OFA YA EID AL HAJJI ... KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) SEHEMU YA 14.. ILIPOISHIA...... "Ooh sawa ila jiandae ukanywe chai Mimi nitakuandalia vitu vyote vya safari. " "Sawa ". Aliinuka ilikuweza kujiandaa na kuelekea palipo andaliwa chai huku akimuacha stellar na taratibu za kuandaa vitu vya safari kwa ajili yake. **************SONGA NAYO**************** Kikao cha haraka kilichotakiwa kufanyika huku akishirikiana na vijana wake wawili wakazi ndicho kilichokuwa kikiendelea katika jumba lile. Repoti kuhusu Stellar ndio kazi hasa waliyotumwa kuifanya kwa wakati ule. "Naam nahitaji kusikia Kutoka kwenu leo ".Aliongea Sam baada ya kusimama mbele ya vijana wake alio waamini na kuwatuma waweze kufatilia maisha ya stellar. "kwa upande wangu nimejua anapoishi ambapo anaishi na mumewe Elly ambaye amezaa naye mtoto mmoja yule wa kike ambaye alifariki siku ile ya ajari pia. " "Okay na wewe? ". Alimgeukia mwingine ambaye muda wote walikuwa kimya kusubiri ruhusa ili aweze kusema jambo. "kwa upande wangu nimegundua stellar alikuwa akiishi na wazazi wake baada ya wewe kuingia kifungoni ikasemekana alipatwa na maradhi ambayo chanzo na hata uhalisia wa maradhi hayo ilibaki kuwa siri ya familia yao baadae ndipo alipo olewa na Sam na kuhusu ujauzito aliokawa nao sijajua imekuwaje ila ukweli ni kwamba aliolewa akiwa hana ujauzito na kwa mara nyingine akabeba ujauzito wa huyu jamaa anaitwa Elly kisha akajifungua huyu mtoto wakike. ". "Ooh asante mungu nilihofia kukikatisha uhai kiumbe changu sasa stellar itabidi anieleze kipo wapi kiumbe changu ".kimya kikatawala kwa muda huku akionekana kutafakari jambo. "sasa naombeni mnisaidie Kumpata Stellar siku mbili hizi sawa? ". "sawa ". Waliitikia kwa pamoja na haraka wakainuka na kila mmoja kujua ni wapi anaanzia ilikuhakikisha ndani ya siku Zile mbili Stellar alikwisha patikana. Mida ya safari ilipo wadia Stellar alikuwa tayari kumsindikiza Elly, wakati anatoka akiwa yeye ndiye muendeshaji wa gari kupitia kioo chake ambacho kilikuwa kikimuonesha wanaomfata kwa nyuma ghafra alishtuka kuliona lile gari ambalo jana yake lilikuwa kwenye harataki za kumfatilia, pia lilikuwa likimfatilia kila alipo kuwa akikatisha na leo ilikuwa hivyo kila alipo kawa anakatisha lilimfata baadae hakuweza kuliona tena hofu ilimjaa ila hakutaka kumueleza mumewe juu ya gari ile akijipa moyo kutaka kujua ni nini kilikuwa nyuma ya panzia. Baada ya kumfikisha Elly Airport alianza safari ya kurejea nyumbani ambapo kichwa chake aliwaza namna ya kumuona Sam peke wakati yupo katika dimbwi zito la mawazo ghafra alishtuka kuiyona gari ndogo Aina ya IST kwa mbele ikimjia na ghafra ikasimama ikiwa zero distance na gari yake .wakati anataka kujikwamua pale alipo bananishwa nyuma yake akaliona gari ile ambayo kukicha ilikuwa ikimfatilia safari hii hakuwemo mtu mmoja , Kati yao mmoja alishuka na kumfata stellar . "Fungua mlango ".Alisikika akisema yule kijana aliyesogelea gari ya stellar. Hakuwa na namna akafunga mlango yule kijana akamsogelea. "sisi ni watu salama kabisa ila sharti letu ni moja tuu inabidi utufate tunako elekea bila shuruti ili uweze kuwa salama sawa? ". "Sawa ". Aliitikia stellar ambaye alionekana kuwa na hofu kupita kiasi hasa alipo gundua watu wale walikuwa wakifatilia nyanja zake kwa muda mrefu. Hatimaye safari ya yeye kuelekea pasipo julikana ilianza taratibu stellar alilifatisha gari ambayo aliambiwa aifate kila inapokatisha huku gari nyingine ikiwa kwa nyuma ikimuwinda. "mungu wangu napelekwa wapi huku ". Alijiongelea mwenyewe baada ya kujiona akiongozwa kuingia katika msitu. Hatimaye akaanza kuliona jumba chakavu ambalo bila shaka ndio alipo takiwa kufika akaruhusiwa kupaki gari na kushuka kisha akaomgozwa alipo takiwa kupita mpaka alipo fika panapo ukumbi mkubwa na kuambiwa asubiri. Baada ya kama dakika tano alionekana mtu aliyevalia kofia yenye kumziba uso Kiasi ilikuwa ngumu kwa stellar kumjua taratibu alikuwa akimsogerea stellar mpaka alipo mfikia Karibu na kuitoa ile kofia. "Sam....? "Alipiga makerere huku akimlukia na kumkumbatia kwa furaha Naam alikuwa Sam ambaye alimpa wakati mgumu tangu kumuona kwake siku ile ya mazishi ya wazazi wake. "Ulikuwa wapi Sam nimekutafuta Sana...? ".Alimuuliza huku akiwa amejikunyata vilivyo katika mikono ya Sam. "Stellar kiko wapi kiumbe changu kipo wapi kiapo cha siri tulicho apa mimi na wewe? ". Aliuliza Sam ambaye alionyesha kutokuwa na furaha juu ya uwepo wa stellar mahali pale. "Sam usiniadhibu tafadhali Niko tayari kwa lolote hata ikibidi kubeba kiumbe chako kingine Elly hakuwa chaguo langu nimejikuta tuu nikiitumikia ndoa yake. " Stellar alijitetea. "Nimekuelewa. " Huo ukawa mwanzo wa kurasa mpya stellar akiwa na Sam mwanaume ambaye kwa upande wake ndiye aliyeridhiwa na moyo wake. Kipindi chote ambacho Elly alikuwa safarini stellar aliitumia nafsi ile vilivyo akijituma kuyarudisha mapenzi ya Sam kwake. *************************************************** "Stellar...? ".Alisikika Sam akipaza sauti baada ya kufika nyumbani kwake na kukuta nyumba imefungwa. "yuko wapi huyu mwanamke Mbona simu yake pia hapatikani ".Alijiuliza mwenyewe baada ya kujaribu kupiga simu ya mke wake na kupewa taharifa kuwa simu ile haikuwa ukipatikana. Alikaa kumsubiri mkewe ambaye hakuwa na Kawaida ya kuondoka bila kumuaga Wala kuzima simu bila sababu ya msingi. Yapata wiki sasa hakuwa na mawasiliano na mkewe kitu ambacho hakikuwa cha kawaida. Mabadiliko ya mkewe yalianza kujionyesha tangu baada ya mazishi ya baba na mama yake pamoja na mtoto wao wapekee Sarah ila haikutosha kumpa wasiwasi wowote juu ya mke wake. Alisubiri hatimaye Giza liliingia pasi na mke wake kurejea ndipo alipoamua kutafuta namna ya yeye kuingia ndani ya nyumba yake na kujipumzisha, akavunja kufuri na kuingia ndani ilipita siku masiku hatimaye wiki Stellar hakurejea nyumbani na bado simu yake ikawa haipatikani. ITAENDELEA BAADA YA MUDA MFUPI hii ni kutokana na kushinda kula nyingi kuliko MERISA lakini pia sitoiacha mbali merisa nitaipost muda ukifika Eid Mubarak

at 4:23 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top