Home → simulizi
→ SISTER MURCIA.
NO. (01).
Ni sister ambaye alikuwa na upako mkubwa na inasadikika alikuwa na uwezo wa kuomba chochote na mungu akamtekelezea. hata kama alikuwa na njaa yeye alishushiwa chakuala mahara popote.
Licha ya kuwa na upeo mkubwa. syster murcia alikwenda kuongeza elimu yake italia.
Baada ya mwaka mmoja alirudi Tanzania kutoka masomoni.
Alipofika akapewa taarifa kuwa kuna kijiji kimoja kinaogopwa hasa. watu wageni na watumishi wa mungu wakienda huko wanauliwa.
Kwa kukatwa katwa mapanga na sehemu zao za siri kuchukuliwa kwa wanaume na wanawake hubakwa na kutupwa misituni kama chakula cha mizimu.
Mbali na hilo pia watu hao wanaamini sana imani za kishirikina.
Baada ya maelezo hayo sister murcia aliombwa yeye aende huko kwenye hicho kijiji cha kutisha kwa ajili ya kuiokoa jamii hio na imani potofu imani ya kishetani na uchawi.
Sister Murcia akakubali kuwa yeye anaweza kulifanya hilo. kwa imani kubwa ya mungu wake.
Safari yake alikuwa ameambatana na mabint wawili. Mercia na Alicia mabint hao walikuwa ni wanafunzi wake. Pia alikuwepo kijana mmoja wa kiume yeye alijulikana kwa jina la Lukas na deleva wa gari. huyu aliitwa kwa jina la Moris. Moris ndiye pekee alikuwa anakijua kijiji hicho. Safari ilianza ya kuelekea katika kijiji hicho cha kutisha.
Wakiwa njiani walikutana na vitu vingi vya kutisha kama vyungu vilivyokuwa vimetanda kila mahara zenye njia panda, mizoga ya wanyama hasa kuku wekundu na njiwa zilikuwa zimefungwa kwenye miti imening'inia. Ilikuwa ni safari ya kutisha kweli muda wote walikuwa wameshikilia Rozari zao wakiomba mungu awafikishe salama katika kijiji hicho. Masaa yalikwenda lakini kufikia tamati ya safari yao ulikuwa ni mtihani mkubwa hatimaye ilitimu mida ya saa moja za usiku hali iliamza kubadilika kabisa sauti na miungurumo za ajabu zikaanza kusikika. Watu wengine walianza kuogopa lakini sister murcia aliwambia wasiogope wamtumainie mungu na bwana aliye hai.
Wakiwa wanaendele kukisogelea kijiji hicho gari ilizima. kupiga sitata ikagoma. Dereva akashuka na Lucas kuangalia nini kinasumbua gari. lakini hakuon tatizo. akaomba mercia, Alicia na sister Murcia washuke wasaidie kuisukuma gari. Ilikuwa ni ngumu sana kwa Alicia na Mercia kushuka kwenye gari, mazingira yaliwatisha sana. Kwa ujasiri wa sister murcia aliwambia vijana wake mericia na Alicia washuke kwenye gari wasaidie kusukuma.
Kwa pamoja walishuka na kuanza kulisukuma gari, lakini ilikuwa aisaidii gari iligoma kabisa kutoka. Waliangaika kama Robo saa lakini hawakufanikiwa gari liligoma liligoma.
Moris aliangalia tena kama kweli kuna tatizo lakini tatizo halikuonekana. Wakiwa wanaangaika, kilitokea kiumbe cha ajabu mbele yao kiumbe hicho kilikuwa kama mtu lakini chenye mapembe. Uso wake umetapakaa Damu. Alicia mercia na Lucas. Wote wakakimbilia kuingia ndani ya Gari. Inje akabaki Sister Murcia pekee.
Kiumbe kile kililisogerea gari lakini kabla akijalifikia ulitokea moto ukakizoa na kutupilia pembezoni mwa barabara na kukiteketeza. Hayo yote yakiwa ni maombi ya Sister murcia. Baada ya tukio hilo
Pale pale na gari likawaka. Soster murcia akaingia kwenye Gari na kuwambia vijana wake. "Hakuna njia njema kama kumwamini mungu na kukaa na imani thabiti msiyumbe shetani atawaingia kirahisi"
Baada ya kuambia hivyo wote waliitikia sawa na gari kuondoka. waliivumilia sana safari yao ya kutisha Usiku mida ya saa mbili na dakika 48 walifanikiwa kukifikia kijiji hicho cha kutisha.
Walilifikia kanisa la kijini hapo. Kanisa lililokuwa njiani tu. Mazingira ya kanisa hilo yalitisha sana kulikuwa pachafu sana mapopo ndio lilikuwa ni makazi yao. Wanyama kama mbwa ndio yalikuwa makazi yao. Kiujumla ilikuwa ni harufu mbaya kila mahara ndani ya kanisa hilo. Kwa uzuri walikuwa na taa zao wakaingia na kuangalia hali ya kanisa ikawashinda. Wakarudi wakamuomba Dereva wa gari(Moris), awapeleke kwa uongozi wa kijiji hicho. Moris aliwambia hapajui na katika kijiji hicho watu wote huwa wanalala saa moja kuanzia saa 12:30 huwa wanajifungia ndani ya nyumba zao. Walipoangalia saa zao tayari ilikuwa imetimu mida ya saa tatu na nusu. Baada ya kuona hivyo syster murcia aliomba walale ndani ya gari wangoje kesho ndio waende kuuona uongozi.
"Sister kwanini tusiende kuwaamsha"
Alicia alisema. Bint huyo aliyekuwa mdogo kuliko wote yeye alikuwa ni muoga hasa mazingira yale aliyaogopa kabisa. Mambo na Vitu alivyokutana navyo njiani pindi wanaelekea ndani ya kijiji hicho yalimtisha. Kijiji hicho kwa jina kilijulikana kwa jina la Shimo la moto kiliogopeka sana hakuna mgeni aliyeweza kufika huko na kudumu. Ila wenyeji tu hata vijana waliokulia huko wakafanikiwa kutokako, waliogopa kabisa kurudiko.
"Alicia we ni mtoto mwema wa mungu ingieni ndani ya Gari hakika ulinzi wa mungu u juu yetu tumekuja kuzipigania Roho za watu wapate uongofu wa mungu"
Sister Murcia alisema.
"Sawa sister Murcia. Lakini hawa inaonekana washagongwa mihuri ya shetani hawawezi kutoka huko"
Alicia alisema.
"Alicia hii ni jamii ya kiafrika hata wewe, babu wa babu yako alikuwa kama hawa je usingekuja ukombozi juu yao kutoka kwa watu kama wewe unazani wewe ungekuwa wapi?"
Sister murcia alimwambia Alicia
Kwa usikivu na utiifu wa mwalimu wao Alicia Lucas na Mercia waliingia kwenye gari.
Wakala chakula chao walichokuwa ameambatana nacho. Walipomaliza kula.
Wote kwa pamoja wakaanza kuisoma sala ya salamu maria kisha Baba yetu uliyembinguni. Walipomaliza kuzisoma izo sister murcia akaingoza sala ya kulala. Vijana wake walilala lakini murcia alitoka ndani ya gari na akatandika kitambaa chake akakiweka kitabu chake kitakatifu cha biblia kisha akapiga magoti na kuanza Maombi.
Hakiwa anaendelea nyuma kilitokea kikundi cha watu.
Usiikose kila siku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: