu aliyeweza kuyafuata mafundisho yao. Walifanya hivyo wiki, bado hawakuweza kupata hata mtu mmoja katika watu wa kijiji hicho. Zaid walizidi kukimbiwa na hata watoto. Kazi hayo haikuweza kuleta matumaini. Ikiwa ndio siku ya tatu katika siku ya tatu ya juma chakula kiliwaishia, sister murcia akamuomba Moris na Chaka/paulo waongozane kwenda mjini kufuata chakula. Kijijini Murcia alibaki na vijana wake watatu. Alicia, Mercia na Lucas. Wakiwa inje ya kanisa wakifanya shughuri ya usafi mida ya saa 4 za asubuhi. Ghafra upepo mkari ulitokea giza nene likatanda kila mahara katika kijiji hicho, upepo ulikuwa mkari, vumbi likatibuka sehemu hio ya kanisa, hakuna aliyeweza kumuona mwenzake. Ilikuwa ni jambo la kushitukiza kwao. Itaendelea

at 4:31 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top