Home → simulizi
→ SISTER MURCIA,
NO.(07).
SISTER MURCIA AJIFUNGIA NDANI YA SAKARASTIA SiKU MBILI AKISALI. AOTA NDOTO MBAYA YA KUTISHA. AIKOLEWA NA MTOTO.
MTOTO AMWITA SISTER MURCIA MAMA.
ILIPOISHIA.
Na hata kwa wanaume pia ni kama ulivyotoa mfano wa mtume paulo alivyo fanya kwa kufuata shauri la Bwana. Lakini hakuna namna inabidi ujitoe kwa ajili ya kizazi hiki"
Murcia wa kwanza alisema.
SONGA NAYO.
Macho ya sister Murcia yalibaki kumtazam Murcia mwenzake. Kichani mwake alikuwa.Akitafakari ni jinsi gani ataweza kubeba mimba na kuzaa na wakati tayari yeye kaisha kula kiyapo kuwa yeye atabaki kumtumikia bwana tu wala si kwa swala lingine.
"Murcia nimeenda kuongeza Elimu yangu kwa ajili ya kuendelea kuwa karibu na Mungu. Mi naamini kabisa Mungu yu pamoja nami, Mungu awezi kuniacha niteseke na kukiacha kizazi hiki kiangamie lazima nitapambana na Mungu atanipa nguvu tu na kunilinda"
Sister Murcia alisema kwa upole.
"Murcia hata Bikira maria alitegemewa kuwa nabii wa bwana lakini akazaliwa mwanamke. Hakuweza kufanya mapenzi mpaka anachumbiwa, kwasababu alikuwa mwnamke mwema Mungu akampa mtoto kupitia Roho matakatifu, ambaye huyo mtoto ndiye mkombozi wa ulimwengu huu. Mungu aliona kuwa ulimwengu umejaa dhambi ndio maana akamtoa mtoto wake kipenzi na wa pekee kwa ajili ya ulimwengu. Tazama Mungu akakubari kumdhalilisha mwana kwa kutundikwa msalabani lakini kwa ajili ya ukombozi. Ingekuwa ni nguvu za Mungu kwa mwanamke si angemwacha Mariam ndiye akaukomboa ulimwengu kutoka Katika dhambi. Tafadhali hili niagizo la Bwana. Limepitia kwangu. Hata usipo amini bado mimi ni mkubwa kwako"
Murcia mkubwa alisema.
Baada ya kusema hayo Murcia huyo alisimama na kusema.
"Nilikuwepo hapa tangu miaka 23 iliyopita na leo naondoka kwakuwa mwisho wangu umepita. Tafadhali wewe ndiye mwenye mamlaka na chumba hiki, tangu sasa. Mtoto utakaye mzaa njoo mkabizi kwenye chumba hiki ili awe karibu na bwana"
Baada ya kusema maneno hayo, Murcia alitoweka kama alivyo tokea.
Akiwa Mwenywe mawazo ajui nini cha kufanya Sister murcia alijinyanyua pale alipokuwa na kutoka ndani ya Sakarastia. Japo alikabiziwa yeye chumba hicho lakini alipotoka tu hata akuugusa mlango wenyewe tu ulijifunga. Alikaa chini ndani ya kanisa akiyatafakari maneno aliyoambiwa ndani ya Sakarastia. Akawa aamini kabisa kama ni kweli machozi yakaaza kumtoka. akiwa bado yuko kwenye mawazo mengi, Alicia alikuja kumuita kwa ajili ya chakula.
Alicia alishindwa hata kumwambia Murcia swala la chakula, naye pia alikaa ili kujua nini kinamsibu mwalimu wao.
"Sister Murcia, nini kinakusumbua mbona unalia?"
Swali hilo Murcia akulijibu, alishindwa aanzeje kuongea na vijana wake kuusu kubeba mimba na kuzaa mtoto ambaye ndiye atakikomboa kijiji hicho cha shimo la moto.
"Naomba unambie kweli mimi nilisema kuwa anapaswa azaliwe mtoto mwema kutoka katika kizazi chema, ili awe mkombozi wa kizazi hiki cha Kichawi?"
Sister Murcia aliuliza kwa kujing'ang'aniza.
"Ndio umesema, tena umeanza kwa kutolea mfano kuwa sisi si wenye imani thabiti. Kuwa nasi ni sawa na mwamvuri wakati wa mvua iliyoambatana na kimbunga"
Maneno hayo sister Murcia aliyasikia lakini akashindwa kuamini kabisa. Ilimbidi amrudishe murcia na kumwambia kuwa waendelee kula yeye ajisikii njaa. Akiwa na masikitiko makubwa sana moyoni. Murcia aliamua arudi ndani ya sakarastia kumuomba Mungu amuoneshee ukweli juu ya jambo hilo.
*******
Murcia alikaa ndani ya Sakarastia siku mbili. siku mbili bila kunywa wala kula. alikuwa kama ni mtu aliyefunga akiomba. Ikiwa ni Majira ya saa sita mchana, Kutokana na njaa Murcia alianguka chini ndani ya Sakarastia. Alipoanguka pale pale, usingizi ulimpitia kabisa. Akiwa usingizini aliota ndoto akiwa polini karibu na mto akionekena mwenye Damu kwenye nguo zake. Alisikitika sana, akazivua nguo zake na kuzifua. baada ya kuzifua akazianika, akiwa bado anasubili zikauke avae, alisikia makelele kama kimbunga na sauti za ajabu kama za watu zikimfuata. Ghafra aliona kundi la watu nane wa ajabu likimsogelea, watu hao walionesha dalili zote za kuwa ni wachawi, walikuwa ni watu wazima kabisa. Wanne wakiwa ni wanawake na wannne wakiwa ni wanaume. Murcia alishindwa afanye nini na kipindi hicho alikuwa hana nguo. Baada ya kuona kundi linazidi kumsogelea alisogea kinyume nyume mpaka zilipokua nguo zake na kuzichukua hivyo hivyo na kujifunga kusitili sehemu za wazi. Akiwa anafanya haraka haraka, sister murcia alipiga magoti na kusema. Eee mungu, nilinde na hili kundi baya la Shetani. Kitendo cha kusema hivyo tu, alitokea mtoto mmoja wa kiume umri kama miaka mitano, mtoto huyo alikuwa kavalia mavazi meupe kama padre mbele yake. Mtoto huyo alilinyoshea tu mkono kundi lile la watu likaanguka chini na kufa pale pale.
Baada ya kitendo hicho, yule Mtoto alimsogelea sister murcia na kumwambia
"Mama nenda kwa Amani kwani ufalme wa bwana uko juu yako nami pia niko mbele yako"
Bado akiwa usingizini aliisikia sauti ikimwiita Mama, amka amka tayari amka. Sister murcia akiwa na njaa kubwa alishituka. Kutoka usingizini huku akiwa anahema, ndoto aliyoita ndio ilisabisha kushituka. Lakini alivyoshituka usingizini macho yake yalikutana na Mtoto kama huyo aliyekuwa naye ndotoni kaweka chakula mbele yake na kumwambia
"Mama kula uwasadie wanafunzi wako kwani hata sasa wanateseka hawana msaada"
Baada ya kusema hivyo yule mtoto alitoweka mbele ya macho yake. Sister Murcia alishindwa kuamini kabisa kile alichokiona, bado alishindwa kayaamini macho yake. Akayapikicha akiamini kuwa yupo usingizini lakini ilikuwa ndio ukweli. Kusimama alishindwa kwasababu ya njaa ikabidi aombe sala ya chakuka.
Akaweka njia ya msalaba.
"Kwajina la Baba na la mwana na la roho mtakatifu amina.
Eee baba yetu uliyembinguni, nashukuru kwa kuniwezesha chakula nile ili nipate nguvu ya kukutumikia vema amina"
Baada ya kumaliza kusali sala hio fupi sister murcia alikila chakula hicho ambacho ilikuwa mikate mitamu iliyoshushwa toka mbinguni. Alipomaliza kula. Akamshukuru Bwana kwa chakula kisha akaomba kutoka.
Mlango wa Sakarastia ulifunguka sister murcia akatoka. Alikuta tayari ni giza kumbe toka alale saa sita za mchana alikuja kuashwa saa moja za jioni. Kanisani aliwakuta wanafunzi wake kila mmoja kajikunja kwenye kona yake kwa uwoga.
Alipotazama inje aliona kundi la watu kama nane wakiwa wameshikila mapanga. Watu wale walikuwa wamekaa tu na walikuwa wanaume tupu. Pembeni yake alimuona chaka kafungwa kamba na akiwa na majeraha usoni, na miguuni sistet Murcia aliumia sana kumuona chaka yupo katika hali ile. Bila kuogopa sister murcia alitoka inje ya kanisa kuwafuata watu hao . Alipotoka tu inje ya kanisa kichwa chake kikaanza kutoa mwangaza wa mkali, watu wale walipomuona tu hivyo wote walikimbia kila mmoja njia yake hakuna aliyebaki kuendelea na kilichokuwa kimemleta. Sister murcia mwenywe alibaki anajishangaa lakini tayari alijua kuwa ni ufalme wa Bwana u juu yake. Alimsogekea Chaka na kumwangalia akagundua kuwa amepoteza fahamu, bila machozi yalianza kumtoka sister Murcia, pale pale jina la kumuita chaka la kikiristo likamuhijia.
"Paulo amka, Amka paulo!"
Maneo hayo mawili mala mbili, majeraha yote yaliyokuwa katika mwili wa chaka/paulo yalififia yote, akarudi katika hali yake na kusimama. Baada ya tukio hilo sister Murcia aliongozana naye mpaka kanisani akawakuta wanafunzi wake Moris, Lucas, Mercia na Alicia. Wote wamejikunja pande zao.
Murcia aliwakusanya ili awaulize nini kimefanywa kwao na watu wale walikuwepo na mapanga.
Wanafunzi wote kwanza walikuwa awaamini kumuona chaka/paulo yupo katika hali ya uzima kabisa.
Share tafadhali. Kufanya hivyo ndio faraja yangu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: