MURCIA, ASIKIA SAUTI YA AJABU KUTOKA NDANI YA SAKARASTIA. AKIMBIA NA KUJIFUNGIA CHUMBANI. Shuka nayo. SISTER MURCIA. NO.{04} ILIPOISHIA. Baada ya tukio hilo kuwa gumu, mkuu yule wa wachawi aliamuru wampeleke Nyangubha katika kifungo asubili adhabu yake ya kukataa kuendelea kuwa mchawi. SONGA NAYO. Murcia na timu yake waliendelea kuomba. Usingizi kwao ulikata kabisa. Maombi ya Murcia yalikuwa ni mungu aweze kuwapa wepesi watu wa kijiji hicho cha kutisha wokovu wa uzima wa milele. Alicia na mercia kwa uwoga wao walipenda hata kulimaliza zoezi hilo kesho asubuhi. Waweze kurudi. Alicia na Mercia walikosa ujasiri kabisa wakuendelea kuomba pamoja na sister Murcia. Mawazo yao yaliwarejesha tena nyuma. Wakavikumbuka vyote walivyo kutana navyo njiani, Hasa mapigo ya moyo yalizidi kwenda kasi. walipokuwa wanamuona chaka jinsi alivyokuwa akionekana. Vazi lake lililokuwa ni kitambaa cheusi kajifunga kiononi, marangi aliyokuwa amepaka usoni. Muonekano wa chaka uliwatisha na kuwaogopesha sana. wakatamani warudi kwenye gari lakini waliona aibu, wakavumilia na kukaa wasubiri mpaka sister murcia amalize. Toka tukuio la wachawi kutokea sister murcia na vijana wake hawakulala walikuwa wanafanya maombi tu usiku kucha. Toka kipindi hicho hakukutokea kitu kingine cha kuwasumbua usiku ulikuwa umetulia ulibadilika ukawa angavu usiku mpaka kucha. Asububi mida ya saa kumi na moja ndio muda ambao Sister Murcia alimaliza maombi. Watu wengine wote walikuwa wanamwangalia tu, wao tayari walikuwa washachoka. Baada ya kumaliza maombi yake sister murcia. Alikaa akawambia vijana wake. "Hakika kweli hili ni shimo la moto hakika ni shimo la moto. Huku tunahitaji tuiokoe jamii ya watu wa huku wapate wongofu wala si kuangamiza, ingekuwa ivyo basi ningemuomba mungu akakiangamiza kijiji hiki chote kwa moto basi naye angefanya. Lakini kwanini hajafanya hata kukiangamiza kijini cha watu hawa. Kwasababu mungu alijua toka hawali kuwa ninyi ndio mtakiokoa kijiji hiki" Sister murcia aliwambiw vijana wake. "Lakini Sister Murcia huyu katoka wapi?" Mercia aliuliza hakiwa anamuoneshea chaka. "Ndio maana nikasema kwenu kuwa mungu kawaleta ninyi akijua kabisa ndio mtamletea ukombozi katika kijiji hiki cha shimo la moto. huyu anaitwa chaka. Tangu sasa ni pamoja nasi kwakuwa tayari yumo ndani ya mikono ya damu ya bwana. "kwani katoka wapi?" Alicia aliuliza. "Huyu kaletwa kwetu na mungu, mungu kamleta kwetu yeye awe njia yetu na mwongozo kwetu kwa kijiji hiki" Sister Murcia alisema. Baada ya kusema hivyo wote walinyamaza kusikiliza maagizo mengine kutoka kwa kongozi wao. Murcia aliwaomba wampe maji Chaka ajisafishe uso na lucas ampatie nguo zake avae. Baada ya kumaliza zoezi hilo sister murcia aliwaomba vijana wake waanze kazi ya usafi kanisani pamoja na vyumba viwili vilivyokuwa vimejengwa nyuma ya kanisa. Kwa ajili ya kulala watumishi wa mu gu. Maji kwao hayakuwa yashida kwani pale pale kanisani kwao kulikuwa na Kisima. Chaka alikuwa anafanya kazi kwa juudi sana kuliko wengine wote. Kitendo hicho kilipelekea sister murcia kuvutiwa naye sana na akamfanya mfano kwa wenzake. Siku nzima kwao ilikuwa ya usafi tu. Kiujumla mazingira ya kanisa yalionekana vizuri kabisa. Kila kitu kinachousu chakula walikuwa nacho kutoka mjini. Kwakuwa mazingira ya kijiji hicho yalikuwa hayana umeme pia walikuwa na Solar waliyoifunga kuwasaidia katika mwanga nyakati za usiku. Toka asubuhi, mchana, jioni hakukutokea kitu cha kuwatisha. Siku hio kwao ilikuwa safi kabisa hata usiku wake walila vizuri tu. Kwelj ulinzi wa mungu ulikuwa juu yao. Ikiwa ni siku nyingine mpya. Ilikuwa siku ya Ijumaa. Sister murcia aliomba afunguliwe chumba cha kuifadhiwa vitu vya kanisa. (SAKARASTIA) Chumba hicho kilikuwa kimefungwa na ijulikani mala ya mwisho kufunguliwa ilikuwa ni lini ingawa walikuwa wanajua kabisa kuwa ni miaka miwili huko nyuma ndio alikuja padri akiyejulikana kwa jina la Joseph. Lakini naye pia haijulikani aliishia wapi. Kwani toka aingie kijijini hapo hakuwahi kuonekana kabisa na wala taarifa zake hawakuwahi kuzipata. Moris wakishilikiana na chaka, pamoja na Lucas waliweza kulibomoa kufuri la chumba hicho kilichokuwa kimefungwa miaka kazaa nyuma. Walipoifungua sakarastia kila mmoja alistaajabu walizani watakutana na harufu mbaya, vumbi kibao na takataka zingine. Lakini kulikuwa angavu mwanga wa ajabu na pakiwa safi kabisa hata makabati yake yalionekana kung'aa. Murcia aliinua mikono juu kumshukuru mungu kwa ulinzi wake kwa vitu vyake kuviweka salama muda wote. Akiwa na wanafunzi wake. Walitaka kuimgia mdani ya chumba hicho lakini walishindwa kabisa, kila walipokuwa wanajaribu bado walishindwa. Ikawa kama vile kuna nguvu iliyokuwa i awasukuma kuwarudisha nyuma. "Sister nini hiki?" Alicia aliuliza. "Sijui lakini huwenda hatujawa wenye imani thabiti na Bwana mungu wetu" Kweli baada ya kusema hivyo tu, Murcia aliisi kama kuna sauti inamuita. "Murcia, Murcia, Murcia" Sauti iliyokuwa inaita kwa kunong'oneza. Sister Murcia aliiskiliza sauti hio akawa anashindwa kuitambua inatoka wapi. Alibaki kujiuliza na kugeuka geuka. "Sister Murcia nini mbona unakuwa hivyo?" Moris au dereva wao, aliuliza?" Bila hata kujibu Morcia aliitoka inje ya kanisa akikimbia kurudi chumbani kwake na kujifungia. Kitendo hicho kilichanganya Alicia, mercia, moris, lucas na Chaka wote wakabaki tu, wamesimama wasitambue nini kimemkuta sister Murcia. Wakiwa bado kila mmoja wao amesimama kwa sitahili yake. Mala mlango wa sakarastia ukajifunga wenyewe hata bila kuguswa. Walipoona mlango umejifunga wakazani ni upepo tu, Moris akajaribu kuushika mlango huo ili afungue lakini hakuweza hata kuufungua. Hakawambia wenzake kuwa mlango ni mgumu kufunguka nao pia wakajaribu lakini wilishimdwa hapo kila mmoja akajawa na uwoga na kutoka inje ya kanisa. SHARE KUNIPA MATUMAINI YA KUENDELEA.

at 4:29 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top