SISTER MURCIA. NO. (02). ILIPOOSHIA. Walipomaliza kuzisoma sala izo sister murcia akaingoza sala ya kulala. Vijana wake walilala lakini murcia alitoka ndani ya gari na akatandika kitambaa chake akakiweka kitabu chake kitakatifu cha biblia kisha akapiga magoti na kuanza Maombi. Hakiwa anaendelea nyuma kilitokea kikundi cha watu. FUATILIA. Kikundi hicho cha watu, kilikuwa ni kikundi cha ajabu watu wale walikuwa wamejipaka marangi usoni, nyuso zao zilionekana kutisha. Sister Murcia yeye aliendelea na maombi bila hata kujua kama kuna kundi la watu Saba nyuma yake wenye kutisha tena wote wanaume wameshikilia mapanga mikononi wamevaa mairizi shingoni mwao na mikononi mwao. Murcia aliiweka Roho yake kwa mungu. "Eeee! Mungu wewe ndiye tegemeo la moyo wangu, wewe ndiye msaada na msimamizi wa kila jambo na mwongozo wa kila nafisi. Nakushukuru kwa kuweza kutufikisha salama katika kijiji hiki cha shimo la moto. Eee bwana mungu, nimejiweka mbele zako kwakuwa wewe ndiye kimbilio la kila nafisi, nami nakukimbilia wewe kwa kuhitaji msaada. Ombi langu kubwa kwako usiku huu nahitaji usambaze jeshi lako la mbinguni kwa ajili ya ulinzi kwetu kwa siku zote tutakazo kuwa hapa......." Bado Sister Murcia akiwa anaendelea watu wa nyuma walizidi kumsogelea lakini kutembea kwao kulikuwa kwa hatua moja wanasimama halafu wanacheza kwa kutikisa vichwa vyao kwa utulivu huku wameng'ata irizi zao zilizokuwa zimening'inia mashingoni mwao. Bado wakiwa wanaendelea kucheza walipomkaribia wakasimama mmoja kati yao alisogea mbele kabisa karibu na sister akainua mkono wake wa kushoto kumkamata kichwa sister Murcia. mkono wake ulipo kikaribia kichwa cha sister Murcia alirushwa mbali kama kapigwa na shoti ya umeme. Wenzake wote wakapotea kimiujiza lakini cha ajabu mtu yule alishindwa kutoka pale akawa analia moto moto. Lakini kelele zake zote sister murcia alikuwa azisikii kabisa bali yeye aliendelea na maombi mwisho yule mtu akazima kabisa lakini bado alienedelea kupumua. "Eee, Bwana ubarikiwe na ushukuliwe, uhidimiwe siku zote milele amina" Sister Murcia alimaliza maombi yake kisha akaichukua biblia yake hakaishika na kitambaa chake alichokuwa katandika chini na kugeuka kwa ajili ya kuingia kwenye gari. Lakini alipogeuka tu akakutana na Mwili wa mtu yule aliyerushwa na shoti ya hajabu. Sister Murcia alishituka kwanza kisha akamsogelea mtu yule alipofikia akamwangalia akagundua kuwa ni mzima. Sister Murcia alimshika kichwan mtu yule kisha akasema. "Eee! Bwana hakika wewe ndiye mwenye kayafanya haya yote basi mfanye huyu apate kuamka" Baada ya maombi hayo mafupi tu. Mtu yule aliamka na kukaa. Macho yake yalipokutana na sister Murcia alishituka akataka kukimbia lakini sister murcia akamshika mkono na kumwambia. "Usiogope kwani tayari upo katika mikono salama iliyojaa ulinzi wa Bwana" Mtu yule hakiwa na wasiwasi naye pia akamuuliza Sister Murcia. "Kwani wewe ni nani?" "Mimi ni naitwa Sister Murcia, nimekuja kwa ajili ya kukiweka kijiji hiki katika mikono salama ya mungu" "Kwani mungu ni nani?" "Mungu ndiye mwenye mamlaka yote ya duniani na mbinguni. Yeye ndiye muumbaji wa kila kiumbe na anamamlaka ya kuuwa na kufufua" Sister murcia alisema. "Lakini mbona niliona moto umekuzunguka nilipokukaribia lakini mbona uko mzima tu hujaungua?" Sister Murcia aliulizwa na mtu yule. "Uliona moto umenizunguka?" Sister Murcia aliuliza kwa mshangao "Ndio niliuona moto Pindi tu nilipotaka kukishika kichwa chako nikarushwa kwa nguvu halafu nikauona huo moto umekuzunguka" Mtu yule alisema. "Sasa ulitaka kufanya nini kichwani kwangu?" Sister mulcia aliuliza. Akiwa anatetemeka mtu yule alisema. "Sisi ni walinzi wa eneo hili, ni kundi la kutisha ambalo liko chini ya kiongozi wa kijiji hiki. Sisi huwa tuanatumwa kuuwa kila mtu amayekuja hapa" Mtu yule alisema. "Kwanini sasa munaua kila mgeni anayekuja hapa?" "Kwasababu, mala nyingi watu wanaokuja hapa wanafika na kuaribu mila zetu za kuiomba mizimu yetu na kuweka utamaduni unao ichukiza mizimu yetu" Mtu yule alisema. "Kwahio wewe bado unataka kuua na kuendelea kuabudu hio mizimu yako?" Swali hilo kutoka kwa sister murcia lilikuwa zito sana kujibiwa na mtu yule. "Hapana nataka kujua kwanini wewe moto ulikuwa umekuzunguka halafu ukuungua na kwanini nilipokukaribia nilirushwa kwa nguvu na wakati sijawahi kushindwa kabisa mimi?" Badala ya kujibu mtu yule naye aliuliza tena. "Moto uliokuwa umenizunguka ni ulinzi wa Bwana mungu wetu aliye hai. Na kurushwa huko ni mungu alitaka kukuonesha kuwa yeye hashindwi na chocbote. Kwani unajua kwanini hujafa?" Sister Murcia aliuliza. "Sijui?" "Basi mungu anakupenda na amekuokoa kutoka katika imani potofu ya kishirikina. imani mbaya ya kumwabudu shetani na jeshi lake" Baada ya kusema maneno hayo mazito yaliyokuwa yamejaa wokovu mkubwa. Mtu yule alisimama kisha akasema basi nami nifanye kama wewe, watu wabaya wakinikaribia basi nami moto unizunguke nao warushwe kama yeye. Sister murcia aliinua macho yake juu akamshukuru mungu kwa muujiza wake, hapo hapo akahesabu tayari anaye mmoja usiku huo. ***** Wakiwa kabisa wanahofu kundi lile la vijana saba walitokezea kwenye mji mkubwa kabisa na mji huo ndio ulionekana mkubwa kuliko zote kwenye hicho kijiji. Ndani ya mji huo kulikuwa na kikao kikubwa cha watu waliokuwa wamekaa mbele yao kulikuwa na kitambaa kikubwa kilichokuwa kinaonesha kila kitu ambacho kilikuwa kinafanywa na Sister murcia. Itaendelea. Tafadhali share kwa marafiki zako Wakijitokeza amsini wa kushare nami nitajitahidi kuiweka nyingi

at 4:29 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top