Home → simulizi
→ SISTER MURCIA.
NO. (03).
ILIPOISHIA.
watu waliokuwa wamekaa mbele yao kulikuwa na kitambaa kikubwa kilichokuwa kinaonesha kila kitu ambacho kilikuwa kinafanywa na Sister murcia.
SONGA NAYO.
Watu wa kikao hicho walikuwa wanaongozwa na mwanaume mmoja mtu mzima.
Walikuwepo watu zaidi ya kumi, watu hao wote walikuwa watu wazima tena umri wao ulikuwa si chini ya miaka 45. mavazi yao wote yalikuwa meusi isipokuwa mmoja tu, mwenye vazi jekundu na weupe uliokuwa umepita kiunoni kama mkanda. huyo ndiye alikuwa mkuu wao. Mavazia yao yalikuwa ni magauni mapana. Walikuwa mchanganyiko. Wanaume kwa wanawake. Nyuso zao zilikuwa zinatisha kabisa kiasi kwamba ukikutana naye hata mchana lazima ukimbie. Vidore vilikuwa na kucha ndefu kwa wanawake.
Kikundi cha vijana sita waliosalia kilipita mpaka mbele wakaanguka mbele ya mkuu. wakamsujudia na kumuomba msamaha kwa kusema.
"Hakika tulicho kiona kwa mtu yule ni cha ajabu sana kwetu kututokea hapo kabla ndio mala ya kwanza ewe mkuu"
Alisema kijana mmoja.
"Ewe mkuu katika Ardhi hii ya shimo la moto basi tusamehe sisi, na hutupe nafasi nyingine tupate kujipanga upya kwa ajili ya mtu huyo na hakika tutamleta kwako mkuu"
Kijana mwingine alisema.
Ingawa kulikuwa na mwanga wa mbalamwezi katika hanga hilo lakini walipokuwa wamekaa kulikuwa si chini ya mti wala ndani lakini kwao kulikuwa hakuna mwanga wa mbalamwenzi lilikuwa giza na walitumia mwanga wa moto waliokuwa wameukoka.
Kabla hajasema chochote yule mkuu alisiamama, kisha akasema.
"Nyangubha, nyamumwi, Nyamwesi, Muhoja, Maengela, na Tulimanywa.
Yalikuwa ni majina ya watu na kila alipokuwa analitaja jina hilo muhusika alisiamama.
"Enenda mche kumpima Omuno yo amanaka kaye"
Mkuu yule alisema maneno hayo kwa Rugha yao ya kichawi akimaanisha.
"Nataka mkampime mtu huyo nguvu zake.
Nyangubha, nyamumwi na Nyamwesi. Hawa walikuwa wanawake, na ndio walikuwa wanaaminika kuliko wengine wote isipokuwa mkuu wao.
Muhoja na Maengela. Hawa walikuwa wanaume ndio waliokuwa wanaaminiwa na mkuu wao kuliko wengine wote.
Baada ya kuambiwa tu waondoke kumpima Sister Murcia nguvu zake. Wote palepale walipotea mpaka eneo la kanisa, mbele ya Gari walilokuja nalo watu wa mungu ndipo walipotokea, sisiter murcia
hakiwa hana Habari kabisa yeye aliendelea kumuuliza kijana yule maswali ili apate kukijua kijiji hicho vizuri.
"Ujanambia unaitwa nani?"
Murcia aliuliza.
"Mimi ninaitwa Chaka.
"Chaka!?"
Murcia aliuliza kwa mshangao.
"Ndio"
"Hapana, nitakubadilishia jina. Majina mazuri yamo ndani ya Biblia. Unajua kusoma?"
"Kusoma?"
"Eee!kusoma?"
"Hapana sijui"
Baada ya kusema hapana sijui, Chaka aliinua uso wake. Macho yake yalikutana na kikundi cha watu watano waliokuwa wametumwa kumpima Sister Murcia, kitendo cha kuwaona wachawi wale tena wakiwa wanacheka, chaka alimgusa Sister Murcia begani kumwashilia ageuke nyuma kuwa kuna jambo la kumshangaza. Sister Murcia aligeuka nyuma kutazama lakini hakuona kitu.
"Kuna nini we chaka?"
Murcia aliuliza.
Hata kabla hajasema chochote Pale pale waliisi kama Ardhi inayumba yumba, kile kikundi cha nyangubha, Nyamwesi, Nyamumwi, Muhoja na maengela kilianza kuonesha nguvu zao.
Bado wakiwa wanaona kama Ardhi anayumba yumba kipindi hicho hicho upepo mkari ulivuma kwa nguvu, mpaka walio kuwa ndani ya gari Alicia, mercia Lucas na Moris wote wakashituka ilikuwa ni kazi nzito sana kwa Murcia kuikabili.
Vyote hivyo vikiwa vinafanyika watu wale walikuwa wamesimama karibu yao kabisa. Huku wameitanua mikono yao kama mabawa ya ndege na wakiyumbisha yumbisha vichwa vyao pande zote, kila walivyozidi kutikisa vichwa ndivyo Sisiter Murcia alizidi naye kuyumba lakini alikuwa akiisoma sara ya Baba yetu moyoni, kipindi hicho chote Chaka yeye alikuwa kaisha anguka chini umepoteza fahamu.
Kwenye gari, kelele ndizo zilizidi kusikika na kutwala. Gari nayo ilionekana kuyumba
"Najua mungu uko pamoja nasi, basi kiangamize kizazi hiki chenye kumwabudu na kumtumikia shetani"
Murcia aliomba ombi hilo baada ya kuimaliza Baba yetu uliyembinguni. Kundi lile la wachawi lilipotea pale pale na hali ikabadilika pale pale na kurudi katika hali ya hawali.
Murcia alishuka chini na kupiga magoti akamshukuru mungu kwa ukombozi mwingine kutoka kwake.
Hali ya pale ilitulia kabisa kabisa.
Ndio muda huo huo, Chaka naye alishituka kutoka kwenye kupoteza fahamu. Moris na Pamoja na wenzake wote waliokuwa kwenye gari walitoka inje kuona nini kimetokea. Sisiter Murcia yeye aliendelea kumshukuru mungu kwa uokovu aliomuonesheakwa mala nyingine.
Alicia na wenzake nao walipoona hivyo wakapiga magoti na kuungana naye kuomba mungu awalinde zaidi ili kulifanikisha zoezi lao la kukikomboa kijiji hicho cha Shimo la moto.
*****.
Ndani ya kambi ya wachawi. Mambo yalikuwa tofauti kabisa na matarajio waliyoyatarajia hali ya nyangubha ilikuwa ni mbaya, alikuwa analia macho tu, macho yake yalipata upofu wa ghafra.
Ingawa wengine hawakujeruhiwa lakini walikuwa wanalia mbele ya mkuu wao na kusema kuwa waliisi vitu kama sindano zimewashukia na kuwachoma mwili mzima.
"Mkuu mimi hapana siwezi tena siwezi tena"
Nyangubha alisema.
Japo kuwa tayari wenzake walijieleza kabisa kuwa walichokutana nacho kilikuwa sio cha kawaida lakini mkuu wao, akutaka kuamini na kusema bado watapambana naye.
Baada ya tukio hilo kuwa gumu, mkuu yule wa wachawi aliamuru wampeleke Nyangubha katika kifungo asubili adhabu yake ya kukataa kuendelea kuwa mchawi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: