Home → simulizi
→ SISTER MURCIA.
NO.(06).
YAWA NGUMU KWA SISTER MURCIA KUKUBARI MANENO ALIYOAMBIWA KUUSU KUZAA.
BAADA YA KUENDELA KUBISHANA SANA MWENYE SAUTI YA AJABU AJITOKEZA.
ILIPOISHIA.
"Murcia jina lenye siri kubwa. Mimi ndiye nasitahili kujitoa kwa ajili ya kizazi chema"
Sister murcia alisema kisha akasimama na kurudi ndani ya Sakarastia.
SONGA NAYO.
Sister Murcia aliisogelea mlango wa Sakarastia lakini ukufunguka akajaribu kuusukuma bado kwake ilikuwa ngumu, akawaita wanafunzi wake wote na kuwambia wajaribu kuusukuma wote kwa pamoja. Badala ya kumsaidia nao pia wakabaki wanamwangalia tu.
"Ninyi badala mje mnisaidie. Mmesimama tu, mananiangalia!"
"Hapana sister hata sisi tunashangaa kwanini umekushinda na wakati unatoka ndani kuja kuingia ulifunguka wenyewe tu?"
"Sasa mnamaanisha nini?"
"Inaonekana mlango huo ukijifunga mpaka utake wenyewe kujifungua"
Alicia alisema.
Baada ya kushindwa kuufungua mlango wa Sakarastia Sister Murcia aliwambia wanafunzi wake waendelee na shughuri zao wamwache mwenyewe kanisani.
"Lakini sister kuna jambo umelisema sisi bado linatupa mashaka!"
Mercia alimwambia sister murcia.
"Jambo gani hilo Mercia?"
Sister murcia aliuliza.
"Umesema kuwa, kwasababu ya udhaifu wetu wa Imani tutasababisha kizazi cha kijiji hiki kishindwe kukombolewa mpaka Azaliwe mtoto kutoka katika kizazi chema. Na huyo mtoto ndiye atakaye kikomboa kijiji hiki!"
Maneno hayo ya kweli kabisa kutoka katika kinywani mwa Mercia. Yalimshangaza Murcia, akabaki kuwaangalia wanafunzi wake asijue azungumze nini.
"Sister Murcia mbona usemi?"
Alicia aliuliza baada ya kuona sister wao kanyamaza kama anatafakari jambo.
"Hapana! Nimesema saa ngapi maneno hayo?"
Murcia aliuliza.
Ulisema kipindi tu, unatoka ndani ya Sakarastia ukiwa umebeba kitabu hicho hivyo hivyo".
"Kweli?"
"Ndiyo!"
Sister Murcia aliuliza kwa mshangao, kwasababu kilichozunguzwa kuwa yeye ndiye kakisema sio kweli, japo ni cha kweli lakini yeye hajasema bali kakisoma kwenye kitabu alichopewa ndani ya sakarastia. Alichokisema Mercia kimetamkwa na malaika mwema wa bwana.
Baada ya kuona kuwa kilichozungumzwa na wanafunzi wake kimemuingia Murcia aliwaomba wanafunzi wake wakendelee na shughuri zao yeye atawapatia majibu baadaye.
Wanafunzi wake walimwacha na kwenda kuendelea na Shughuri zao.
Akiwa mwenye mawazo mengi, akitafakari alichokisoma na alichoambiwa vyote vinafanana, lakini ni nani kakisema ambacho Ameambiwa na Mercia kuwa yeye ndiye kakitamka. Hilo lilikuwa ni swali alilokuwa akilitafakari sana Sister Murcia.
Baada ya kufikiri kama dakika tano bila majibu aliamua arudi kwa Bwana mungu wake. Huko alijua majibu lazima hayapate.
Murcia aliisogelea Bikira maria na kuanzia kusali sala ya salamu Maria. Baada ya kumaliza aliyainua macho yake akaanza kuomba alichokuwa anakihitaji kwa Mwenyezi mungu, akiwa anaendelea kusali, Mlango wa Sakarastia ulifunguka, sauti ya Ajabu ikaanza kumuita kutoka ndani ya Sakarastia. Kwa utulivu kabisa aliisikia sauti hio, ikimuita. Baada ya kuisikia sauti hio, sister murcia alijinyanyua na kuelekea kwenye Sakarastia. Alipoingia tu mlango ukajifunga.
"Murcia umesoma kitabu hicho?"
Sauti iliuliza.
"Ndio nimesoma!"
Sister murcia alijibu.
"Kipi ambacho ujakielewa?"
Sauti iliuliza.
"Mengi tu sijayaelewa na sijui kwanini!"
Murcia alisema.
"Najua hujaelewa lakini mimi nimekaa miaka yote hio 23, tena ndani ya Sakarastia humu, humu. Huwenda wewe kipindi hicho ndio ulikuwa na miaka 12, uwezo wangu wa kuongea na mungu ni mkubwa kuliko wewe, vigezo mimi nalala humu humu, nakula humu, na macho yangu yamejizuia na kuona mambo ya Dunia. Wakati wote yanasoma na kutazama mamlisho ya mungu. Kinywa changu Akifanyi kingine zaidi ya kulitaja jina la Bwana mungu wetu aliye hai mbinguni"
Sauti ilisema.
"Murcia sasa wewe, kwanini aliamua kukaa humu na kushindwa kukiokoa kijiji hiki cha wachawi?"
Sister Murcia aliuliza sauti Ambayo pia mwenye nayo anadai ni Murcia.
"Nilibaki mwenyewe tu, sikuweza hata kufanya chochote, hapo niliamua nimuombe mungu aniifadhi humu mpaka nitakapokufa!"
Baada ya kuambiwa Hivyo sister Murcia hakutaka kuuliza chochote kuusu maisha ya Murcia kwasababu alikuwa anajua kabisa sifa zao, Murcia wote ndio kawaida yao. Walikuwa ni watu wa kufungamana na mungu muda wote. Alibakiwa na maswali mawili tu ambayo yalimuusu yeye.
"Nimesoma katika kitabu umesema jina la Murcia ni la siri kubwa. Napenda kujua?"
Sister Murcia aliuliza.
"Soma historia yako. Wewe uliitwa Judith. Jina hili lilikufa tu, baada ya kukulia katika chuo cha utawa, kilichopo katika kanisa la Mtakatifu Joseph. Dalili za kwanini wewe Uliitwa Murcia ni kwamba wewe, ulikuwa na Upeo mkubwa wa kuongea na Mungu. Namaanisha ulikuwa unaomba chochote lazima kitimilizwe, watu wa aina hio tu ndio wanaitwa Murcia. MURCIA ni neno la kirumi lenye maana. UKARIBU KWA MUNGU"
Maneno hayo kutoka kwa Murcia ambaye Sauti tu ndio inasikika yalimuingia sister Murcia na kuayaelewa.
"Nimesoma kwenye kitabu, kuwa Kijiji hiki hakiwezi kukombolewa na Mwanamke mpaka azaliwe mtoto mwema wa kiume kutoka katika kizazi chema. Na ukanipendekeza mimi ndio nastahili kumzaa mtoto huo?"
Sister Murcia aliiuliza Sauti.
"Dalili zote ushaziona. Na nazani Mungu hakupitisha kwangu tu taarifa hizo. bali kazipitisha kwako kupitia mwanafunzi wako.
Murcia si lazima we kufanya hivyo lakini tayari utabili kutoka kwa mungu siku zote huwa wa kweli na wala huwa haupingiki wala kukimbiwa.
Kumbuka wewe nikiumbe chema murcia hata ikienda wapi, mikono ya Mungu itakuwa juu yako tu, ndio maana wewe unastahili kubeba mimba kutoka kwa mwanaume mwema ili umuzae mtoto aliyemwema kwa ajili ya kijiji hiki. Hakika sisi wanawake tuna udhaifu mkubwa ingawa tayari historia yetu sisi wanawake mabikira tunaomuenzi Bikira maria ni strong kutoka ulipoanzishwa"
Sauti ilisema, kwa msistizo maneno hayo yalimuingia sisiter Murcia lakini bado ilikuwa ngumu kukubaliana nayo.
"Ebu angalia hata katika kitabu sisi wanawake mabikira tulivyo na sifa ya kipekee. Kufuatana na mifano ya Yesu Kristo na Bikira Maria, Agano Jipya linatoa habari za wanaume na wanawake waliojinyima ndoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu, kama vile mabinti wanne wa Filipo mwinjilisti waliokuwa mabikira na manabii (Mdo 21:9). Hasa mtume Paulo aliwahimiza Wakristo wowote wanaoweza wafanye hivyo kama alivyofanya mwenyewe kwa kufuata shauri la Bwana (taz. 1Kor 7:25-34). Nitaanzia wapi kuzaa wakati tayari nishakula kiyapo kikubwa, Murcia bora nipambane mimi mwenywe"
Sister murcia alisema tena mpaka kwa kuutoa mfano mwema wa wanawake Bikira kutoka ndani ya biblia.
Baada ya kusema hivyo, ghafra mwanga mkubwa ulitokea mbele yake. Kilichotokea pale alikuwa mwanamke mzuuri mwenye mng'aro wa pekee.
"Mimi ndiye Murcia wa kwanza kwako. Hata mimi nasikikitika lakini lengo ni kukikomboa kijiji hiki.
Kumbuka Lengo la Ubikira kwa wanawake ni kumuenzi na kumtukuza Mtakatifu aliyebarikiwa kuliko wanawake wote. Pia ni sifa ya kipekee kuonesha ukristo ulivyo na nguvu kuliko kikingine chochote.
Na hata kwa wanaume pia ni kama ulivyotoa mfano wa mtume paulo alivyo fanya kwa kufuata shauri la Bwana. Lakini hakuna namna inabidi ujitoe kwa ajili ya kizazi hiki"
Murcia wa kwanza alisema.
ITAENDELEA.
SHARE TAFADHALI ILI NAMI NIENDELEE KUIANDIKA.
TAFADHALI SAIDIA KUIKUZA PAGE NA RAFIKI ZAKO WAIONE. NAPENDA UFURAHI LAKINI MUDA NAO TUMIA SI MDOGO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: