Ofa Ofa Ofa kwa msimu huu wasikukuu KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) MTUNZI : ZAYNAB TALY SEHEMU YA 15 ILIPOISHIA...... Alisubiri hatimaye Giza liliingia pasi na mke wake kurejea ndipo alipoamua kutafuta namna ya yeye kuingia ndani ya nyumba yake na kujipumzisha, akavunja kufuri na kuingia ndani ilipita siku masiku hatimaye wiki Stellar hakurejea nyumbani na bado simu yake ikawa haipatikani. ********* SONGA NAYO ********** Jitihada za dhati alizozifanya ilikuweza kugundua ni wapi alipo mke wake kipenzi ziligonga mwamba, hakukuwa polisi na hata mahospitalini hakubahatika kumuona. Maisha Yalikuwa magumu kwa upande wa stellar ambaye kukicha Sam hakuonyesha mapenzi kwa upande wake ,kikubwa aliwaza kumuharibia maisha yake huku akijiapiza kumpa mateso katika kipindi kifupi cha maisha yake kilichobaki. Afya yake ilianza kuwa zaifu kila kukicha na kujikuta akikondeana bila sababu. Sam aliyekutana naye hakuwa Sam yule ambaye siku zote alimpenda na kumnyenyekea kwa mapenzi yote. Alikuwa mwanaume katili kuwahi kutokea huku akifosi kupewa penzi kinyume na maumbile hali ambayo ilikuja kumletea madhara makubwa mno hasa katika sehemu zake za uzazi. "Stellar majibu yako yapo tayari ila inaonyesha unayo maradhi ya kupandikizwa katika mwili wako huku ukionekana kuharibika zaidi sehemu zako za aja kubwa, hili nitatizo ambalo uwakuta Wanawake wengi bila wao kujua kama wanahatarisha afya Zao ila kuhakikisha wanaridhisha nafsi za waume Zao sijui kwa upande wako imekuwaje ila inaonekana unatatizo la namna hiyo". Yalikuwa maneno ya daktari baada ya kuhakikiwa Damu na baadhi ya vipimo vingne kulingana na maelekezo yake juu ya vile anavyojisikia. Ghafra alianza kuchanganyikiwa hasa alipo ambiwa kuwa hakukuwa na namna ya kumsaidia kwa lolote maana bacteria hatari walikwisha tembea vilivyo katika sehemu zake za siri japo walijitahidi kumpatia Dawa mbali mbali ilikuweza kumsaidia kukausha maji maji na kumpunguzia maumivu ambayo alikuwa akiyapata wakati wa kukaa na kwenda haja. Hali yake ilizidi kuwa mbaya kila kukicha maumivu aliyokawa akiyapata kila kukicha yakamjengea picha mbaya kichwani mwake akawa mfano wa mtu aliye pungukiwa Kiasi Fulani cha ufahami kichwani mwake, Mara awe na akili timamu Mara anakuwa mtu wa kuvuluga mambo mwisho wa siku Sam pia akamkimbia yote ilikuwa baada ya kuhakiki kweli Stellar hakuwa wakupona na yale ndo maisha ya mateso juu ya kiapo cha siri walichokiapia. Akiwa ndani ya ndege asijulikane alikuwa alielekea wapi Sam aliyatazama mawingu na kuta za ndege ile ambayo Ndo kwanza ilikuwa ikiianza safari yake ya kupaa angani. "Samahani Sana Stellar ila nikiapo ambacho wote tulikuwa radhi nacho nilirudi ilikukitimiza na ninaondoka kwakuwa nishakusudia nilicho kidhamiria nimekuwa na maisha magumu zaidi kupitia wewe ila tangu sasa sio Mimi Sam masikini tena pia kupitia wewe nitaitwa tajiri. " Hali aliyokuwa nayo stellar ilizidi kumtesa na kumnyong'onyesha mwili wake kila alichoachiwa na wazazi wake Sam alikiuza ikuweza kujipatia kipato na kuendeleza maisha yake . Jioni moja ikiwa tulivu mno kwa upande wangu nikiwa natoka maeneo ambayo nilikuwa nikifanyia kazi na kujisogeza palipo kituo cha usafiri iliniweze kurejea nyumbani ghafra nilikutana na sauti nyembamba iliyopambwa na mikwaruzo ya dhiki na matatizo yakila namna. “NAJUTIA MAPENZI YAKE…..Ndio najutia sana kumpenda najuta kwanini pia niliyajua mapenzi.Hivi unajua kama majuto yangu ni makubwa zaidi tangu nilipokutana na wewe bila shaka siku wahi kujuta maishani wangu kamaninavyojutia uwepo wako leo hii nakuchukia nakuchukia sana nakuchukia zaidi ya unavyojua kama unachukiwa na mimi”. Nilimsikia vyema yule binti aliyekuwa ameketi karibu na pale nilipokuwa na pita.Nilitamani kuendelea kuongeza hatua na kusonga mbele na safari yangu ila nafsi yenye kuhurumia iliniteka na kunisukuma nimsogelee yule binti aliyejiinamia pale chini. “Habari yako?” Ndio ilikuwa salamu pekee niliyoweza kumtolea mwanadada yule.Aliinua kichwa na kunitazama pasi na kusema chochote huku machozi yakitengeneza mifereji isiyokauka juu ya mashavu yake. Alionekana kudhohofu mno machoni wake niliona picha nyingi zenye kuuzunisha.Sura yake ilijawa na huzuni alionekana ni mtu aliyekata tamaa juu ya maisha, tumaini la kuishi akiwa na furaha ilikuwa ndoto kwake.Alionekana kufubaa kwa jua na mvua za kila siku zilizo shiriki vyema kuangamiza unadhifu wa ngozi yake nyeupe. “Habari yako?”.Niliuliza tena walau nipate kujua anasumbuliwa na nini.Ila bado jibu lilikuwa kimya kizito.Aligutuka mfano wa mtu aliyetoka katika dibwi zito la mawazo akajifuta machozi kisha akajikooza kidogo na kutengeneza tabasamu bandia. “Salama tuu kaka angu”.Alinijibu kwa upole huku akijilazimisha chozi lisiweze kuanguka. “Unatatizo?”. “Hapana kaka angu nipo sawa”.aliendelea kulazimisha tabasamu huku akificha tatizo lililo muweka mahali pale.Nikweli isingekuwa rahisi kuniamini na kuniambia tatizo hasa lililokawa linamsimbu maana tulikutana tuu kama wapita njia. Pembeni kulikuwa na kimgawaha kidogo nilipotazama saa yangu ya mkononi niligundua ilikuwa yapata saa nane na nusu.Nilimkongoja msichana yule na yeye akafata sapoti yangu akainuka na sote tukaelekea panapo mgahawa ule wa chakula. “Unakula nini?”.Nilimuuliza baada ya kuketi na kutulia kwa muda kidogo tukimsubiri muhudumu. “Nitakula chochote wenisaidie kuagiza”.Sauti yake ya upole ilionekana kutoka katika chumba cha moyo wa yule msichana chenye kuhifadhi maumivu ilipenya vema kwenye masikio yangu.Nilimuagizia chakula kikaletwa na sote tukawa tunashiriki vyema kuweza kuyaridhisha matumbo yetu.Alikipamia chakula huku akionekana kama aliyekosa chakula kwa kipindi kirefu mno na baada ya muda mfupi tayari alikuwa amekwisha maliza. “Naam Dada angu mimi naitwa Naseeb sijui unaitwa nani?”. “Naitwa Stellar ”.kwa mara ya kwanza alinitajia jina lake. “Ooh..shukrani,Umekutwa na nini dada yangu mbona unaonekana haupo sawa?”.Lilikuwa swali gumu kwake maana alitamani iwe siri yake peke yake,alitamani kutomueleza yoyote juu ya maisha yake yale yenye kumuumiza. “Nitakuelezea siku tukija kuonana tena kwasasa na shukuru kwa msaada wako naomba niende”. “Mmh sawa basi niambie unaishi wapi” “Naishi mitaani kama hivi leo uliponiona pale ni makazi yangu kwa siku ya leo, kesho nitaenda pengine kesho kutwa hadi mtondogoo sina makazi maalumu kusema sehemu fulani ukinitafuta utanikuta”.Yalikuwa maneno yaliyonipa ushawishi wa hali ya juu na kunifanya nitamani kujua mengi zaidi kuhusu yeye. “Sikia naweza kukusaidia pakukaa maana ninaishi mwenyewe na nimepanga vyumba viwili sijui naweza kukupeleka kwangu?”. Swali langu halikupata jibu la haraka nadhani ni kutokana na kutoniamini kama kweli ninaweza mpa msaada wowote ule. Hali ya hewa ilikwisha badilika wingu lilitanda na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha wakati huo,Mimi na Stellar tulikuwa tumekwisha fika sehemu ambayo nilikuwa nikiishi na Stellar alikuwa tayari kunieleza juu ya kile kilichomfanya awepo mahali pale nilipo mkuta mchana ule. Harufu mbaya ambayo nilikuwa nikiisikia kutoka kwa mwanadada yule ilinipa ushawishi zaidi kujua nini kilimkuta mpaka Kuwepo katika hali ile. Harufu ile haikuwa ikifanana na ile ya mtu kuto kuoga muda mrefu au kubeba kinyesi au uchafu mwingine wowote harufu ile ilikuwa mfano wa mtu anaye oza ndani kwa ndani. “Penzi la kweli kutoka ndani ya moyo wangu ndo limenifanya nifike hapa huku usaliti kwa wazazi wangu ukichochea kwa kiasi kikubwa kama laana juu ya maisha yangu na kunifanya niwe mwenye kupotea katika kila njia niliyoiyona ni sahihi kwangu kupita. .Ni kweli leo nikipata nafsi ya kurejea tena kwa mume wangu nitamtaka radhi juu ya kila nilicho mkosea na kumfanya asahau kila ubaya ambao niliwahi kumfanyia.Kweli mshahara wa madhambi mauti ila adhabu ninayoitumikia leo hii ni mara mbili ya mauti." Aliongea maneno hayo huku akionekana kuumizwa mno na Jambo Fulani. "nilimpenda niliyempenda pasi nakujali thamani ya ndoa yangu na nini hasa walikimaanisha wazazi wangu awali nilipo kuwa tayari kuolewa na mwanaume niliyemtaka mimi. Japo kweli walikuwa namakosa kwa kulipinga chaguo langu ila Leo na elewa maana yao kiapo cha siri nilichokila bila kujua nikiasi gani leo hii kingenisulubu Kiasi hiki Sina pesa sina chakula Wala pakulala natanga tanga tuu mitaani kana kwamba sikuwa na wazazi wenye uwezo na kunisihi katika kila njia niliyopita najuta mno kuwa na mwanaume yule ambaye kanisababishia mateso zaidi. Naseeb ongea na Wanawake wote kupitia njia yoyote ile wasimame na ndoa Zao hata kama watajikuta hawapo katika chaguo la mioyo yao basi wadumu na kuvumilia maana hakuna ndoto ya mwanadamu iliyo bora kushinda mipango ya muumba wetu. Ndio yaliyokuwa maneno yake ya mwisho siku ile Nilimruhusu kujipumzisha nami nikawa nikitafakari namna yakumsaidia hasa juu ya afya yake hakuwepo ndugu jamaa Wala rafiki aliyehitajia kumuona hata kujua yuko wapi. Asubuhi ilipo fika nilijiandaa vyema na kumuandalia chai kisha nikawa nikimsubiri aamke aweze kunywa chai. Sikutaka kumgongea maana nilijua nikitambo Sana alikuwa akiishi maisha ya dhiki uwenda hakuwa mwenye kulala kwa Amani kutokana na matatizo aliyokawa akiyapitia. Nikimsubiri kwa muda mrefu lakini Mara Nilianza kuingiwa na shaka baada ya kuona harufu mbaya ikizidi kutawala ilikuwa harufa ya mfano wa mzoga uliokufa na kukaa muda mrefu na kuozeana. Nikajaribu kugonga mlango wake ili aweze kunifungulia haikuwezekana niligonga kwa muda mpaka nilipo ingiwa na woga nikausukuma mlango na taratibu ukawa ukiacha Mara nilikutana na mwili uliokuwa ukishambuliwa na inzi na kutoa harufu Kali mno. Tukio lile lilinijuza kuwa hakukuwa na mawasiliano baina ya mwili na nafsi ya stellar kwa Wakati ule. Nilifanya jitihada za kuwaondoa inzi wale kisha nilipo hakikisha kwa Kiasi Fulani nimesitili aibu ile ya maiti nilimfunika na Shuka nyeupe kisha nikamuita mmoja wa majilani zangu na kumueleza kinaga ubaga. Japo haikuwa rahisi ilinibidi kupata kibali juu ya mazishi ya maiti ile ambayo haikuwa na ndugu na mimi nilikuwa na lengo la kumsaidia. Nilipo pata ruhusa sikuwa na chakunifanya nisubiri niliamua kumzika stellar ambaye alikufa akiwa na maumivu ya mapenzi alikufa kwa ajili ya uthamini wa kiapo cha siri ambacho ndio pekee kilicho mtesa Kiasi kikakatisha uhai wake. baada ya Sam kutaka kulipiza kisasi katika Damu ya kiumbe chake ambacho kiliuliwa pasi na hatia. KIAPO CHA SIRI....... MWISHO............! Ulikuwa nami Zaynab Taly tukutane katika simulizi nyingine. ...

at 4:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top