Home → simulizi
→ KIAPO CHA SIRI
(damu yangu haipotei)
MTUNZI : ZAYNAB TALY
SEHEMU YA 13
ILIPOISHIA....
Taratibu akagonga na baada ya muda mlango ulifunguliwa alikuwa msichana wa makamo akifunga kanga moja katika Kifua chake bila shaka alikuwa akitoka katika dimbwi la usingizi.
****** SONGA NAYO ********
"Habari yako Dada Karibu? ".Aliongea yule Dada aliyefungua mlango.
"Asante nilikuwa namuhitajia mwenye chumba hiki."
"Ooh mimi ni mkewe unaweza kunieleza tuu Amna tatizo mwenyewe kupumzika ".
"Hapana ni muhimu nimuone mwenyewe".
"Ooh okay acha basi nimuamshe ".
Akaingia ndani yule Dada huku nje zilisikika sauti za mtu Kuitwa na baada ya muda mlango ulifunguliwa kwa mara nyingine. Alikuwa pande la mtu mrefu mweusi aliyejazia.
"Habari..? "Alisalimia baada ya kukutanisha macho na stellar ambaye hakuwa na kumbukumbu za kukutana naye popote pale.
"Salama, wewe ndo mwenye chumba hiki..?
"Aliuliza huku akionekana kutawaliwa na hofu.
"ndio mimi. "
"Ooh hapa Kuna kijana alikuwa anaishi chumba hiki nikitambo kidogo miaka kama mitano sita hivi iliyopita unaweza kunisaidia kujua chochote kuhusu yeye? "
"Mmh kiukweli hapa mimi nimeamia tuu na kwa tetesi nilizo zipata ni kwamba mpangaji wa mwanzo hapa alikamatwa na polisi na mpaka sasa hajatoka kwa kosa ambalo hakuwepo mwenye kulitambua hasa kiundani ".
"Mmh okay na vipi hapa jirani kulikuwa na Dada anaitwa Dada Anna bado yupo..? "Aliuliza Anna.
"Hapana Dada Anna alifariki miaka miwili iliyopita kwa kuishiwa Damu mwilini "
"Daah Okay asante Sana. "alishukuru kisha akashika njia na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake. Akiwa na mawazo mengi kichwani huku maswali kibao yakiongozana akijiuliza ni nani hasa atamshika mkono juu ya kuweza kumpata Sam .
Mara alishitushwa na gari ndogo nyeusi iliyowekwa tinted pande zote huku dereva akionekana kuvalia kepu ambayo ilikuwa ngumu kumtambua ni nani kupitia kioo chake cha gari.
Gari ile ilikuwa ikimfatiria kila hatua aliyokawa anaipiga tangu alipokanyaga vingunguti kwa mara ya kwanza pasi na yeye mwenyew kujua kama alikuwa akifatiliwa. Hatua chache mbele alisimamisha gari ambapo alitaka kuhakiki kusudio la gari lile hasa ni nini gari ile ikaongeza mwendo na kumpita pale alipo kawa amesimama.
Baada ya muda aliwasha tena gari yake na kuendelea na safari ghafra alishangaa kuliona tena gari lile likiwa nyuma yake. "Mmh kwani Kuna nini kilichojificha hapa Mbona sielewi". Alijiuliza huku akiendelea kumuangalia kwa makini dereva wa gari ile hatimaye alibahatika kumuona sura ila hakuwa akimfahamu Wala kukumbuka kama aliwahi kumuona mahali.
"Sasa kwanini anaonekana kunifatilia hatua zangu ". Lilikuwa ni swali jingine ambalo hakulipatia jibu.
Hatimaye alifika kwake Salama na kuendelea na majukumu mengine kama mama wa familia kisha akajitupa kitandani ambapo usingizi ulimchukua bila kukusudia.
"mamaaaa.. ".Alipiga kerere baada ya kuhisi mtu akimshika.
"Mmh vipi..? "
"Aah usingizi tuu nilikuwa mbali kweli aliongea baada ya hofu kumpotea alipomjua aliyekawa akamshika.
"Mbona umelala saizi Unaumwa...? Alfu milango umeiacha wazi mtu akiingia je?".
"Aah niwie radhi mume wangu hata sikutegemea kama ningelipitiwa na usingizi ".
"Sawa akija haribika kitu maana nimerudi nafikiri kila kitu kipo sawa. "
"Okay chakula kipo tayari ".
"niandalie maji kwanza nioge kisha nitakula ".
Taratibu akainuka na kuandaa maji na baada ya muda wakawa mezani wakila kwa pamoja. Meza yao ilitawaliwa na upole ambao sio wakawaida hasa kwa upande wa stellar alionekana kutokuwa na raha kabisa.
"Uko Salama mke wangu? ".Aliuliza Elly ambaye alianza kupata shaka juu ya hali aliyokuwa nayo mke wake.
"Ndio Niko sawa ". Alijibu kisha akainuka na kuelekea chumbani.Baada ya muda Elly pia alikwisha Maliza chakula na kumfata mkewe.
"Inaonekana Haupo sawa na mimi ndiye mtu pekee ninaye weza kukupa tumaini hivi sasa Niambie tafadhali unasumbuliwa na nini ?".alimuuliza mkewe ambaye alionekana kuwa katika hali ambayo sio ya kawaida lakini jibu lilikuwa kimya. Hakuwa namna ilimbidi kutulia mpaka Asubuhi iliaweze kujua nikipi ambacho kilikuwa kikimpa wakati mgumu mke wake.
Asubuhi na mapema Stellar aliamka na kufanya usafi wa nyumba kama ilivyo kawaida na kumuandalia mumewe kila alichokihitaji kwa Asubuhi ile ili aweze kuelekea kuzini. Alipo Maliza alirejea chumbani ambako alimkuta mumewe amekwisha amka .
"Ooh Umeamka Mbona ujaenda kuoga? ".
"Hapana leo siendi kazini jana nilishindwa kukuambia chochote hukuwa katika hali ya kawaida niambie kwanza ulifikwa na nini? ".
"Hapana mume wangu kichwa tuu hakikuwa sawa ila usijali kwa sasa naendelea vyema niambie kwanini Leo auendi kazini.?"
"nina safari ya kikazi arusha nitakuwa huko kwa muda wa wiki tatu, nitaondoka na ndege ya jioni ".
"Ooh sawa ila jiandae ukanywe chai Mimi nitakuandalia vitu vyote vya safari. "
"Sawa ". Aliinuka ilikuweza kujiandaa na kuelekea palipo andaliwa chai huku akimuacha stellar na taratibu za kuandaa vitu vya safari kwa ajili yake.
ITAENDELEA.....
KARIBU TENA KATIKA KURASA YANGU YA MKONO WANGU... ULIKUWA NAMI MWANADADA ZAYNAB TALY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: