SISTER MURCIA. NO. (05) SISTER MURCIA ARUDI TENA NDANI YA SAKARASTIA SAUTI YA AJABU YAJA. APEWA KITABU CHA UKWELI KUUSU KIJIJI CHA SHIMO LA MOTO. ALICHOKIKUTA KIMEANDIKWA NDANI CHAMSHANGZA. ILIPOISHIA. Moris akajaribu kuushika mlango huo ili afungue lakini hakuweza hata kuufungua. Hakawambia wenzake kuwa ni mgumu kufunguka nao pia wakajaribu lakini wilishindwa hapo kila mmoja akajawa na uwoga na kutoka inje ya kanisa. SONGA NAYO. Vijana wote wanne kila mmoja alibaki akijuiliza kwanini Sakarastia imejifunga pekee kunanini. mbali na hilo Kazi waliyoifanya ya kulisafisha kanisa ilikuwa si ya mchezo ilikuwa ni kazi kubwa kutokana na uchafu lakini ndani ya Sakarastia kulikuwa safi. ingawa ilikuwa imefungwa lakini hata vumbi wala utando wa buibui hukuwemo. Kila mtu alikuwa na lake. Wakiwa kwenye wimbi la mawazo hivyo hivyo Alicia na Mercia walienda kwenye chumba chao. Kumwangalia Sister Murcia lakini walikuta kaufunga mlango, wakajaribu kuita hakuweza kuitika. Walipoona hivyo wakaenda kuchungulia dirishani wakamkuta sister murcia anasali. Walikaa wakamsubili amalize ndio wafanye shughuri, zingine. Alikaa muda sana ndani ya chumba murcia akisali. Alitumia kama saa moja na nusu ndio akatoka Inje na kwend moja kwa moja mpaka kanisani. Murcia aliusogelea mlango wa Sakarastia, alipoukaribia tu, ukafunguka wenyewe. Sister Murcia akaingia. Pindi yote hayo yanafanyika Mercia, Alicia, moris, Lucas na chaka walikuwa wanaona. Sister Murcia alipongia tu ndani mlango wa sakarastia ukajifunga kama ulivyokuwa. Murcia akasalia ndani peke yake. Hakiwa huko huko ndani ya Sakarastia sauti ya Hajabu tena ikaanza kuliita jina lake, sauti hio Murcia alishindwa kutambua ni yanani. Aliendelea kuisikiliza sauti hio ambayo yeye mwenyewe alikuwa haitambui kabisa kabisa inatoka wapi na ninani anayeitamka. "Murcia, Murcia, murcia. Sogea upande wa kulia mwa kabati hio yenye vitabu kuna box ndogo ya mbao uifungue utakacho kikuta ukichukue" Sauti hio ambayo Murcia alikuwa hajailewa inatoka wapi na ninani anayeizungumza ilianza kumuongoza. Bila kusita Murcia naye alifuata maelekezo ya sauti hio ya ajabu. Alipoichukua box alioambiwa kuichukua akaifungua akakuta kitabu kidogo kabisa akakichukua kama alivyo ambiwa. Baada ya kukichukua kitabu hicho Murcia alisema. "Bila shaka we utakuwa ni malaika wa bwana, uliyetumwa kwangu ili kuniongoza na kunilinda. Basi niongoze katika ukweli na unilinde kama Bwana mungu wetu alivyokuagiza" Sister Murcia alisema. Baada ya kusema hivyo ile sauti ilimjibu. "Hapana Murcia, hapana mimi siye maraika wa bwana bali binadamu kama wewe" Sasa kama ni binadamu mbona sikuoni?" Sister murcia aliuliza. "Soma kitabu hicho kwanza basi nami utanijua ni nani, ukimaliza utarudi" Sauti ile ilisema kisha ikanyamaza. Akiwa anataka kuzungumza kitu mlango wa Sakarastia ukafunguka. Sister murcia kwa hofu, akijiuliza mwaswali mengi kuusu sauti hio, alitoka inje ya sakarastia. Alipotoka tu na mlango ukajifunga. Vijana wake walikuwa wakimsubiri sister ndani ya kanisa wakingoja wamuulize ni kwanini hayo yanatokea. Wengine mpaka wakaanza kuogopa. Lakini hata kabla hawajauliza wao sister murcia yeye ndiye aliwauliza. "Nazani hata sasa, mmejawa na hofu na maswali mengi vichwani mwenu yamerundikana. Kwani si mwataka kuuliza?" Kila mmoja alishangazwa na alichokisema sister Murcia. "Sasa kajuaje kama sisi tunamaswali?" Wote waligeukiana wakaulizana, isipokuwa chaka kwasababu yeye alikuwa bado hajui chochote kuusu habari za kanisa zaidi yeye alikuwa akijua hasa maswala ya uchawi. "Amin nawambieni ninyi. hakika imani zenu ni ndogo. Imani zenu kwangu ni sawa na kutembea na mwamvuri, wakati wa mvua iliyochanganyika na kimbunga. Je unazani utakusaidia?" Baada ya Murcia kusema maneno hayo wanafunzi wake wote walipiga magoti na kumuomba msamaha. Chaka naye bila kujua akapiga magoti naye kuomba msamaha. "Tazama nawambieni mimi. Ninyi mmefanya mpaka kizazi chema kitakachotoke katika tumbo la mtu mtakatifu na mwema ndicho kije kukikomboa kizazi hiki kwani ninyi si wenye kuweza" Kauli hio ilimshitua kila mtu pale. Mercia, Alicia, Moris na Lucas walikuwa wakijua kuwa ni maneno kutoka kinywani mwa Sister murcia kumbe hata yeye alikuwa kanyamaza tu akiwaangalia wanafunzi wake hao. Sauti hio ilikuwa ni ya Malaika wa bwana iliyekuwa juu ya kichwa cha Murcia. "Kizazi cha mtu huyo mwema ni miongoni mwenu" Malaika wa bwana alisema tena. Baada ya kusema tena hivyo na wanafunzi wote wakiwa wamepigwa na bumbuwazi kwa maneno waliyoamini kuwa yanatoka kwenye kinywa cha murcia kumbe hapana bali kutoka kwa malaika mwema wa bwana. Alipotea na kumwacha Murcia peke yake. "Unajua mimi nawashangaa. Badala muandae chakula cha mchana tule ninyi bado mmekaa. mnajiuliza nini mbona mmezubaa sana?" Hio ndio ilikuwa kauli ya Sister murcia. Bila hata kuzungumza chochote wanafunzi wake. Yaani, Mercia, Alicia, Moris na Lucas pamoja na chaka wakatoka inje na kutekeleza alichokisema mwalimu wao. Sister murcia yeye alibaki kanisani kukisoma kitabu alicho pewa ndani ya Sakarastia. Murcia alikigeuza kitabu chake kwa upande wa mbele akakuta kimeandikwa. Ukweli kuusu kijiji cha shimo la moto na ukombozi wake. Maneno hayo yalimshangaza sana sister murcia, ikambidi akifungue kitabu na kuanza kukisoma. Jina langu ni Murcia na hiki ndicho kijiji cha shimo la moto. Nilifika katika ukanda huu mnamo mwaka 1991 mpaka sasa yapata miaka 23, nipo katika kijiji hiki cha shimo la moto. Nilifika huku na padre John Joseph. Mimi nilizaliwa katika mji wa BUKOBA TANZANIA. nilianza kulitumikia kanisa tangu nikiwa na umri wa miaka mitano tu, muda wote nilimtumainia Bwana mungu wangu nilifanya kila jambo kwa kumtegemea mumgu. Nikiwa na Umri wa Miaka kumi nilikuwa tegemezi kubwa katika maombi kwa mungu. Nikawa nauwezo wa kuwaponya wagonjwa, kupitia imani kubwa ya bwana. Baada ya wazazi wangu kuliona hilo waliona si vema kukaa Tanzania, Tukasafiri nao kunipeleka Vatican katika kanisa kuu Takatifu la Roma duniani. Ndani ya kanisa nilifundishwa taratibu za utawa, jina langu la kuzaliwa niliitwa Joyce, ilipofika kule nikaitwa jina la MURCIA, jina hilo linasiri kubwa na huwa ni kwa watu maalumu. Ndani ya kanisa takatifu la Vaticani moyo wangu ulikuwa umefungamana na mungu. Muda mingine sikutaka hata kula nilijifungia ndani ya chumba changu nikifanya ibada ya kumtukuza na kumuomba mungu wangu moyo wangu ukafungamana na mungu mungu kuliko watawa wote. Na hata nilipo hisi njaa peke yangu ndani ya chumba. chakula kiliweza kusushwa na Malaika wa Bwana nikala nikashiba. Nilipofikisha umri wa miaka kumi na tano. Uongozi wa kanisa takatifu ulipendekeza niwe kiongozi wa watawa wote ndani ya kanisa. Sikutegemea kama ningeweza kuwa na cheo kikubwa vile. Nilikubali nami nikawaongoza watawa wote. sielewi akili na Busara zangu zilitoka wapi, lakini kila Mtawa mwenzangu alipokuwa ananitazama lazima ainame na kuniitii. wangine wakawa wanapiga magoti mbele yangu. Muda wote huo bado nilikuwa sielewi kwanini wananifanya hivyo. Kumbe kichwa changu kilikuwa na nuru. niliweza hata kuomba chochote kutoka kwa bwana basi nami nilipewa. Mnamo mwaka 1989. Ndio siku ambayo nilikutana na Padre John joseph, alipokuja Kuongeza elimu yake ndani ya vatican. Padre Joseph alizipata taarifa zangu akanifuata na kuongea nami kuusu kurudi nyumbani. Tanzania, nikiwa mwenye furaha hasa, nilikubari kurudi Tanzani hata kwa wiki basi. Nikiwa nimeongzana na padre Joseph tuliianza safari ya kuja Tanzani. Tulifikia ndani ya kanisa kuu la Mtakatifu joseph jijini Dar es salaam. Tulikaa siku mbili lakini katika hizo siku mbili padre john joseph hakunitambulisha hata kwa watawa wala hawakunijua. Kwakuwa hata kipindi hicho kiswahili nilikuwa sikujui nilishindwa kuzungumza nao. Lugha yangu ilikiwa ni kiitaliano basi, hio ni kwasababu nimekulia Italia toka nikiwa mdogo. Baada ya siku hizo mbili kukaa pale. Tuliondoka tukaja hapa morogoro, mpaka kwenywe hiki kijiji cha shimo la moto. Pindi tunakuja katika kijiji hiki kulikuwa tulivu sana. Tulifika hapa wawili tu na Padre Joseph. Kanisa hili lilikuwepo na inasadikika lilijengwa miaka 80 iliyopita na wakorono wa kijerumani. Baada ya kufika hapa siku mbili Padre John joseph aliniomba tukitembelee kijiji hiki cha Shimo la moto tena ilikuwa ni majira ya saa moja za usiku, kipindi hicho kijiji hiki, kilikuwa hakina sifa za kutisha. Nilikubali nikaongozana naye mpaka kwa kiongozi wa kijiji hiki. Ambaye ndio kiongozi wa kundi la upande wa mashariki wa wamtumikiao shetani. Tulipofika hapo yule kiongozi alisema neno moja kwa padre john kuwa TAYARI. Sitolisahau neno hili. Kamwe sitolisahau. Baada ya kusema neno hili niliombwa kuingia ndani nyumba ya kiongozi huyo. Sikuelewa mabadiliko yalitokea wapi niliisi kizunguzungu na kuanguka kisha nikapoteza fahamu. Baada ya hapo nilijikuta tu, niko inje ya kanisa, bahati nzuri sikuwa na jeraha lolote namshukuru sana mungu. Sababu iliyonifanya niweze kunguka kumbe ulinzi wa mungu hukuwa kwangu, basi uchawi uliweza kuniingia na kupoteza fahamu. Mapenzi makubwa ya Bwana mungu wetu ndio yaliyonitoa ndani ya nyumba ya kiongozi huyo mpaka hapa kanisani. Baada ya kufika kanisani niliingia ndani ya Sakarastia. mpaka leo makazi yangu ndio haya. Inasemekana kijiji hiki uchawi ulikuwa ni wakwao na lakini ulikuwa si wa nguvu kiasi kama cha leo. Japokuwa katika kijiji hiki kila mtu ni mchawi. Uchawi wa vita ulianza tu, pale waliposhindwa kunitoa mimi Kafara lao, hapo ndipo mgawanyiko wa uchawi ulipoanzia. Ukawa ni vita ambayo ilizuka baina ya kundi la Padre joseph na kiongozi wa kijiji hiki. Vita hio ilikandamiza watu wote wa ngazi ya chini wengi walikufa kwa kukosa nguvu kubwa ya kichawi. Hapo ndipo ulipotokea mgawanyiko wa makundi mawili makubwa ya kichawi upande wa Mashariki na Magharibi. Kijiji hiki si wapumbavu wote bali kuna maprofessa wanaokiongoza na wasomi wakubwa wanaokitumia kwa ajili ya manufaa yao. Ukombozi wa kijiji hiki si kwa mwanamke na haitawezeakana labda kwa Kizazi cha kiume kutoka katika tumbo la mtu mwema na mume mwema. Mtoto atakaye zaliwa kutoka katika kizazi cha watu wema wawili, huo ndiye atakuwa chaguo halisi la kukikomboa kizazi hiki. Mtoto huyo atalindwa kutoka katika kizazi chema atakuwa chini ya mamlaka ya mungu na ulinzj mkubwa kamwe mkono wa shetani hutomfikia. Kwa Mwanamke itakuwa ngumu kwa sababu ikifika wakati wa siku mbaya ni vigumu sana mungu kuyapokea maombi yake katika uzito wake. Bali nikatika ulinzi tena usiomkubwa. Hizo ni siri ambazo washirikina wa hapa wanazo na wanazitumia. hutojua siku watakayojua wewe huko katika wakati mbaya bali utashangaa tu unaingia katika mtego mbaya. vita ni vichache ulivyo viona. Bado vita kubwa kutoka pande mbili ikiwemo upande wa padre joseph, ambaye yeye ndiye kiongozi wa upande wa magharibi. Murcia wewe ndiye unafaa kwa ajili ya kizazi chema kukikomboa kijiji hiki. Baada ya kukisoma kitabu hicho kidogo alichokitoa ndani ya sakarastia Murcia alichoka. "Murcia jina lenye siri kubwa. Mimi ndiye nasitahili kujitoa kwa ajili ya kizazi chema" Sister murcia alisema kisha akasimama na kurudi ndani ya Sakarastia. ITAENDELEA Kweli Murcia hatakubali kuuwacha utawa afunge ndoa ili ajifungue mtoto wa kiume hatakaye kikomboa kijiji cha Shimo la moto.

at 4:30 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top