Home → simulizi
→ KIAPO CHA SIRI
(Damu yangu haipotei)
MTUNZI : ZAYNAB TALY
SEHEMU YA 12
ILIPOISHIA.....
"Stellar usije ukanisumbua tena tafadhali kila kitu kimeshakaa sawa utake usitake utaolewa na Elly na huyu mpuuzi wako ataozea jela. "yalikuwa maneno makali aliyekuwa akiongea mzee SUDDEIS kwa binti yake wapekee ambaye ulipita Mwezi sasa hakumuona nyumbani baada ya tukio la utambulisho kufeli.
********* SONGA NAYO *****
"Baba siwezi kuolewa na Elly maana tumboni nina kiumbe cha mtu nimependaye sitarajii na Wala sitaki mwanangu aishi kwa kupata tabu au kuishi na baba mwingine. "
"Nini ..? Stellar unaujauzito..? ".Aliuliza mzee SUDDEIS ambaye alionekana kuchukizwa zaidi na kitendo cha binti yake kubeba ujauzito nje ya ndoa.
Haraka bila kusubiri jibu kutoka kwa binti Huyo alimvuta na Kutoka naye nje mpaka palipo maegesho ya gari na kisha akafunga mlango na kumtia garini hali ya kuwa stellar asijue ni wapi alikuwa naelekea.
"Baba ni wapi huku unanipeleka ?".Aliuliza baada ya Mzee SUDDEIS naye kuwamo ndani ya gari na safari kuanza.
"uwezi nitia aibu Kiasi hiki huo ujauzito utatoa ".
"nini baba...? "
"nimesema utatoa ".
"Sasa baba hiki kiumbe kimekukosea nini mpaka unataka ukikatishe uhai baba kimekukosea nini ".Alilalamika stellar ambaye alikuwa anatarajia kuonewa huruma.
Lakini cha ajabu baba yake hakuwa mwenye kusema chochote mpaka walipo fika sehemu ambayo hasa mzee SUDDEIS alikusudia kisha akashuka na kumchukua binti yake mkono kwa mkono mpaka palipo chumba kilicho andikwa SPECIALIST DOCTOR.
Upande wa Sam alifikishwa mpaka kituoni na pasi na kuhojiwa chochote akawekwa mahabusu ilikusubiri wakati ufike na kesi yake iwe yenye Kufikwisha mahakamani na ipatikane hukumu sahihi juu kile kinachosemekana kuwa alikuwa akiishi na binti wa watu mwenye umri mdogo pasi na idhini ya wazazi wake kitu ambacho hakikuwa sahihi kwa upande Fulani .
Alijuta nakujilaumu Sana juu ya uwamuzi wake wa kukubali stellar aweze kuishi pale kwake na kujikuta akitamani kurudisha siku nyuma na kufikia siku ile kisha kumtimua nyumbani kwake bila uwoga Wala kuhofia madhara ambayo yange mfika stellar kwa wakati ule.
Historia ya maisha yake ilimtesa kila kukicha kwa kuishi bila kimjua baba ,mama na hata ndugu Wa karibu lakini iliongezeka historia nyingine ambayo ilisimama upande wa kulala maabusu pasi na hatia yoyote.
"Najua yote nina stahili kwasababu ya kiapo ila lazima awepo wakulipa kulingana na kiapo hiki hiki cha siri. "Aliongea mwenyewe baada ya kutafakari Sana namna na siku atakayo toka ndani mule na kukosa jibu sahihi.
"Naam Dokta naomba unisaidie tafadhali huu ujauzito austahiki Kuwepo kwa mwanangu ni aibu mno kwangu binti yangu wa pekee kupata ujauzito nje ya ndoa. "Aliongea mzee SUDDEIS ambaye alikwisha kutana na daktari aliyemkusudia.
"Lakini mzee Mbona rahisi Sana kuificha aibu hii Si umuozeshe tuu binti haraka kwani tatizo Liko wapi maana kwa watoto wasiku hizi na vyakula wanavyo kula huwa vinawapa madhara katika vitu Kama hivi ".
"siwezi muozesha binti yangu kwa mpuuzi yule naomba tafadhali unisaidie katika hili ".Yalikuwa maongezi ya siri ambayo hakupaswa yoyote nje yao kusikia yalisindikizwa na kitita cha pesa ili kuendelea kuweka usiri juu ya swala lile ambalo lilikuwa likipigwa vita Sana na selikari.
Hatimaye Stellar alitolewa ujauzito ,lakini hali yake haikuwa nzuri Sana alionekana kama kuchanganyikiwa kisaikologia na mara kadhaa alionekana kupoteza kumbukumbu za kujitambua kuwa yeye ni nani.
Lawama nyingi zilimuelekea mzee SUDDEIS japo bado iliendelea kuwa siri ya familia elimu aliyokuwa nayo na uwezo wakifedha hauku msaidia kujua madhara ya kutoa mimba kwa binti yake.
Akafosi ilikujiepusha na aibu na fedhea ambayo angeipata kutoka kwa marafiki zake na matajiri wenzie wa kubwa kwanza kwa binti yake kupata ujauzito nje ya ndoa pili kutaka kuolewa na mwanaume ambaye hakuwa na uwezo ni masikini wa kutupwa.
Wakati ulienda na masiku yalisogea ikapita siku masiku wiki na hatimaye mwezi Sam asijue hatima yake ndani ya maabusu ile mwisho wa siku alichukuliwa na kupelekwa katika gereza la watu walio kwisha hukumiwa na kutumikia kifungo asicho kielewa.
Muda ulisonga na hatimaye Stellar alipata auheni taratibu za harusi ya kifahari zilifanyika, harusi iliyotikisa jiji zima lenye kila kituko cha dunia. Harusi ilipambwa vyema kutokana na umaarufu wa baba wa bi kharusi mzee SUDDEIS.
Naam bi kharusi alipendeza mno alionekana mwenye furaha kipindukia huku akiwa hana kumbukumbu kamili juu ya jana yake ambayo alikuwa akielea katika maumivu makali ya mapenzi juu ya kijana masikini.
Kwa mara ya kwanza stellar ilimjia kumbukumbu ambayo alikwisha isahau miaka mitano iliyopita.
"mungu wangu Sam alipatwa na nini kwani baada ya pale..? "Alijiuliza tena swali ambalo jibu la swali lile alikuwa nalo Sam pekee.
Haraka akajiandaa na kuchukua gari yake na safari ya kuelekea vingunguti ikaanza, Baada ya dakika kadhaa alikwisha wasili eneo ambalo alilikusudia haraka akatembea huku akiwa ajiamini mpaka alipoufikia mlango wa mbao miongoni mwa milango mingi iliyopo mahali pale ambapo ndipo hasa alipo pakusudia.
Taratibu akagonga na baada ya muda mlango ulifunguliwa alikuwa msichana wa makamo akifunga kanga moja katika Kifua chake bila shaka alikuwa akitoka katika dimbwi la usingizi.
ITAENDELEA SIMULIZI HII PIA HUPATIKANA KWA WHATAPP NA EMAIL PIA KWA BEI NAFUU ZAIDI COMMENT NAMBA YAKO NIKUADD KWENYE GROUP LA SIMULIZI ZA ZAYNAB TALY UNASUBIRI NN JUMATANO NITAKUJA NA SEHEMU YA KUMI NA TATU......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: